Simba Chaliii!!

July 24, 2008
Yachapwa na URA ya Uganda kwenye Nusu fainali
Kimoja tu hoii

Kimoja tu hoii

Simba ya Tanzania leo imeshindwa kufanya kile walichotazamiwa kukifanya baada ya kuchapwa na URA ya Uganda 1-0 katika mchezo wa kwanza wa Nusu Fainali wa kombe la Kagame, Pamoja na Simba kupata penati dakika za mwishoni penati ambayo mchezaji wa Simba Mnigeria Emeeh Izechukwu  alipiga fyongo na kipa wa URA kuicheza jambo lililofanya mashabiki kuloa ukimya, Hii inawapa watani wao cha kusema kwani nao leo katika uwanja huo mpya wanakutana na Tusker ya Kenya, Yanga ambao jana walikuwa wakishangilia kwa kuimba Aki na Ukwa… aki na ukwa.. ikiwa ni kejeli kwa watani wao wa jadi ambao wamesajili wachezaji wawili toka Nigeria. Simba watakutana na timu itakayopoteza mchezo wa leo. URA, washindi wa kwanza wa kundi la Morogoro ambao walianza kwa kuichakaza Rayon Sports ya Rwanda kwa mabao 4-1 na kuonyesha safu kali ya ushambuliaji. habari ndiyo hiyoo.

Advertisements

Mwali kamuona mwali…

July 24, 2008
Warembo wa Miss Tanzania, Picha na Father Kidevu

Warembo wa Miss Tanzania, Picha na Father Kidevu

baadhi ya warembo wanao wania taji la Vodacom Miss Tanzania 2008 wakiwa katika picha ya pamoja katika gari ambalo mshindi wa kwanza atazawadiwa. gari hilo Suzuki Grand Vitara linathamani ya sh milioni 42.


Brazili wako Singapore

July 24, 2008
Brazil

Brazil

Nyota wa Brazili Ronaldinho akiwasili kwenye hotel huko Singapore tayari kwa chakula cha mchana leo hii  July 24, 2008. Timu ya Taifa ya Brazil iko Singapore kwa ajili ya matayarisho ya michezo ya Olympic itakayoanza baadaye mwezi ujao huko Beijing China. (AFP PHOTO)


Yanga yatinga Robo Fainali

July 24, 2008

Yaitwanga Vital’O ya Burundi 2-0

Kikosi cha Timu ya Yanga ambacho kiliitoa Kamasi Vital'O ya Burundi, Picha na Mrocky Mrocky

Kikosi cha Timu ya Yanga ambacho kiliitoa Kamasi Vital'O ya Burundi, Picha na Mrocky Mrocky

YANGA imewapa raha Watanzania baada ya kuiadhibu Vital’O ya Burundi kwa mabao 2-0 na kufuzu kuingia nusu fainali ya Kombe la Kagame ambako sasa itakutana na Tusker ya Kenya, kesho.

Tusker, ilifuzu kwa mbinde katika mchezo wa awali ilifuzu kwa hatua hiyo baada ya kuilaza kwa penalti 7-6 Rayon Sports ya Rwanda. Read the rest of this entry »


Blanchard Deplaizir kurekodi na Jay Dee, Ali Kiba pamoja na Akudo

July 23, 2008
Blanchard De Plaizir katika pozi

Blanchard De Plaizir katika pozi

Mwanamuziki anayekuja kwa kasi toka Jamhuri ya Congo Blanchard Deplaizir amesema kuwa yuko katika maandalizi ya kwenda Dar Es Salaam kwa ajili ya kurekodi nyimbo tatu ambazo amesema atafanya kolabo na wanamuziki wa Kitanzania. Blanchard ambaye anapiga muziki wenye mahadhi ya Rhunba, na hata Rap pia maskani yake yako jijini London baada ya kuhamia huko yapata miaka 20 iliyopita na shughuli zake za kimuziki anaziendeleza huko.

De Plaizir akiwa na kikosi chake mbele ya mashabiki lukuki nakati ya Londone.

De Plaizir akiwa na kikosi chake mbele ya mashabiki lukuki nakati ya Londone.

Akiwa Tanzania Blanchard atafanya kolabo na Ali Kiba, Lady Jay Dee na Akudo ili kuweka vionjo vya muziki wa Africa Mashariki hasa Tanzania ambao anasema kwa kiasi kikubwa anauhusudu sana.

Akiongea na Spoti na Starehe jioni hii Blanchard alisema, “nimeongea na Meneja wa Lady Jay Dee Gadna Gee Habash, kimsingi wamekubaliana na terms na nia yangu nafikiri safariitakuwa mwezi wa nane au hadi wa tisa”

“Nimesikia nyimbo za Akudo nimewapenda sana wanaimba vizuri nafikiri safari yangu itakuwa na mafanikio huko” aliongeza Deplaizir.

Aidha kwa sasa Blanchard anasema anafanya kazi na Bongo Dj, timu ya madj watanzania walioko nchini Uingereza ambao ni mabingwa wa matamasha kwa wanamuziki toka Afrika hasa Tanzania, katika mwezi ujao Blanchard atafanya maonyesho mawili yaliyoandaliwa na Bongo Family/DJ tarehe 22 atakuwa reading na tarehe 23 watafanya Milton Keynes, hii yote ni live band akishirikiana na akina dada mastage shoo wake.

Katika Albamu yake ya sasa Blanchard alishirikisha watu mbalimbali akiwemo Titina Alcapone ambaye alipata kuwa mwanamziki wa Wenge BCBG kwa muda mrefu kabla ya kwenda kwa Koffi Olomide na kisha kutoka kivyake.


TID aswekwa Segerea!

July 23, 2008
TID

TID

MSANII maarufu wa muziki wa kizazi kipya (Bongofleva), Khalid Mohamed maarufu kama T.I.D jana amehukumiwa kutumikia kifungo cha mwaka mmoja jela kufuatia kupatikana na hatia ya kushambulia na kujeruhi.
T.I.D mwenye umri wa miaka 26 alisomewa adhabu yake hiyo na Hakimu Hamisa Kalombola wa Mahakama ya wilaya ya Kinondoni baada ya Hakimu huyo kuridhika na ushahidi ulitolewa na mashahidi wanne walioletwa mahakamani na upande wa mashtaka.
katika utetezi wake TID aliiomba mahakama imhurumie kwani alitenda kosa hilo sababu ya ulevi na kuwa familia yake inamtegemea hasa mama yake.
Hata hivyo Hakimu Kalombola alitoa hukumu hiyo kwa kumwambia mshtakiwa “kwa vile huwezi kujimudu ukilewa na huwezi kujizuia kunywa na kuhukumu uende jela mwaka mmoja ujifunze ili usiwe unakunywa hizo pombe” Read the rest of this entry »


Asha Baraka aja kivingine

July 23, 2008

Mkurugenzi wa Kampuni ya African Stars Entertainment Tanzania (ASET) Asha Baraka (kulia) Akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo juu ya kuanzishwa kwa bendi yake mpya itakayofahamika kama Vibration Sound.Kushoto kwake ni Eriston Angai (kiongozi wa bendi hiyo) na anayefuatia ni mwimbaji wa bendi hiyo Dispatch. PICHA NA GPL


%d bloggers like this: