Fouta Djallon na mbirime vyake Koffi Olomide

April 12, 2009

Weekend tulivu nakuacha na kibao cha Fouta Djallon toka kwake Gwiji Koffi Olomide wakati huo team ikiwa imekamilika pamoja na akina Suzuki na wengineo.

Sikiliza jinsi jamaa anavyolalamika na sauti yake halafu utaniambia.

Kisha sikiliza hiki cha Mbirime


Maofisa wa Kandanda washikiliwa Ivory Coast

April 12, 2009

Mmoja wa Majeruhi akitolewa uwanjani wakati wa maafa hayo.

Mmoja wa Majeruhi akitolewa uwanjani wakati wa maafa hayo.

ABIDJAN, Ivory Coast

MAOFISA wa Shirikisho la Soka la Ivory Coast (FIF) juzi walitiwa mbaroni kwa muda na polisi kama sehemu ya uchunguzi wa matukio ya vifo vya mashabiki 22 na wengine zaidi ya 100 katika mchezo wa kufuzu kwa fainali za Kombe la Dunia kati ya nchi hiyo na Malawi mwezi uliopita. Miongoni mwao ni Albert Kacou Anzouan, mwenyekiti wa kamati ya mashindano ya shirikisho hilo ambaye alikamatwa tangu Jumatano akihojiwa kuhusiana na mauzo ya tiketi.

Maofisa wa FIF wameliambia Shirika la Habari la AFP kwamba wengine walikuwa ni mchapishaji wa tiketi za mchezo huo, mhasibu mkuu wa FIF, Jean-Baptiste Beugre. Hao walikuwa maofisa wa kwanza wa ngazi za juu kukamatwa tangu kuanza kwa uchunguzi huo Machi 31, siku mbili baada ya tukio hilo baya.

Mashabiki wenye uchu wa kuwaona wachezaji wao nyota, Didier Drogba na wengine walilazimisha kuingia uwanja wa Abidjan wenye ujazo wa watu 35,000 na kusababisha kuporomoka kwa jukwaa na kuwakandamiza hadi kufa baadhi yao. Wengi wao walikuwa na tiketi za kuona mchezo huo, lakini walikasirishwa na kuzuiwa kuingia uwanjani, ameeleza mmoja wa mashuhuda, akiwatuhumu maofisa usalama kwa kupokea hongo na kuwaacha mashabiki wakiingia uwanjani kuona mechi.


Lt. Irin, Komandoo mdada.

April 12, 2009

Irin

Pichani ni Ltn. Irin wa Kikosi cha Commandoo cha Malaysia, akiwa na umri wa miaka 23 amekuwa ni kati ya Makomandoo wa kike wadogo katika jeshi hilo. Irin alipamba vyombo vya habari kwenye maonyesho ya Jeshi yaliyofanyika hivi karibuni hapa Kuala Lumpur Malaysia.


%d bloggers like this: