Patchou Lumiere, Nyota mpya ya kizazi kipya cha Kongo

December 11, 2008

kila siku kuna sauti mpya, wimbo mpya, mwanamuziki mpya, Hivi karibuni kundi la Rhumba la Muziki lilifanya rekodi ya albamu yake chini ya Kiongozi Pitshou Lumiere na mwanamuziki huyu anasemekana kutumia pesa nyimngi katika kutengeneza Video za Nyimbo za Albamu yake, kwa sasa Koffi Olomide anatajwa kuwa ndiye Mwanamuziki wa Zaire ambaye hutumia pesa nyingi katika kutengeneza Video za nyimbo zake ikiwa ni kuanzia Kampuni ya Utengenezaji, Mavazi na sehemu anazotengenezea Video hizo, lakini Video za Muziki za Pitshou zilipigwa kwa mbwembwe kama picha zinavyoonyesha.

Kava la juu la CD ya Bendi ya Rhumba la Muzika
Kiongozi Pitchou Lurmiere akiwa kwenye shooting ya wimbo wa Chez Ntemba

Mbwembwe za Pitshou wakati wa shooting ya wimbo wa Moise Katumbi unaopatikana kwenye Albamu hiyo.
Vimwana wakiwa wamekula pozi wakati wa shooting ya wimbo wa Chez Ntemba kwenye albamu ya kundi la Rhumba la Muzika.
Lumiere akiwa na Vimwana katika moja ya vibwagizo vya nyimbo zake.

Wanamuziki wa Kongo katika suala la burudani ya muziki wa dansi wamepiga hatua, kuliwahi kuzuka mjadala wa kuhusu kitendo cha kundi la TOT Respect chini ya uongozi wa Kamarade Ali Choki kwenda Kongo kutafuta wanamuziki kwa ajili ya kuipa nguvu kikosi chake lilipigiwa kelele na wengi wakaonyesha kuwa ni kuua na kutothamini muziki wetu, lakini katika dunia ya leo ya utandawazi ambapo kimsingi hakuna mipaka kila mmoja anajaribu kuangalii kama si unafuu basi kiwango katika kukamilisha liziko la nafsi (satisfaction). Je ni kweli kuna haja ya kufanyiwa mabadiliko muziki wetu? Kwani tumeona jinsi bendi zilnazopiga muziki wetu kuchanganya na Rhumba ya Congo kama Twanga Pepeta zinavyofanikiwa.

Tembea uone; Under Water Wedding

December 11, 2008

Siku ya Kuoa au kuolewa ni siku pekee ambayo mtu anatakiwa asiisahau kwani kwa wengi wanaoamini siku hii huja mara moja ila kama tuu kutakuwa na ndoa ya mitala. Inaitwa Under water Wedding, ni maarufu kwa kipande hii ya Asia (Malaysia na Thailand) kwa Malaysia Chama cha Waogeleaji ndio mtaji wao mkubwa wakishirikiani na Hotel kubwa ambapo utapenda Harusi yako ifanyike. Package ya harusi hii ni Malaysian Ringit 160 (55,000 Tsh) kwa kila kichwa na idadi ya chini ni watu 60. Hii inakuwa ni pamoja na Vinywaji na Vilaji kwa waalikwa wako, Keki kwa ajili ya maharusi, Champagne 5, Mitungi ya Gas kwa ajili ya maharusi na yeyote atakaye hitaji kuzamia, Albamu ya Picha pamoja na DVD moja ya kumbukumbu ya tukio zima, Fataki 10Kg, pamoja na gharama za kuiandikisha ndoa na Cheti cha Ndoa kwa anayetaka anakaribishwa kuja Malaysia hakuhitaji VISA kwa Mtanzania.

TID atoka Segerea kwa msaamaha wa Rais

December 11, 2008
TID

TID

Na Dina Ismail wa Tanzania Daima
MSANII wa muziki wa kizazi nchini Khalid Mohammed ‘maarufu kama TID’ aliyekuwa akitumikia kifungo cha mwaka mmoja katika gereza la Segerea, jana aliachiwa huru kupitia msamaha kwa wafungwa uliotolewa na Rais Kikwete katika maadhimisho ya miaka 47 ya Uhuru.

TID ambaye Julai 23, mwaka huu alihukumiwa katika mahakama ya Kinondoni kutokana na kujeruhi, alikuwa ni mmoja ya wafungwa 4,306, walionufaika na msamaha huo ambao ni kwa mujibu wa Ibara ya 45 (1) (d) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kwa mujibu wa Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa jana na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Lawrance Masha, ana imani wafungwa watakaoachiliwa watarejea tena katika jamii kushirikiana na wenzao katika ujenzi wa taifa na watajiepusha kutenda makosa ili wasirejee tena gerezani.

Kutokana na kuachiwa huru huko kwa TID, mashabiki wa msanii huyo jana walikuwa katika furaha za aina yake kwa kupita katika maeneo ya Kinondoni yalipo makazi ya msanii kuyo na kushangilia huku baadhi yao wakiwa wamevua mashati.

TID alirejea nyumbani kwake akiwa ndani ya gari aina ya Pajero, akisindikizwa na magari kadhaa alionekana ni mpole na mtulivu tofauti na alivyozoeleka kabla ya kukumbwa na kifungo hicho.


%d bloggers like this: