Chelsea yasemekana kumtema Drogba

Aomba Msamaha.

Kuna habari kuwa Klabu ya Chelsea iko mbioni kumtema mchezaji wake mahiri Didie Drogba kwa kumuuza kwa Klabu yeyote itakayotoa donge nono.

Hii inatokana na kitendo cha mchezaji huyo hivi karibuni kutoa maneno machafu mbele ya hadhara (dunia) kupitia Luninga kwenye mtanange wa Ligi ya Mabingwa (Champions Leagu) dhidi ya timu ya Barcelona katika kuwania nafasi ya kucheza Fainali na Mabingwa watetezi Manchester United.

Gonga Player kusikia alichosema Drogba, Tunasikitika maneno haya sio mazuri kuyarudia mbele ya jamii, hivyo bonyeza kwa matakwa yako binafsi-Mhariri

Drogba ambaye kama washabiki na wachezaji wengine alikerwa na kitendo cha refa kukataa Penalti nne za wazi kwa timu yake ya Chelsea na uamuzi mbaya kwenye mechi hiyo ambao ulipelekea timu yetu aaah samahani Timu ya Chelsea kupoteza mchezo huo.

Pamoja na kuomba msamaha bado kikao cha Uongozi kitaamua hatua zaidi ya kuchukua kama Klabu kwa Drogba ambaye ameonyesha utovu wa nidhamu na dharau kubwa, “…"Nilipandwa na mori na kujikuta ninatamka maneno yasiyostahili. Ninaomba msamaha," alisema Drogba. "Ninakiri kwamba matamshi yangu hayakufaa na hayakutoa mfano mzuri kwa wale waliokuwa wakitizama televisheni, hasa watoto." alisema Drogba kwenye maelezo yake kwa uongozi na maelezo kama hayo yaliyokaririwa kwenye mtandao wa Klabu hiyo.

Mchezaji huyo analipwa mshahara wa Paund 91,000 kwa wiki kwa sasa na kumfanya kuwa miongozni mwa wachezaji aghali pia.

Advertisements

One Response to Chelsea yasemekana kumtema Drogba

  1. I think that is an informative submit and it is educated and pretty helpful. I’d prefer to thank you for your efforts you have got manufactured in writing this post.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: