Lady Jay Dee kuwania tuzo KORA 2008

Judith Wambura AKA Lady Jay Dee

Judith Wambura AKA Lady Jay Dee

Mwanamuziki nyota wa Tanzania, Judith Wambura ‘Lady Jaydee’ ameteuliwa kuwania tuzo ya Mwanamuziki Bora wa Afrika Mshariki katika Tuzo za Kora 2008. Kwa mujibu wa gazeti la New Vision la Uganda, Jaydee ni mwanamuziki pekee kutoka Tanzania kuchangulia kwenye kinyang’anyiro cha mwaka huu.

Jaydee ambaye anawania tuzo hiyo pamoja na Susan Kerunen, Klear Kut, Michael Ross na Blu3 kutoka Uganda na nyota wa Kenya, Nameless, Valerie Kimani na Wahu. Mwanamuziki huyo pekee wa bongo fleva kutoka Tanzania anawania kunyakua tuzo hiyo ambayo fainali zake zitafanyika Desemba 6, Tinapa, Nigeria.

Kwa mara ya kwanza msanii bora wa Afrika ataondoka na kitita cha dola za Marekani milioni moja kutoka First Bank of Nigeria. Tuzo za Muziki za Kora ni kubwa Afrika zinazojumuisha wakali kutoka nchi mbalimbali.

Jaydee ambaye amewahi kutwaa tuzo kadhaa za kitaifa na kimataifa aliwahi kuchaguliwa kuwania tuzo za Kora mwaka 2003 (Mwanamuziki wa kike anayechipukia Afrika) na mwaka 2005 (Mwanamuziki Bora wa Kike Afrika). Katika tuzo za mwaka jana Ambwene Yesaya ‘AY’ alikuwa ni msanii wa Tanzania aliyechaguliwa kuwania tuzo hizo. (Na Habari Leo)

Advertisements

7 Responses to Lady Jay Dee kuwania tuzo KORA 2008

 1. nathan says:

  hongera jay, keep it up!

 2. michelle says:

  Wala asipoteze muda wake hana jeuri hiyo, mlinganisheni na makoma waliwahi kutwaa tuzo hiyo je anaweza kuwa kufika hata nusu ya hiyo, acheni upuuzi mwataka kujiaibisha tu.

 3. Michaelmas says:

  Hello!

  Wowwwwwwww! Hongera sana Binti Machzoi….Jamani watanzania wote tujitahidi kumpigia kura Lady Jay Dee ili aweze kuitangaza nchi yetu vizuri…….!

  Tanzania tutatoka! Jay Dee!

 4. juma numbi says:

  congratulation dada

 5. Judith Joseph says:

  niambie wa wajina, nakufill sn km kuna m2 anakuchukia hana lake,kaza buta waache wenye roho mbaya

 6. Fairly particular he’ll possess a fantastic read through. Thank you for sharing!

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: