Mama wa miaka 50 na mwanaye mjamzito wakutwa na madawa ya Kulevya

December 17, 2008
im Ah Mooi (left) and her pregnant daughter Hwei Wen Chiu

im Ah Mooi (left) and her pregnant daughter Hwei Wen Chiu

WATAHUKUMIWA ADHABU YA KIFO WAKIKUTWA NA HATIA

George Town, Malaysia: Hwei Wen Chiu mwenye miaka 27 amefikishwa mahakamani akiwa pamoja na mama yake mzazi Lim Ah Moon (50) kwa kosa la kukutwa na madawa ya kulevya aina ya Heroin.

Ilidaiwa kuwa Hwei Wen Chiu ambaye anamimba ya miezi miwili na pia ni mama wa mtoto mdogo wa mwaka mmoja alikutwa na madawa hayo yenye uzito wa takriban Gram 882 akiwa na mama yake mzazi siku ya tarehe 5 December ndani ya Tawi la Bank ya RHB Bank Berhad, Lebuh Pantai, tarehe 5 Dec. Kwa mujibu wa sheria za Malaysia watuhumiwa hao pichani wakikutwa na hatia watahukumiwa adhabu ya KIFO.

Hakimu Noor Fadzila Ishak  alilikataa ombi la wakili wa washtakiwa Mh. Jagdeep Singh Deo kuwapa dhamana ambapo alidai kuwa wateja wake mmoja ni mzee na afya yake haimruhusu kwenda rumande na wa pili ni mja mzito wa miezi miwili na kusema kuwa katika kipindi hiki hapaswi kulala rumande kwani anahitaji uangalizi wa karibu. Kesi imehairishwa mpaka tarehe 8 January itakapohamishiwa Mahakama kuu kwani uzito wa kesi hii ni wa mahakama kuu.


Namba yangu ndio hiyo NIPIGIE!!

December 17, 2008

.

.

Mwanadada wa kijapani akimuwekea kikaratasi mfukoni mwa mchezaji wa Manchester United Cristian Ronaldo walipokuwa wakiwasili uwanja wa ndege huko Japan mapema majuzi kwa ajili ya mchezo wa nusu fainali ya Club World Cup. alipoulizwa na mwandishi wa habari mwanadada huyu alisema amefanikisha ndoto yake ya kumpa mchezaji huyo namba pamoja na email yake, hata asipompigia leo anaimani ipo siku atamkumbuka. Bwana wee acha tuu!!. Pichani chini wachezaji wakiwasili Tokyo International Airport huko Narita karibu na Tokyo.

.

.

Pichani chini baadhi ya mabango ya kuipokea Manchester United huko Japan

.

.


%d bloggers like this: