Lady Jay Dee ni zaidi ya mwanamuziki

n590146649_2170467_667435

Ukinitajia mwanamuziki Lady Jay Dee kwangu ninayojinsi  ninavyomuangalia mwanadada huyu. Napenda sana ubunifu alionao na jinsi anavyoimba kwa kutumia sauti asilia ambayo inaandikika kimuziki, nikiwa namaana kuwa muziki wake uko kwenye Note za kimuziki hasa na hivyo kutompa kazi prodyuza yeyote au wapiga vyombo wake.

Nilipopata nafasi ya kuongea na Maneno Uvuruge (Gonga hapa usome mahojiano naye)ambaye kwa wakati fulani aliwahi kufanya kazi na Machozi Band yake Lady Jay Dee anasema kuwa kati ya watu alifanya kazi nao basi hatomsahau Lady Jay Dee kwani walikuwa wakiongea lugha moja “unajua kama mtu anayeimba anaimba kwenye note hupati taabu mpiga ala, ila kama muimbaji anatoka nje ya note anakupa taabu wewe kumfunika ili washabiki wasielewe, alisema Uvuruge ambaye anapiga Solo kwenye Band ya Kilimanjaro Connection inayopiga muziki nchini Malaysia kwa sasa.

Kwangu mimi Lady Jay Dee ni zaidi ya Mwanamuziki.

Hivi karibuni mwanamuziki huyu alitembelea huko mikoa ya kusini na kugawa Vyandarua kwa ajili ya kampeni ya kutokomeza Malaria na huko alikutana na Mwanamuziki maarufu Barani Africa Balozi wa Malaria Afrika Princess Vyone Chaka Chaka.

11

Lady Jay Dee akisalimiana na Waziri Mkuu Mizengo Pinda huko Ntwara.

12

Akichangia jambo pamoja na Waziri Mkuu na Yvone Chaka Chaka Kulia.

n590146649_2161315_1150291

akiwa Hospitali na kugawa Vyandarau kwa akina mama wajawazito

Sikiliza kibao cha Siwema toka kwake Lady Jay Dee anayepiga gitaa mwanzo kulia ni Maneno Uvuruge.

Advertisements

4 Responses to Lady Jay Dee ni zaidi ya mwanamuziki

 1. Mpwaa says:

  Mpwaa unanifurahishaga sana mi pia namkubali sana huyu dada, ila siku hizi naona kama natoka nje ya style yake ya uimbaji kama huu wimbo uliouweka umenikumbusha mbali sana.

 2. Najma says:

  Nakubaliana na wewe hapo juu
  nyimbo za zamani za Jay Dee zilikuwa nzuri sana ingawaje hata za sasa hivi ni nzuri but i like more Oldies

 3. johnso bella says:

  allo mimi niko johnson na ishi canada yani nilikuwa nawatumiya hiyi message ili niangaliya kama muna weza kujibu samahani kwa kiswahili lakini acha niwa ache mukiona hiyi message munijibu pls ina nifurahisha na tena mutakuwa mumefanya vuzuli ansanteni bye

 4. Jeni says:

  Naungana na nyie kwamba huyu dada ni hatali tena anatisha maana anaimba kwa sauti yake mwenyewe sio zile za kuiga eti ni za kisasa

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: