Post Zilizotangulia kwa Mwezi huu

July 14, 2008

Wapenzi wasomaji, nimehamisha Post zote toka anuani yangu ya zamani ya http://spotistarehe.blog.com kuja https://spotistarehe.wordpress.com. Hapa utaweza kuziona Post zote lakini hutoweza kusoma Comments kwa sababu zilizo nje ya uwezo. Pia kwa Post za Miezi iliyopita zinapatikana hapo Juu kwenye viungio vya Kuanzia May na June. Pius

Mpira si lelemama atii…

In this photo released by CBF, Brazil's soccer player Ronaldinho jumps as physical trainer Paulo Paixao instructs him from behind as Ronaldinho trains for the Beijing Olympics in Porto Alegre, Friday, July 11, 2008. Ronaldinho said he plans to play for Brazil at the Olympics in defiance of the wishes of his FC Barcelona club.

Mchezaji wa soka wa Brazil Ronaldinho akiruka juu kwenye mazoezi ya viungo huku mwalimu wa mazoezi hayo Paulo Paixao akimuongoza pembeni walipokuwa wakifanya mazoezi kwa mara ya kwanza kwa ajili ya michezo ya Olympic itakayofanyika baadaye mwezi ujao huko Beijing China. Pia timu ya AC Milan imetangaza mikakati ya kukamilisha kumchukua mchezaji huyu wa FC Barcelona club. (AP Photo/CBF)

Simba yaanza vibaya Kagame lakini yaweka historia…

SIMBA imeanza vibaya michuano ya Kombe la Kagame baada ya kufungwa na Tusker ya Kenya mabao 3-2 katika mchezo wa ufunguzi ambao pia imeifanya michuano hiyo ianze kwa karamu ya mabao.

Pichani Mchezaji kiungo wa Simba ya Tanzania, Henry Joseph akiwatoka wachezaji wa Tusker ya Kenya, katika mchezo wa fungua dimba wa Kombe la Kagame kwenye uwanja wa Taifa Dar es Salaam jana. Simba ililala 3-2. Katika mchezo huo wa Leo Simba pia imeweka historia ya soka nchini kuwa timu ya kwanza ya klabu kucheza kwenye uwanja mpya wa Taifa jijini Dar es Salaam, itakapopambana na Tusker ya Kenya. (Picha na Mwananchi)

Kocha mpya wa Portugal

Manchester United manager Sir Alex Ferguson (R) and assistant Carlos Queiroz hold the trophy after the UEFA Champions League final May 21.
Carlos Queiroz (L), ambaye alimsaidia Sir Alex Ferguson katika mtanange wa Champions League na hatimaye kushinda kikombe hicho, ametangazwa kuwa ndiye kocha mpya wa Portugal ambaye atabeba mikoba ya Fellipe Scolari ambaye kwa sasa amejiunga na Klabu ya Chelsea. (Picha na Get Image)

Friday, July 11, 2008

Miss Tanzania EU ajitoa kinyang’anyiro cha Miss Tanzania

Miss Tanzania EU 2008 – LUCY MWIZA FUNDIKIRA amejitoa katika kinyang’anyiro cha Miss Tanzania kinachotarajia kutifua baadaye mwezi ujao jijini Dar Es Salaam.

Akizungumza na wanahabari Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya Lino Agency waandazi wa Miss Tanzania Uncle Hashim Lundenga amesema kuwa walipata taarifa toka kwa muaandaaji wa shindano hilo EU kuwa Miss Fundikira hatoshiriki kwenye kinyang’anyiro hicho bila kusema kiundani sababu hasa za kufikia maamuzi hayo.
Hata hivyo habari zinasema Miss Lucy ni mmoja wa mamiss wanne ambao hawatoshiriki kwenye kinyang’anyiro hicho.
Mrembo namba mbili Kinondoni, Joan Faith pia amejitoa katika shindano na nafasi yake imechukuliwa na Miss Temeke namba nne Lilian Shayo baada ya warembo namba nne na tano wa kanda hiyo kushindwa kufika katika kambi hiyo,” alisema Lundenga.

Ze Comedy waenda Mahakamani

KUNDI la wasanii wa vichekesho la Ze Comedy limefungua kesi dhidi ya Televisheni ya EATV, Chama cha Hakimiliki Tanzania (COSOTA) pamoja na Msajili wa Nembo za biashara, likiomba Mahakama iwazuie kuingilia biashara zao na kuruhusu kutumia jina lao.

Kwa mujibu wa Mawakili wanaowawakilisha kundi hilo Moses Kalua na Peter Swai, kesi hiyo ilifunguliwa mwishoni mwa wiki katika Mahakama Kuu Kitengo Cha Biashara.

Kwa mujibu wa hati ya mashitaka iliyoko mahakamani hapo inaiomba Mahakama hiyo kutoa tamko kuwa walalamikaji hao ni wamiliki wa jina la Ze Comedy kabla na baada ya kuingia makubaliano na walalamikiwa.

Pamoja na maombi hayo pia wasanii hao wanaiomba Mahakama hiyo kuamuru walalamikiwa hao kulipa fidia ya Sh milioni 200 kama adhabu kwa usumbufu waliousababisha. Endelea kwa kusoma Habari Leo

Serikali yaruhusu Kagame Cup Wanja Jipya

SERIKALI imekubali kutumika kwa Uwanja Mkuu wa Taifa, Dar es Salaam kwa ajili ya mashindano ya Kombe la Kagame yanayotarajia kuanza kesho.

Akizungmza Dar es Salaam jana, Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Leodeger Tenga, alisema serikali imekubali utumike kwa baadhi ya michezo, ambapo mingine itafanyika kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam (uwanja wa zamani) na Jamhuri, Morogoro.

Alisema mchezo wa ufunguzi kesho kati ya Simba na Tusker kwa Kundi A na ule wa Jumapili Kundi C kati ya Yanga na APR itafanyika kwenye uwanja huo ambao ni mpya na wa kisasa, ambapo pia michezo ya robo fainali na nusu fainali itafanyika kwenye uwanja huo kama timu za Tanzania zitaingia hatua hiyo.

Pia alisema mchezo mwingine utakaofanyika kwenye uwanja huo mpya ni wa fainali na kuongeza kuwa timu za Tanzania zinapaswa kucheza kwa bidii kwani zimepata nafasi ya kuutumia. (Na Majira)

Wanasoka Gabriel, Nizar waelekea Ulaya kwa soka la kulipwa

WACHEZAJI wawili wa kimataifa wa Tanzania, Emanuel Gabriel na Nizar Khalfan wanatarajiwa kuondoka nchini kwenda barani Ulaya kusakata soka la kulipwa.

Katibu mkuu wa TFF, Fredrick Mwakalebela alisema Gabriel, ambaye anafunga ndoa Julai 14, ataondoka nchini Julai 19 kwenda Israel kufanya majaribio ya kucheza soka la kulipwa, wakati Nizar anatakiwa Hungary.

”Kinachomchelewesha Gabriel ni harusi yake, anafunga ndoa mwezi huu tarehe 14. Isingekuwa harusi ungekuta ameshaondoka,” alisema Mwakalebela.

”Nizar pia yupo mbioni siku yoyote kuanzia sasa kwenda Hungary. Awali suala la viza ndilo lililomkwamisha, lakini kila kitu sasa hivi kinakwenda vizuri na ataondoka wakati wowote kuanzia sasa,” alisema.

Wachezaji wote wawili wana uzoefu wa kucheza nje ya nchi. Gabriel ameshakwenda Arabuni kucheza soka la kulipwa mara mbili na alirejea nchini mwishoni mwa msimu uliopita, wakati Nizar alikuwa nchini Kuwait kuchezea klabu ya Odlaham iliyomnasa wakati Stars ilipokwenda Uswisi kwa mazoezi.

Mwakaleleba pia alisema kuwa kiungo wa zamani wa Simba, Pius Kisambale na Erick Majaliwa wameondoka nchini juzi kwenda India na tayari wamesaini mkataba wa kuichezea klabu ya Dispot India ya nchini humo.

Alisema mbali na nyota hao pia beki wa Simba, Said Sued yupo kwenye hatua za mwisho za kukamilisha safari yake ya kwenda barani Ulaya kusaka soka la kulipwa. Sued aligoma kusaini Simba msimu huu.

Mbali na wachezaji hao kutimkia nje, beki aliyeachwa na Yanga, Lulanga Mapunda na Uhuru Selemani, ambaye klabu yake ya Coastal Union imeshuka daraja, wamemwaga wino kuichezea Miembeni ya Zanzibar.

Mwakalebela alisema wachezaji hao wapo kwenye orodha ya kikosi cha Miembeni kitakachoshiriki Kombe la Kagame inayoanza kesho jijini Dar es salam na Morogoro.

Wakati huo huo Mwakalebela amesema Cheti cha Uhamisho wa Kimataifa (ITC) cha kipa mpya Mserbia wa Yanga, Obren Curkovic kimewasili. (Na Na Mwananchi)

Blatter yuko sawa: Ronaldo

Mchezaji wa Ureno na Manchester United Cristiano Ronaldo, amesema kuwa Rais wa shirikisho la Mpira wa Miguu duniani Sepp Blatter alikuwa sahihi alipotakiwa kutoa maoni yake juu ya sakata la wachezaji pale alipomtolea mfano yeye na sakata la kuhama Manchester United na kusema huu ni “Utumwa wa kisasa” na Ronaldo ni mhanga wa aina hii ya utumwa. Blatter alisisitiza kuwa mpira ni ajira kwa hawa vijana na kuzitaka klabu ziwe nyepesi kuruhusu mtu akitaka kuhama.

Soka ya wanawake si lelemama atii

Brazil's Tania, center, and Maurine (15) attempt to score on Canada goalie Karina LeBlanc, left, during the first half of a friendly soccer match in Toronto, Thursday, July 10, 2008.
Mchezaji wa timu ya wanawake ya Brazil Tania, katikati, na Maurine (15) wakifanya mashambulizo kwenye lango la Canada huku golikipa wa Timu ya wanawake ya Canada Karina LeBlanc akijiweka tayari kutoa hatari langoni mwake, Hii ilikuwa jana wakati wa mchezo wa kirafiki kati ya timu zao uliochezwa Toronto Canada (ESPN)

Liverpool yaongeza nguvu

Liverpool Football Club manager Rafael Benitez (centre) welcomes new signings, Swiss defender Philipp Degen (L) and Italian defender Andrea Dossena, at their Melwood training ground in Liverpool, north-west England, on July 10.

Meneja/Kocha wa timu ya Liverpool Football Club Rafael Benitez (katikati) akiwakaribisha vijana wake wapya mara baada ya kudondoka wino, defender mswiss Philipp Degen (shoto) na muitaliano Andrea Dossena, Ukaribisho huu uulifanyika jana huko Melwood kwenye wanja lao la mazoezi mjini Liverpool. Timu nyingi duniani ziko kwenye usajili kwa sasa zikijiandaa na msimu mpya wa ligi zao. (AFP)

Warembo washawasili Bagamoyo

WAREMBO WASHATIA KAMBI BAGAMOYO!
Hivi sasa Warembo wanaowania taji la juu la Miss Tanzania mwaka huu washatia kambi Bagamoyo na leo wanapewa semina. Kumjua mshindi wa mwaka huu, pengine ni bado mapema, lakini atajulikana muda si mrefu pindi watakapoanza kuwekwa hadharani na wale waliotoka mikoani. (Na GPL)

Wednesday, July 9, 2008

Chama cha riadha na TOC wavutana kuhusu wadhamini


Li-Ning

Kumekuwa na mvutano kati ya makampuni mawili ya Vifaa vya michezo kuhusu Ni vifaa vya kampuni gani Timu ya Taifa inayokwenda kwenye michezo ya Olympic itumie. Kampouni hizo ni Puma na Li-Ning ya China ambayo inakuja kwa kasi katika lebo ya vifaa vya michezo. Mvutano huu ni kati ya Chama cha Riadha Tanzania na Kamati ya Olimpiki Tanzania TOC.

WAKATI Chama cha Riadha Tanzania, AT kikisema hakitatumia vifaa vilivyotolewa na Kampuni ya kutengeneza vifaa vya michezo vya Puma kwa wanariadha wanaokwenda Beijing, China, Kamati ya Olimpiki Tanzania, TOC imesema washiriki wa michezo hiyo wanapaswa kutumia vifaa hivyo na si vinginevyo.
Kauli hiyo ya TOC inafuatia ile ya AT kuwa wanaridha wake watatumia vifaa vya Kampuni ya Li- ning ambayo ndiyo iliyoingia nayo mkataba wa kutumia vifaa vyake wakati wa michezo ya Olimpiki.

Kambi Miss Tanzania iyooo

Baadhi ya washiriki wa Vodacom Miss Tanzania 2008, katika picha ya pamoja kabla ya kuelekea Bagamoyo kuanza kambi ya maandalizi ya shindano hilo mapema Agosti. Wakati huo huo imefahamika kuwa mrembo wa Vodacom Miss Tanzania mwaka huu ataondoka na Sh8.8milioni ikiwa ni ongezeko la Sh800,000 ikilinganishwa na mwaka jana pamoja na gari ambalo hata hivyo thamani yake haijawekwa wazi. Akizungumza na waandishi wa habari meneja udhamini wa Vodacom, Emilian Rwejuna alisema mshindi wa pili atapata Shmilioni 6 wakati wa tatu ataondoka na Sh3.8milioni .

Mshindi wa nne, Sh2 .7 milioni na mshindi wa tano atajipatia Sh2.2milioni na washindi wa sita hadi wa 10 wataondoka na Sh1.3milioni kila mmoja.

Miss Temeke 2007 kwa Jicho la Michuzi

miss tmk 2008 angella luballa akiwa na (kati) akiwa na mshindi wa pili rona swai na wa tatu florence josephat
Miss Temeke 2008 akivishwa bibu na miss Temeke 2007

Miss Temeke 2008 angella luballa akiwa katika vazi la ufukweni

Tano bora Miss Temeke 2008 (Picha/Habari: Muhidini Michuzi)

Emperor Orlando na Saida Karoli katika na kitu Nsonyiwa

Muungano wa vipaji na kolabo za wanamuziki wa Uganda na Tanzania hauna mipaka, Hapa leo tunakuletea Emperor Orlando toka nchini Uganda akimshirikisha Saida Karoli kwenye wimbo Nsonyiwa. Sikiliza sauti kinanda ya Saida Karoli inavyo kwenda sambamba na sauti nzito ya Orlando, wimbo umeimbwa kwa lugha ya kiswahili na kunakshiwa na Kilugha, kwa kweli ni starehe na burudani tupu.

Afrika Kusini huenda Ikapokwa uandazi Kombe la Dunia 2010

Mbombela Stadium, Nelspruit, South Africa

Nchi ya Africa ya Kusini huenda ikanyang’anywa nafasi ya kuandaa mashindano ya Kombe la Dunia kwa kile kinachosemwa suala la usalama, akizungumza na idhaa ya kiswahili ya BBC Mjumbe wa kudumu wa CAF Said El Maamry alisema ni kweli minong’ono hiyo ipo na siku za karibuni imezidi, pia aliongeza Africa Kusini wamejiimarisha kwa maandalizi yote ikiwemo viwanja na mahoteli lakini tatizo ambalo watu wanaliona kwa sasa ni la kiusalama zaidi ambapo hivi karibuni kumeshuhudiwa watu wakiuana kwa ajili ya sababu za kimaisha jambo linalotishia usalama kwa wageni katika kipindi cha mashindano hayo. Lakini Elmaamry alionyesha wasiwasi wake juu ya jambo hilo na kusema kama watatumia hiyo ndio sababu basi mbona hata nchi ya Uingereza kila kukicha mnapigana visu? alihoji Elmaamry
Akijibu swali la mtangazaji Salum Kikeke juu ya Sitaki nataka ya FIFA kuhusu kufanyika kwa mashindano haya Afrika, Bw. El Maamry alisema kuwa Blatter ni kati ya watu ambao walitaka mashindano haya yafanyike Africa kwa nguvu zote na hii ni kutokana na ile Block Vote aliyoipata toka Afrika ikiwa ni jitihada zake za kuipigania Afrika na vile vile angependa kuweka historia kwa kuleta mashindano haya Afrika, na katika jitihada zake si tu kutaka yaje Africa bali kuja nchi ambayo ni ya Waafrica Weusi ukiziondoa nchi kama Tunisia, Morroco, Misri na nyingine ambazo zina waafrica Waarabu.
Elmaamry alisema kuwa ni kweli kulikuwa na bado kuna upinzani mkubwa toka kwa Executive members wa FIFA baadhi ambao hawakutaka mashindano haya yaje Afrika ya Kusini, sasa linapotokea hili la kiusalama wao wanapata sababu ya kukandamiazia na El Maamry alionyesha wasiwasi wake kuwa jambo hili linakuzwa zaidi na zile nchi ambazo zinataka kunyakua nafasi hii.
Baadhi ya viwanja vya Africa ya Kusini kwa ajili ya mtanange huo:-

Soccer City, Johannesburg, South Africa

King Senzangakhona Stadium, Durban, South Africa

King Senzangakhona Stadium usiku.

Port Elizabeth Stadium, Port Elizabeth, South Africa

Peter Mokaba Stadium, Polokwane, South Africa

Tuesday, July 8, 2008

Maboss wa Manchster na Liverpool

Newly elected ECA member of the board, CEO of FC Liverpool, Rick Parry, left, talks to Manchester United CEO, David Gill, right, after the first general assembly of the new European Club Association, ECA, at the UEFA Headquarters in Nyon, Switzerland, Monday, July 7, 2008. The European Club Association (ECA) is an new organization representing football clubs in Europe. Formed on the dissolution of the G-14 group in January 2008, it has 103 members, with at least one from each of the 53 national associations.

Newly elected ECA member of the board, CEO of FC Liverpool, Rick Parry, left, talks to Manchester United CEO, David Gill, right, after the first general assembly of the new European Club Association, ECA, at the UEFA Headquarters in Nyon, Switzerland, Monday, July 7, 2008. The European Club Association (ECA) is an new organization representing football clubs in Europe. Formed on the dissolution of the G-14 group in January 2008, it has 103 members, with at least one from each of the 53 national associations.

Ronaldo afanyiwa operesheni ya Ankle

Manchester United winger Cristiano Ronaldo, seen here in June 2008, has had "successful" surgery on his ankle in Amsterdam, the club confirmed in a statement on Monday.

Winga Tereza wa Manchester United Cristiano Ronaldo, akionekana kwenye picha hii ya June 2008, Habari zinasema Operesheni alofanyiwa Ronaldo huko Amsterdam Holland imefanikiwa na kwa sasa anauguza maumivu kabla ya kurudi uwanjani rasmi. Ronaldo anasubiri msimu uanze ajue takaa nje kwa muda gani, hii inamaanisha kuwa hatocheza mechi ya ufunguzi na New Castle. Mchezaji huyu ambaye bado akigombewa na Real Madrid na Manchester bado hajatoa maamuzi ya maisha yake yajayo kisoka kama atajiunga na Real Madrid au atabaki Man U, ingawa kitita cha Pound Milioni 135 kinaweza kumtamanisha na Sir Alex Furguson kumuachia.

Yanga yamshangilia Kaseja, Simba Yamzomea

Baada ya purukushani kuhusu usajili wake baina ya watani wa jadi Simba na Yanga na hatimaye Klabu ya Jangwani ya Yanga kufanikiwa kumchukua golikipa Juma Kasea Juma, jana klabu ya Yanga ilimtumia Kaseja pamoja na wachezaji wengine wapya iliyowachukua kwa msimu huu wa Ligi katika mchezo wake na Express ya Uganda.

Kaseja alikuwa na wakati mgumu wakati alipotoka kwenye vyumba vya kubadilishia kwa ajili ya mazoezi ya kupasha mwili.

Alipotoka tu mashabiki wa Yanga walimshangilia kwa nguvu na kuwabeza mashabiki wa Simba.

Mashabiki wa Simba, ambao pengine walikuwa hawaamini macho yao, mara walipomwona akiingia na wachezaji wenzake wa Yanga, walianza kumzomea na kumrushia matusi akiwa na wenzake, Mkenya George Owino na Nurdin Bakari, ambao pia walikuwa Simba msimu uliopita.

Kaseja, ambaye hata hivyo, hakupata purukushani kubwa katika mchezo wa jana, alikuwa na taabu , ambapo kila alipogusa mpira alikuwa akizomewa na mashabiki wa Simba wakati wale wa Yanga walikuwa wakimpa moyo.

Nurdin, ambaye alikuwa akicheza soka ya hali ya juu, naye alijikuta mara kwa mara akitukanwa na mashabiki wa timu yake ya zamani.

Pamoja na wachezaji hao waliokuwa na wakati mgumu, Yanga pia kwa nyakati tofauti iliwatumia wachezaji wake wapya, Godfrey Bonny, Kigi Makassy, Ally Shamte na Iddi Ally. Wachezaji wa zamani waliocheza walikuwa ni pamoja na Shadrack Nsajigwa, Athumani Iddi, Fred Mbuna, Ben Mwalala, Laurent Kabanda na Gaudence Mwaikimba.

AC Milan yakaza msuli kumnyakua Adebayo, Drogba

AC Milan technical director Brazilian Leonardo admitted Monday the Italian club were running the rule over Chelsea striker Didier Drogba and Arsenal's Emmanuel Adebayor, pictured in April 2008.
Mkurugenzi wa ufundi wa Klabu ya AC Milan Mbrazil Leonardo amesema kuwa Klabu yake ya Italy bado haijakata tamaa na iko kwenye mazungumzo ya maamuzi ya majaliwa ya wachezaji Didier Drogba wa Chelsea na Emmanuel Adebayor wa Arsenal, pictured in April 2008.

Lampard atabaki Chelsea: Scolari

New Chelsea Manager Luiz Felipe Scolari (L) attends a press conference at the Hilton Cobham hotel in Kent, south east England on July 8, 2008. Luiz Felipe Scolari revealed Tuesday that Frank Lampard has told him he wants to stay at Chelsea but the London club's new boss was unable to offer fans similar reassurance about the future of Didier Drogba. Inter Milan have made a formal approach for England midfielder Lampard, who has only a year left on his current contract and has reportedly been considering a move to link up with former Chelsea manager Jose Mourinho, who is now in charge of the Italian champions. AFP PHOTO/Leon Neal (Photo credit should read Leon Neal/AFP/Getty Images)
Mapaparazi kazini

New Chelsea Manager Luiz Felipe Scolari attends a press conference at the Hilton Cobham hotel in Kent, south east England on July 8, 2008. Luiz Felipe Scolari revealed Tuesday that Frank Lampard has told him he wants to stay at Chelsea but the London club's new boss was unable to offer fans similar reassurance about the future of Didier Drogba. Inter Milan have made a formal approach for England midfielder Lampard, who has only a year left on his current contract and has reportedly been considering a move to link up with former Chelsea manager Jose Mourinho, who is now in charge of the Italian champions. AFP PHOTO/Leon Neal (Photo credit should read Leon Neal/AFP/Getty Images)

Meneja mpya wa Chelsea Luiz Felipe Scolari akiwa kwenye mkutano na waandishi wa habari mara baada ya kutambulishwa rasmi kwao huko Hilton Cobham hotel ,Kent, Kusini Mashariki mwa England Leo July 8, 2008. Luiz Felipe Scolari pamoja na mambo mengine alisema kuwa Frank Lampard amemhakikishia kuwa atabaki Chelsea chini yake kama Meneja na Kocha mpya wa Club hiyo ya Darajani pia imesemekana kuwa ujio wa Felipe umehakikisha na majaliwa ya mchezaji Mkongwe Didier Drogba. Inter Milanbado wamekaza msuli wakimtaka Lampard kwa msimu ujao, kwani kwa sasa amebakiza msimu mmoja tu na Klabu ya Chelsea. Lampard amesemwa kuwa ni mshirika mkubwa wa Kocha wa zamani wa Chelsea Jose Mourinho, ambaye kwa sasa anaifunza klabu hiyo ya mabingwa wa Italy.

Bado naweza kuisaidia Lone Star: George Weah

Kepteni wa zamani wa Liberia na mchezaji bora wa FIFA kwa mwaka 2005 George Opong Weah amesema bado anajiona anajukumu la kufanya juu ya timu yake ya Taifa ya Liberia Lone Star.

Weah ambaye kwa sasa yuko USA kwa masomo amesema kwa sasa hawezi kuwa na nafasi ya kudumu kuifunza timu hiyo ya Lone Star.

Weah alikiambia kipindi cha BBC Fast Track kwamba kocha wa Liberia Antoine Hey hatumii ujuzi wake kwa ajili ya timu ya Liberia.

“Naweza kuwapa ushauri wa kiufundi, ninachoweza kwa sasa ni kufanya kazi na kocha pamoja na wachezaji, kuongea nao kuwafanya waone umuhimu wao kwa Taifa na kwa maisha yao pia, hicho ni kitu wanahitaji sana” alisema Weah.

“Nilimtaarifu [Hey] kuwa kuna wachezaji nimewavumbua vipaji vyao na wangemfaa kwa ajili ya kikosi cha Taifa, lakini alisema hapana anataka kutumia watu anaowajua yeye” alisema Weah kwa masikitiko.

Liberia ilicheza kombe la mataifa huru ya Africa mwaka 1996 na 2002, wakati huo Weah akiwa kepteni.

Prof Jay achana live Miss Vyuo vikuu

Wasanii wa muziki wa kizazi kipya, Hamisi Mwinjuma ‘Mwanafalsafa’ (kushoto), na Joseph Haule ‘Prof. J’ wakilishambulia jukwaa wakati wa shindano la kumtafuta mrembo wa Vyuo vikuu. Kwa picha zaidi mtembelee Michuzi na Anuani yake mpya http://michuzi-blog.com

Dunga awaitwa Ronaldinho na Robinho kikosi cha Olympic

SAO PAULO, Brazil (AP)—Ronaldinho na Robinho (Pichani) ndio watakao ongoza kikosi cha Brazil kwa ajili ya mashindano ya Olympic kuwania medali ya dhahabu kwa michezo ya mwaka huu.

Nyota huyo wa Barcelona, Robinho pamoja na kikosi kingine cha wachezaji wengine 16 pia wameitwa na kocha Dunga kukamilisha kikosi hicho zikiwa zimebakia siku 15 kabla ya kuanza kwa mazoezi kwa ajili ya mashindano hayo.

Olympic ndio mashindano pekee ambayo mabingwa hao wa Kombe la dunia kwa mara tano wameshindwa kutamba nayo. Tangia mashindano hayo yaanze Brazili imefanikiwa kuchukua medali ya Silver mara mbili mwaka 1984 huko Los Angeles na 1988 huko Seoul Korea. Brazil pia walishinda medali ya bronze mwaka 1996 huko Atlanta ambapo Nigeria walishinda Dhahabu.

Dunga pia amemchukua defender wa Fluminense Thiago Silva ambaye ana miaka zaidi ya 23 pamoja na Ronaldinho and Robinho ukilinganisha na kikosi hicho cha Olympic ambacho nia yake ni kuchukua dhahabu, Dunga alisema wachezaji wengi walichaguliwa wamezaliwa 1885, pamoja na udogo wao wengi wao wana uzoefu wa kimataifa.

Kati ya hao wenye uzoefu ni pamoja na Diego, Mchezaji wa Manchester United Anderson, Lucas wa Liverpool na Alexandre Pato wa AC Milan.

Kaseja, Bonny, Owino waing’arisha Yanga

Mwaikimba aizima Express Dar

TIMU ya Yanga jana iliifunga Express ya Uganda bao 1-0 katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa, uliofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, huku ikiwatumia wachezaji wake wengi wapya waliosajiliwa katika msimu huu.

Bao pekee la Yanga lilifungwa na Gaudence Mwaikimba aliyeingia kipindi cha pili akichukua nafasi ya Laurent Kabanda, dakika ya 69 kwa kichwa akiunganisha krosi ya Fred Mbuna ambaye alichukua nafasi ya Shadrack Nsajigwa.

Wachezaji wapya wa Yanga waliocheza jana na kuonesha kiwango cha kuridhisha ni kipa Juma Kaseja, Nurudin Bakari na George Owino waliotokea Simba, Kigi Makasi wa Mtibwa, Shamte Ally kutoka Kagera Sugar Godfrey Boniface wa Prisons na Idd Ali aliyepandishwa kutoka Yanga B.

Yanga ilianza mchezo huo kwa kushambulia lango la Express, huku mshambuliaji wake Bernard Mwalala akikosa nafasi nyingi za wazi hasa dakika za 19, 21 na 24, ambapo mashuti yake yalitoka nje na mengine kudakwa na Wahabu Geofrey.

Katika mchezo huo beki wa Yanga, Nadir Haroub ‘Canavaro’ ililazimika kukimbizwa hospitali kwa matibabu zaidi baada ya kuchezwa rafu mbaya na Lubwana Richard ambaye alitolea nje kwa kadi nyekunndu.

Dakika ya 40 Express waligoma kuendelea na mchezo kwa dakika tano, baada ya mchezaji wao kutolewa kwa kadi nyekundu wakidaia haikuwa rafu ya kutolewa nje, lakini viongozi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) waliingilia kati na kuendelea na mpira.

Yanga: Juma Kaseja, Shadrack Nsajigwa/ Fred Mbuna, Nurudin Bakari, George Owino, Nadir Haroub ‘Canavaro’/ Wisdom Ndhlovu, Godfrey Boniface, Sahamte Ali/ Vicent Barnabas, Athumani Idd, Ben Mwalala/ Idd Ali, Lurent Kabanda/ Gaudence Mwaikimba na Kigi Makassy/ Amir Maftar. (Na Erasto Stanslaus wa Majira)

Richard kutoka na Filamu ya kukemea Mauaji ya Maalbino

Kutokana na imani za kishirikina na mauaji ya Albino yaliyotanda katika jamii yetu yule Mshindi wa shindano la Big Brother Afrika kwa Mwaka jana Richard Bezuidenhout amewaomba wakazi wa mikoa athirika ya tatizo hilo kujitokeza kwa wingi katika kupinga Imani hiyo potofu na yupo njiani kuandaa filamu itakayokemea imani hizo mbaya.

Richard ambaye alikuwa Jijini Mwanza hivi karibuni katika kampeni zake za kupinga vitendo hivyo wanavyofanyiwa Maalbino hao aliyasema hayo akiwa na Mwenyekiti wa Chama cha Maalbino wa kanda hiyo Alfred Kapore

Alisema, kwa kuthamini maisha ya Watanzania na majukumu yake kwa jamii, ameona analo jukumu la kuwaelimisha wananchi kwa kupitia filamu ili waondokane na imani za kishirikina na hivyo wasijihusishe na vitendo vya kuwaua albino ambao wanastahili kuishi katika jamii kama walivyo wengine. (Na Dar 411)

Wanazi wa mbio za magari

Niko na wanazi wa Mbio za Magari hii baada ya kuzifata Tanga ingawa mtu wetu hakushinda lakini si haba, asubuhi watu wakaamkia Mombasa maisha yakaendelea. Toka shoto Six, Tameem, Cathy, Mimi na Berty.

Temeke yahitimisha kwa Angela kunyakua taji

Usiku wa kuamkia leo Temeke imefunga pazia la Mkoa wa Dar es Salaam kutafuta wawakilishi wake katika kinyang’anyiro cha Miss Tanzania 2008 kwa kumuibua mtoto anayejiamini kuwa,siyo tu Miss Temeke,bali Miss Tanzania na hata Miss World 2008.si mwingine ila ni Miss Angela Lubala,akiwa na wenzake waliomfuata,Florence Josephat na Lona Swai. (Na Haki Ngowi/Abdallah Mrisho Salawi)

Monday, July 7, 2008

Torres: Benitez ndiye mchawi wangu!!

Spain's Fernando Torres poses with the Euro 2008 trophy in Madrid in late June. Torres has said that Liverpool coach Rafael Benitez was the inspiration behind his goal-scoring exploits which helped Spain to Euro 2008 glory.
Spain’s Fernando Torres akiwa na kikombe cha Euro 2008 huko Madrid wiki iliyopita, Torres amesema kocha wake wa Liverpool Rafael Benitez ndiye chachu ya mafanikio yake katika ufungaji wake wa magoli na hata goli lililoipa ushindi nchi yake ya Spain kwenye mchezo wa Fainai, mbali na hiyo Torres amesema hana wazo wala mpango wa kukihama klachu yake ya Liverpool kwa sasa. AFP.

Raha inapogeuka karaha michezoni

Tunisian football club Etoile du Sahel fans demonstrate during the Tunisia Cup final football match Etoile du Sahel vs Esperance de Tunis at Rades Stadium in Tunis, on July 5, 2008. Esperance won 2-1. AFP PHOTO FETHI BELAID (Photo credit should read FETHI BELAID/AFP/Getty Images)
Mashabiki wa mpira wa timu ya Etoile du Sahel ya Tunisia wakifanya fujo baada ya mchezo wa fainali ya ligi ya Tuniasia kati ya Etoile du Sahel vs Esperance de Tunis huko Rades Stadium Tunis, July 5, 2008. Esperance walishinda 2-1. AFP

“Operesheni Vikombe” ya Chelsea yamtaka KAKA

Chelsea have put a big-money offer on the table for Brazilian playmaker Kaka,, seen here in March 2008, AC Milan vice-president Adriano Galliani said, without giving further details of the proposed deal.
Chelsea wameweka kitita kikubwa cha pesa kwa ajili ya kumnunua Mbrazili Kaka pichani, Makamu wa Rais wa AC Milan Adriano Galliani alisema jana bila kusema kiundani ila alisema ofa hiyo inajadiliwa na uongozi, hizi zitakuwa ni jitihada za kuimarisha kikosi chake ambacho kinaanza msimu chini ya kocha Phillip Scholari ambaye amepewa jukumu la Operesheni Vikombe. Chelsea watakuwa ziarani nchini Malaysia mwezi huu ambapo watacheza mchezo mmoja kwenye uwanja wa Shah Alam tarehe 29 July.

Wanachama wamcharukia Rais Barcelona FC

FC Barcelona's President Joan Laporta is about to give a news conference after the final result of a no confidence vote at the new Camp stadium in Barcelona on July 06, 2008. Joan Laporta survived a confidence vote held Sunday that was brought against him by a supporter who was angered by the Spanish club's second straight season without any major title, according to an exit poll. AFP PHOTO/JOSEP LAGO (Photo credit should read JOSEP LAGO/AFP/Getty Images)
Rais wa FC Barcelona Joan Laporta akiongea na mapapa na mamarazi mara baada ya matokeo ya mwisho ya upigaji wa kura ya kutokuwa na imani naye (vote of no confidence) tukio lililofanyika huko New Camp stadium, Barcelona jana July 06, 2008. Joan Laporta aliponea ncha ya sindano baada ya raundi ya mwisho ya upigaji kura . Hii ni baada ya wanachama wa Klabu ya FC Barcelona kulalamika matokeo mabaya ya Klabu yao kwa kwenda mwaka wa pili bila kikombe chochote wala mafanikio mazuri. Je tunajifunza nini hapa kwa vilabu vyetu vya Tanzania? (Na AFP)

Akina mama wa Afrika Kusini na Soka

Women play a game of soccer in the Nkowankowa Township July 6, 2008 in Limpopo, South Africa. The grannies play twice a week to keep fit and show their support for the 2010 Soccer World Cup being held in South Africa. (Photo by Lefty Shivambu/Gallo Images/Getty Images)

LIMPOPO, SOUTH AFRICA – JULY 6: Wakinamama wa wakicheza soka huko kwenye mji wa Nkowankowa nchini Africa ya Kusini jana. Akina mama hawa hucheza mara mbili kwa wiki kujiweka fit na pia kuonyesha support yao kwa nchi yao kuandaa mtanange wa Kombe la Dunia 2010. Akina mama wa Tanzania mpoo? (Na Get Image).

Je Kitaeleweka leo?

Cristiano Ronaldo
Lile sakata la mchezaji Cristiano Ronaldo kuhamia Real Madrid litafikia kikomo leo ambapo maboss wa Manchester na wa Real Madrid watakutana uso kwa uso kumaliza kitendawili hiki, tungoje tuone atabaki Mn U au ndio safari Real Madrid ten? Wacgunguzi wa mambo ya ki spoti wanasema Ronaldo ndio kwaheri Man U.

Saturday, July 5, 2008

Fay Antony ashinda Miss Kinondoni 2008

Pichani Kati ni mshindi wa kwanza aliyelinyakua taji la miss Kinondoni 2008, Fay Antony yaliyofanyika jana usiku katika ukumbi wa Msasani Club,kushoto ni mshindi wa pili Joonfaith John na kulia ni mshindi wa tatu Amata Chryspin,aidha katika walimbwende hao kila mmoja aliibuka na kitita cha laki nane taslim

Pichani ni Miss Tanzania 2007 Richa Adhia akimvisha taji miss kinondoni 2008 Fay Antony usiku wa jana baada ya kulinyakua taji hilo. Giraffe Ocean View Hotel walidhamini wa shindano hili. (Picha/Habari Michuzi Jr)

Venus amshinda dadake kwenye fainali

Venus was all smiles.
Venus Williams amepata ushindi wake wa Tano wa wimbledon jana jumamosi ikiwa ni ushindi baada ya kumshinda dada yake Serena 7-5, 6-4 katika sets mbili ngumu, Baada ya dada hawa waili kufanikiwa kufika Fainali, baba yao mzazi ambaye ndio Kocha na Meneja wao aliamua kurudi nyumbani kwa kile alichosema hakupenda kushuhudia fainali hizo kwani wanaocheza wote ni wanaye hivyo kuwaacha Mama yao mzazi na mdogo wao wa kike ambao walikuwepo uwanjani wakati Venus akimuangusha Serena.
(Picha na Yahoo Sport)

US Venus Williams is applauded after beating her sister Serena during their final tennis match of the 2008 Wimbledon championships at The All England Tennis Club in southwest London, on July 5, 2008. Venus Williams won 7-5, 6-4.    AFP PHOTO / Adrian Dennis (Photo credit should read ADRIAN DENNIS/AFP/Getty Images)

Hughes: Nipeni Ronaldinho nimrudishe kwenye nafasi yake

Barcelona warned Friday that it would not sell its Brazilian striker Ronaldinho, who has been deemed surplus by the Spanish side's new coach Pep Guardiola, at a discount.
Boss wa Manchester City Mark Hughes amesema anaamini kuwa kama Ronaldinho atakubali kuhamia timu yake basi atamrudisha kwenye kiwango chake cha uchezaji na upachikaji magoli. Hughes aliponda wazo la Mbrazil huyu kwenda Chelsea na kusema huko hatoweza kwani Ronaldinho anataka timu ambayo itajali na kutambua uwepo wake na kumpa Special attention ambayo si rahisi kuipata akiwa Chelsea.

Man City ambayo imetoka kumsajili Mbrazil Jo kwa kitita cha Pound 19 milion akitokea CSKA Moscow imeonyesha nia ya kumtaka Ronaldinho.”watu wanahoji uwezo na nafasi ya Ronaldinho kwa sasa, mi namuona bado ananafasi kubwa ya kung’aa na anaweza kuvutiwa na program yetu ya mazoezi na kutengenezea ya kwake rasmi kuliko atakapo kwenda kwenye klabu kubwa ambapo wao watataka afanye kutokana na ukubwa wa jina lake” alisema Hughes.
Kwa sasa Ronaldinho yuko ziara ya Asia akitangaza bidhaa za Nike.
Man City wako tayari utoa Pound Milion 10 kama ada ya uhamisho kwa Barcelona ambayo itakuwa ni kwa mkataba wa miaka mitatu ambayo inathamani ya zaidi ya Pound 100,000 kwa wiki.

uwepo wakeBarcelona warned Friday that it would not sell its Brazilian striker Ronaldinho, who has been deemed surplus by the Spanish side’s new coach Pep Guardiola, at a discount.

Kura yako lwa Amanda tafadhali

Wakati shindano la kumtafuta Miss Universe 2008 liko kwenye mchakato mbali mbali shime watanzania tunapewa changamoto ya kumpigia kura Mrembo wetu Amanda, Shindano hilo litafanyika July 13 Jijini Nha Trang Vietnam nje kidogo ya mji wa Hanoi. Amanda Ole Sululu mnyange wa Kimasai ndio muwakilishi wetu kwenye mtanange huo. Pichani anaonekana Amanda akiwa ndani ya Vazi la Taifa, Hili ndilo Vazi ambalo mnaombwa kumpigia Kura ili ashinde kipengele hiki ambapo mchakato mzima wa kupiga kura unaanza Jumatatu tarehe 7, Kwa kupiga kura Bofra hapa kubonyeza hapa. Kumbuka kura nyingi ndio zinaweza kumpa nafasi Amanda. Kwa mapicha zaidi Gonga hapa

(Na Maria Sarungi)

Friday, July 4, 2008

Bushoke awarudishia Kili Music award tuzo yao


Msanii Ruta Bushoke ametangaza kuirudisha tuzo ya muziki ya Kilimanjaro aliyotunukiwa mwishoni mwa wiki. Bushoke alishinda tuzo ya wimbo bora wa ‘zouk’, kwenye tamasha lililofanyika kwenye Hoteli ya Kempinsky jijini Dar es Salaam.


Bushoke alitwaa tuzo hiyo kupitia wimbo wa ‘Mbali Nami’ lakini amesema wimbo huo si wa kwake na unaitwa ‘Usiende.’

Akizungumza na gazeti la Mwanaspoti Bushoke alisema ameamua kurejesha tuzo hiyo kwa kuwa wimbo pamoja kwamba ameutunga yeye, lakini ni mali ya Juliana Kanyomozi wa Uganda.

“Mimi sielewi hawa mabwana wanafanya kazi vipi, kama ni nyimbo zangu zipo nyingi tu lakini kwa wimbo huo walipaswa kuwasiliana na mimi hata kunieleza nimeteuliwa badala ya kukurupuka na kunipa tuzo ambayo si yangu,” alilalamika.

“Ingekuwa tuzo ya uandishi wa wimbo ingekuwa yangu, lakini tuzo ya wimbo inatakiwa kwenda kwa Juliana kwa Juliana. Kwenye redio nyingi sana wimbo huo upo kwenye ‘tip 10’ na unatangazwa kuwa ni wa Juliana Kanyomozi akiwa ameshirikiana na Bushoke sasa wenyewe lipi hapo ambalo hawakujua,” alihoji msanii huyo. (Spoti & Starehe iliwahi kuandika kuhusu wimbo huo)

Meneja wa Bushoke, Athuman Tippo naye alisema wamechukua uamuzi huo wakiamini ni wa busara kwa kuwa isingekuwa vema Bushoke kujivunia kitu ambacho si chake.

“Bushoke ni kati ya wasanii bora na ana uwezo wa kufanya vitu vikubwa hivyo si vema akachukua tuzo ya mtu hata kama amepewa. Ipo siku atafanya hivyo kwa uwezo wake mwenyewe sababu anao,” alisema.

Bushoke, ambaye ni mtoto wa mkongwe katika miondoko ya dansi Maximilian Bushoke sasa anatamba na wimbo wa ‘Dunia Mapito’ ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya albamu yake mpya. Msimamo huo wa Bushoke umezidi kuonyesha namna utoaji wa tuzo za Kilimanjaro unavyoyumba na kusababisha lawama kwa wasanii mbalimbali. Waandaaji wa Kili Music Award wamezidi kulalamikiwa kutokana na mchakato mzima wa kuwapata washiriki na ugawaji wa Tuzo, Hivi majuzi muaandaaji wa muziki Bw. Said Comorein naye alilalamika kuwa yeye ndiye aliyetengeneza nyimbo nyingi zaidi ya nusiu zilizoshinda lakini yeye kama Prodyuza hakuambulia kitu
Gonga Player usikie wimbo wenyewe:

MAsikini Ngwea

Ngwea awekwa ‘bondi’ Mwanamuziuki wa kizazi kipya Albert Mangwea AKA Ngwea hivi karibuni aliripotiwa na vyombo mbali mbali vya habari kuhusu hali yake hasa ya kimaisha na kimuziki kuwa ni mbaya.
Hivi karibuni Mangwea ameripotiwa kuwa anaishi nyumba ya kulala wageni (Guest House) na alisababisha kufungiwa na wenye Guest hiyo (Jina Kapuni) baada ya kushindwa kulipa pango (Bofya hapa). Kwa wanaomjua Ngwea wanasema bwana huyu kimziki alikuja wakati mzuri ambapo Bongo Flava imeshakubalika na wanamuziki walikuwa wakilipwa vizuri na kipindo hicho alishaingiza Albamu sokoni na kupata mshiko wa haja, Pia Ngwea ambaye alishiriki kwenye matamasha kadha wa kadha ikiwa ni pamoja na yanayodhaminiwa na makampuni makubwa kama TBL, Coca Cola, Celtel, Tigo na mengineyo ambayo hutoa mshiko mzuri kwa wanamuziki.
Wadau mbali mbali waliozungumza na dawati hili wanasema kimsingi hawaoni sababu ya Mwanamuziki huyu kuishi maisha hayo anayoishi kwa sasa kwani hata wanamuziki wenzie wanamkimbia kwani akikuona lazima akupige mzinga.
Mtangazaji wa kipindi cha Planet Bongo Salama Jabri aliwahi kuliongelea suala la wanamuziki kujisahau kwa kina na mapana na hata juzi kwenye mahojiano ya SS na mwanamuziki mkongwe wa Bongo Flava Solo Thang aliongelea kitu hicho (Bofya hapa uone).
Wanamuziki wengi wa ujio wa Ngwea wametoka kimaisha ingawa wengine sio sana lakini wanacho cha kuonyesha kidole, Sio nia ya safu hii kusema kuwa lazima Ngwea afike mahala fulani kimaisha la hasha ila kimsingi hakupaswa kuwa hapo alipo na bado ana nafasi ya kufanya mambo makubwa kwani ni mwanamuziki mzuri na anakubalika, “Ups and downs” ni sehemu ya maisha.
Ngwea ambaye awali alifahamika kama mkali wa Free Style alijizolea sifa nyingi na mashabiki wengi hasa kwa vibao vyake na wengi walipenda kumshirikisha katika nyimbo zao kwani kwa mujibu wa wanamuziki wenyewe wanasema Ngwea aukimpa maudhui ya nyimbo hata mkiwa Studio basi ndani ya dakika chache anaweza kukupa Mistari ya kutosha na mkaingiza sauti kwenye beat na mambo yakawa mswano na usipoangalia hata akakufunika wewe mwenye nyimbo. Nwea ameshirikiswa na wanamuziki kibao kama Jay Moe, Sarah Kaisi, John Mtembezi, Mchizi Mox, Feruz, Rah Pee, Daz Mwalimu, na wengineo wengi.
Pata Burudani toka kwake kibao Kimya Kimya toka kwa Jay More akimshirikisha Ngwea
(Picha na GPL)

Wazee wa Ngwasuma kazini

Wanamuziki wa bendi ya FM Academia a.k.a Waze wa ngwasuma, wakitumbiza wakati wa utoaji wa tuzo za muziki za Kili 2007 katika ukumbi wa hoteli ya Kempinski,jini Dar hivi karibuni.

(Picha na MichuziJr)

Thursday, July 3, 2008

Mfungwa Schapelle Corby aruhusiwa kwenda Salon/Shopping

Face mask … Schapelle Corby tries to hide her face from photographers after spending three hours yesterday in a beauty salon in Denpasar, Bali.

Mshtakiwa Mrembo Schapelle Corby akijaribu kufunika uso mbele ya wapiga picha jana alipokuwa akitoka Gardenia Salon kutengeneza nywele salon huko Denpasar, Bali.
Picha: AFP

Schapelle Corby ambaye anatumikia kifungo cha miaka 20 jela kwa kukuttwa na madawa ya kulevywa jana aliruhusiwa kwenda Saloon na kutengeneza nywele huko kwa muda wa masaa matatu na ushehe huko katika kisiwa cha Bali anakotumikia kifungo chake.

Corby anatumikia kifungo hicho tangu mwaka 2005 alipokamatwa na maofisa wa Polisi wa Indonesia huko Bali na kuhukumiwa kifungo hicho, kwa sasa ana miaka 30. Corby alipatikana na kilo 4.5 za Bangi siku alipokamatwa huko Indonesia mwaka 2005 ambapo aliziingiza akitokea Australia.

Ikumbukwe Indonesia ni nchi yenye waislamu wengi zaidi duniani na katika kisiwa cha Bali ni maarufu kwa watalii wa kila aina na huko kuna beach na mahoteli mazuri ya kitalii na ndio maana kuna matukio mengi ya Ugaidi katika kisiwa cha Bali ambayo yanaaminika kutoka kwenye vikundi vya Waislamu wenye siasa kali ambao wanapinga utamaduni wa magharibi unaingizwa huko na watalii na wenyeji wa maeneo hayo.

Corby ambaye kesi yake toka kukamatwa kwake imekuwa ni gumzo kipande hiki cha Mashariki ya Mbali ya Asia ameonekana mchangamfu na mwenye afya njema alikubaliwa kununua nguo kwenye shopping mall na pia alinunua viburudisho kama Ice Cream na kushiriki na ndugu zake.

Huku akisindikizwa na Polisi wawili wenye silaha za moto na Pingu hawakuruhusu mtu yeyote kumsogelea Corby ambaye siku za karibuni magazeti yaliandika alikuwa na mpango wa kujiua.

Kwa sheria za nchi nyingi za Asia ukikutwa na madawa ya kulevya na ikathibitishwa ni yako basi unanyongwatena kwa nchi kama Malaysia ninayoishi mimi au Singapore niliyopata kuishi kabla sijahamia Malaysia, Kukutwa na madawa ya kulevya yapaswa huku yako iwe imekamilishwa ndani ya masaa 48.

Corby alikuwa nchini Indonesia akijishughulisha na urembo ambapo alijipatia umaarufu sana kwa Indonesia, Malaysia, Singapore, Thailand na hata Hong Kong na Uchina.

Pichani ni Corby akiwa ameshikiliwa na wanausalama akirudishwa Jela baada ya rufani yake kutupiliwa mbali, hapa alionekana mdhoofu sana.

Mwezi uliopita Corby alilazwa kwa kuwa na Msongo wa Mawazo (depression) alilalamika kuwa angependa kwenda kutumikia hukumu hiyo ambayo kama atamaliza atatoka akiwa na miaka 50, Nchini kwake Australia makundi mbali mbali yanajitahidi kufanya kampeni za kutaka serikali imhurumie na kumfutia adhabu Corby kama sio kumpunguzia muda wa kuitumikia adhabu hiyo.

Judges Hand Down Schapelle Corby Verdict

Mkalimani Eka Sulistiowati (shoto) akimshika Corby baada ya Jaji kusoma hukumu ya miaka 20 dhidi yake mwaka 2005

MISSTemeke 2008 wametangaziwa zawadi

Na Msimbe Lukwangule
MISSTemeke 2008 wametangaziwa zawadi zao na waandaaji wa Shindano hilo litakalofanyika jumapili ijayo TCC Chang’ombe Dar es Salaam
Akizungumza na waandishi wa Habari leo Mratibu wa Onyesho hilo Benny Kisaka alisema wanasababu kuu mbili za kutoa zawadi za kulingana, kwanza warembo watakuwa na siku mbili za kujiandaa na fainali za taifa ambapo watatakiwa kuingia kambini julai 9, hivyo kiwango cha pesa kutawawezesha kufanya maandalizi kuliko kuwapa vitu.
“Warembo watatu wa kwanza katika fainali hiyo watapata Sh 800,000 kila mmoja sanjari na kujipatia tiketi ya kuiwakilisha wilaya ya Temeke katika fainali za Vodacom Miss Tanzania 2008” alisema Kisaka

Aidha, alisema washindi wa wanne na watano kila mmoja atapata Sh 300,000 na waliobaki watapata kifutajasho cha Sh 100,000 kila mmoja.
Kiingilio cha Shindano hilo ni Sh. 50,000 kwa viti maalumu itakayoenda sambamba na chakula kamili cha jioni na Sh. 10,000 kwa viti vya kawaida.
Pia litaenda sambamba na burudani kutoka kwa Bushoke na Bendi ya B band ikongozwa na Banana Zoro na baba yake Zahir Zorro.

Warembo watakaochuana katika shindano hilo kutoka kitongoji cha Kigamboni ni Rona Swai, Florence Josephat, Kitongoji cha Kurasini ni Caroline Sechuma, Evanuru Isaac na Glory Charles.
Soma Zaidi Kwa Msimbe Lukwangule

FIFA nayo yamchinja Rage

Ismail Aden Rage

*Mwenyewe hatambui, adai TFF imemfitini
*Ahoji iweje ‘kuoga aoge yeye, itakate TFF’

Na Sophia AShery wa Majira

SHIRIKISHO la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA), limemtolea nje aliyekuwa Makamu wa Pili wa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania Ismail Aden Rage kurudi katika nafasi yake na kumtaka kusubiri Uchaguzi MKuu kama anahitaji kuwa kiongozi wa TFF.

Hatua hiyo imetokana na majibu ya barua aliyoandika Rage kwenda FIFA akipinga uamuzi wa kutorudishwa katika nafasi yake uliotolewa na Kamati ya Nidhamu ya TFF iliyokutana Aprili 26 mwaka huu.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Katibu MKuu wa TFF, Fredrick Mwakalebela alisema TFF ilipokea barua kutoka FIFA iliyoandikwa Juni 24 mwaka huu na kusainiwa na Katibu Mkuu Jerome Valcke.

Mwakalebela alisema katika barua hiyo FIFA imesema uamuzi uliotolewa na Mkutano MKuu wa TFF kumuondoa Rage katika nafasi hiyo ni sahihi kwa kuwa katiba ya TFF inafanya kazi, hivyo uamuzi huo umezingatia katiba. Kwa Habari Zaidi Bofya Hapa

Samaki mkunje angali mbichi

Brazilian soccer star Ronaldinho, top center, poses with South Korean middle school soccer players during his Asia Tour in Seoul, South Korea, Wednesday, July 2, 2008.
Ronaldinho akiwa kwenye picha ya pamoja baada ya kutoa mafunzo kwa vitendo kwa watoto wa Shule maalum ya michezo, Wenzetu wanaanzia mbali

Brazilian soccer star Ronaldinho, center, jumps as South Korean middle school soccer players look on at a lesson during his Asia Tour in Seoul, South Korea, Wednesday, July 2, 2008.

Nyota wa Brazil Ronaldinho, katikati akiruka juu pamoja na watoto wa Shule maalum inayofunza soka huko Korea Kusini, Ronaldinho alitembelea shule hiyo kutoa mafunzo ya vitendo ikiwa ni sehemu ya ziara yake itakayo mtembeza nchi mbali mbali za Asia akitangaza bidhaa mpya za Nike ikiwepo kiatu kipya cha michezo. July 2, 2008. Shule hii ni jitihada binafsi za Korea Kusini ambayo imedhamiria mwaka 2014 kuingiza kikosi kabambe kwenye kombe la Dunia na wanategemea vijana hawa mwaka 2014 watakuwa na umri wa miaka 18 hadi 20, kwa mujibu wa wavuti wao huo ndio utakuwa mwanzo mwisho na kulibakiza Kombe kwao.

– Sie tunang’ang’ana na wazee!! –

Ni usajili kwa kwenda mbele…

Barcelona's new signing Daniel Alves of Brazil, center, Barcelona club president Joan Laporta, right, and Barcelona´s coach Pep Guardiola, right, are seem, during his official presentation as new player for FC Barcelona in Barcelona, Spain, Tuesday, July 2, 2008.
Mchezaji mpya wa timu ya Barcelona Daniel Alves toka Brazil, kati, Rais wa Klabu ya Barcelona Joan Laporta, kulia, na Kocha wa Barcelona Pep Guardiola, wakiwa katika picha ya pamoja walipokamilisha usajili wa Mbrazili huyo hapo jana.

Karibuni Nyumbani vijana wangu…

Russian President Dmitry Medevedev speaks during his meeting with the Russian national soccer team at Meindorf residence outside Moscow, Wednesday, July 2, 2008. Russia was defeated by Spain in their Euro 2008 semi-final soccer match.
Rais wa Russia Dmitry Medevedev akiongea wakati alipokutana na timu ya Taifa ya Russia katika makazi yake huko Meindorf nje kidogo ya jiji la Moscow, Jana July 2, 2008. Russia walipoteza mchezo wa nusu fainali dhidi ya Waispaniola.

Jo ajiunga na Man City

Manchester City signing Brazilian striker Jo poses at The City of Manchester Stadium. Jo joined Manchester City from CSKA Moscow on Wednesday for what the English Premier League side said was a "club record" undisclosed fee.
Manchester City wamemsajili Striker Mbrazil Jo, Hapa anaonekana akiwa kwenye Uwanja wa The City of Manchester Stadium. Jo amejiunga Manchester City akitokea CSKA Moscow kwa gharama ambayo Manchester City wamegoma kuiweka bayana. (Na AP)

Wednesday, July 2, 2008

Mambo ya Bongotyube.com

Mdau Issa Michuzi anawaambia hivi:-


KAMA JINA HILO LINAVYOELEZA LIBENEKE HILI NI ZAO LA GLOBU HII YA JAMII NA AMBALO LENGO LAKE LIKIWA KUWAUNGANISHA WADAU DUNIANI KOTE KWA NJIA YA VIDEO. HAPO UTAKUWA NA FURSA YA KUONA NA KUSIKIA MAMBO MBALIMBALI NA PIA KUTOA MAONI YAKO KAMA KAWA. NAKARIBISHA MAONI AMA MAWAZO ENDELEVU KATIKA KUFANIKISHA LIBENEKE HILIKATIKA http://www.bongotyube.com MDAU UNAKARIBISHWA KUJISAJILI NA KISHA KUTUMA VIDEO ZA MATUKIO NA MAMBO MBALIMBALI AMBAYO UNADHANI YATAFAA KUONEKANA NA KUSIKILIZWA NA JAMII YETU, HUSUSAN INAYOTUMIA LUGHA YA KISWAHILI POPOTE PALE ULIMWENGUNI.MCHANGIAJI MKUU KATIKA HILI NI WEWE MDAU, NA SIO MIMI PEKE YANGU.
HIVYO JISIKIE HURU KUTUNGIKA VIDEO ZAKO KWA KUFUATA MAELEKEZO NA MIIKO, IKIWA NI PAMOJA NA KUHAKIKISHA KWAMBA UNACHOTUMA HAKITOCHAFUA HALI YA HEWA NA PIA HAKINA UTATA WA HAKIMILIKI. SOMA VIGEZO KWA MAKINI KABLA YA KUANZISHA LIBENEKE.
VIDEO ZILIZOMO KATIKA http://www.bongotyube.com/ NI ZILE AMBAZO ZILITUMIKA KWA UTAFITI NA MAJARIBIO KWA MUDA WA KARIBU MWAKA MMOJA ILI KUHAKIKISHA LIBENEKE HILI HALIDODI. HIVYO ZISIKUTISHE ILA WEWE MWAGA TU VITU VYAKO ILI NASI WADAU TUFAIDI UHONDO…
Habari na Issa Michuzi

Tuesday, July 1, 2008

Kaijage wajibu Wazalendo hawa…

Kufuatia sakata la kudaiwa Jezi kwa mchezaji wa Taifa Stars baada ya kubadilishana na mchezaji wa Cameroon Samuel E’too, Timu ya Tanzanite fc Ya Atlanta Ga inayoundwa na wazalendo imetoa salamu kwa TFF

“Habari yako,

pole na shughuli nzito ya kuwakilisha jamii.Sisi Vijana wa Tanzanite fc Ya Atlanta Ga tunasikitika na habari tuliyosoma juu ya mchezaji wetu aliyewakilisha timu yetu ya taifa huko Cameroon kwa kuadhibiwa kwa kulipia jezi ya timu ya taifa aliyobadilishana na mchezaji mwenzie wa Cameroon(Etoo) tumeona kwamba ni swala la aibu kwa chama cha soka cha Tanzania kumdai mchezeji huyo hasa ukizingitia mchango wake kwa Taifa.
Sisi Tanzanite fc tungependa kujitolea kulipa deni hilo la huyo mchezaji. Je ni utaratibu gani tuutumie kuwakilisha mchango huo, na je ni kiasi gani?Tunatanguliza shukrani zetu kwa msaada wako kutufanikishia swala hili.
Wako
Tanzanite fcAtlanta,GA.
USA”

HAYA KAKA KAIJAGE

Majaji wanakazi bwana…

Aaaa majaji wana kazi sana wakati mwingine, Hii ilitokea kwenye kumtafuta Idol ya West Africa

Tenga: Jezi mali ya mchezaji Taifa Stars

Raisi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Leodgar Chilla Tenga(pichani).

*Ampa tano Cannavaro kumvulia jezi Eto’o.

Na Erasto Stanslaus wa Majira

RAIS wa Shiriksho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Leodegar Tenga amempongeza beki wa timu ya Taifa ‘Taifa Stars’, Nadir Haroub ‘Canavaro’ kubadilishana jezi na mchezaji wa kimataifa wa Kameruni, Samuel Eto’o katika mchezo wa marudiano wa kuwania kufuzu fainali za Kombe la Dunia na Mataifa ya Afrika 2010 uliofanyika mjini Younde, Kameruni.

Baada ya mchezo huo kumalizika ‘Cannavaro’ alifuatwa na Eto’o anayecheza klabu ya Barcelona ya Hispania akitaka wabadilishane jezi baada ya pambano hilo kumalizika ambapo Stars ilichapwa mabao 2-1 yaliyofungwa na mchezaji huyo.

Tukio hilo limeibua mjadala baada ya Ofisa Habari wa TFF, Florian Kaijage akikaririwa na vyombo vya habari akisema ‘Cannavaro’ atakatwa sh. 20,000 kwa kitendo cha kubadilishana jezi na Eto’o.

Mchezaji mwingine iliyeingia katika mzozo huo ni Jerry Tegete ambaye alibadilishana jezi na mchezaji Jean Makoun wa Kameruni anayevaa 11. Tegete alivaa jezi nambari 10 katika mchezo huo.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Tenga alikata mzizi wa fitina na kutoa ufafanuzi wa kina kuhusiana na sakata hilo na alimpongeza beki huyo akisema amefanya kitendo cha kishujaa kutoa jezi ya Taifa bila kujali kama atadaiwa au la.

“Canavaro amefanya kitendo cha kishujaa kwani sasa tunakwenda na wakati kwani angekataa kutoa jezi kwa kuhofia kudaiwa ulimwengu usingetuelewa na kutoa jezi ni kuitangaza nchi,” alisema Tenga.

Nahodha huyo wa zamani wa timu ya Taifa, alisema kuanzia sasa TFF imepitisha uamuzi kila mchezaji wa Stars ataondoka na jezi aliyovaa siku ya mchezo bila kujali alicheza uwanjani au la baada ya pambano kumalizika na itakuwa mali yake.

Tenga alisema kimsingi waliokuwa wakimdai ‘Cannavaro’ jezi hiyo walikuwa wakitimiza wajibu waliojipangia kati ya uongozi wa Stars na wachezaji lakini alionya kuwa walishindwa kuangalia mazingira halisi ya tukio husika.

Baadhi ya wadau wa mpira wa miguu wameuponda uongozi wa TFF kutokana na kitendo hicho hicho na walikuwa tayari kuwalipia gharama za jezi hizo ‘Cannavaro’ na Tegete

S.S – Inampongeza Bwana Tenga kwa kutoa ufafanuzi huo.
Tunaomba na vingine vyenye utata mjitokeze mapema kutoa ufafanuzi kabla mambo hayajaaharibika au kuwafanya mashabiki na wapenzi kuwa na fikra mbadala.
Spoti na Starehe

Lucy Fundikira ndiye Miss Tanzania EU.

Picha/Habari na Nashe Mvungi wa Ujerumani.Mgeni rasmi Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani Mheshimiwa Ngemera akimvisha Taji la ushindi, Bi Lucy Fundikira baada ya kutangazwa mshindi wa Miss Tanzania EU, Lucy atashiriki kwenye Miss Tanzania huko Dar Es Salaam.


Miss Tanzania EU 2008 – LUCY MWIZA FUNDIKIRA (holland), 1st Runner up – SABRINA BASHIR (Germany), 2nd Runner up – JACQUILINE SABANYA (Germany)


Washiriki wakitupa karata ya mwisho mbele ya mashabiki na majaji.

Mkurugenzi wa Ethiopian Airlines kanda ya Ujerumani na Central Europe Mr. Esayas Hailu Akimkabidhi mshindi tiketi ya ndege ya kwenda na Kurudi Dar Es Salaam.


Miss Tanzania EU 2008 – LUCY MWIZA FUNDIKIRA akipita mbele ya washabiki baada ya kutangazwa mshindi jana usiku.

Mwanamuziki Ali Kiba akipagawisha mashabiki wakati wa shindano la Miss Tanzania EU.
Godlove Muliahela mwenye kofia ndiye aliye aliye imba wimbo wa Taifa wakati wa mashindano hayo akiwa na washindi wa pili na watatu na wadau.

Lucy akionyesha Ticket aliyopewa na wadhamini wa shindano hilo ambayo itamuwezesha kwenda Tanzania na kurudi kushiriki kwenye shindano la Miss Tanzania mwezi August. Tiketi hii imetolewa na Ethiopian Air Lines na kampuni ya EAS logistic ya Köln imetoa 20kg cargo ya kwenda Dar, ikiwa ni mizigo ya yake na vifaa vya maandalizi.
(Picha zote na Nashe Mvungi wa Ujerumani)

Pata kionjo cha mwanamuziki Ali Kiba wakati wa mashindano hayo:-

Ballack ana “gundu” na dhahabu!

MIDFIELDER ------
<!– if (document.getElementById) { document.getElementById(‘picGalleryNoScript_0’).style.display = ‘none’; } //–> Name: MICHAEL BALLACK —— Country: GERMANY —— Club: CHELSEA, UK

Baada ya kupoteza Ubingwa mwezi may kwenye Champions League akiwa na Chelsea, Michael Ballack juzi alikuwa looser tena baada ya timu yake ya Ujerumani kulikosa Kombe la EURO2008 na kuambulia medali ya Silver.
Ballack alikuwa kikosi kilicho chapwa na Manchester United na kuchukua Kombe katika mchezo uliochezwa Moscow Urusi na juzi ameshuhudia Fernando Tores wa Liverpool akipachika kagoli kamoja na hivyo kuwanyima ushindi.

Hii sio mara ya kwanza kwa Ballack, mwaka 202 alipokuwa akichezea Bayer Leverkusen walichapwa 2-1 na Ral Madrid kwenye fainali ya Champions Ligi. wakati Kepteni wa Spain Iker Casillas ambaye alikuwa Real Madrid walishinda kwa upande wao.
Ballack ambaye aliumia siku ya ijumaa kabla ya mtanange wa juzi na hivyo alikuwa na hati hati ya kucheza hadi dakika za mwisho Daktari wake aliposema anaweza kucheza.
Aliwahi kukaa miezi saba bila kucheza baada ya kuumia mguu pia mwaka 2007, na kurudi dimbani mwezi wa pili walipocheza mechi ya kirafiki na Austria na kuwatwanga 3-0.
Ballack alikosa mechi 10 kwa timu yake ya Taifa, na ndio ilikuwa ya kwanza kupata tiketi ya michuano hii.
Ballack mkataba wake na Chelsea unamaliziaka 2009 na 2010 itakuwa nafasi pekee kwake na timu ya Taifa kupigania kikombe kikubwa kwenye mtanange wa Kombe la Dunia nchini Afrika ya Kusini.

David Villa, Mfungaji bora EURO 2008

Villa stays loyal to Valencia
Michuano ya EURO ndio imemalizika na Spain ndio wamechukua kikombe, Mashindano ya mwaka huu yalishuhudia Vigogo wakihenyeshwa na Timu nyingine kuonyesha makali, record kadhaa kuvunjwa nk.
Jina la David Villa (pichani juu) bado ni mwiba kwa baadhi ya Timu kwani aliwatungua bila huruma, Pamoja na kutokucheza Fainali dhidi ya Ujerumani bado Bado Villa amechukua nafasi ya ufungaji bora baada ya kupachika kimiani mabao manne katika michuano hiyo.

Villa alifunga jumla ya mabao hayo manne kwenye mechi mbili pekee za mwanzo za Spain , ikiwa ni matatu walipocheza na Russia na goli moja walipocheza na Sweden.

Ufungaji wake wa magoli matatu kwenye mechi yao na Russia ilimfanya kuwa ndiye mfungaji aliyefunga magoli matatu katika mechoi moja tangu mwaka 2000 ambapo Mholanzi Patric Kluvert alifanya hivyo.

Villa mwenye miaka 26 hivi sasa anasakamwa na Vilabu vikubwa ili kumchukua kwa msimu ujao wa ligi zao, inasemwa Chelsea, Arsenal, Real Madrid na Liverpool ni moja ya vilabu ambavyo vinamhitaji mchezaji huyo.

Villa aliwaongoza Lukas Podolski wa Ujerumani, Roman Pavlyuchenko wa Russia, Hakan Yakin wa Switzerland na Semih Senturk wa Turkey walipata jumla ya magoli matatu kila mmoja.

Pia wachezaji 12 walifanikiwa kufunga magoli 2 kila mmoja kwenye michuano hii, Daniel Guiza na muuaji wa wajerumani Fernando Torres, wote toka Hispania. Mjerumani Michael Ballack, Miroslav Klose na Bastian Schweinsteiger wao pia walifunga magoli mawili kila mmoja.

(Picha na GI)

Advertisements

Kumbukumbu mwezi Juni

July 14, 2008

Mashabiki bwana!!

A supporter of the Turkish team has his national flag painted on his head ahead of the Euro 2008 championships semi-final football match Germany vs. Turkey on June 25, 2008 at Saint Jakob-Park stadium in Basel, Switzerland. AFP PHOTO DDP / PHILLIPP GUELLAND -- MOBILE SERVICES OUT -- (Photo credit should read PHILLIPP GUELLAND/AFP/Getty Images)
Shabiki wa Turkey akiwa na Bendera ya nchi yake kichwani.
Germany supporters cheer before the start of the Euro 2008 championships semi-final football match Germany vs. Turkey on June 25, 2008 at St Jakob-Park stadium in Basel, Switzerland. AFP PHOTO / VALERY HACHE -- MOBILE SERVICES OUT -- (Photo credit should read VALERY HACHE/AFP/Getty Images)
Mashabiki wa Ujerumani chiboko!!
Supporters of the German team cheer ahead of the Euro 2008 championships semi-final football match Germany vs. Turkey on June 25, 2008 at St Jakob-Park stadium in Basel, Switzerland. AFP PHOTO DDP / TORSTEN SILZ  -- MOBILE SERVICES OUT -- (Photo credit should read TORSTEN SILZ/AFP/Getty Images)

Nusu Fainali EURO 2008 Nani ni nani?

Germany:

German supporters play instruments outside the Germany national soccer team Hotel in Basel, Wednesday, June 25, 2008. Germany reached the semifinal stage of the Euro 2008 European Soccer Championships in Austria and Switzerland and will face Turkey. From AP Photo by LUCA BRUNO.
Mashabiki wa Timu ya Taifa ya Ujerumani wakiwa nje ya Hotel wanapokaa wachezaji wao huko Basel leo, Timu ya Ujerumani inaingia dimbani kumenyana na Turkey, chochote chweza tokea.

Hii ni timu nzuri inayocheza kwa kujituma ila inashindwa kuwa na motivation at times.Ila katika siku yao hakuna timu inayoweza ishinda.Kwa jicho la karibu naona bado wana hali ngumu dhidi ya Uturuki kutokana na ukweli kwamba Waturuki wameonekana kuwa vichwa ngumu karibu katika kila kazi waliyokutana nayo

…………………………………………………………………………….

Waturuki:

Supporters of the German and Turkish teams wave their national flags in the "Fanmeile" (Fan zone) in Berlin, ahead of the Euro 2008 championships half-final football match Germany vs Turkey held on June 25, 2008 at the St. Jakobs-Park stadium in Basel, Switzerland. AFP PHOTO  DDP / MICHAEL KAPPELER (Photo credit should read MICHAEL KAPPELER/AFP/Getty Images)
Mashabiki wa Ujerumani na Turkey wakiwa pamoja wakichemshana hii ikiwa ni muda kabla kuanza kwa mchezo kati ya timu zao.

Hawa jamaa mpira wao sio mbaya ila kutokana na kutokuwa na majina makubwa inafanya kazi kwao iwe rahisi.Nafasi waliyofikia ni mafanikio tayari kwao.Hawana presha yeyote ya kujidhihirisha zaidi ya waliyofikia tayari.Hii inafanya game kwao iwe rahisi zaidi ya Ujerumani.

…………………………………………………………………………….

Waspeini:

Spain's Cesc Fabregas signs autographs after a training session of the national soccer team of Spain in Neustift im Stubaital, Austria, on Tuesday, June 24, 2008. Spain will play Russia in the semifinal at the Euro 2008 European Soccer Championships in Austria and Switzerland. From AP Photo by Bernat Armangue.

Cesc Fabregas wa Spain akisaini Autograph mara baada ya kumalizika kwa mazoezi ya timu yao hapo jana.

Hawa kwa rekodi wana tabia ya kupata matokeo mabovu lkn kwa matokeo yao dhidi ya Italia yanarudisha imani ya kuweza kufanya mengi japo bado wana presha kutokana na kupewa nafasi kubwa na mashabiki na wataalamu wengi wa soka.Kwa upande wangu nawapa nafsi kubwa ya kucheza final.

…………………………………………………………………………….

Warusi:

Russian supporters cheer and wave Russian flags prior to the Euro 2008 Championships Group D football match Spain vs. Russia on June 10, 2008 at Stade Tivoli Neu, in Innsbruck, Austria. From Getty Images by AFP/Getty Images.
Mashabiki wa Russia wakishangilia timu yao, usilogwe kuingia kwenye anga zao hawa jamaa ni noma.

Hawa jamaa kama ilivyo ada hawakupewa kabisa nafasi lkn waliyofanya tayari yamelipa matarajio na hivyo wanaingia kwenye hii game wakiwa na imani kuwa timu walidhodhani ni ngumu kwamba nazo zinafungika.Hii inakuwa rahisi kwa wao kukumbana na waspeini ila tatizo kwao ni kwamba wana wachezaji wengi wa kikosi chak wanza ambao hawatacheza kwenye hii game hivyo kupunguza matunda ya kikosi imara chao.

Wachezaji wa kuangaliwa kwa hii hatua ni bastian schweinsteiger,Fernando Torres,Arda Turna na Andrei Arshavin

Review By Tanzania Dream, Pamoja Kaka.

Bibisiya Mfwengi, Dansa wa Werrason anayedatisha jukwaani

Anaitwa Bibisiya Mfwengi, huyu ndiye kiongozi wa kikosi cha wachezaji cha Werason, mdada anatisha na kudatisha awapo jukwaani kwanza kwa umbile lake pia anavyokizungusha. Mara nyingi kwenye Sebene la Werrson huyu mdada huwa akipewa nafasi mashabiki hawataki aongoke na inakuwaga kazi kweli kweli, Werrason anaingia Dar Leo hii, habari kamili muda si mrefu. Pata kionjo.

Muangalie na HApa Pia

Tuesday, June 24, 2008

Master J, CEO MJ Records

Master J
PROFESSION: Producer
COMPANY: MJ Records
NATIONALITY: Tanzanian

Joachim Kimaryo a.k.a. Master J as he is fondly known in Tanzania’s growing music industry founded in 1996 what is today one of Tanzania’s foremost digital recording studios – MJ Records.

This man is undisputedly one of the pioneers of ‘Bongo Flava’ a distinctive predominantly hip-hop Tanzanian sound that has taken the continent by storm. He has played an integral role in the development of Bongo Flava and the growth of the broader music industry in Tanzania.

Master J holds a degree in electronics engineering from City University of London, and has always had a keen interest in music. Recording almost all genres of Tanzanian music from gospel, Bolingo to the famous Bongo Flava, Master J has worked with the best in the Tanzanian music industry.

Khangalicious. na Changamoto ya Vazi la Kitaifa

Mustafa Hasanali na Ma modela wake mara baada ya shoo ya Khanga licious

Mwanamitindo mkongwe kuliko wote duniani, Bibi Kidude akipita jukwaani kuonyesha vazi la khanga lililobuniwa na mbunifu Mustafa Hassanali.

Nakumbuka miaka hii ya 2000 na ushehe(naomba kusahihishwa) Serikali kupitia wizara ya Elimu ilikuwa na shindano la vazi la Taifa ambalo fainali ilifanyika Dodoma, Watu wengi walionyesha kutoridhishwa na mchakato mzima na hata Vazi lenyewe kwani tangu hapo sikuwahi kuona wala kusikia vazi lililoshinda likienziwa, inawezekana nipo mbali kihabari lakini sidhani kama hata we msomaji umesikia, Najaribu kuangalia hili onyesho la Khangalicious lililoletwa na Mustafa Hasanali na umuhimu wa changamoto ya vazi la kitaifa, Je lipi hapo linaweza kuwa Vazi la kitaifa angalau ukivaa unasema nimevaa vazi la Kitanzania? Picha na Father Kidevu

Flaviana Matata

Kwa wengi,nchini Tanzania na duniani,anabakia kuwa mrembo kutoka nchini Tanzania aliyeiwakilisha nchi yake katika shindano la dunia la Miss Universe mwaka 2007 na kuwa mshiriki wa kwanza aliyeamua kulipanda jukwaa akiwa kipara.Kwa wengine,wakiwemo ndugu,jamaa na marafiki zake,anabakia kuwa Flaviana Matata.

Hivi karibuni alilivua rasmi taji lake la Miss Universe Tanzania 2007 baada ya kulitumikia kwa muda wa mwaka mzima.Tulipata nafasi ya kuongea machache na Flaviana baada ya kumkabidhi rasmi mrembo mwingine,Amanda Sululu, taji la Miss Universe Tanzania. Hivi tunavyoongea tayari Amanda yupo nchini Vietnam tayari kabisa kwa shindano la Miss Universe litakalofikia kilele nchini humo tarehe 13 Julai mwaka huu.

Flaviani amefanya Mahojiano na Bongo Celebrity gonga hapa upate Kujua anasemaje?

Da Chemi amaliza uigizaji The Surrogates

DADA Chem ambaye ameshiriki katika filamu ya The Surrogates itakayotoka majira ya kiangazi mwakani amemaliza kucheza nafasi yake katika filamu hiyo na kurejea kijiweni kwake.
Dada Chemi ambaye pia ni mwanachama wa Screen Actors Guild (SAG) amesema kazi ya kuigiza ilikuwa bomba.
Amesema katika blogu yake kwamba katika filamu hiyo ambayo kinara wake ni Bruce Willis amecheza kama Dred.
Nafasi ya kucheza aliipata mwezi wa tatu wakati alipoitwa kwenye audition ya sinema hiyo.
Ingawa hakupata sehemu aliyofanyiwa audition alipewa nafasi ya kucheza Dred na alicheza vyema nafdasi hiyo akiwa mchafu na kuvaa nguo zilizochakaa akionekana kama kama ombaomba.
Isome Zaidi kwa Lukwangile Entertainment

Ngoma Africa na Muziki wa Dance ughaibuni

Habari hii imeletwa na Msemakweli

Mwanamziki nyota Ebrahim Makunja alimaarufu Ras Ebby Makunja na ´bendi yake The Ngoma Africa banad wenye makao yao huko Ujerumani wamefanya kweli na wamedhihirishia ulimwengu kuwa bongo dansi la Tanzania ni sawa na moto wa mstuni! habari za kuaminika kutoka katika mashirika mbali mbali ya habari ya kimataifa kama vile jarida hili la South Africa BIZ, gazeti la kenya http://www.coastweek.com/3124-19.htm ,shirika la habari la scandinavia http://www.nanews.net huko spain nako jarida la http://www.fundicuionsur.com/spip.php?article1308 na kama hilivyo mila na desturi za waswahili kuwa ndio wenye watoto wao wazee wa http://www.bongocelebrity.com wamefanya kweli kwa kuweka wimbo huo! wastarabu wa Engaland http://www.tzuk.net nao hawakuwa nyuma katika kuwa nafasi vijana wao The Ngoma Africa,Nchini Holland majarida mengi nayo yamewafagilia Ngoma africa. Ukiachia mbali mitandao na majarida hayo kuna majarida ma kubwa ya inside world ya New Zerland,africa News la Italy. Pia habari za kuaminika zinaeleza kuwa song hilo jipya limeshapokelewa katika nchi zaidi ya 50, zikiwemo visiwa vya Caribean Dominica Rep.Antigua,Baadhi ya Radio za Brazili nazo zimepokea mdundo huo na kuukubali japo hawajui kiswahili. Raha ya mdundo huo hata kama ujui kiswahili hule mrindimo wa beat zake ni Raha juu ya raha! na ukikijua kiswahili basi utakubali kuwa mtunzi huyo Ebrahim Makunja ni mtunzi anaye yafahamu matatizo ya jamii yake ya Uswahilini,kuwa Pombe ni mojawapo ya Tatizo kubwa!linalo isumbuwa jamii.

Ras Makunja au Ebrahim Makunja ni mtunzi aliyebobea katika shughuli yake hiyo ya kutunga nyimbo na kuimba katika kuishauri jamii au hata kutoa onyo lakini mara nyingi huwa ni mwanamziki mwenye kuzua hoja kama utamsikiliza sana katika tungo zake za RUSHWA NI ADUI WA HAKI,hiliyopo katika CD ya “Anti-Corruption Squard” na ule mjadala wa mchezo mchafu wa “Mama Kimwaga”(Sugar mum)katika album hiliyobeba jina la “Mama Kimwaga”! kwa watu waliyo karibu na Ras Makunja na bendi ya The Ngoma Africa wanatonya kuwa jamaa hao ni watu utani sana na Ras Makunja mwenyewe ni mtu mwenye kupenda mizaa sana !lakini hawapo jukwaani na ukimsikiliza sana nyimbo zake zina maneno ya ukweli napenginepo yanachoma moyoni,na hakiona kuwa unamwangalia sana huwa anaimba na kufunika uso kwa kutumia kiganja cha mkono wake moja au kuvaa miwani ya jua mkubwa hata kama usiku !akimaliza kuimba uwazawadia washabiki kwa tabasamu ya kicheko ambalo uwariwadha !


Ujumbe uliomo katika nyimbo za Ngoma africa band kila wakati unasindikizwa na mlindimo au mdundo wa nyuzi kali zinatoka vidoleni mwa wanamziki mahili wa bendi hiyo wakiwamo mcharaza solo Gitaa machachari Mr.Christian Bakotessa aka Chris-B,ambaye mara nyingi uhimba pamoja na Ras Makunja,pia kuna yule mpiga gitaa la Bass Said Vuai aka Prince Jazbo Vuai,wapo kakribani wanamziki 7 hivi.

Tamazi ya habari tumalizie kwa kutoa wito kuwa wanamziki wa nyumbani hizi ndizo habari njema msiogope wala kusita kuzitoa nje kazi zenu,kuwa mziki wa dansi wa Tanzania sasa unakubalika. Hongera Ras Makunja Na wenzako The nGoma Africa Band au kama wanavyojilikana “the Golden Voice of East africa”.
Gonga hapa usikilize

Monday, June 23, 2008

basketball wapata mdhamini

Kampuni ya Uniliver imedhamini Sh milioni 10 kwa michuano ya kikapu ya Miji Mikuu ya Afrika Mashariki kati na kusini

inayotarajiwa kuanza kutimua vumbi kesho katika Uwanja wa Ndani wa Taifa na Uwanja wa Sigara.

Akichonga na wanahabari Rais wa Kamati ya Mpira wa Kikapu Miji Mikuu ya Afrika Mashariki Kati na Kusini, Simon Msoffe alisema Kampuni hiyo imetoa kiasi hicho kwa ajili ya shughuli mbalimbali za michuano hiyo.

“Tunatarajia Kampuni zingine zitajitokeza kufanikisha michuano hiyo ili ikonge nyoyo za mashabiki wa mpira wa kikapu waliopo hapa Tanzania, ” alisema

Msofe. Majiji yanayoshiriki michuano hiyo kutoka Tanzania ni Dar es Salaam, Mwanza, Arusha, Mbeya na Tanga, Kenya ni Nairobi na Mombasa, Uganda ni Kampala, na jiji jingine ni Mogadishu.

Mashindano hayo yaliyoanza toka mwaka 1999 na kufanyika kila mwaka, mwaka jana bingwa wa michuano hiyo ilikuwa ni Nairobi walioifunga Dar es Salaam katika fainali iliyofanyika Nairobi, Kenya.

KIli Music Award yaiva

Wasanii wa muziki wakae mkao wa kula kwani zile tuzo za ‘Dandu’ zitatolewa Juni 28 mwaka huu ndani ya Hoteli ya Kempisky. Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi hayo Oscar Shelukindo alisema mwaka huu wahudhuriaji hawataingia kwa tiketi bali kadi maalum.
Pichani kushoto ni Afisa Uhusiano wa Kampuni iliyoandaa tuzo hizo Oscar Shelukindo na Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya inshu hiyo, John Mhina wakionesha aina ya tuzo zitakazotolewa siku hiyo wakati wakiongea na waandishi wa Habari katika Ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Jijini Dar es Salaam leo mchana. Tuzo hizi zilianzishwa na mwanamuziki James Dandu ambaye hivi sasa ni marehemu. Picha/Habari na GPL

Kolabo ya Juliana na Bushoke

Wimbo ni wake Juliana Kanyomozi toka nchini Uganda akimshirikisha Bushoke wa Tanzania, Wimbo huu ambao uko kwenye Albamu ya sasa ya Juliana bado unawika kwenye chat za Uganda na Afrika Mashariki kwa ujumla, Kwa mengi yamhusuyo Juliana gonga hapa, na kwa kusikiliza wimbo huu gonga player.

Hispania wafuzu Nusu Fainali kwa mbinde!

Spain 4 – 2 Italy

Spain celebrates

Wachezaji wa Spain wakisherehekea mara baada ya kumalizika kwa hatua ya kupigiana penati na Italy hapo jana.

Hispania wamekwenda hatua ya Nusu fainali za michezo ya Euro 2008 baada ya kufikia hatua ya kupigiana penati kwenye mechi kali kati yake na Italy hapo Ernst-Happel Stadium jana.

Golikipa wa Hispania Iker Casillas aliokoa mishuti ya penati toka kwa Daniele De Rossi na Antonio Di Natale hii likuwa ni baada ya dakika 120 za bila kufungana kabla ya mchezaji matata Cesc Fabregas kufunga penati yake ya mwisho na kuwainua mamia kwa maelfu ya mashabiki waliokuwa uwanjani na mitaani.

Kwa upand wake Cassillas, aliokoa mkwaju kwa mguu uliopigwa na Mauro Camoranesi, ulisaidia kuiweka Spain kwenye matokeo mazuri ambayo hata kwa penati ilobaki Italy wasingeweza kufikia magoli ya Hispania.

Italy walishinda kombe la Dunia mwaka 2006 kwa Penati dhidi ya Ufaransa lakini Buffon ambaye alikuwa shujaa kwenye fainali zile jana alishindwa kuonyesha makali yake na badala yake golikipa wa Spain Casillas akawa ndio shujaa.

Lakini ikumbukwe pia kipa huyu wa Italy ndiye aliyewafikisha kwenye hatua hiyo baada ya kuokoa mkwaju wa Adrian Mutu walipocheza na Romania, na hata hivyo aliicheza penati ya nne ya Daniel Guiza hapo jana.

Kwa matokeo haya Hispania watakutana na Russia hapo tarehe 26 Juni huko Vienna Austria ambapo bingwa atacheza na mshindi kati ya Ujerumani na Turkey ambao watacheza tarehe 25 Basel.

Mechi za Awali Kombe la Mataifa na Kombe la Dunia kwa Afrika

Matokeo kadha ya mechi za kufuzu Kombe la Mataifa ya Afrika na Kombe la Dunia 2010 ya mechi za Jumapili tarehe 22 Juni 2008

Kundi la 2
Zimbabwe 0 Kenya 0

Kundi la 3
Angola Uganda (mechi iliahirishwa Jumapili hadi Jumatatu)
Benin 2 Niger 0

Kundi la 7
Msumbiji 3 Bukini 0

Kundi la 8
Ethiopia 6 Mauritania 1

Kundi la 10
Congo 2 Chad 0

Kundi la 12
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo 5 Djibouti 1

Mechi za Jumamosi tarehe 21 Juni 2008

Kundi la 1
Cameroon 2 Tanzania 1

Kundi la 4
Nigeria 2 Equatorial Guinea 0
Afrika Kusini 0 Sierra Leone 0

Kundi la 5
Morocco 2 Rwanda 0

Kundi la 6
Senegal 3 Liberia 1

Kundi la 9
Tunisia 2 Burundi 1
Burkhina Faso 4 Ushelisheli 1

Kundi la 11
Zambia 1 Swaziland 0

Mechi zilizochezwa Ijumaa tarehe 20 Juni 2008

Kundi la 5
Libya 4 Lesotho 0

Kundi la 6
Algeria 1 Gambia 0

Mashindano ya Pool kuanza Juni 27

Pichani mmoja wa wachezaji Pool maarufu Dar, Robert William Mwafrika akiwafundisha vijana zaidi ya 20 sheria za mchezo wa Pool huko Kijijini Mlimba, Morogoro hivi karibuni.

Mashindano ya taifa ya mchezo ya pool 2008 yanayotarajiwa kushirikisha timu kutoka baadhi ya mikoa ya Tanzania bara yanatarajiwa kuanza kutimua vumbi Juni 27 mwaka huu jijini Dar es Salaam.

Kwa kuzingatia umuhimu wa mashindano hayo, chama cha waamuzi wa mchezo huo wa Pool mkoa wa Dar es Salaam -DAPORA-kimeandaa semina kwa waandishi wa habari iliyohusu mchezo huo na sheria zake.

Mashindano hayo yameandaliwa na chama cha mchezo wa Pool mkoa wa Dar es Salaam-DARPA- na kudhaminiwa na kampuni ya bia Tanzania- kwa kupitia bia aina ya safari.

Miss Arusha ajinyakulia gari

Miss Arusha 2008, Glory Emson akiwa ndani ya gari yake Toyota Sprinter mpyaa aliyokabidhiwa mara baada ya kushinda hivi karibuni, gari hii imetolewa na wadhamini wa Miss Arusha TanzaniteOne
(Photo by Nicky Mchau)

Sunday, June 22, 2008

Huu ndio unazi!!

Dutch supporters look dejected at the end of the Euro 2008 Championships quarter-final football match the Netherlands vs. Russia on June 21, 2008 at St. Jakob-Park in Basel. Russia won 3-1.AFP PHOTO / JOHN MACDOUGALL -- MOBILE SERVICES OUT --       (Photo credit should read JOHN MACDOUGALL/AFP/Getty Images)
Mashabiki wa Holland juu na chini wakiwa wamebaki wawili tu jukwaani mara baada ya mpira kumalizika kati ya Holland na Russia na Holland kubugizwa 3-1.
Dutch supporters look dejected after Russia won the Euro 2008 Championships quarter-final football match the Netherlands vs. Russia on June 21, 2008 at St. Jakob-Park in Basel. Russia won 3-1.  AFP PHOTO / PATRICK HERTZOG  -- MOBILE SERVICES OUT --                                                                           (Photo credit should read PATRICK HERTZOG/AFP/Getty Images)

Russia yawafungisha Virago wakali Holland

Netherlands 1-3 Russia

Netherlands' Edwin van der Sar grabs the ball out of the net after failing to save a shot by Russia's Dmitri Torbinski, unseen, during the quarterfinal match between the Netherlands and Russia in Basel, Switzerland, Saturday, June 21, 2008, at the Euro 2008 European Soccer Championships in Austria and Switzerland. Russia defeated Netherlands 3-1.
Golikipa wa Holland au Dutch au Uholanzi au Netherland Netherlands’ Edwin van der Sar akiokota mpira kimiani baada ya kufungwa goli la pili na Dmitri Torbinski,
Russian forward Andrei Arshavin
Wandamba wanasema MATU!! Ndivyo anavyoelekea kuwaambia Andrei Arshavin mashabiki wa Holland ambao walikuwa wakiishangilia timu yao kwa nguvu baada ya kupachika goli la tatu dakika ya 116.

Netherlands' Wesley Sneijder, bottom, is comforted by a teammate as goalkeeper Edwin van der Sar, right, walks past, while Russian players celebrate in background after the quarterfinal match between the Netherlands and Russia in Basel, Switzerland, Saturday, June 21, 2008, at the Euro 2008 European Soccer Championships in Austria and Switzerland. Russia defeated Netherlands 3-1.
Mchezaji wa Holland Wesley Sneijder, chini akipoozwa na mwenzake huku golikipa wao Edwin van der Sar akipita mara baada ya mechi kuisha, kwa mbaali Russia wakijipongeza,

Russian soccer fans celebrate their team's victory after the quarterfinal match between the Netherlands and Russia at the Euro 2008 European Soccer Championships in Red Square in Moscow, early Sunday, June 22, 2008. Russia defeated the Netherlands 3-1.
Russian soccer fans celebrate their team's victory after the quarterfinal match between the Netherlands and Russia at the Euro 2008 European Soccer Championships, in the center of Moscow with the Kremlin and historical museum in the background, early Sunday, June 22, 2008. Russia beat the tournament favorite 3-1 in extra time to secure its first ever European Championship semifinal appearance.
Kama kawa mashabiki mitaani wakisherehekea.

Magoli yaliyofungwa na Dmitri Torbinski na Andrei Arshavin dakika za majeruhi yameiwezesha Russia kucheza nusu fainali na kuwafungisha virago Holland ambao walianza kwa mkwara.

Mpaka dakika 5 kabla ya mpira kumalizika Holland walikuwa wameshalala kwa goli moja bila ndipo Ruud van Nistelrooy aliposawazisha kwenye dakika ya 86 na kufanya dakika za nyongeza ziongezwe.

Russia ambao walizidi kuongeza spidi ya mpira na dakika kadhaa walifanikiwa baada ya Torbinski kupachika bao la pili baada ya kazi ngumu ikiwa ni dakika ya 112 ya mchezo, Goli hili liliwachanganya kidogo Holland ambao walipewa nafasi kubwa ya kucheza hata fainali hasa baada ya kuwabwaga vigogo kama Italy na Ufaransa ambao kwa pamoja walikuwa hili “kundi la kifo” na dakika nne baadaye Arshavin akaongeza goli jingine na kufanya uwanja ulipuke kwa mashabiki waRussia na kuleta majonzi kwa mashabiki wa Holland ambao waliupamba uwanja kwa rangi yao ya chungwa kama kawa.

Kocha wa Russia mholanzi Guus Hiddink kwa ajana ameonekana kama msaliti lakini alikuwa kibaruani kwani ameitoa timu ya nchi yake na uzalendo kuonyesha kumshinda, binasi simlaumu!

Kwa sasa Russia watakutana na Spain au Italy jijini Vienna siku ya Alhamisi na kufanya kuwa timu ya tatu kufikia hatua ya nusu fainali. Rafiki yangu Tanzania Dream hongera kwa kubashiri, natumai ubashiri wako utakwenda sawia.

Taifa Stars Yafa Kiume!! yatoka 2-1 na Kameroon

TIMU ya Taifa ya Tanzania, ‘Taifa Stars’ imekufa kiume ikiwa ugenini mjini Yaounde, baada ya kufungwa mabao 2-1 na Kameruni katika mchezo wa marudiano kuwania kufuzu fainali za Kombe la Dunia na Mataifa ya Afrika 2010.

Katika mchezo wa kwanza uliofanyika Uwanja Mkuu wa Taifa, Dar es Salaam Jumamosi iliyopita, Stars iligangamala na kutoka suluhu na Kameruni. ‘Indomitable Lions’ inaongoza kundi hilo ikiwa na pointi 10.

Stars imebakiwa na pointi mbili baada ya kutoka sare 1-1 na Mauritius, ilichapwa bao 1-0 na Cape Verde, ilitoka suluhu na Kameruni kabla ya jana kufungwa mabao 2-1 na wapinzani wao. Timu hiyo imebakiwa na michezo miwili dhidi ya Mauritius na Cape Verde.

Katika mchezo huo, Stars ilicheza vizuri na kuwabana Kameruni iliyosheheni nyota wengi wanaocheza mpira wa kulipwa katika klabu za Ulaya licha ya kupoteza mchezo huo.

Kameruni ilianza kupata bao lake dakika 66 lililofungwa na mshambuliaji wa Barcelona, Samuel Eto’o baada ya kipa Ivo Mapunda kuutema mpira wa krosi uliopigwa kutoka pembeni kulia mwa uwanja. Eto’o alifunga bao la ushindi dakika 88.

Stars ilitulia na kucheza pasi fupi fupi ambazo zilichangia kuwapa wakati mgumu mabeki wa Kameruni ambao walianza kupoteana na kutoa mwanya kwa Danny Mrwanda na Nizar Khalfan kumsogelea kipa wa Kameruni, Idriss Kameni.

Kasi ya Stars ilimchanganya nahodha wa Kameruni, Rogobert Song ambaye alifanya makosa yalimpa nafasi, Mrwanda kupachika bao la kusawazisha dakika 77 akifunga kwa shuti lililompita kipa Kameni kabla ya kujaa wavuni.

Kiungo wa pembeni wa Stars, Mrisho Ngassa alifanikiwa kuitoka ngome ya Kameruni dakika 11 lakini mpira wake wa krosi aliopiga kutoka upande wa kuliwa mwa uwanja uliokolewa na beki wa kati, Rogobert Song.

Kameruni ilijibu shambulizi hilo dakika 24 baada ya kiungo, Alexander Song kupenyeza mpira katika ngome ya Stars lakini beki Nadir Haroub ‘Cannavaro’ aliokoa hatari hiyo.

Dakika mbili baadae Stars ilitulia na kuanza kupanga mashambulizi ambapo Nizar Khalfan na Shaaban Nditi waligongeana vizuri kabla ya mabeki wa Kameruni kuokoa.

Stars ilibisha hodi langoni mwa Kameruni dakika 32 kabla ya mabeki wa Kameruni kuokoa hatari hiyo na kuwa kona ya kwanza kwa kikosi hicho iliyopigwa na beki wa kushoto, Amir Maftah ambayo haikuzaa matunda.

Eto’o alifanikiwa kuitoka ngome ya Stars dakika 37 na kufumua shuti lililotoka nje ya lango kabla ya dakika mbili baadae beki wa kulia, Geremi Njitap kupiga shuti lililowababatiza mabeki wa Stars kabla ya kuokolewa.

Kameruni iliendelea kutawala sehemu ya kiungo iliyokuwa ikichezwa na Godfrey Boniface na Nditi ambao walimpa nafasi Song kuwalisha mipira washambuliaji wa Kameruni walioongozwa na Eto’o.

Kameruni iliwatumia zaidi mabeki wa pembeni, Njitap aliyecheza upande wa kulia na Thimotheo Atouba ambao walikutana na vikwazo kutoka kwa Maftah na Nsajigwa Shadrack ambao walicheza kazi kupunguza kasi ya mashambulizi.

Baada ya kumalika mchezo huo, Eto’o alivua jezi yake nambari 9 na kumpa ‘Cannavaro’ ambaye naye alimpa ya kwake.

Stars: Ivo Mapunda, Nsajigwa Shadrack, Amir Maftah, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Salum Sued, Godfrey Boniface, Henry Joseph, Shaaban Nditi, Danny Mrwanda, Nizar Khalfan na Mrisho Ngassa/ Emmanuel Gabriel.

Saturday, June 21, 2008

KAMBI YA MISS TANZANIA EU KUANZA JUMATATU,

 • TIKETI ZAUZWA KAMA NJUGU

Kambi ya washiriki wa kumtafuta mrembo wa kitanzania katika nchi za Schengen yaani miss Manzania Schengen,inatarajiwa kuanza jumatatu hii ambapo vimwana 10 kutoka nchi mbalimbali za jumuiyayaUlaya watashiriki.Mashindano hayo yanatarajiwa kufanyika jumamosi ijayo katikaukumbi wa EFES mjini Essen Ujerumani ambapo mgeni Rasmi anatarajiwa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani, Mh Ahmada Ngemera.

Mratibu wa shindano ambalo kwa mara ya kwanza linafanyika katika nchi za Schengen, Nashe Mvungi amesema kuwa maandalizi yote yamekamilika ikiwa pamoja na kuongezeka kwa wadhamini.

Amesema kuwa wadhamini hao ni Gazeti la African Positive lililoko Dortmund nchini Ujerumani ambalo pia linamiliki magazeti mengine maarufu kwa jamii yawaafrika barani Ulaya, African Heritage na African Courier.Mkurugenzi mtendaji wa kampuni hiyo Bi Veve Tata amesema magazeti hayo yataingia mkataba na mrembo atakayeshinda ili kumtafutia mikataba yaurembo katika nchi nyingine hapa barani Ulaya.

Wadhamini wengine wa shindano hilo ni shirikala ndege la Ethiopea airline pamoja na kampuni ya utalii ya Western Tours ya Bonn Ujerumani.

Katika shindano hilo linalosubiriwa kwa hamu kubwa na wadau kutoka nchi mbalimbali za ulaya msanii wa kizazi kipya kutoka Tanzania anayetamba na kibao chake Cinderela Ali Kiba atatumbuiza,pamoja na msanii kutoka Cameroon wa miondoko ya Makossa Eyum Anneh.

Tiketi za onesho hilo zimekuwa zikiuzwa kwa kasi katika vituo mbalimbali.Bei ya tiketi hizo ni euro 10,lakini kwa wale watakaonunua mlangoni ni euro 15 pamoja na kinywaji kimoja bure.

Innomizizi na Kiuno Viuno

Weekend ya leo nakuacheni na kibao toka kwake Innomizizi cha Kiuno Viuno. Mambo ya Mombasa haya na wale watu wa Pwani wanafurahia sana wakisikia midundo hii, pata starehe… na Weekend njema. Hemed safari njema ya kurejea Dar, Rashid kaka Maandalizi mema ya harusi, Abdul Kareem mwako humu Raithiiii, Mamaa Fardhana na Minah vya Pwani hivi!!! lol

TAIFA STARS TUPENI RAHA LEO

“…Furaha ya Watanzania milioni 37 ipo miguuni kwenu, Tupeni raha.
Dawati la Spoti na Starehe linaungana na watazania kukutakieni kila la heri kwenye mchezo wa leo na Kameroon, msiogope majina, kama walishangaa uwanja wetu hakuna cha kushangaa kule hata kamoja tuu kanatutosha kufurajia.”

Werrason Kutua Dar July

MWANAMUZIKI wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Werrason Ngiyama Makanda anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika onesho maalum la utambulisho wa mashindano ya marepa utakaofanyika Juni 26, mwaka huu, Dar es Salaam. Mashindano yenyewe ni July 4, Akizunguza jana mmoja wa waandaaji wa mashindano hayo Kim (Kim and The Boys) alisema Werason ndiye atakuwa mgeni rasmi, hii inawapa matumaini mashabiki ambao kwa nyakati tofauti walikuwa wakiulizia kuhusu ujio wa Werrason, Bila kulizungumzia kwa Kina Kim alisema kuwa Werason anakuja jijini, Pichani chini ni Werasoni na kikosi chake wakiwa kwenye moja na matamasha. Werrasoni ambaye anatamba na nyimbo zake mpya bado haijajulikana kama atafanya matamasha mangapi ila habari za ujio wake tu ni furaha tosha kwa mashabiki wake wa Dar Es Salaam akina Big Producer Maghambo, Mukubwa Mwemtsi, Collins na Fikiri wazee wa USA, Boss Chizenga na wapenzi wote wa Werrason inawahusu hii. Weekend njema
Gonga player hapo chini Kupata Sebene la Werason na vijana wake, Muangalie kwa makini stage show wa Wera anaitwa Bibiceya Mufwengi. Selamat Datang…

Libya yaichapa Lesotho 4-0

Libyan fans watch a World Cup qualifier football match between Libya and Lesotho in Tripoli on June 20, 2008. Libya won 4-0. AFP PHOTO / MAHMUD TURKIA (Photo credit should read MAHMUD TURKIA/AFP/Getty Images)
MAshabiki wa Libya wakiangalia mechi ya awali ya kombe la Dunia kati ya timu yao ya Libya na Losotho, mchezo uliochezwa Tripoli Libya juni 20. Libya iliibugiza Lesotho mabao 4-0.

Turkey yasonga mbele

Croatia 1 – 3 Turkey

Croatia's Ivan Klasnic, left, scores the opening goal during the quarterfinal match between Croatia and Turkey in Vienna, Austria, Friday, June 20, 2008, at the Euro 2008 European Soccer Championships in Austria and Switzerland. Turkey beat Croatia 3-1 on penalties after a 1-1 draw in extra time.

Mchezaji wa Croatia Ivan Klasnic, shoto akifunga goli wakati wa mchezo wa robo fainali dhidi ya Turkey huko Vienna Austria jana left, Turkey walishinda kwa 3-1 kwa mikwaju ya Penati baada ya timu hizo kutoka suluhu ya goli moja kwa moja. Hivyo Turkey itakutana na Ujerumani kwenye mchezo wa Nusu fainali.

A Croatian fan react after the quarterfinal match between Croatia and Turkey in Vienna, Austria, Friday, June 20, 2008, at the Euro 2008 European Soccer Championships in Austria and Switzerland. Turkey beat Croatia 3-1 on penalties after a 1-1 draw in extra time.
Sabaiki wa Croatia akiwa anahuzunika mara baada ya kumalizika kwa mchezo wa jana kati ya Croatia na Turkey.

A police cordons off Croatian fans after the quarterfinal match Croatia against Turkey in Vienna, Austria, Friday, June 20, 2008, during the Euro 2008 European Soccer Championships in Austria and Switzerland. Turkey defeated Croatia 3-1 in the penalty shoot-out.
Polisi wakijenga ukuta kuwazuia mashabiki wa Croatia ambao walikuwa wakipita mitaani wakifanya fujo baada ya timu yao kuondolewa hapo jana.

Turkish soccer fans sit on top of a car as they celebrate the victory of the national soccer team of Turkey over Croatia in the quarterfinal match in Vienna, Austria, early Sunday, June 21, 2008, at the Euro 2008 European Soccer Championships in Austria and Switzerland. Turkey defeated Croatia 3 - 1 in the final penalty shoot-out.
Mashabiki wa Turkey wakipita mitaani Austria wakishangilia timu yao baada ya kuichapa Croatia 3-1 hapo jana, Mji wa Viena ulikuwa ni nyekundu tupu!

Friday, June 20, 2008

Mshindi wa Talaku kuzawadiwa Gari

Mwandaaji wa pambano ya marapa, Abdulhakim Magomelo ‘Kim’ akizungumza na waandishi wa habari, kuhusu shindano la kumsaka ‘rapa’ mkali linalotarajiwa kufanyika Julai 4 mwaka huu jijini Dar es Salaam. Mshindi wa shindano la nani mkali katika marapa anatarajia kuondoka na zawadi ya gari.

Abdurahakimu Magomelo alisema shindano hilo limeandaliwa na taasisi ya kukuza vipaji (THT) na kuwa zawadi kamili zitatangazwa Alhamisi kwenye mkutano wa kutambulisha washiriki hao.
“ THT imeamua kuandaa shindano la kumpata nani zaidi katika marapa, lengo likiwa ni kuonyesha uwezo wa wasanii na kuthamini mchango wao katika muziki,” alisema. Gonga hapa uzisome zaidi

Salama naye aachia…

TUPHOTOE YA UKWELI Adam Mchomvu akiwa katika picha ya pozi na mtangazaji wa kituo cha Luninga na Redio cha East Afican Salama Jabir mara baada ya mkutano wa Kelly na waandishi wa habari kumalizika ndani ya Hotel ya Kilimanjaro.
hapo jana, Habari zinapasha kuwa Salama ambaye alipata umaarufu kwa kipindi chake cha Planet Bongo kilichokuwa kikirushwa hewani na East African Television ameacha kuendesha kipindi hico bila kuelezea kiundani zaidi. PICHA NA CHRISTOPHER LISSA / GPL.

Wachezaji Taifa Stars walamba mapesa!!

 • Kila Mchezaji ajinyakulia 1.2 milioni.
 • Timu imendoka kwenda Cameroon na matumaini

Kikosi cha Taifa Stars pichani ambacho kilicheza na Cameroon hivi majuzi

SIKU moja kabla ya timu ya Taifa ‘Taifa Stars’ kuivaa Kameruni katika mchezo wa marudino wa kuwania kufuzu fainali za Kombe la Dunia na Mataifa ya Afrika, wachezaji wa kikosi hicho wamejazwa mapesa ambapo kila mmoja amevuna kitita cha sh. milioni 1.2.

Taifa Stars na Kameruni ‘Indomitable Lions’ zinatarajiwa kukwaana kesho mjini Younde, ukiwa ni mchezo wa marudiano baada ya kutoka suluhu kwenye Uwanja Mkuu Mpya wa Taifa, Dar es Salaam wiki moja iliyopita.
Katika mchanganua huo, Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limetoa sh. 34,000,000 ikiwa ni motisha kwa wachezaji hao wakati benki ya NMB ambao ni wadhamini wa timu hiuo ilitoa sh. 6,200,000.

Kutokana na fedha hizo kila mchezaji atapata sh. milioni 1.2 katika kikosi cha wachezaji 27 na benchi la ufundi litapata sehemu ya fedha hizo.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa Shirikisho hilo, Frederick Mwakalebela, alisema TFF imeamua kutoa fedha hizo ili kuwapa changamoto wachezaji wanaojiwinda na mchezo huo mgumu dhidi ya Kameruni.

Mwakalebela alisema TFF imeamua kutoa fedha hizo kwa kutambua mchango mkubwa wa wachezaji wa Stars na benchi la ufundi.
Alisema kutokana na motosha hiyo ana uhakika wachezaji hao wataweza kufarijika na kujituma zaidi na hatimaye kupeperusha vizuri bendera ya Tanzania katika michezo yake ya kuwania kufuzu kucheza fainali za Kombe la Dunia.

“Vijana wamefanya kazi kubwa sana katika mchezo wao wa awali dhidi ya Kameruni na pia bado wana kazi ya kuhakikisha wanafanya vema katika mchezo wa marudiano hivyo fedha tulizotoa zitawapa changamoto kubwa,” alisema Mwakalebela.

Akizungumzia mchezo wa marudiano dhidi ya Kameruni unaotarajia kufanyika leo mjini Younde, Kocha Mkuu wa Stars Marcio Maximo, alisema mchezo huo ni mgumu kwa timu yake ambayo inahitaji ushindi.
Maximo alisema hata hivyo anatarajia kupata matokeo mazuri kwa timu yake baada ya kufanya maandalizi ya kutosha na kuhakikisha inakabiliana na Kameruni ikiwa ugenini.

Maximo alisema timu yake ipo katika hali nzuri na wachezaji wake wamejengwa kisaikolojia licha ya kuwa na majeruhi wachache ambao anatarajia kuwatumia katika mchezo huo akiwa na matumaini ya kurejea katika hali nzuri.

Stars inatarajiwa kuondoka leo alfajili ikiwa na wachezaji 21, viongozi saba wakiongozwa na Mbunge wa Singida Magharibi Mohamed Misanga ambaye atakuwa mkuu wa msafara kwa upande wa Serikali.
Taifa Stars ina pointi mbili baada ya kutoka sare 1-1 na Mauritius, imefungwa bao 1-0 na Cape Verde kabla ya kutoka suluhu na Kameruni.
Habari na Majira, Picha na Mpoki Bukuku

Wazee wa Ngwasuma kupamba Miss Morocco Leo

mambo yameshaiva na tayari warembo takriban 10 wako tayari kugombea taji la miss morocco, kitongoji kinachosifika kwa walimbwende wilaya ya kinondoni. mambo yatakuwa pale new msasani club nyuma ya ubalozi wa marekani kuanzia saa mbili usiku ambapo fm academia wana wa ngwasuma wanaotamba na kibao cha ‘si kila mwanamke aendaye baa ni malaya’ watakuwepo kusindikiza usiku huo unaosimamiwa na mama wa mitindo aisa idarous, Habari hii na Muhidini Issa Michuzi ambaye ni mmoja wa wadhamini wa shindano hilo. Hii inaonyesha ni jinsi gani watanzania wameamka na kuanza kuzipa nafasi Blog kama sehemu ya Media na mchango wake kuthaminiwa katika jamii.

Bado anatakiwa….

Both Real Madrid and Manchester United want his services for next season, but Portugal's Cristiano Ronaldo must now reveal his future plans after his Euro 2008 heart-break on Thursday.
Zote Real Madrid na Manchester United zinamtaka kuwachezea kwenye msimu ujao wa ligi zao, Yampasa Ronaldo kutulia na kufikiria zaidi hatma yake kisoka kutokana na utashi wake binafsi. hasa baada ya timu yake ya taifa ya Portugal kusimamishwa na Ujerumani hapo jana.

Ronaldinho kwenda Galaxy?

FC Barcelona's Brazilian Ronaldinho plays with the ball during a training session, at Camp Nou stadium in Barcelona in April 2008. Manchester City owner Thaksin Shinawatra is determined to bring Ronaldinho to Eastlands.

Na Yahoo Sports News:
Mchezaji wa FC Barcelona Mbrazili Ronaldinho akicheza na mpira wakati wa mazoezi ya timu yake huko Camp Nou stadium, Barcelona April mwaka huu, Habari zinapasha kuwa timu ya Galaxy ya Marekani ambayo imemchukua David Beckham imetoa Ofa ya kumchuua Ronaldinho kwa mkataba wa dola milioni 16 na dola milioni 16 nyingine kwa haki miliki ya Picha yake. Habari zinasema mazungumzo yapo pazuri.

Masikini Portugal!!, Ujerumani yapaa Nusu Fainali

Portugal 2 – 3 Germany

Portugal goalkeeper Ricardo (left) and Germany's Michael Ballack

Mchezaji wa Ujerumani Michael Ballack (kulia) akipachika bao la tatu kwa timu yake.

German players celebrate after the Euro 2008 Championships quarter-final match Portugal vs. Germany on June 19, 2008 at St. Jakob-Park in Basel. Germany won 3-2. AFP PHOTO/JOHN MACDOUGALL -- MOBILE SERVICES OUT -- (Photo credit should read JOHN MACDOUGALL/AFP/Getty Images)
Wachezaji wa Ujerumani wakisherehekea ushindi mara baada ya mchezo wao na Portugal kumalizika

Portuguese soccer fans react as they watch the live TV broadcast of the Euro 2008 European Soccer Championship quarterfinal soccer match between Portugal and Germany, at a public viewing zone in the city center of Porto, Portugal, Thursday, June 19, 2008. Germany defeated Portugal 3-2.
Mashabiki wa Portugal wakiwa hawaamini macho yao mara baada ya kipyenga cha Mwisho
Supporters of the German team use their national flag to protect themselves against the rain and celebrate as they watch the Euro 2008 quarter final match of Germany against Portugal held in Basel, Switzerland, during a public viewing session on June 19, 2008 in Berlin. Germany won 2-3 and qualified for the semi-final.  AFP PHOTO  BARBARA SAX (Photo credit should read BARBARA SAX/AFP/Getty Images)

Macho yote yalikuwa kwa Cristiano Ronaldo jana lakini mambo hayakuwa hivyo kwani ilikuwa ni kinyume chake na mchezaji wa Ujerumani mwenye namba yaka yake Bastian Schweinsteiger ndiye aliyeng’ara jana na kuihakikishia Ujerumani nafasi ya kusonga mbele kwenye hatua ya Nusu Fainali na kuwatupa Portugal nje.

Nyota ya Bayern Munich Schweinsteiger alifunga goli moja na kutengeneza mengine mawili kwa Miroslav Klose na Michael Ballack, mpaka mapumziko mabao yalikuwa ni 2-1 huku ujerumani wakiongoza na bao la Portugal lilifungwa na Nuno Gomes kwenye dakika ya 42 ya kipindi cha kwanza.

Kipindi cha pili kulianza kwa mshike mshike kweli kweli huku mashabiki wakishangilia goli toka kwa Michael Ballacks mnamo dakika ya 62, mashabiki wa Portugal walionyesha kukata tamaa kidogo. Ujerumani ambao kwa kiasi kikubwa walianza michuano hii kwa kusuasua na watu waliitaja zaidi Portugal kucheza Fainali jana walionyesha uhai na ile ladha ya Mpira ambao wapenzi wameizoea kwa Ujerumani.

Kwa matokeo hayo Ujerumani itakutana na ama Croatia au Turkey, timu ambazo zote hazitabiriki.

Huu ni mhitimisho wa mkataba wa miaka mitano wa kocha Luiz Felipe Scolari ambaye atajiunga na Club ya Chelsea mapema baada ya michuano hii kwani alitazamiwa kumaliza ‘s five-year reign as Portugal coach to an inglorious end before he heads off to become Chelsea mamkataba wake kwa mafanikio ya kikombe hiki.

Kocha wa Ujerumani Joachim Low, hakuweza kukaa kwenye benchi la akiba la Ujerumani kwa kuwa alifungiwa mechi moja mapema wiki hii alipokwaruzana na Kocha mwenzie wa Austria Josef Hickersberger na kutolewa nje ya uwanja. Mpaka mwisho wa mchezo matokeo ni 3-2.

German fans celebrate at the end of the Euro 2008 Championships quarter-final match Portugal vs. Germany on June 19, 2008 at St. Jakob-Park in Basel. Germany won 3-2. AFP PHOTO/JOHN MACDOUGALL -- MOBILE SERVICES OUT --    (Photo credit should read JOHN MACDOUGALL/AFP/Getty Images)
Shangwe nderemo hoi na vifijo ghafla vilitawala kwenye jukwaa la Ujerumani ambayo ilikuwa kwenye hati hati kwani Portugal walionyesha mchezo mzuri tangu mwanzo mwa mashindano haya.

Thursday, June 19, 2008

Manchester kucheza na Portsmouth nchini Nigeria mwezi ujao.

Timu za Manchester United (Pichani) na Portsmouth zote za Uingereza zinatarajiwa kucheza mechi ya Kirafiki nchini Nigeria mwishoni mwa mwezi ujao wa July. Mpaka Sasa Timu ya Manchester United imekwisha thibitisha habari hizo na kusema itacheza mchezo mmoja tuu, ilihali timu ya Portsmouth wao watacheza na timu ya Taifa Super Eagle. Tayari Uingereza imekwisha tuma maofisa wake nchini Nigeria kufanya maandalizi ya timu zake ikiwa ni pamoja na kuukagua Uwanja kwa ajili ya mechi hiyo.

Mabondia wa Tanzania walikuwa na jumla ya kilo 6 za madawa!!

Polisi jijini Dar Es Salaam wamethibitisha habari zinazohusu Kukamatwa kwa wachezaji wa Timu ya Taifa ya Ndondi ambayo ilikuwa nchini Mauritius.

Akizungumza na waandishi wa habari Kaimu Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai Peter Kivuyo alisema kuchelewa kwa jeshi la polisi kutoa tamko kuhusiana na sakata hilo ni kwa kuwa ilibidi Jeshi la Polisi kupitia kitengo cha Interpool kuwasiliana na wenzao wa Mauritius ili kupata habari na undani wa mkasa huo. Kamanda Kivuy alisema kuwa katika kamata kamata hiyo kuna mwanamke Mkenya pia yuko kwenye mkasa huo ambao unajumuisha Watanzania sita na Mkenya mmoja. Habari zaidi zinasema Mwanamama huyo ambaye aliingia nchini humo Juni 10 mwaka huu alikuwa akifuatiliwa kwa karibu na maofisa wa upelelezi wa Mautius baada ya nyenendo zake kutiliwa shaka. tarehe 11 vijana mambondia wawili wa Tanzania walikamatwa Indre Street nchini Mauritius wakiwa na jumla ya pipi 373 zenye jumla ya kilo 6 ni dawa aina ya Heroin. Baada ya kukamatwa hao wawili ilibidi Polisi waende kuwachukua na wenzao wanne ambao walikuwa hotelini kwa kipindi hicho.

Watuhumiwa hao walifikishwa kwenye mahakama jumatatu wiki hii mjini Port Luis.
Kamanda Kivuyo amesema watanzania hao wanashitakiwa kwa makosa ya aina mbili.
i) Kujihusisha na biashara haramu ya madawa ya kulevya
ii) Kuingiza nchini Mauritius Madawa hayo.
na Mama wa Kikenya atashtakiwa kwa kushirikiana na watu hao.
Jeshi la polisi bado linafanya uchunguzi kujua kama madawa hayo waliondoka nayo hapa au la.

Muungano wa Africa Mashariki na Magharibi Kimuziki

NI RAY C NA RF CHORD

Original ya wimbo huu uliimbwa na Ray C Peke yake ikiwa ni Remix ya wimbo wa Sikuhitaji wenye mahadhi ya Taarabu enzi hizo alipopachikwa jina la Kiuno bola mfupa, Wanamuziki wa Bongo Flava wameamua kwenda kimataifa kwani Ray C aliamua kuukarabati huu wimbo na kuuimba tena akishirikiana na mwanamuziki RF Chord toka Siera Leone ambaye makazi yao ni nchini, RF Chord ni wanachama wa UMPA [Union Movement of Performing Artists of Sierra Leone] ,Wakiwa ni moja ya vikundi vya muziki vyenye chart ya juu kabisa nchini mwake Siera Leone.

RF Chord ambaye anatumia zaidi mtindo wa “Dance Hall” huku akichanganya na midundo ya asili kwa nyimbo zake nyingi amejipatia umaarufu sana na Wimbo huu aliopiga na Ray C.Hii inasaidia kuufanya muziki wa Kizazi kipya kutambulika zaidi ingawaje kwenye wimbo huu Ray C aliuimba kwenye mahadhi ya Kipwani zaidi, ukiwa ni Remix ya wimbo wake wa Sikuhitaji ambayo ilipigwa kitambo kidogo, Hivi karibuni tumesikia Mwanamuziki toka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo anayeishi Uingereza Blanchard Deplaizir akitangaza kutaka kufanya Kolabo na Ali Kiba na majuzi tena Ali Kiba huyo huyo amesikiaka akiingia Studio na Vijana wengine, Shime kumekucha muziki huu umekubalika nchini ni wakati wa kuuza kimataifa na kwa jinsi hii mtatoka.


Pata burudani kwa kubofya Player…

Banana na Hafsa kuwapa “Pressure” mashabiki Club Afrique

Siku: Ijumaa

Ukumbi: Club Afrique

Wakisaidiwa na

DJ Dubwise – Voice of Africa Radio

Jessie – Afrique

Talent – Afrique Tallent

Biggz – Afrique/Nytce

wasiliana na

Lawrence -07931819416, Jesse-07944545555, jimmy-07877418535

Starehe Mita 1800 juu ya usawa wa Bahari

Sehemu ya Genting kama inavyoonekana jioni, taa zinazoonekana kwa mbali ni mji wa Kuala Lumpur unavyoonekana toka Milima ya Genting.

Panaitwa Genting Highland, Ni umbali wa Kilomita 50 toka Kuala Lumpur mjini kuelekea Genting Highland, sehemu ya milima nchini Malaysia, kwa kawaida Malaysia ni nchi ya joto kama ilivyo Dar Es Salaam lakini tofauti ni kuwa joto la malaysia ni 30c to 36c na Fukuto ila kuna mvua mwaka mzima, wastani wa mvua kunyesha ni kila baada ya siku 2 hadi tatu. Hii hufanya mji huu kuwa wa kijani mwaka mzima lakini huwezi amini kuna sehemu ya Malaysia jotoridi lake ni 12c to 20c na wakati wa baridi hasa kunadondoka barafu, Huku ndio kunaitwa Gentini umbali wa Mita 1800 toka usawa wa bahari.
Huku hasa ni mji wa mapumziko, naita mji kwani panajitosheleza kwa kila kitu kuanzia mahoteli hadi Hospitali ambapo watu hupendelea kwenda kupumzika na kupata starehe mbali mbali kama Cable Car ambazo zina urefu wa Kilomita tatu na nusu, na inapita katikati ya misitu minene ya Tropiki na ubaridi mwanana pia utaona ndege na wanyama kama nyani wakiruka kwenye miti huku ukipita kwenye kijikombe kilichobebwa na mkanda (cable) ambacho kina tembea mwendo wa wastani wa kilomita 10 kwa saa, ni burudani tosha ambayo inahitaji ujasiri kwani kama hujazoea utatamani kushuka.

Genting Highlands Malaysia
'xxxx'
Safari ndio imeanza ndani ya “Cable Car”


Ndani ya Cable Car kule kwenye ukungu ndio tunakoelekea na ndio raha zote zilipo, kuzifikia sasa kasheshe.

wadau washafika kwenye safari ya mashaka
Siku yapili “vakesheni” inaendelea

Baadaye unafika Theme Park huku kuna michezo zaidi ya 60 ya kila aina ikiwa ni pamoja na Roller Coaster yenye urefu wa Kilometa moja, Train, Speed Car, Speed Boat, Mashua, Michezo ya Jukwaani, Maonyesho ya Wanyama mbali mbali, Muziki, Vyakula vya kila aina, utamaduni, Bustani ya Ndege, Bustani ya Mamba, Bustani ya Nyoka, kwa ujumla panakufanya ujione uko mahali tofauti.


Live Performances usiku ni sehemu ya starehe za Genting

Pia kuna ukumbi wa Concert mkubwa ambao una uwezo wa kuchukua watu zaidi ya 10,000 na ukumbi huu ni full kipupwe, ambapo wanamuziki maarufu wakija pia hutumbuiza huko.Usiku kuna burudani za aina mbali mbali ikianziwa na sarakasi toka kwa akina dada ambao nadhani hawana mifupa, ije ngoma na utamaduni wa Wamalay (kama taarab) hadi Vikundi vya Kizazi kipya na nyimbo za kimagharibi pia, Kwa ujumla ni raha yaani mpaka unaona unapewa zaidi kuliko gharama halisi.

Image Hosted by ImageShack.us
Mambo ya mwambao hata huku yapo atii

Pia kuna uwanja wa Golf kwa wenye mchezo wao, ambao wengi ni wageni mahoteli zaidi ya 30 yaliyopo kwenye kijiji hiki cha maraha. Mbali na hiyo kuna Casino kubwa, hii ndio Licensed Casino kwa Malaysia na inakusanya wacheza kamali toka Singapore, Malaysia, Indonesia na Brunei ambao wote hufika kucheza kamali hapa.

Wednesday, June 18, 2008

SERIKALI YAONGEZA MKATABA KWA MAXIMO

Baada ya majadiliano ya watanzania kuhusu kama kuongezwa au kusitishwa mkataba wa Kocha wa Taifa Stars Marcio Maximo, hatimaye kocha wa timu ya taifa ‘Taifa Stars’ Marcio Maximo ameongezwa mkataba na Shirikisho la soka Tanzania (TFF) baada ya kuridhika na kaiz aliyoanza kuifanya ambayo imeipandisha chati Tanzania katika medani ya soka.

Rais wa TFF, Leodegar Tenga alisema hayo Juni 18 jijini Dar es Salaam mwezi mmoja kabla ya kumalizika kwa mkataba wa kocha huyo wa miaka miwili. Mkataba wa miaka miwili aliosaini kocha huyo kutoka Brazil utamalizika mapema mwezi ujao.
“ Maximo aliingia mkataba nasi wa miaka miwili kuanzia Julai 28,2006 hivyo mkataba wake huo utakamilika Julai 2, mwaka huu hivyo tumeona ni vema tulizungumzie jambo hili mapema na tumeamua kumwongezea mkataba huo kwa miaka miwili mingine” alisema Tenga
Hatahivyo Tenga alisema pamoja na TFF kuamua kumwongeza mkataba wa kwa miaka miwili mingine na Kocha Maximo katika mazungumzo yao juu ya kuongezwa mkataba huo ameomba uongezewe mwaka mmoja tu kutokana na sababu zake binafsi ambazo hakuzitaja.
Akizungumza mara baada ya Tenga kutangaza uamuzi wa TFF kumwongezea mkataba wa kuinoa Stars, Maximo alisema sababu kubwa ya kufurahia jambo hilo na kushukuru kwa ushirikiano aliopewa kutekeleza majukumu yake na kueleza kuwa sababu yake ya kuomba apewe mwaka mmoja tu katika mkataba mpya ni kutoa nafasi kwa makocha wengine kuendeleza pale alipofikia katika programu ya kuinua na kuendeleza soka la Tanzania.
“ Unajua mtu huwezi kutekeleza programu ya miaka 10 ya kuinua na kuendeleza soka la nchi pekee yako kwani kila programu ya kocha ina muda wake wa kukamilika hivyo katika mikaka hiyo 10 kuna ulazima wa kocha mwingine kuja kuendeleza pale nilipofikia” alisema Maximo
Aidha Tenga alisema uamuzi huo kuongeza mkataba wa Maximo umefikiwa baada ya Shirikisho hilo kutathmini kazi ya kocha huyo na kuonekana ametekeleza majukumu yake ipasavyo kutokana na hadidu rejea alizopewa na kuifanya TFF kuridhishwa na utendaji wake.
Akizungumzia suala la kocha huyo kuomba kuongezewa mkataba wa mwaka mmoja tu katika mkataba huo mpya Tenga alisema wamekubaliana kuwa endapo Taifa Stars itafuzu kushiriki fainali ya michuano ya kombe la dunia na zile za Mataifa ya Afrika za mwaka 2010 nchi Afrika Kusini na Angola ataendelea na kazi ya kuinoa timu hiyo.

Maximo ambaye kutokana na kuinyanyua soka ya Tanzania kwa kiwango kikubwa kwa kipindi hiki cha miaka miwili kuna taarifa kuwa kuna mataifa matano yanamnyemelea ili aende kuzinoa timu za mataifa hayo.

Holland yaendeleza kichapo

Holland 2-0 Romania
Dutch players celebrate at the end of the Euro 2008 Championships Group C football match Netherlands vs. Romania on June 17, 2008 at the Stade de Suisse Wankdorf in Bern. Holland beat Romania 2-0 on Tuesday in Berne with goals from Klaas-Jan Huntelaar and Robin van Persie in their Group C match, a result which sent the Romanians crashing out of Euro 2008. AFP PHOTO / PATRICK HERTZOG -- MOBILE SERVICES OUT --    (Photo credit should read PATRICK HERTZOG/AFP/Getty Images)
Wachezaji wa Holland wakijipongeza na mashabiki mara baada ya kuwachapa Romania 2-0.

Magoli ya Klaas-Jan Huntelaar na Robin van Persie katika kipindi cha pili yailiipa Holland ushindi wa 2-0 dhidi ya Romani, Huu ni muendelezo wa ushindi kwa timu ya Holland ambayo imeshinda mechi zake zote.

Wa dutch wamemaliza ratiba ya awali kwa ushindi mzuri na sasa kwenye hatua ya Robo Fainali watakutaka na Sweden au Russia.
Romania ambao walihitajika kushinda mechi yao ya jana ili waweze kusonga mbele waliishia kusononeshwa tuu na waholanzi ambao hawakuwa na mchezo huku wakishangiliwa na wapenzi wao waliufanya uwanja mzima kuwa rangi ya machungwa.

Masikini Ufaransa, Italy yapaa

France 0 – 2 Italy

Celebrating a second-half goal.
Ushindi wa Italy wa mabao 2-0 dhidi Vibonde Ufaransa umeiwezesha Italy kufuzu kuingia hatua ya Robo Fainali, hii ni kutokana na mkali wa Kundi hili Holland kuichapa Romania na hivyo kufanya wanaokwenda mbele kundi hili kuwa ni Holland na Italy.

Andrea Pirlo ndiye alikuwa wa kwanza kupata bao kwa mabingwa hao wa dunia katika dakika ya 25 kwa penati baada ya Eric Abidal kumchezea madhambi Luca Toni ndani ya kumi na nane.

Abidal alipewa kadi nyekundu kwa tukio hilo na kuwaacha Ufaransa wakihangaika kuupanda mlima kufuatia mchezaji mwingine Frank Ribery kuwa majeruhi.

Italy walicheza kufa na kupona huku Ufaransa wakijitahidi kutaka kusawazisha bao mcheza ukawa wa vuta ni kuvute lakini mnamo dakika ya 62 Italy wakapata tena mpira wa adhabu ukaenda kupigwa na Daniele De Rossi na moja kwa moja ukaingia nyavu ndogo na kufanya Italy kuongoza kwa mabao mawili.

Ufaransa wamekuwa na wakati mbaya kwani angalao waliambulia sare kwenye mechi yao ya ufunguzi kabla hawajaja kubugizwa na Holland 4-1 na sasa Italy, Ikumbukwe kuwa Fainali za Kombe la Dunia ziliwakutanisha Iyaly na Ufaransa, ndio huku mchezaji wa Ufaransa Zinedine Zidane alimchapa kichwa cha kufa mtu Materazi.

Italy, ambao wamemaliza wakishika nafasi ya pili nyuma ya Dutch itakutana na mshindi wa Kundi D Spain siku ya jumapili katika hatua ya Robo Fainali huko Vienna lakini Waitaliano watawakosa wachezaji wao mahiri Pirlo na Gennaro Gattuso, ambao kwa pamoja walipata kadi kwenye mchezo wa jana.

Tuesday, June 17, 2008

Mzee Mwinyi akatiza safari ya Mlima Kilimanjaro

Pichani ni Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi akiwa kwenye moja ya njia za Mlima Kilimanjaro, Mzee Mwinyi alikatisha safari yake hiyo.Hakuna maelezo kutoka kwa wadhamini wa safari yake lakini imeelezwa kuwa amekatisha kwa sababu binafsi.Rais mstaafu alikuwa anakwea mlima huo mrefu katika kipindi kigumu kabisa cha mvua na baridi kuchangia wale wanaoishi na VVU katika mustakabali ambao unaendeshwa na mgodi wa dhababu wa Geita.

Pichani rais mstaafu (katikati)akiwa na wafanyakazi wa Celtel Tanzania,Prisca Tembo (kulia) na Cuthbert Raphael (kushoto),muda mfupi kabla ya kupanda Mlima Kilimanjaro.Picha hii ni kwa hisani ya Celtel.

Kelly atembelea uwanja wa Fisi!!


Msanii maarufu wa Marekani Kelly Rowland (mwenye mtandio juu na chini), ametinga uwanja wa fisi Manzese Dar es salaam jioni ya leo baada ya kusikia sifa za maeneo hayo ya uswahilini tangu akiwa USA. Msanii huyo ametua nchini kwa tiketi ya MTV kupitia taasisi yake inayojishughulisha na kampeni za kupambana na Ukwimwi (Staying Alive Foundation) ya nchini Marekani, Kelly akiwa balozi wake. Akiwa Uwanja wa Fisi, ambako kunasifika kwa ufuska wa kupindukia na rate kubwa ya maambukizi ya virusi vya ukimwi kwa wasichana wadogo, Kelly alitembelea NGO ya EYG (Elizabeth Youth Group) inayojishughulisha na kutoa misaada ya elimu ya HIV/AIDS, uchangudoa, ulevi pamoja na uvutaji bangi kwa vijana nchini. Pichani juu akiongea na waandishi wa habari katika hoteli ya Kempinsk jioni ya leo mara baada ya ziara ya Manzese na Tandale. PICHA: CHRISTOPHER LISSA wa GPL

Salamu za Cynthia Masasi

“…Welcome everybody on my New Website http://www.cynthiamasasi.com its been a while since i updated my website but its ON now..i will be chatting with my Fans,friends on my msg board everyday..So feel free to ask any question u have and i will try to answer all the questions as soon as possible..

Why im writing this msg is b’cause im shutting my HI5 profile down by June 20th 2008,so i wont have HI5 anymore friends..Welcome to my world i will have all the cool staff from video’s,new pictures,shows and many more cool things..And if u have any questions about modeling or tryna get into it holla at ya girl cause i gotchu..

Woooo i forgot one thing LOL i will be in columbus ohio for the old school party on July 4th weekend so everybody is welcome its gonna be bananas trust me The number one DJ Bon Luv from Tanzania will be in the building..People u dont wanna miss that come on so we can PAAAARTYYYY..

Love Cynthia masasi..

Gonga Player hapo upate kuona moja ya Video ambamo ameshiriki Cynthia

ZIKO: Scolari atawafungulia Brazili Uingereza

Mchezaji matata wa zamani wa Brazili Ziko amesema Luiz Felipe Scolari atakuwa na mafanikio makubwa na klabu ya Chelsea na atamfurahisha mmiliki wa klabu hiyo.

Scolari amechanguliwa kuifundisha klabu ya Chelsea kwa mkataba wa Paundi million £6 kwa mwaka akiwa na jukumu gumu la kukichukua kikombe cha Premier Ligi kutoka kwa Manchester na lililo muhimu ni kuchukua kikombe cha UEFA Champions Ligi kwa mara ya kwanza.

Kocha huyo wa Brazili ambaye kwa sasa anaifunza timu ya Taifa ya Portugal katika michezo ya fainali ya EURO 2008 ameshatajwa kutaka kuwachukua wachezaji mahiri kama Kaka, Ronaldinho, Franck Ribery, Rafael van der Vaart, Samuel Eto’o, Deco, Fernando Torres na David Villa ambaye anaongoza kwa ufungaji kwenye michezo ya EURO 2008.

Kujiunga kwa Scolari kwenye ligi ya Uingereza kutaifanya Brazil na wachezaji wengi wa Brasili kuiangalia ligi hiyo kwa jicho jingine ambapo wengi wa wa Brasili walipendelea kucheza sehemu nyingine za Ulaya sio Uingereza kikubwa ilikuwa ni Lugha na pia jinsi utamadubni wa waingereza ulivyo tofauti.

Zico anaamini kuwa hii itawanufaisha sio tu Premier League ila pia Brazil, na akasema: “Kufika kwa Scolari huko Chelsea ni mafanikio makubwa kwa Brazili na majaliwa ya soka la Brazili pia, tuna tatizo, hatupendi waingereza wanavyofanya mambo yao, na tunapingana hapo tuu inabidi kubadilika hiyo ndio maana yangu aliongeza Ziko.

“Hii ni nafasi kwa wachezaji wa Brazili kutoka Brazili na kwenda kucheza Uingereza itaifungua BRazili na soko la wa Brazili Uingereza pia. na sisi tutajifunza mengi si tu mpira hata maisha na utamaduni pia, soka inalipa kwa Uingereza, watu kule wanapenda soka na wanmefanikiwa kuianya ligi yao kupendwa ulimwenguni huko ndio kwa kwenda kucheza, aliongeza Zico.sement

Hatimaye Ujerumani wavuka

Austria 0-1 Germany
(From L) German defender Christoph Metzelder, German midfielder Michael Ballack and German midfielder Thomas Hitzlsperger wave to the crowd after winning 1-0 during the Euro 2008 Championships Group B football match Austria vs. Germany on June 16, 2008 at Ernst Happel stadium in Vienna.    AFP PHOTO / JOE KLAMAR    -- MOBILE SERVICES OUT --  (Photo credit should read JOE KLAMAR/AFP/Getty Images)
Wachezaji wa timu ya taifa ya Ujerumani toka shoto Christoph Metzelder, Michael Ballack na Thomas Hitzlsperger wakiwapungia mashabiki baada ya mchezo wao kumalizika jana dhidi ya Austria na kushinda goli 1-0.

Michael Ballack ndiye aliyefanya booking ya Ujerumani kwenye nafasi ya Robo fainali kwa shuti safi kipimo iliyopatikana kwa mpira wa adhabu ikiwa ni dakika ya 49 ya mchezo mara tu baada ya kipindi cha pili kuanza na kuwanyamazisha kabisa wenyeji Austria katika mchezo wa mwisho wa kundi B.

Mchezaji huyu wa Klabu ya Chelsea ambaye mapema jana alilalamika kuwa hafurahii kiwango alichoonyesha kwenye michuano hii aligeuka ghafla na kuwa mwiba wa sumu kwa Austria.

Austria ambao nao walipoteza mchezo mmoja a kutoka droo mmoja walikuwa wanategemea ushindi wa jana na kuombea mabaya mchezo wa Poland na Croatia ili wajihakikishie nafasi ya Robo fainali lakini bahati haikuwa yao jana.

Ballack anakwenda kukutana na Kocha wake mpya kwa klabu ya Chelsea Philipe Scolari kwenye mchezo wa Robo Fainali kati yao na Portugal mchezo ambao mashabiki wanaungoja kwa hamu. Luiz Felipe Scolari, ndiye ataifundisha Chelsea kuanzia msimu huu na atajiunga na Klabu hiyo mara baada ya michuano hii kumalizika.

Ujerumani wanabahati mbaya kwani hawatakuwa pamoja na Kocha wao kwenye chumba cha kubadilishia nguo na wala benchi huko Basel’s St Jakob-Park siku ya alhamisi ambapo watamenyana na Portugal, baada ya kutolewa nje mechi ya jana baada ya kutupiana maneno na mwenzie na maofisa wa UEFA. Mpaka mwisho wa mchezo Austria 0-1 Germany.

Sheria ni msumemo…

German coach Joachim Loew (L) speaks with Austrian coach Josef Hickersberger (R) after being ordered out of the field during the Euro 2008 Championships Group B football match Austria vs. Germany on June 16, 2008 at Ernst Happel stadium in Vienna.   AFP PHOTO / OLIVER LANG   -- MOBILE SERVICES OUT --    (Photo credit should read OLIVER LANG/AFP/Getty Images)
Kocha wa Ujerumani Joachim Loew (L) akiongea na Kocha wa Austria Josef Hickersberger (R) baada ya kutakiwa kutoka nje ya uwanja katika mchezo baina ya Timu zao jana.

Do or Die ya Ufaransa Leo

French forward Thierry Henry reacts after missing a goal opportunity during their Euro 2008 Championships Group C football match vs the Netherlands in Bern, Switzerland, last week which Holland won 4-1. France go into their do or die clash with Italy beset by doubt, reports of internal strife and player fatigue.

Mshambuliaji wa Ufaransa Thierry Henry akihudhunika baada ya kukosa bao katika mchezo wao na Netherland wiki ilopita ambapo waliloweshwa 4-1, Ufaransa wanakutana na Italy katika mchezo wa Kundi C ambapo kama wakifungwa basi watakuwa wmeaga mashindano haya. kwani kundi hilo linaongozwa na Netherland ambao wana Pointi 6 mpaka sasa kwa kushinda michezo yao miwili kwa jumla ya mabao 7, na kufuatiwa na Romania ambao wana pointi 2 kwa kutoka sare mara mbili na Itally ana pointi moja kwa sare yake na Romania na Ufaransa ambaye ameoteza mchezo mmoja na kutoka sare mmoja katika mchezo wa Kundi C.

Croatia haoooo Robo fainali

Poland 0-1 Croatia
Croatian midfielder Nikola Pokrivac (R) walks on the pitch with a ball under his jersey next to Polish defender Adam Kokoszka after the Euro 2008 Group B football match Poland vs. Croatia on June 16, 2008 at the Woerthersee Stadium in Klagenfurt, Austria. Croatia beat Poland 1-0 here on Monday in their final Euro 2008 Group B match here on Monday.   AFP PHOTO / DDP - RONNY HARTMANN  -- MOBILE SERVICES OUT --    (Photo credit should read RONNY HARTMANN/AFP/Getty Images)
Mchezaji wa Croatian Nikola Pokrivac (R) akitembea huku ameweka mpira tumboni baada ya kuifunga Poland kwenye mchezo wa jana wa Kundi B. anayemuangalia ni Mchezaji wa Poland Adam Kokoszka.

Goli lililofungwa na Ivan Klasnic katika dakika ya 52 ya kipindi cha pili liliwafanya Croatia kumaliza mechi zake zote tatu toka kundi B kwa ushindi. Croatia ambao awali waliifunga Australia 1-0, wakaifunga Germany 2-1, na jana wameifunga Poland 1-0, matokeo yaliyowapeleka moja kwa moja Robo Fainali ambapo watakutana na Mshindi wa pili wa Kundi A ambaye ni Turkey.

Ndoto ya Poland kufika mbali haikuweza kufanikiwa kwani waliihitaji kushinda mchezo huu na pia hata kushinda kwao kulitegemeana na matokeo kati ya mchezo wa Australia na Germany ambapo Australia alikuwa ame droo mara moja na na kuwa na point 1 na Germany alishinda mara moja dhidi ya Poland na kuwa na Point tatu. na Poland ame droo mara moja na kuwa na point 1 ambapo kama angeshinda jana basi angefikisha point 4 na kama Australia na Germany wangetoka Droo pia Germany angekuwa na Point 4 ambapo labda wangezidiana magoli.

Fans of the national soccer team of Croatia celebrate Croatia's 1-0 win over Poland in the EURO 2008 soccer match in the city center of Frankfurt, central Germany, on Monday, June 16, 2008.

Mashabiki wa Croatia mitaani

Hata hivyo mchezo wa jana ambao kila timu ilihitaji kushinda ulikuwa mzuri kwa kila timu kuonyesha mashambulizi ya hapa na pale na huku Poland wakionyesha dhahiri kukamia ushindi ila bahati haikuwa yao.

Turkey ambaye alipoteza mchezo wake na Portugal katika kundi A anakibarua kigumu akija kukutana na Croatia ambao wao kwao ushindi ndio nguzo yao na wanacheza kwa kujiamini dakika zote. Tungoje tuone.

KELLY ROWLAND NDANI YA BONGO

Bila shaka utakuwa bado unalikumbuka kundi maarufu la muziki lililokuwa linajulikana kama Destiny’s Child kutoka nchini Marekani. Miongoni mwa mabinti waliokuwa wanaunda kundi hilo ni Kelly Rowland(pichani).Wenzake walikuwa ni Beyonce Knowles(mke wa Jay Z hivi sasa) na Michelle Williams. Kundi hilo lilivunjika rasmi mwaka 2005 ingawa mara moja moja bado huwa inatokea wakafanya maonyesho pamoja. Bonngo Celebrity wameiweka kwa mapana zaidi

Miss Tanzania UK kapatikana


MISS TANZANIA 2008 UK!

Kimwana Tusekile Mwakibinga alitawazwa rasmi juzi kuwa Miss Tanzania Uk 2008 kwenye sherehe zilizofanyika ndani ya Silver Spoon New Light Complex karibu na wembley Stadium.Pichani Miss Tanzania Uk 2008 Tusekile Mwakibinga akiwa katika picha ya pamoja na First Runner Up Miss. Jacqui Majebele(kushoto) na Second Runner up Miss. Alice Kapya.

Washiriki na washindi wa shindano la Miss Tanzania Uk 2008 wakiongozwa na Miss Tanzania Uk 200 Tusekile Mwakimbinga wakiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Uingereza Hon Mwainda Maajar.

Washiriki wakijinadi mbele ya majaji

Mshiriki wa Big Brother Africa 2008 kutoka Tanzania Richard Bezuidenhout (kulia)nae alikuwepo Miss Tanzania Uk 2008

Mwenyekiti wa Kamati ya Miss Tanzania Hashim Lundenga (Kulia)nae alikuwepo kwenye shindano la Miss Tanzania Uk 2008. Picha na Habari zote kwa hisani kubwa kabisa ya Blog ya Haki Ngowi, Bonyeza Hapa kupata Picha Zaidi

Monday, June 16, 2008

Akudo Impact kupekecha na Miss Sinza

BENDI maarufu ya muziki wa dansi nchini ya Akudo Impact ‘Wazee wa Masauti’ wataongoza burudani katika mashindano ya kumsaka mrembo wa kitongoji cha Sinza Ijumaa kwenye Ukumbi wa Vatican City, Sinza.

Akudo kwa sasa ambayo inakubalika na mashabiki wengi wa muziki wa dansi inatamba na wimbo wa Binadamu� huku nyota ya rapa na muimbaji wake, Christian Bella ikiendelea kung’ara zaidi.

Mratibu wa mashindano hayo, Somoe Ng’itu alisema jana kwamba tayari kwa takribani wiki mbili sasa wanamuziki wa bendi hiyo walikuwa wakifanya mazoezi kwa ajili ya mashindano hayo.

Somoe alimtaja msanii wa kizazi kipya, Kassim Mponda Cassim anayetamba na Siamini na Awena na kwa upande wa muziki wa asili ni Mrisho Mpoto anayefanya vizuri katika nyimbo mbalimbali ukiwamo Mjomba alioshirikishwa pamoja na Wanne Star ambaye ni maarufu kwa kucheza na nyoka katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati.

Tumeamua kuchanganya burudani ili kila mtu apate anachotaka japo kikubwa watu wataona pia burudani ya kutosha kutoka kwa warembo bomba, alisema.

Wadhamini kadhaa wamejitokeza kudhamini shindano hilo ni pamoja na Mama Tike Hair Fashions, Redds, Multchoice Tanzania, Vannedrick (T) Ltd, 2080 Fashions, Break Point, Coca Cola, Vodacom, gazeti la Tanzania Daima na Clouds FM 88.4.

Msondo usipime!!

Bendi ya Msondo Music usiku wa kuamkia leo ilifanya makamuzi ya kufa mtu katika Ukumbi wa Africentre uliopo Ilala jijini Dar es Salaam, kama kawaida yake, naye mnenguaji mwenye mbwembwe wa bendi hiyo Nacho Said, eikeiei Mama Nzawisa, alianza mbwembwe hizo kama ifuatavyo. Pichani Mama Nzawisa akimpelekesha puta jukwaani mwamuziki wa bendi hiyo Roman Mng’ande ‘Romario. Picha na Richard Bukos wa GPL

Etoo kazuliwa kijambo!!

Pichani Samuel Etoo katika picha ianyosemekana alitoroka kambia na kulia ni dada aliyekuwa naye.

Kama kawaida kwenye wengi kuna mengi, Timu ya Taifa ya Kameroon ilikuwa Tanzania kucheza na Taifa Stars katika mchezo wa awali wa kuwania tiketi ya Kombe la Dunia, Ikiwa imekwenda na Wachezaji wake mahiri kama Samuel Etoo na Song iliambulia Sare na Taifa Stars, Je wajua kilichotokea nyuma ya pazia kwa Striker wa Kameroon Samuel Etoo? Gonga hapa uisome!!

Karibu Malaysia!!

Selamat Datang Ke Malaysia, Hikli tangazo limo ndani ya Train ya Umeme sasa OLE wako!! Hii ndio Malaysia!. Hahaha Denda maana yake ni Adhabu!!, (USd 1=3.2 RM-Malaysian Ringit)

Turkey yawafungisha virago Czech

Turkey 3 – 2 Czech
Young Enes, a supporter of the Turkish national soccer team, is reflected in the roof a car as he celebrates the victory of his team after the Euro 2008 soccer match between Turkey and Czech Republic on the streets of the district Kreuzberg in Berlin, on Sunday, June 15, 2008.
Mashabiki wa Turkey wakiwa mitaani

Nihat Kahveci ndiye aliyekuwa nyota wa mchezo wa jana kwa kufunga magoli mawili dhidi ya matatu ambayo Turkey walishinda na kuwafungisha Virago Jamhuri ya Czech kwenye mchezo wa fainali wa undi A jijini Geneva.

Kwa ushindi huo Turkey wamejihakikishia nafasi ya pili ya kundi A kwa kufikisha Point 6 kama Portugal baada ya kushinda mchezo wake wa mwanzo dhidi ya Switzerland kwenye mchezo wa ufunguzi.

Mpaka dakika wa 62 Czech walikuwa wakiongoza kwa 2-0 mabao yaliyofungwa na Jan Koller dakika ya 34 na Jaroslav Plasil dakika ya 62.

Turkey ambao walibadilika kabisa hasa dakika 25 za mwisho za mchezo iliwachukua hizo hizo dakika 25 kupachika mabao matatu yaliyowapa ushindi.

Mabao ya Czech yalifungwa dakika ya 75 na Arda Turan (75), dakika ya 87 na Nihat Kahveci (87) na la tatu dakika ya 89 na Nihat Kahveci (89). na kuwanyong’onyeza kabisa mashabiki wa Czech ambao walikuwa wakiishangilia kwa nguvu timu yao na kujua wameshinda mchezo huo.

Kwa ushindi huo Turkey wanaungana na wenzao Portugal kwenye hatua ya Robo Fainali ambapo Turkey watapambana na mshindi wa kundi B.

Switzerland yazizima Mbwembwe za Portugal

Switzerland 2 – 0 Portugal
Swiss forward Eren Derdiyok 9top0 vies with Portuguese defender Pepe during the Euro 2008 Championships Group A football match Switzerland vs. Portugal on June 15, 2008 at Jakob-Park stadium in Basel.  AFP PHOTO / DANIEL MIHAILESCU  -- MOBILE SERVICES OUT -- (Photo credit should read DANIEL MIHAILESCU/AFP/Getty Images)
Forward wa Swiss Eren Derdiyok akiwa kwenye heka heka na na na beki wa Portugal Pepe wakati wa mchezo wa Kundi A ambapo Swiss waliibuka washindi kwa 2-0.

Magoli mawili yaliyofungwa na Hakan Yakin dakika ya 71 na 83 ndio yaliyowakosesha raha mashabiki wa Portugal (nikiwemo mimi), na kuipa ushindi Switzerland wa 2-0 dhidi ya Portugal.
Ushindi huo umewasaidia waandaaji hao angalao kuambulia ushindi na kwao ni ushindi mwanana kwani wameifunga na kuishinda timu ambayo haijapoteza mchezo hata mmoja tangu mashindano haya yaanze.

Pamoja na kichapo hicho Portugal wanakwenda Robo fainali kama washindi wa kundi A na Swiss wamejikongoja baada ya kupoteza michezo yao yote miwili ya awali hivyo ushindi wa jana umefanya wafikishe pointi 3 pekee.
Yakin alifunga bao la kwanza baada ya pasi toka kwa Eren Derdiyok ikiwa ni dakika ya 71 ya mchezo na kuachia shuti toka umbali kama wa yadi 15, shuti lililopita tobo golikipa wa Portugal na kuandika goli la kwanza.

Dakika 12 baadaye Yakin aliifungia timu yake goli la pili kwa njia ya Penati.
Portugal wanacheza Jumamosi hii na mshindi wa pili wa kundi B.

Sunday, June 15, 2008

Klynn

Anaitwa Klynn, Miss, Mwanamitindo na Mwanamuziki, mtembelee kwenye wavuti wake kwa kubofya hapa au waweza Tembelee 8020 uone Wadrobe yake na Mamaa Zeze.
Nawaacha na Video yake ya Crazy Over You…… Jumapili Njema,
Papaa Pius

Mke wa Snoop Dogg Mbaroni kwa kuendesha akiwa amelewa

Habari zinapasha kuwa mke wa Mwanamuziki Snoop Dogg alikamatwa na Police huko Calfornia kwa kosa la kuendesha gari huku amelewa.
Luteni Craig Brower alisema maofisa wake walimsimamisha Shante au Shahn-taye (32) pichani kulia (Picha iliyotolewa na Police baada ya kukamatwa) majira ya saa sita na robo usiku wa jana jumamosi huko Sherman Oaks na wakamchukua na kumtupa lupango lakini baadaye jana hiyo hiyo aliachiwa kwa dhamana lakini atafikishwa kortini.
Maofisa wa polisi walisema kuwa MNkwe wa mwanamuziki huyo alikuwa peke yake kwenye gari,.Snoop na mkewe wana miaka 11 ndani ya ndoa yao na wana watoto watatu.

Jioni ya “KHANGALICIOUS” June 20

Mustafa Hassanali Juni 20,2008 atafanya onyesho kubwa la mavazi yanayotokana na Khanga. Maonyesho hayo yatafanyika katika hoteli ya kitalii ya Moevenpick Royal Palm na yamepewa jina la “KHANGALICIOUS”,Kwa maneno yake mwenyewe onyesho hilo limelenga kutunza umaarufu wa vazi la khanga ambao umetamba katika mwambao wa Afrika Mashariki kwa miaka mingi.

Miss Ubungo 2008 huyu hapa

Miss Ubungo Amatha Chrispin (katikati) akipunga mkono kufurahia taji hilo (kulia) kwake ni mshindi wa pili wa taji hilo, Ansia Kweka, na Rahma Gege. Picha na Issa Mnally.

Jk Boys waliowatoa Kamasi Cameroon

Picha hii iliyopigwa na Global Publishers Inaonyesha wachezaji wa Taifa Stars wakiomba Dua kabla ya mechi yao na Cameroon jana, Sala ambayo kwa kwa kiasi kikubwa ilisaidia na Mungu akajalia kukinga kifua.

Kikosi cha Taifa Stara – JK Boys kilichoumana na Cameroon hapo jana, waliosimama nyuma toka kulia ni Dan Mruanda, Nadir Haroub ‘Canavaro’ (kipenzi cha Maximo), Athumani Iddi ‘Chuji’, Shaaban Nditi na Salum Swedi. kati toka kushoto ni Nizar Khalfani, Shadrack Nsajigwa, Godfrey Bonny, Mrisho Ngassa na Amiri Maftaha. mbele ni Ivo Mapunda –Tanzania One, Picha na Mpoki Bukuku

Keeping Up With the Kardashians mitaani Monaco

Wakiwasili sehemu ya mapumziko ya Hotel

Wakila boti ku zunguka baharini kidogo!

Mtu na nduguye Kim na Kourtney Kardashian ndani ya Ferrari mitaani Monaco

Mitaani
Kwa waangaliaji wa E! Channel mdada huyu si mgeni kwenye Reality show ya Keeping Up With the Kardashians, Kila mwanaume aulizwapo mdada gani humvutia basi atamtaja Kim Kardashian na kweli huwatoa udenda wakware si kitoto, kwani ana vituko vya makusudi hasa, Hivi karibuni kamera za mapaparazi zilimnasa akila maraha huko Monaco(pichani) akiwa na dada yake Kourtney Kardashian. Pata picha na habari zaidi za mwanadada huyu kwa kubofya Website yake ambapo yeye mwenyewe huandika kila kitu anachokifanya kila siku!.

Saturday, June 14, 2008

Villa aibeba tena Spain dhidi ya Sweden

Spain 2 – 1 Sweden
Wachezaji wa Spain wakimpongeza Villa mara baada ya kupachika bao la pili huku mashabiki wa Sweden wakiangalia kwa uchungu.
Goli lililofungwa na David Villa dakika ya 90 limewapa Spain ushindi wa 2-1 dhidi ya Sweden katika mechi ya mashindano ya EURO kundi la D. Spain waliongoza kwa kupata goli katika dakika 15 ya mchezo toka wa Fernando Tores lakini Sweden walijitahidi na kufanikiwa kurudisha goli hilo katika dakika ya 34 ya mchezo kipindi cha kwanza kupitia kwa Zlatan Ibrahimovic ambaye alipachika mpira huo kimiani. Dakika ya 90 mwishoni mchezaji mahiri na matata Villa aliipatia Spain goli la ushindi na hili kuwa ni goli lake la nne tokea mashindano haya yaanze.
Mpaka sasa Spain wamefanikiwa kufikisha pointi 6 na Sweden 3. Greece ambao ni mabingwa watetezi wanacheza na Rushia usiku huu huko Salzburg.

Zali, Jezi ya Etoo

Kijana mdogo wa Kikosi cha kuokota mpira uwanja wa Taifa akiwa amevaa Fulana ya mchezaji wa Cameroon Samuel Etoo, Kijana huyu aliamua kuivaa Fulana hiyo baada ya kuona dalili za kunyang’wanywa na wababe. Hii ni baada ya mechi kati ya Taifa Stars na Cameroon ambapo Stars waliilazimisha sare ya 0-0.
Picha na Mpoki Bukuku.

Malawi yaichapa Egypty 1-0

MABINGWA wa Afrika, Misri wamepata mshtuko baada ya kupata kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa Malawi mjini Blantyre.

Katika mchezo huo wa jana wa kufuzu kucheza fainali za Kombe la Dunia na Mataifa ya Afrika mwaka 2010, Misri iliamini mchezo huo ungeisha suluhu.

Misri, ambayo inafundishwa na Hassan Shehata ilifungwa bao hilo pekee ndani ya dakika tatu za majeruhi, ambalo lilifungwa na Chiukepo Msowoya wa Malawi.

Katika mchezo mwingine, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo iliifunga Djibout mabao 6-0 katika mchezo uliofanyika juzi.

Kwenye mchezo mwingine jana, Tembo wa Ivory Coast walilazimishwa sare nyingine walipocheza na Botswana.

Dipsy Selolwane aliipa Botswana bao la kuongoza dakika ya 25 mjini Gaborone na kuwafanya Ivory Coast wasubiri mpaka dakika ya 64 kusawazisha bao kupitia kwa Kanga Akale.

Ni mara ya pili kwa Ivory Coast ambao walicheza bila Didier Drogba kutoka sare ndani ya mwezi huu kwani wiki iliyopita walibanwa na kutoka suluhu na Madagascar.

Taifa Stars yailazimisha Sare Cameroon

Taifa Stars 0 – 0 Cameroon
Picha na Mpoki Bukuku habari na Mwananchi


Haya huyu jamaa rigobert Song aliamua kuwafanyizia vijana kwa kuwachezea faulo za nguvu imagine hapa anamfanyizia Amir maftah!

Hakutosheka akaamua kumweka kipepsi Athumani Idd, jamani vijana wanatisha tuache kuwakatisha tamaa!

Msajigwa leo katisha katika mechi kafanya mambo kichizi kawachanganya wacameroon!

Jamaa hapa alipita mpira ukabaki yaani ilikuw amsalie Mtume kama tungekuwa na wafungaji wazuri jamaa wangekoma.


Mchezo kati ya Taifa Stars na Cameroon umemalizika jioni hii katika uwanja wa Taifa kwa Timu hizo kutoka droo ya bila kufungana.

Katika mchezo huo ambao Taifa Stars walionyesha kuumudu vilivyo kutokana na Timu hiyo kuipa Upinzani wa hali ya juu timu ya Cameroon ambayo kila mmoja aliipa nafasi ya ushindi.

Viungo wa Stars; Athuman Idd, Geofrey Bonny, Shaabani Nditi na Nizar Khalfan walifanya kazi kubwa kutibua mipango ya Cameroon.

Ingawa Stars walipiga mashuti matatu tu langoni mwa Cameroon, lakini yalikuwa ya hatari na hasa kama Danny Mrwanda ambaye aliwasumbua sana angetulia.

Dakika ya 13, Mrwanda alikosa bao baada ya kutengenezewa pasi nzuri na Athuman Idd lakini mpira huo uliondoshwa na Rigobert Song ambaye baadaye alionekana kuhamaki kutokana na kasi ya Danny Mrwanda na Mrisho Ngassa.

Kama Ulaya!!!! Golikipa wa Taifa Stars Ivo Mapunda akiondoa hatari golini mwa Taifa Stars, Katika mchezo wa Leo ambapo naye aliwakatisha tamaa Wa Cameroon mara kadhaa

Cameroon, ambao walionekana kucharuka kuanzia dakika ya 20, walipata kona tatu mfululizo ambazo hazikuwa na madhara kwani Mapunda alipangua kichwa cha Eto’o na mabeki wakafanya kazi kubwa kuondoa kona nyingine zilizokuwa zinapigwa na

Njitap.

Matumaini ya mashabiki wa soka yalikuwa makubwa baada ya kuona Cameroon ikikubali kwenda suluhu mpaka wakati wa mapumziko huku Ngassa na Mrwanda wakionekana tishio.

Kipindi cha pili kilikuwa kizuri zaidi kwa Stars kwani walionana kwa muda mwingi na kukaba vizuri huku sehemu ya kiungo ikimiliki vizuri.

Mabeki wa Stars, Shadrack Nsajigwa, Salum Sued, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ na Amir Maftah walifanya kazi nzuri ya kuwadhibiti Eto’o, Achille Webo na Jean Makoun ambao hawakuleta madhara licha ya kuonekana hatari kila walipogusa mipira.

Mwamuzi bora Afrika, Bonaventure Kofi Kodjia wa Benin alilalamikiwa na mashabiki kwa kushindwa kutoa penalti wakati Mrwanda alipoangushwa eneo la hatari na Andrey Bikey dakika ya 75 wakati akienda kumuona kipa Idrissa Kameni dakika ya 75.

Dakika kumi za mwisho, Mrwanda alionekana kuwa tishio lakini alishindwa kuzitumia nafasi, huku Cameroon wakionekana kuhamaki kutokana na kushindwa kwenda sawia na kasi ya Stars.

Maximo aliwatoa Nizar na Athuman Idd na kuwaingiza Abdi Kassim pengine kwa kutaka mashuti ya mbali na Kigi Makasi kwa lengo la kutaka kuimarisha upande wa kushoto kama ambavyo Maximo amewahi kusema siku za nyuma.

Stars: Ivo Mapunda, Shadrack Nsajigwa, Amir Maftah, Salum Sued, Nadir Haroub, Geofrey Bonny, Shaaban Nditi, Athuman Idd/Kigi Makasi, Danny Mrwanda, Nizar Khalifan/Abdi Kassim na Mrisho Ngassa. Leo ni Mauritius na Cape Verde.

Watoto wa Mitaani na Bendi yao

Wiki iliyopita niliandika habari ya Vijana wa Ifakara wanaoburudisha watu na kuelimisha kuhusu janga la Ukimwi (Bofya hapa usome tena) , kutokana na vifaa duni wanavyo tumia nashukuru Mdau mmoja msomaji wa Blog hii toka Japan anafanya mipango ya kuwapatia vyombo vya muziki vijana hao na mambo yakikamilika tutawaletea habari kamili, Wiki hii tunakutana na vijana wa Mitaani ambao waliamua kuanzisha Bendi yao katika kujitafutia lizki na kutumbuiza mitaani jijini Dar es SalaamVijana hawa walinaswa na Kamera ya Global Publishers hivi karibuni maeneo ya Soko kuu la Kariakoo jijini Dar es Salaam wakiburudisha watu kwa kuwapigia muziki ili kujipatia chochote. Vijana kama hawa wanatakiwa wapewe msaada na kuendelezwa.

Sanaa na wasanii

kivazi.jpg
Picha hii ya Bob Sankofe inaonyesha Vijana wa Zawose ni matata sana. Cheki hawa jamaa vivazi vyao. Hivi vivazi ni zaidi ya vivazi, ni vyombo vya muziki pia. Jamaa wakiruka juu na kurudi chini vivazi hivi vinatoa mlio fulani murua sana, lakini inabidi uwe na sikio la kimuziki kuweza kutumia ala hii la sivyo ukipewa kama huna hicho kipaji utaishia kuharibu muziki mzima kwa kukosa kitu wataalamu wanaita ‘tempo’ au mwendokasi wa muziki. Mzee wangu Edwin Mikongoti anampenda sana Zawose, Heshima kwako.

Mabondia wa Tanzania Mbaroni Mauritius kwa Madawa ya Kulevya

Breaking News!!!! wabongo sita, wakiwemo mabondia wanne, inasemekana wametiwa mbaroni huko mauritius leo asubuhi kwa kile kilichoelezwa kukutwa na madawa ya kulevya.

Isome zaidi kwa Issa Michuzi

Patchou Lumiere, Nyota mpya ya kizazi kipya cha Kongo

kila siku kuna sauti mpya, wimbo mpya, mwanamuziki mpya, Hivi karibuni kundi la Rhumba la Muziki lilifanya rekodi ya albamu yake chini ya Kiongozi Pitshou Lumiere na mwanamuziki huyu anasemekana kutumia pesa nyimngi katika kutengeneza Video za Nyimbo za Albamu yake, kwa sasa Koffi Olomide anatajwa kuwa ndiye Mwanamuziki wa Zaire ambaye hutumia pesa nyingi katika kutengeneza Video za nyimbo zake ikiwa ni kuanzia Kampuni ya Utengenezaji, Mavazi na sehemu anazotengenezea Video hizo, lakini Video za Muziki za Pitshou zilipigwa kwa mbwembwe kama picha zinavyoonyesha.
Kava la juu la CD ya Bendi ya Rhumba la Muzika
Kiongozi Pitchou Lurmiere akiwa kwenye shooting ya wimbo wa Chez Ntemba

Mbwembwe za Pitshou wakati wa shooting ya wimbo wa Moise Katumbi unaopatikana kwenye Albamu hiyo.

Vimwana wakiwa wamekula pozi wakati wa shooting ya wimbo wa Chez Ntemba kwenye albamu ya kundi la Rhumba la Muzika.
Lumiere akiwa na Vimwana katika moja ya vibwagizo vya nyimbo zake.

Wanamuziki wa Kongo katika suala la burudani ya muziki wa dansi wamepiga hatua, hivi karibuni mjadala wa kuhusu kitendo cha kundi la TOT Respect chini ya uongozi wa Kamarade Ali Choki kwenda Kongo kutafuta wanamuziki kwa ajili ya kuipa nguvu kikosi chake lilipigiwa kelele na wengi wakaonyesha kuwa ni kuua na kutothamini muziki wetu, lakini katika dunia ya leo ya utandawazi ambapo kimsingi hakuna mipaka kila mmoja anajaribu kuangalii kama si unafuu basi kiwango katika kukamilisha liziko la nafsi (satisfaction). Je ni kweli kuna haja ya kufanyiwa mabadiliko muziki wetu? Kwani tumeona jinsi bendi zilnazopiga muziki wetu kuchanganya na Rhumba ya Congo kama Twanga Pepeta zinavyofanikiwa.

JB Mpiana: Fally, Celeo, Ferre i kizazi cha nne si cha tano.

JB Mpiana Bin Adam Tshituka Papa Cherry

Jumatatu ya Wiki hii mtangazaji wa kituo cha Clouds FM Sophia Kessy kupitia kipindi chake mwanana cha Afrika Bambataa alifanya mahojiano na Mwanamuziki toka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo toka kundi la Wenge BCBG, JB Mpiana Bin Adam Tshituka Papa Cherry.

1. vipi amefikia wapi kuhusu kutoa albam na werasoin

kuhusu kutoa nyimbo na werasoine ni kweli lakini kwa sasa tumeanza na sigle ya publicity na tutakapo maliza tutafanya kazi nzuri kwa sababu ni gharama sana kufanya kazi hii.

2. unaongeleaje kuhusu kumeguka kwa bendi yako hasa kwa watu kama akina alen mpela ambae inasemekana hata kwenye onyesho lako la hivi karibuni hakuwapo?

kuhusu kutoka kwa vijana ni kawaida ni sawa na baba mwenye watoto wanapo kuwa wakubwa huamua kutoka kujitafutia maisha yao , mimi binafsi nimefurahi kwa hilo kuona kuwa wanaweza kujitegemea sasa sina tatizo juu ya hilo nawaombea kwakuwa wakinufaika, pia ni sifa kwangu kwakuwa wametoka kwangu na hata kama hawata fanikiwa wakiona mambo yanaenda vibaya wakiomba kurudi nitawapokea ni wangu sitawatupa.

Sofia Kessy wa Clouds Fm, Afrikan Bambataa

3. muziki nu burudani kwanini mnakuwa na uaduni na mtu kama werason mpaka wapenzi wenu wanakuwa wanaumizana na hii imekuwa ikitokea mara kwa mara

ni ngumu kumtuma mashabiki kuwafanya wagombane akili tunayo itumia katika kazi ndio inayo wapelekea wao kutoelewana kila mtu anamuona mwenzie ni bora zaidi na kila msahabikianaamua kuvutia upande wake. ndio maana unaona kwa sasa kongo kuna chama kinaitwa MAISHA PARK, ambapo ukigundulika umegombana na mwezio basi wanakuiteni na kuwapatanisha lakini pia wanashauri kutogombana, ni baya kutukanana, na hii ndio inaleta umoja sasa katika muziki maisha park, ugomvi sikuzote unarudisha muziki nyuma.

4.unazungumziaje ujio wa wanamuziki chipukizi kama Fally Ipupa, Celeo scam, Ferre Gola ambao kwa kiasi kikubwawanaubadili muziki wa kongona kusemwa kuwa ndio kizazi kipya cha tano baada ya kizazi chanu cha nne.

kwanza ni vijana na wananfanya kazi vizuri, ninacho washauri mimi ni kuwa wawe na adabu, mungu atawasaidia lakini kuna jambo moja nataka kusema kuweka wazi kuwa zamani watu walituita wenge kizazi cha nne kwasababu hatukutoka katika bendi yoyote kongo tuliibuka tu tulikutana tukaunda kikundi chetu wenyewe tukiamini kila mmoja anaweza tulitoka nyumbani kwa kifupi, sio jibe katoka kwa zaiko, au wera katoka kwa tabu lay, sio blaiz bula katoka kwa papa wemba hapana sisis wote tulitoka nyumbani tukaunda kundi letu la wenge na ndio maana tulikubalika na wakatuita kizazi cha nne lakini kuhusu fally na ferre na tutu kaluji, na celeo scam,hawa ni kizazi cha nne kwasababu kuitwa kizazi cha tano sio kweli kwasababu wanamuziki hao wametoka kwangu na kwa kofi na kwa wera, na bendi walizotoka ni kizazi cha nne hivyo watu waelewe si kizazi cha tano bali ni cha nne na kizazi cha tano ni kizazi ambacho hakijajulikana kwenye bendi yoyote.

Pamoja na mambo mengine aliulizwa kuhusu chakula anachopendeleani mchicha, samaki, na wali maharage, pia aliulizwa timu anayoipendelea na kusema ni Brazil

JB Mpiana aliweka bayana kuwa anawatoto 7 wasichana wawili wavulana wa tano wa kwanza miaka 19 wa pili miaka 17 wa tatu miaka 15 wa nne miaka 14 wa tato miaka 12 wa sita miaka 10 na wasaba miaka 9

kuhusu kuja tanzania ni muda wowowte yupo tayari mara baada ya manager wake kumpa ushauri wa kufanya hivo.

Mji wa Bern ni rangi ya chungwa tupu!!

Mashabiki wa Holland wakiwa mitaani wakisherehekea ushindi dhidi ya Ufaransa, Mashabiki wa Holland ambao wanaongoza kwa staili yao ya ushangiliaji na mavazi ya rangi ya chungwa wamejaa na wanazidi kumiminika mjini Bern ambapo ndio kituo cha Timu yao, mji mzima umekuwa rangi ya Chungwa.

Ufaransa Mbendembende kwa Holland


Uholanzi 4 – 1 Ufaransa

MDutch Andre Ooijer (L) akiubeba mpira langoni mwa Ufaransa baada ya Dirk Kuyt kupachika bao la kwanza dakika ya nane ya mchezo katika mchezo wa kundi C.
Uholanzi jana walifanya maajabu kwa mara ya pili tena baada ya kuitandika bila huruma Ufaransa kwa 4-1 na kujihakikishia nafasi ya kucheza robo fainali huku wakiwafungisha Wafaransa virago katika michuano hiyo.

Dirk Kuyt ndiye aliyefungua karamu ya magoli kwa Waholanzi na baadaye kufuatiwa na Robin van Persie, Arjen Robben na Wesley Sneijder. huku goli pekee la Ufaransa lilifungwa na Thiery Henry. Kipondo hiki ni muendelezo wa kipondo kama hicho walichompa Italy jumatatu.

Mshabiki wa Ufaransa akiwa amelowa majonzi kwa kutoamini macho yake baada ya timu yake kula kichapo cha 4-1.

Ufaransa wanakutana na Italy jumanne ijayo ambapo wote wanawania kijinafasi lakini nafsi yao inategemeana na matokeo ya mchezo kati ya Romania na Uholanzi ambap Romania inashika nafasi ya pili katika kundi hilo, kwani Romania ikiishinda Holand itakuwa na nafasi hiyo hiyo ya pili. Wadatch wameweka historia kwa kuzichapa timu mbili ambazo zilicheza Fainali ya kombe la dunia 2006 kwa jumla ya mabao 7.

Italy yajitutumua kwa Sare

Italy 1 – 1 RomaniaMchezaji wa Romania Muttu shoto akipiga penati ambayo golikipa wa Itali aliicheza kwenye mchezo wao wa Jana.

Italy imeponea chupu chupu kupata kichapo jana baada ya kudumisha sare ya 1-1 na Romania, Sala za waitaliano zilisikika pale Romania walipopata penati na Golikipa wa Italy Gianluigi Buffon akaicheza.

Straika wa Fiorentina Adrian Mutu ndiye aliyefungua mlango kwa kuipachikia Romania goli la kwanza dakika ya 55. Lakini goli hilo lilidumu kwa dakika moja tu waitaliano wakasawazisha kupitia kwa Christian Panucci.
Matokeo ya Droo angalao yamewapunguzia machungu Italy ambao bado wanakidonda cha kichapo cha 3-0 walichochapwa na Holland ambao wanaonyesha makali kwenye kundi hilo la C.

Romania walipata penati dakika 5 kabla ya mchezo kumalizika baada ya Panucci kumchezea madhambi Daniel Niculae ambayo kwa kiwango kikubwa iliwanyong’onyeza Italy na washabiki wao na Romania walimchagua Mutu kupiga penati hiyo ambayo aliipiga kiufundi iende kwenye post lakini kipa Buffon wa Italy aliicheza na kusababisha mayowe toka kwa mashabiki wao ambao walikuwa wameshakata tamaa.

Kwa matokeo haya Italy inatakiwa ishinde mechi yake ijayo na Ufaransa ili waweze kujihakikishia kusonga mbele.

Waitaliano jana walilalamikia maamuzi ya refa wakidai aliwabana sana wao, Refa huyo Mnorwee hasa pale alipokataa goli la Italy kwa kudai mfungaji Luka Toni alikuwa ameotea.. Mpaka mwisho wa mchezo Italy 1 – 1 Romania.

Friday, June 13, 2008

Maneno ya mwisho ya “KUNGWI”

Kocha wa Stars Maxio Maximo akipiga saikolojia kwa vijana wake homa inayowapata watzania ni kama homa ya wakati ule tulipocheza na Senegal na kuibuka kidedea, naimani mchezo wa kesho tutashinda kama tutacheza kama timu, kwa kujiamini na kujali mafunzo yaliyochanganyika na vipaji binafsi vya wachezaji wetu. Kila la heri Stars

KUMRADHI: Haha habari ndio hiyo!!

Naomba radhi kwa kushinda kuweka habari toka jana usiku hii ni kutokana a sababu ambazo zilikuwa nje ya uwezo wetu. lakini naomba mburudike na Video ya kwake AY inayoitwa Habari ndio hiyo!!

Vimwana wa Miss Dar City Centre

Pichani ni Washiriki wa shindano la Miss Dar City Center, ambo leo wamefanya kitu cha maana cha kuzuru gari lao ambalo wanashindania.Katika picha hii warembo hao wakiwa wamezunguka gari hilo. Shughuli ya kumsaka mrembo wa kitongoji hicho muhimu itafanyika Jumamosi Juni 14,2008 kwenye ukumbi wa Cine Club, jijini Dar es Salaam.

Thursday, June 12, 2008

haki miliki yawabana Ze Comedy

Kundi la ucheshi la Ze Comedy leo mchana limekilalamikia kituo cha Televisheni cha East Africa kwa kuwawekea pingamizi la kutumia staili za ucheshi walizokuwa wakitumia walipokuwa kituo hicho kama wataamua kuendelea kufanya shughuli hiyo iliyolipatia kundi hilo umaarufu mkubwa.

Kundi hilo limesema limekatazwa kutumia staili za kijotijoti, Masanja Mkandamizaji amekatazwa kutumia jina hilo na mtindo aliokuwa akiutumia, Wakuvanga amekatazwa kutumia staili ya kujiremba kama mwanamke na kutumia jina hilo wala kuigiza kama Lowassa, na waigizaji wengine wote wa kundi hilo wamepigwa top na COSOTA. Kwa kiasi kikubwa kilicholalamikiwa ni haki miliki ambapo East Africa Television wanadai kumiliki walivyovitaja.
Haya wadau mwalionaje hili?
Pata kipande cha Shoo yao hapa:-

video

Maelfu wajitokeza Kununua Tiketi za Stars na Kameruni

Na Mwananchi

MAELFU ya wapenzi wa soka jijini la Dar es Salaam wamejitokeza kununua tiketi za mechi baina ya Tanzania na Cameroon itakayofanyika kesho, huku polisi wakizuia maandamano yaliyopangwa kufanywa na chama cha siasa cha DP kupinga viingilio.

……………………..

Tiketi hizo zitauzwa kwa viingilio vya Sh 50,000 kwa V.I.P, Sh 40,000 kwa V.I.P B na Sh 20,000, Sh 10,000 na 7,000 kwa mzunguko

……………………………

na vituo vilivyopangwa kwa mauzo ya tiketi hizo ni mgahawa wa Steers, Uwanja wa Zamani wa Taifa, Zizou Fashion, hoteli ya Royal Prince na kituo cha mafuta cha Big Bon cha Kariakoo.

Pia kuna vituo vya Shule ya Sekondari ya Benjamini Mkapa, vituo vya mafuta cha Kobil na Oil Com, hoteli ya Mbezi Beach Park na Wizara ya Miundo Mbinu.

Mwananchi ilishuhudia mistari mirefu ya wapenzi wa soka wakisubiri kununua tiketi hizo zilizokuwa zikitolewa kupitia kwenye magari kuanzia saa 4.00 asubuhi huku kukiwa na ulinzi wa askari polisi wenye silaha.

“Mimi nimeridhika na utaratibu wa uuzwaji wa tiketi kwani umezingatia muda, lakini pia pongezi zangu ni kwa TFF kwa kuongeza idadi ya vituo vya kuuzia tiketi kwani umepunguza adha ya kulundikana sehemu moja kwani mimi nimekuja muda huu na nimeshapata,” alisema shabiki aliyejitambulisha kwa jina la Yassin Adballah.

Mechi hiyo itakuwa ya kuwania tiketi ya kucheza fainali za Kombe la Dunia zitakazofanyika Afrika Kusini na pia itatumika kama michuano ya awali ya Kombe la Mataifa ya Afrika, ambayo fainali zake zitafanyika Angola mwaka 2010.

Wakati mashabiki wakijazana vituoni kutaka tiketi hizo, kamishina msaidizi wa Polisi wa kanda maalumu ya Dar es salaam, Selemani Kova alisema kama DP, inayoongozwa na Mchungaji, Christopher Mtikila kama imekosa kiingilio, iangalie mpira kupitia kwenye luninga na si kufanya maandamano yasiyo rasmi.

Kova aliongeza kuwa endapo mwanachama au mtu yeyote atakaidi amri hiyo ya jeshi la polisi, hatua kali zitachukuliwa dhidi yao.

Sebene la Koffi usipime!!

Koffi Olomide anasemwa kuwa anawajali sana mastage show wake na kuna kipindi aliwahi kukorofishana an JB Mpiana kwa kuwa alimchukulia mcheza shoo wake. na ukitaka kukosana naye basi gusa stage shoo wake huwa anasafiri nao mwenyewe kwa kawaida akiwa na shoo anatangulia yeye kwenda nchi husika na akitangulia basi huenda ndege moja na vimada wake.
Gonga chini hapa uone ni kwa nini huwapenda sana hawa wacheza shoo wake, Mopao Mokonzo Sakozy!! Kuna mtu anaitwa Abuu MWenda mpenzi mkubwa wa Koffi na Big Producer Maghambo salute kwenu!!

Felipe Scolari akabidhiwa Mikoba CHELSEA

Klabu ya Chelsea imethibitisha kumchukua kocha wa timu ya Taifa ya Portugal Mbrazir Luiz Felipe Scolari kama Manager na Kocha mkuu wa timu hiyo. Mbrazir huyu ndiye aliyeonekana kuweza kurithi mikoba ya Grant darajani Stamford.

Kwa sasa kocha Scolari yuko na timu ya Taifa ya Portugal kwenye michezo ya Euro 2008, na hakutarajiwa kuweka bayana mustakabali wake mpaka mwisho wa mashindano.
Chelsea walisema kwenye taarifa yao “Chelsea Football Club inayofuraha kuwajulisha kuwa Luiz Felipe Scolari ndiye atakuwa kocha mpya wa Klabu ya Chelsea mkatabu atakaoanza kuutumikia tangu July 1, 2008. ‘Felipe ana viwango vya hali ya juu. Ni mmoja wa makocha wa renki ya juu kabisa Duniani, akiwa na rekodi nzuri ya Vilabu na Timu mbali mbali za Taifa alizofundisha. atakuja kuungana na kikosi cha wachezaji bora na wenye moyo wa kucheza mpira wenye viwango nafikiri tutakuwa na Combination nzuri.
Ni muda mzuri wa kumtangaza kocha Scolari kwani kwa sasa timu yake ya Portugal inafanya vizuri tuombe Mungu huko mbeleni na hata wachukue Kikombe, Inshallah.

Vilabu vyapigana vikumbo kwa Villa

Baada ya kuonyesha maajabu kwenye mchezo wa juzi mchezaji wa Spain David Villa ameanza kusakamwa na madalali wa wachezaji wakimtamanisha kwa donge nono ili afikirie kusajili na timu zinazowakilishwa na Maajenti hao. Habari zinapasha kuwa maajenti wa Vilabu vikubwa vywa Uingereza ndio wanaongoza kwa kutaka kufanya mazungumzo na Villa.

“Kitakuwa ni kipindi kigumu katika maisha yake kuamua anakazi kubwa lakini ni wakati mzuri kwake kwani thamani yake kwenye soko imeonekana na kila mtu yuko tayari kutoa kitika awe naye” alisema Vah Geuella ambaye ni agent wa wachezaji toka Spain.

Nyota huyo anayechezea Valencia aling’aa kwenye mchezo wa Spain na Russia jumanne ya juzi kwa kuipachikia timu yake magoli 3 kati ya manne ambayo Spain ilishinda.

Vilabu ambavyo vinamnyemelea ni pamoja na Chelsea na Arsenal, pamoja na bingwa wa La Liga Real Madrid na klabu kubwa ya Catalan Barcelona, ni miongoni mwa vilabu vikubwa ambavyo vinaongoza kuisumbua kambi ya Spain na inatazamaiwa huenda Villa akajiunga na mmoja ya vilabu hivi.

Turkey yawafungisha Vilago wenyeji Switzerland

Switzerland 1 – 2 TurkeyWachezaji wa Turkey wakishangilia ushindi baada ya kuibwaga Switzerland 2-1

Mchezaji wa Turkey Arda Turan aliwaliza Switzerland katika dakika za majeruhi na kuipatia timu yake ushindi wa mabao 2-1 na kuwafanya wenyeji hao Switzerland kuyaaga mashindano hayo.

Hakan Yakin ndiye aliyefungulia mashambulizi na kupachika bao la kwanza kwa timu yake ya Switzerland kwa bao dakika ya 32 ya mchezo. Switzerland ambao kwa mchezo wa jana walijitahidi washinde lakini bahati haikuwa yao, Mchezaji wa akiba Semih Senturk alisawazisha bao kwa timu ya Turkey na kufanya droo ya moja moja.

Mchezo uliendelea hivyo hadi dakika za mwishoni ambapo umati ulishatarajia mchezo utamalizika hivyo kufumba na kufumbua Arda mchezaji wa Turkey akapachika kimiani goli lapili katika dakika za majeruhi kabisa.

Shuti lake la kulia lilipita ngome ya Swiss na kwenda moja kwa moja kimiani na kuzima nderemo za waswiss ambao walikuwa wakiishangilia timu yao kwa nguvu zote.

Swiss walikuwa na nafasi ya kufunga goli lakini kipa wa Turkey Volkan Demirel kwa kiasi kikubwa aliwakatisha tamaa kwa kuokoa mpira uliopigwa na Yakin hapa na hapa ambao mashabiki walishainuka wakidhani ni goli.

Turkey watakutana na Czech Republic kwenye game ya mwisho ya Kundi A hapo jumapili ilihali n Swiss watakutana na timu isiyofungika Portugal.

Portugal haooo Robo Fainali

Czech Republic 1 – 3 Portugal

Baada ya usshindi wa magoli 3-1 dhidi ya Jamhuri ya Czech hapo jana, na baadaye Switzerland kupoteza mchezo Portugal wamefanikiwa kuingia hatua ya Robo Fainali ya EURO 2008. kimsingi wan kila sababu ya kusherehea hatua hii.

“Sisi ni kati ya Nchi nane bora kisoka katika Ulaya” alisema kocha wa Portogal Luiz Felipe Scolari said. “hatujaridhika tunahitaji zaidi ya hapo, na ninamatumaini makubwa ya kufika huko juu zaidi.”

Kiwango cha Portugal kwenye michuano hii kiko juu na kama wataendelea kucheza kwa kiwango hiki basi lolote laweza kutokea.

Portugal walipata goli la kwanza dakika ya nane ya Mchezo lililofungwa na mchezaji Deco lakini goli hilo lilidumu kwa takriban dakika tisa tu kwani Czech walisawazisha dakika ya 17 kupitia kwa Libor Sionko (17). Mpaka mapumziko magoli yalikuwa droo ya 1-1.

Kipindui cha pili kilianza kwa speed kali huku Portugal wakiongeza mashambulizi langoni mwa Czech huku kukiwa na kosa kosa za hapa na pale na dakika ya 63 huku akicheza kwa kuonana vizuri na Deco Cristiano Ronaldo akafanya alichotarajiwa kufanya kupachika bao la pili kwa timu ya Portugal baada ya kupata pasi toka kwa Deco. Czech ambao walikuwa na kibarua kigumu cha kumlinda Ronaldo jana iliwabidi wafanye kazi ya ziada kwani kijana hakabiki!. Dakika za majeruhi dakika ya 90 mchezaji kipenzi changu Ricardo Quaresma akaipatia timu yake goli la tatu.

Mpaka kipyenga cha mwisho, Portugal 3- 1 Czech.

Wednesday, June 11, 2008

Jalamba

Wachezaji wa Italy toka shoto Daniele De Rossi, walinzi Andrea Barzagli, Marco Materazzi na Fabio Grosso, striker Luca Toni na forward Marco Borriello wakipiga jalamba wakati wa mazoezi ya timu yao kwa ajili ya michuano ya Euro 2008 huko Maria Enzersdorf karibu na jiji la Vienna leo June 11, 2008. Italy watacheza na Romania katika mchezo wao wa kundi C tarehe 13 keshokutwa.

Utambulisho ndoa ya Dotnata

Aliyekuwa muigizaji maarufu Husna Shabani ‘Dotnata’ na mumewe Mohamedi Poshi wakivishana pete mara baada ya kutambulishana katika sherehe iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Msasani Beach ambako kulikuwa na hafla ya ya kuitambulisha ndoa yao kwa ndugu, jamaa na marafiki iliyofanyika usiku wa kuamkia leo.
Mmoja wa Ma-Mc kati ya Ma-Mc 10 waliokuwepo ukumbini humo msanii wa fani ya maigizo Muhsin Awadh ‘Dk Cheni’ akimwaga sera zake kwa maharusi Dotnata na mumewe Mohamedi Poshi.
Habari na Picha na Global Publishers

Czech na Portugal Usipime!!

Mashabiki wa Czech na Portugal wakishangilia kabla ya mechi kati ya timu zao leo, Mpambano huu unatazamiwa kuwa mkali kwani kila timu ina kiwango kizuri cha mchezo.

Teddy wa Total Knockout!!

Anaitwa Teddy Kalonga, Ni Model na ametumika sana kwenye matangazo ya TV hasa ta TBL na mengineyo, kwa sasa Teddy yuko Ughaibuni katika kujiendeleza. Teddy ni Blogger chini ya Total Knockout amejikita kwenye Burudani na Mitindo, kama una habari inayohusu burudani, vipaji, fashion au urembo, kama wataka kuwa featured na story yako binafsi basi wasiliana naye. kwa Kugonga hapa!

Under Water Wedding

Siku ya Kuoa au kuolewa ni siku pekee ambayo mtu anatakiwa asiisahau kwani kwa wengi wanaoamini siku hii huja mara moja ila kama tuu kutakuwa na ndoa ya mitala. Inaitwa Under water Wedding, ni maarufu kwa kipande hii ya Asia (Malaysia na Thailand) kwa Malaysia Chama cha Waogeleaji ndio mtaji wao mkubwa wakishirikiani na Hotel kubwa ambapo utapenda Harusi yako ifanyike. Package ya harusi hii ni Malaysian Ringit 160 (55,000 Tsh) kwa kila kichwa na idadi ya chini ni watu 60. Hii inakuwa ni pamoja na Vinywaji na Vilaji kwa waalikwa wako, Keki kwa ajili ya maharusi, Champagne 5, Mitungi ya Gas kwa ajili ya maharusi na yeyote atakaye hitaji kuzamia, Albamu ya Picha pamoja na DVD moja ya kumbukumbu ya tukio zima, Fataki 10Kg, pamoja na gharama za kuiandikisha ndoa na Cheti cha Ndoa kwa anayetaka anakaribishwa kuja Malaysia hakuhitaji VISA kwa Mtanzania.

Kelly Rowland naye kutua Bongo

IJUMAA SHOWBIZ!

Kwa mara nyingine tena Wabongo wengi watakuwa wakisubiri kwa hamu kubwa kumwona supastaa mwingine kutoka Marekani. Sasa ni zamu ya Kelly Rowland, ambaye atatia maguu nchini mapema mwezi huu.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kituo cha Televisheni cha MTV, Kelly yupo katika ziara ndefu akizunguka sehemu mbalimbali duniani kwa ajili ya kutimiza majukumu yake kama Balozi wa mfuko wa MTV Staying Alive Foundation.

Mwanamuziki huyo ambaye ni mtunzi na mkali wa kuimba staili ya R&B ni miongoni mwa warembo watatu waliokuwa wakiunda kundi maarufu la Destiny’S Child, kabla hawajaamua kila mmoja kutoka kivyake.

Khadija Kopa kupamba Kimasomaso keshokutwa

Pichani Kushoto (Khadija Mwanamboka na Mama Asia Idarous wa FABAK Fashions) ambao ni moja ya viongozi wa shirika lisilo la kiserikali la Tanzania Mitindo house wakizunguza na waandishi wa habari hivi karibuni jijini Dar kuhusu onesho lao la mavazi watakaloliita KIMASO MASO litakalofanyika ukumbi wa Waterfront juni 13/08,Kuanzia saa Moja Usiku,Kwa Kiingilio cha 12000/= Tu.
Khadija alisema kuwa katika onyesho hilo litajumuisha Wabunifu 10 nao ni ROSE VALENTINE, ASIA IDAROUS, ANGELO MLAKI, MUSTAFA HASSANALI, JAMILA SWAI, FANCISCA SHIRIMA, MONICA LIHAWA , HILDA BANDIO, KHADIJA MWANAMBOKA na Wataonyesha Mavazi ya
KITCHEN PARTY/ BAG PARTY ,

SENDOFF

HARUSI

Aidha kwa upande wa burudani Khadija alisema kuwa burudani itatolewa na Malkia wa Mipasho KHADIJA KOPA, SABAHA MUCHACHO na Kikundi cha Ngoma ya BAIKOKO kutoka Tanga.

Alisema onyesho la KIMASOMASO limedhaminiwa na Sabuni ya OMO, Kampuni ya simu za mkononi TIGO, Kinywaji cha REDD’S, SHEAR ILLUSIONS, GOLDEN TOUCH SALOON, BIG TV, VISUAL LAB: NEXT LEVEL, LEOPARD MODELLING AGENCY, VAYLE SPRINGS NA RAQEY.COM
Khadija alimaliza kusema kwa kuvitaja vituo vya tiketi kuwa ni: MANYWELE BEAUTY COSMETICS- KINONDONI, CHOCOLATE PRINCESS – MASAKI, SUMMER MIX FASHION – NAMANGA SHEAR ILLUSIONS – MILLENNIUM TOWERS.

Temptation kwa Jicho la ZEZE

Mnaweza kuwa pamoja lakini kila mtu ana jicho lake kila mtu anataka kuona chake, Camera ya Zeze kwenye Usiku TEMPTATION NA ALLY REMTULLA ilipata ya kupata kwani waliohudhuria pia walikuwa burudani kwa kupeneza kwa mavazi, ungana na Zeze kwenye 8020.


MAMBO YA TEMPTATION YA ALLY REMTULLA

Eto’o, Song, Njitap watua Dar

*Eto’o agoma kuzungumza na waandishi wa habari

*MO ahamasisha ushangiliaji

Na Majira
Timu ya Kameruni jana iliwasili nchini ikiwa na nyota wake wote tayari kuikabili timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ katika mchezo wa michuano ya kutafuta tiketi ya kufuzu fainali za Kombe Dunia zitakazofanyika Afrika Kusini mwaka 2010 na Kombe la Mataifa ya Afrika nchini Angola uliopangwa kufanyika Jumamosi kwenye Uwanja Mpya wa Taifa, Dar es Salaam.

Kameruni iliwasili jana alasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimul Nyerere, Dar es Salaam ikiwa na kikosi cha wachezaji 20 wakiwemo Samuel Eto’o anayecheza Bacelona ya Hispania, Geremi Njitap na nahodha Rigobert Song.

Timu hiyo baada ya kutoka nje ya Uwanja wa Ndege ilikwenda moja kwa moja kwenye gari waliloandaliawa huku Eto’o na Kocha Mkuu wa kikosi hicho, Pfister Otto wakigoma kuzungumza na waandishi wa habari.
Song beki wa kati mwenye nguvu, alisema wamejiandaa vizuri kuikabili Stars ingawa hawana taarifa kuhusu uwezo wa kikosi hicho na kuongeza kuwa anatarajiwa pambano hilo litakuwa gumu.

Naye Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ Marcio Maximo amekifananisha kikosi hicho na gari ya kubeba abiria (daladala) ambayo haiogopi kugongana na gari ya kifahari.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Maximo alisema timu yake itakuwa daladala itakapovaana na Kameruni katika mchezo wa kimataifa wa kuwania kufuzu fainali za Kombe la Dunia nchini Afrika Kusini mwaka 2010 na Mataifa ya Afrika yaliyopangwa kufanyika Angola.

Maximo alisema Stars inateremka uwanjani huku ikijua kuwa inavaana na kigogo cha mchezo huo Afrika ambacho kinaundwa na nyota wanaotamba na klabu kubwa duniani hatua ambayo anafananisha wachezaji wake (daladala) na gari la kifahari.
Alisema hata hivyo amewaandaa kikamilifu wachezaji wake kucheza kufa au kupona katika mchezo huo na amewaambia wasiogope ukubwa wa majina ya nyota wa Kameruni na wacheze mpira.

Maximo alisema katika mchezo huo anatarajia kuwatumia wachezaji wake wawili wa kiungo waliokuwa majeruhi, Mrisho Ngassa na Abdi Kassim ambao wamepona. Wachezaji hao walikosa michezo miwili ya Stars ilipomenyana na Mauritius na Cape Verde.

Maximo alisema ana imani wachezaji hao watakuwa msaada mkubwa katika mchezo huo na kuongeza kutokana na uwezo wao uwanjani ambapo Kassim anasifika kwa mashuti makali wakati Ngassa ni mahiri kwa chenga za maudhi dhidi ya mabeki wa wapinzani wao.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mohamed Enterprises, Mohamed Dewji amesema Kameruni inafungika licha ya kuundwa na wachezaji nyota ambapo amewataka Watanzania kujitokeza kwa wingi uwanjani kuishangilia Stars katika mchezo huo.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Dewji alisema Watanzania wanatakiwa kuipa nguvu Stars katika mchezo huo bila kujali majina ya wachezaji wa Kameruni ambao wengi wao ni maarufu.
Alisema hakuna sababu ya mashabiki wa soka kwenda uwanjani vichwa chini wakiihofia timu hiyo licha ya Stars kufanya vibaya katika michezo miwili ya awali kwa kutoka sare 1-1 na Mauritius kabla ya kufungwa bao 1-0 Cape Verde.

Alisema Stars ilipocheza na Senegal na Burkinafaso ikiwa ugenini wachezaji wa kikosi hicho walicheza kwa nguvu dakika zote za mchezo bila kuangalia ukubwa wa majina ya nyota wao wanaocheza Ulaya.
Mwaka jana Dewji alitumia zaidi ya sh. milioni 100 katika mkataba wake na Stars ambazo zilitumika kwa ajili ya shughuli za uendeshaji wa timu hiyo ikiwemo kambi na mambo mengine.

Kameruni inaongoza kundi A ikiwa na pointi 6 baada ya kushinda michezo miwili dhidi ya Cape Verde mabao 2-0 kabla ya kuibanjua Mauritius 3-0. Inafuatiwa na Cape Verde yenye pointi 3,Tanzania inashika nafasi ya tatu na Mauritius inakamata mkia.

“Ukiwa Makka basi ishi kama watu wa Makka…”

Mchezaji wa Los Angeles Galaxy David Beckham akiwa na mwanaye Brooklyn akipozi kabla ya mchezo wa Ligi ya kikapu kati ya Boston Celtics na Los Angeles Lakers jana jumanne, Bekham amekuwa gumzo tangia aingie USA na kila anapokwenda watu hujitokeza ku chill naye.

Faida ya Magoli kwa KAKA

Pichani ni mchezaji wa Brazili Ricardo Izecson dos Santos Leite, au Kaka, anaonekana akiwa na mkewe Caroline na mtoto wao wa kiume Luca, huko Sao Paulo, jana jumanne, June 10, 2008. Caroline Celico Leite alijifungua mtoto huyo jana saa 1:05 a.m, Taarifa zinasema mtoto ana kilo 3.6 na anaendelea uzuri.

Spain yaisambaratisha Russia 4 – 1

Spain 4 – 1 Russia
David Villa ndiye aliyekuwa Stearing wa mchezo wa jana baada ya kufanya mauaji kwenye mashindano ya mwaka huu ya Euro 2008 kwa kupachika magoli 3 kati ya manne wakati wa mchezo kati ya Spain dhidi ya Rusia ambao ulimalizika kwa 4-1.

“Magoli matatu kwenye mechi moja tena ya ufunguzi ni mwanzo mzuri kwa kweli aliesema Vila mara baada ya mchezo wa jana. Hii ni mara ya kwanza kwenye mashindano haya kufungwa mabao matatu na mtu mmoja mara moja tangu mwaka 2000ambapo mchezaji Patric Kluivert wa Netherland alipoifungia timu yake.Tumeanza vizuri ingawaje kuna mechi zinakuja lakini mwanzo utawaogopesha hata wapinzania wetu aliongeza Villa. Spain itakuja kukutana na Greece na Sweden kwenye mechi za kundi hilo la D. ambapo inategemea kukutana na kaupingamizi toka kwa Sweden ambao walionyesha mchezo mzuri jana.

Ni katika kundi hili rafiki yangu Tanzania Dreams anasema mshindi atatoka, sijui naona mechi zinatabiri kwa bingwa Greece kuonja kichapo. Goli moja la Spain lilifungwa na Mchezaji wa ArsenalFrancesc Fàbregas Soler au Cesc Fabregas ambao kwa pamoja walitengeneza karamu ya magoli.
Bao pekee la Russia lilifungwa na Roman Pavlyuchenko.

Sweden yaikomalia Greece 2-0

Strika wa Sweden Zlatan Ibrahimovic ndiye aliyeakuwa wa kwanza kufungua safu ya ufungaji kwa timu yake ya Sweden ilipowalaza mabingwa Greece 2-0 kwenye mchezo wa kundi D wa michuano ya EORO 2008 hapo jana jijini Salzburg.

<>Ibrahimovic pichani, ambaye hajafunga goli kwa timu yake ya Taifa tangu October 2005 aliifungia timu yake bao maridadi mnamo dakika ya 67 ya mchezo.
<>

Timu ya Greece ilikuwa kama imechanganyikiwa ngome yao kutokana na mchakamchaka wa jana ambapo Sweden walionyesha mchezo mzuri na kwa kiasi fulani kuumudu mchezo.
Dakika tano baada ya goli la kwanza Sweden walipata goli la Pili kutoka kwake Petter Hansson baada ya mabeki wa Greece kujichanganya. Mchezo huo wa kwanza ulikuwa muhimu kwa timu zote kwani unajiweka kwenye nafasi nzuri kipindi chwa mwanzo, Kwa mchezo walioonyesha Greece jana wanatakiwa kufanya kazi ya ziada ili kuendelea kuwepo kwani kazi bado Pevu mbeleni.

Tuesday, June 10, 2008

Kilichowaponza Taifa Stars

-Exclusive toka kwa Haki Ngowi-

Picha juu ni vimwana ambao ni washangiliaji wa timu ya Cape Verde wakifanya vitu vyao juzi kwenye mpambano wao na Taifa Stars nakuwalamba 1-0.kufungwa kwa Taifa Stars kumesababisha Baadhi ya Mashabiki kukata tamaa na hata kupoteza matumaini ya mchezo ujao dhidi ya Cameroon.
Stars itapambana na Cameroon katika mchezo wa tatu wa michuano hiyo utakaofanyika Jumamosi kwenye Uwanja Mkuu waTanzania jijini Dar es Salaam.Picha hizi kutoka Cape Verde kwa msaada mkubwa wa Mdau Saleh Ally. (Kaka Robert Mwafrika wa Azam ananiambia Taifa Stars walikuwa wakikodolea macho vimwana hahahahaa)

Wanyange wa Miss Tanzania UK 2008

Picha mwanana za washiriki mbalimbali wa shindano la Miss Tanzania Uk 2008 linalotarajiwa kufanyika jmosi ya Tarehe 14-06-2008 ndani ya Silver Spoon New Light Banqueting Suize ambapo Mgeni Rasmi anatarajiwa kuwa Balozi wa Tanzania Nchini Uingereza Bi Mwanaidi Maajar.

KAseja: Nimesign Yanga lakini nina Mkataba na Simba!!

Kaseja akianguka saini mbele ya Madega.
SIKU moja baada ya kipa wa Simba, Juma Kaseja kukiri amesaini mkataba wa kuichezea Yanga kwa ajili ya Ligi Kuu Tanzania Bara na michuano ya kimataifa msimu ujao, amesema bado ana mkataba na klabu yake.

Kauli hiyo ni mara ya kwanza kwa kipa huyo nambari moja kuitoa hadharani baada ya kusaini mkataba wa mwaka mmoja kuwatumikia mabingwa hao wa mpira wa miguu Tanzania Bara.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Kaseja alisema amesaini mkataba na uongozi wa klabu ya Yanga huku akijua mkataba wake na Simba unamalizika mwakani.

Kaseja alisema kabla ya kusaini mkataba mpya na uongozi wa Yanga aliwaonesha kopi ya mkataba wake wa Simba lakini uongozi wa klabu hiyo ya Jangwani ulimtaka asaini na wao wangefikia muafaka na wenzao wa Simba.


Ufaransa yashindwa kutamba

Timu ya Taifa ya Ufaransa imeshindwa kufurukuta mbele ya Romania kwa kulazimishwa sare ya 0-0 kwenye mchezo wa Euro 2008 kundi la C, Kundi hili ambalo ni moja kati ya makundi magumu kwani Ufaransa ina kibarua kigumu itakutana na Italy na Netherlands (waliomchapa Muitaliano 3-0) Mchezo ulikuwa mzuri kila timu ikionyesha mchezo mzuri lakini nafasi za umaliziaji za Ufaransa zimeonyesha kupwaya huku wakicheza bila Thiery Henry na Captain wao Patric Viera. Kipindi cha kwanza Romania walisimamamia kulinda lango lao zaidi huku France wakitoa mashambulizi ya hapa na pale ila umaliziaji butu. Nicolas Anelka ambaye jana alicheza nafasi ya Henry alikosa magoli mawili ya wazi dakika ya 9 na dakika ya 17 kwa kupaisha nje ya goli mipira yote.
Hadi mwisho wa mchezo Ufaransa 0 – 0 Romania.

Italy Mbendembende kwa Netherlands

Netherlands 3-0 ItalyUshindi wa magoli 3-0 walioupata wa Dtch dhidi ya waitaliano umeinua nderemo si tu kwa kushinda mechi hiyo bali kusherehekea ushindi wa kwanza dhidi ya Italy tangu mwaka 1978, Pichani mchezaji wa Netherlands Ruud van Nistelrooy (R) akifunga goli la kwanza wakati wa Mchezo wa kundi C wa Euro 2008 didi ya Italy. Netherlands waliwabugiza mabingwa wa Kombe la Dunia mabao 3-0. Katika mchezo ulikuwa mkali na wa kusisimua, goli la pili la Netherlands lilifungwa na Wesley Sneijder dakika ya 31 na kufanya Netherlands waende mapumziko kwa kuongoza 2-0. Kipindi cha pili kilianza kwa piga nikupige huku Italy wakuionyesha matumaini kidogo lakini ushambuliaji na Ngome ya Netherlands vilikatisha tamaa waitaliano na dakika kumi kabla ya mchezo kumalizika Giovanni Van Bronckhorst akaipatia timu yake bao la tatu na kuhitimisha karamu hiyo ya magoli, Rafiki yangu Tanzania Dreams wa India alitabiria kuwa hawa jamaa wamo katika watu wanaweza kuondoka na kikombe mwaka huu na dalili zinaonekana.

Mzee anacheza leo!!


Sylvie van der Sar, Mke wa golikipa wa Dutch Edwin van der Sar, akisubiri kuanza kwa mchezo wa Kundi C wa mashindano ya Euro 2008 kati ya Netherlands vs. Italy jana June 9, 2008 katika uwanja wa stade de Suisse huko Bern.

Monday, June 9, 2008

YANGA yamsajili Kaseka kwa USD 30,000

*Asajiliwa kwa makeke kumbadili Ivo, atamba kazi itafanyika
*Friend’s of Simba wachanga ‘vijisenti’ kumkomboa,waning’inia
*Asaini mkataba unaoeleza atakuwa kipa wa kwanza Yanga

Na Majira

KIPA mahiri nchini Juma Kaseja wa Simba ya jijini Dar es Salaam, jana alisaini fomu za mkataba kwa ajili ya kuichezea Yanga pia ya jijini katika michuano ya kimataifa mwakani, pamoja na Ligi Kuu Tanzania Bara.

Habari zilizopatikana mapema jana zilieleza kuwa kipa huyo alisaini fomu hizo mchana, baada ya mazungumzo yaliyochukua karibu saa tatu, ambayo ni mwendelezo wa mazungumzo ya kusaini fomu hizo yaliyoanza Ijumaa jioni.

“Tumemalizana naye ni fedha ambayo kila mwenye akili timamu hawezi kuiacha, hata kama ungekuwa wewe, huwezi kuacha kusajili, sasa ni Kaseja wa Yanga si Simba tena.

“Tunasajili kwa akili, hatukurupuki, tunajua tunachokifanya, Yanga itatisha, kijana amefika mahali alipokuwa akipataka,” kilieleza chanzo chetu ndani ya Yanga na kudokeza kuwa kwa jana tu kipa huyo alikabidhiwa dola 30,000.

Chanzo hicho kilieleza kuwa awali Kaseja ilikuwa asajiliwe leo, lakini kutokana na habari hizo kuvuja kwenye gazeti hili jana, pamoja na gazeti dada la Spoti Starehe, suala hili lilifanyika jana katika moja ya ofisi za mdau nyeti ndani ya Yanga.

Alisema licha ya juzi kutokuwepo fomu za usajili za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), lakini pia suala la mkataba wa kipa huyo na Simba lilikuwa likisumbua, ambapo mkataba huo unaonesha unamalizika mwakani.

Hata hivyo mkataba huo wa Kaseja unaeleza kuwa kila mwaka kutakuwa na mazungumzo kuhusiana na usajili na kama wakishindwa kuafikiana, yupo huru kutafuta timu nyingine, hivyo kama Simba watahitaji watalazimika kuilipa Yanga kiasi alichopewa kipa huyo pamoja na ahadi nyingine nyingi, ambazo utekelezaji wake tayari umeanza.

Gazeti la majira lilimpata kipa huyo ambaye alikiri kusaini fomu za Yanga na kusema ana imani kazi kubwa itafanyika kwenye ligi na michuano ya kimataifa.
“Elimu yangu ni mpira, maisha yangu ni mpira, nimeamua kusaini Yanga na nina imani Mungu ataniongoza nifanye vizuri, wamenipa kiasi kizuri sana, nami nitawapa raha uwanjani.

“Mimi si wa kwanza kucheza Simba kisha nikaenda Yanga, au kucheza Yanga nikahamia Simba, naomba mashabiki wa soka waelewe hilo,” alisema Kaseja.
Alikiri kusaini mkataba wa dola 30,000 na kwamba ni wa mwaka mmoja, ambapo moja ya vipengele vilivyopo ni kuwa yeye ndiye atakuwa kipa wa kwanza wa timu hiyo, hali itakayomfanya kipa wa sasa Ivo Mapunda kukaa benchi, au kutafuta timu nyingine.

Kaseja alisema kabla ya kufikia uamuzi huo aliwasiliana na baadhi ya viongozi wa Simba na kuwajulisha kuhusiana na dau la Yanga, ambao walimjulisha hawana uwezo kulifikia na kwamba yupo huru kuondoka.
“Niliwaeleza kiasi Yanga walichoniahidi wakanambia hawawezi kunipa, pia wakanipa baraka kuwa hela haikataliwi, nikasaini Yanga mkataba wa mwaka mmoja, ambao utahusu ligi ya 2008/2009,” alitamba kipa huyo.

Awali jana asubuhi, mmoja kati ya wanazi wa Simba wanaounda kundi la vibopa wa timu hiyo lijulikanalo kama Friend’s of Simba alipiga simu kwenye ofisi za gazeti hili akielezea kuhusiana na habari zilizoandikwa kwamba Yanga imemficha Kaseja.
“Si kweli Yanga haijamficha, ila mnataka kumsaidia Kaseja apewe dau kubwa Simba, hilo tunalijua,” alilalamika mdau huyo ambaye jina tunamhifadhi.

Hata hivyo alipoelezwa kwa undani kuhusiana na habari hizo, alionekana kushangaa na kuahidi angepiga mchana jana, ili asaidiwe kuelezwa alipo kipa huyo, kwani kulingana na maelezo aliyopewa na gazeti hili aliamini kweli Kaseja anaenda Yanga.

Kigogo huyo alipiga simu baadaye jioni jana na kusema tayari Friend’s of Simba walipata uhakika wa taarifa hizo na walichanga kiasi cha sh. milioni 20 ili wampe Kaseja, lakini alipoelezwa fedha aliyopewa ni nyingi zaidi aling’aka: “Ha. Huyu mtoto sisi tunamsaidia sana, lakini anatusaliti ngoja aende (anasonya), sisi hela hiyo hatuwezi kumpa.

“Lakini nasi tutalipa kisasi, hatuwezi kukubali kufa kikondoo, mwambie kila la kheri, kwanza hata Taifa Stars haitwi,” alilalama mdau huyo kwa kauli ya mfa maji, ambaye haishi kutapatapa.
Katibu Mwenezi wa Simba, Said Rubeya alipoulizwa jana kuhusiana na taarifa hizo alisema anachojua Kaseja ni kipa halali wa Simba.

“Habari hizi zimeandikwa katika gazeti lenu, hivyo mwandishi aliyeandika anajua zaidi, si mimi, lakini ninachojua fomu za usajili bado hazijatoka, Kaseja ni wa Simba,” alisema Rubeya.
Naye Katibu Mwenezi wa Yanga, Francis Lucas alipoulizwa alidai habari zilizoandikwa hazina ukweli na zina nia ya kumpigia debe Kaseja.

“Hatujazungumza naye, wala hakuna nia ya kumsaini Kaseja, haya mambo wala hatuyatambui,” alidai Lucas.

Angeline Jolie na Jack Black

Angeline Jolie akiwa na Jack Black walipokutana kwenye tamasha la filamu la Canes, Inasemwa Angeline amejifungua mapacha na Mashuirika makubwa ya Habari yametangaza dau kubwa kwa ajili ya picha ya kwanza ya Watoto/Mtoto wa Jolie. Kazi kwenye mapapa na mamamarazi.

Kwa akina Dada tu

Anaitwa Kim Kardashian, Mwanadada huyu huwaacha “Wakware” mate yakiwatoka kila apitapo kwa shepu yake hutoa Tips za urembo kwa akina dada kwenye Blog yake, picha hii ilipigwa wakati yeye pamoja na wifi yake wakifanya Shoping ya Furniture. Gonga hapa utapata vitu vyake

Chelsea yairuhusu AC Milan kufanya mazungumzo na Drogba

Klabu ya Chelsea imeipa ruksa klabu ya AC Milan kuongea na Drogba kuhusu nafasi ya mchezaji huyo kujiunga na AC Milan ila wamesema hawako tayari kumuachia alisema Makamu wa Rais wa timu ya AC Milan.
Chelsea wameturuhusu kufanya mazunguzmo na Drogba na tunatarajia mazungumzo yatafikia mafanikio mazuri alisema Adriano Galliani alipokuwa akiongea na gazeti la michezo la La Gazzetta dello Sport. Kwa sasa wasiwasi wetu uko kwa Shevchenko. Chelsea wanasema huyu hauzwi hii itakuwa imetunyima combination nzuri ambayo tunataka kuifanya aliongeza.

Galliani alisema kuwa Timu yake ambayo ni mabingwa wa Ulaya mara 7 wameanza kufanya mazungumzo na nyota mwingine toka klabu ya Barcelona Samuel Eto’o. Alisema Mcameruni huyo alikuwa anawaniwa na klabu nyingine ila wamempatia ofa yao kupitia kwa ajenti wake wanatumai majibu yatakuwa mazuri, vile vile imefahamika kubwa klabu hiyo pia ilifanya mazungumzo ya agenti wa Adebayo ingawa habari zinasema Arsenal hawako tayari kumuuza mchezaji huyo. Gillian alisema hawa wawili ni mapema kusema chochote ila maongezi yakifanyika tutatoa taarifa.

Croatia 1 – 0 Austria,

Mchezaji wa Croatia Luka Modric, kulia akikimbia kushangilia baada ya kufunga kwa mkwaju wa penati huku golikipa wa Austria Juergen Macho, akibaki hana la kufanya katika mchezo wao wa kundi B jana.

Mchezo mwingine wa kundi B ulikuwa kati ya Croatia na Austria, Mchezo ulianza kwa kasi kwa Croatia kumiliki kipindi cha kwanza na hatimaye kujipatia goli ambalo lilidumu hadi mwisho wa mchezo.
Kipindi cha pili kilikuwa ni azamu ya Austria walifanikiwa kwa kiasi fulani kuumiliki mchezo lakini jitihada za milki yao hazikuzaa matunda.

Luka Modric aliifungia Croatia kwa njia ya Penati katika dakika ya nne tu ya mchezo.
“Goli la mwanzoni mwa mchezo limetusaidia sana alisema kocha wa Croatia, lilitufanya kuwa na uhakika ama wa kuongeza goli au kulinda hayo matokeo ya moja bila, Tulimiliki kipindi cha kwanza lakini kipindi cha pili kiligeuka, tuliwapa nafasi nyingi za free kick ila Mungu yuko pamoja na jitihada zetu, alimalizia kusema kocha huyo. Mpaka kipyenga cha mwisho magoli ni moja kwa Bila.

Germany 2-0 Poland

Magoli mawili yaliyofungwa na Lukas Podolski ameipa Ujerumani nafuu na ahueni kubwa kwa kujiweka kanafasi kazuri kwenye mhcezo wao wa kwanza wa kundi B hapo jana. Mshambuliaji huyo ambaye ni mzaliwa wa Poland alipata wakati mgumu kwani ilibidi atetee Taifa lake kwa kuimiza nchi alikozaliwa lakini alifanya kama Kumkoma nyanyi vile. Poland walionyesha uhai kipindi cha pili kwa mashambulizi mazuri lakini ilikuwa kama mbwa aliyekosa meno!! na kuachia matokeo kubaki mbili bola.
Pichani Lukas Podolski (L) akipachika mpira kimiani wakati wa mashindano ya Euro 2008 kundi B dhidi ya Poland jana June 8, 2008 huko Woerthersee stadium, Klagenfurt, Austria. German walishinda 2-0.

Sunday, June 8, 2008

Matokeo ya Michezo mbali mbali ya awali ya kuwania Kombe la Dunia inayoendelea Ulimwenguni, Gonga sehemu ya Magoli kupata Data zaidi ikiwa ni pamoja na wafungaji

WC 2010 qual. – Asia (Group 1)
02:06 June 8
FT Iraq 1 – 0 Australia
WC 2010 qual. – Asia (Group 2)
03:06 June 8
FT Oman 1 – 1 Japan
FT Bahrain 1 – 1 Thailand
WC 2010 qual. – Asia (Group 3)
03:06 June 8
FT Jordan 0 – 1 Korea Republic
WC 2010 qual. – Asia (Group 4)
02:06 June 8
FT Uzbekistan 1 – 0 Singapore
FT Lebanon 1 – 2 Saudi Arabia

DSTV na EURO

Jana, pale MovenPick Hotel, MultiChoice Tanzania ilitangaza rasmi kuonesha michuano ya UEFA kwenye mtandao wake wa DSTV iliyoanza rasmi jana. Pichani ni Meneja Uhusiano wa kampuni hiyo, Lucy Kiwhele, akinadi mpira katika bahati nasibu iliyochezeshwa hotelini hapo kwa wageni waalikwa!

Misri, Aljeria zatisha Afrika

Misri 4-0 Jibuti.Amr Zaki wa Misri ndiye alifungua karamu ya Magoli

Wakati Taifa Stars ikishindwa kutamba mbele ya Cape Verde , Timu ya Taifa ya Misri imepanda kileleni mwa Kundi la 12 katika michuano ya kutafuta nafasi ya kufuzu fainali za Kombe la Duniab 2010 na fainali za Matifa ya Afrika pia mwaka hu, baada ya juzi kuiadhibu bila huruma Jibuti mabao 4-0 .

Katika mechi hiyo mabingwa hao wa Afrika walianza mechi hiyo kwa kasi lakini iliwabidi kusubiri hadi dakika 40 ilipopata bao mfungaji akiwa Amr Zaki.

Misri ambao walikuwa wageni waliongeza bao la pili dakika 47 , mfungaji akiwa Hosni Abd Rabo, kabla ya nahodha wa timu hiyo, Ahmed Hassan kupachika la tatu dakika 54 na Ahmed Abdelmalik kufunga la nne muda mfupi baadaye.

Mechi nyingine za kundi hilo la 12 zinatarajiwa kuendelea leo, wakati timu ya Taifa ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo DRC itakapoikaribisha Malawi mjini Kinshasa.

Mbali na mechi hiyo pia juzi kulikuwepo na mechi nyingine ya Kundi la 6 kati ya Algeria na Liberia ambapo katika mechi hiyo iliyofanyika mjini Blida , Algeria waliibuka na ushindi wa bao 3-0

Yanga wamemficha Kaseja

Na Majira

KIPA galacha (maarufu) nchini, Juma Kaseja amefichwa na klabu ya Yanga ya Dar es Salaam kwa nia ya kumsajili kwa ajili ya Ligi Kuu Tanzania Bara msimu ujao na michuano ya kimataifa.

Habari za uhakika kutoka ndani ya Yanga zilieleza kuwa tangu juzi kipa huyo amekuwa katika mazungumzo na baadhi ya viongozi wa Yanga (majina tunayo) kuhusiana na kusaini fomu hizo.

Jana mchana kipa huyo alionekana katika ofisi ya mmoja wa wadau wakubwa wa Yanga, ambapo haikuwa rahisi kwa watu wa kawaida kumtambua.

“Ni kweli tupo na Juma, amezungumza na watu muhimu ndani ya Yanga, ni jukumu letu kuhakikisha tunamalizana naye,” kilieleza chanzo cha uhakika ndani ya Yanga.

Chanzo hicho kilieleza kuwa kwa asilimia 80 Kaseja wamemalizana naye Yanga, lakini kuna fomu za mkataba kutoka Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), ambazo hazikuwepo, hivyo atazisaini wakati wowote.

“Kilichopo sasa tumemuweka chini ya himaya yetu hadi hapo atakaposaini hizo fomu, hata namba ya simu tumembadilishia,” kilisema chanzo hicho cha uhakika.

Hatua ya kumchukua kipa huyo aliyefungwa mara moja na Yanga, tangu ajiunge Simba karibu miaka saba iliyopita, inaonekana ni Yanga kutaka kukomoa baada ya kushindwa kuwasaini wachezaji wa Simba Henry Joseph na Kelvin Yondani. Wachezaji hao walisaini mkataba wa kuchezea tena timu hiyo wiki hii.

Katibu Mwenezi wa Yanga, Francis Lucas alipoulizwa jana kuhusiana na suala hilo alisema hakuwa na taarifa hizo kwa wakati huo. “Sina taarifa hizo, sidhani kama tunaweza kumsaini, si katika wachezaji wanaotajwa kusajiliwa Yanga. Lakini pia wachezaji wapo Simba tu?

“Hili la kumficha pia silijui, lakini hiki ni kipindi cha usajili mengi utayasikia, ila sisi Yanga usajili anafanya kocha, si viongozi,” alisema Lucas.

Gazeti hili (majira) lilijaribu kuwasiliana na kipa huyo kwa namba yake ya kawaida ambayo haikuwa hewani, hadi baadaye kipa huyo alipatikana kwa namba yake mpya na alipoulizwa alishtuka kwa kiasi kikubwa.

“Hapana mimi nipo na mambo yangu, nimebadili namba kwa masuala yangu binafsi, ambayo sidhani kama ni habari, suala la mimi kutakiwa si jambo la ajabu, mimi ni mchezaji, hivyo aliyekupa taarifa hiyo ndio akueleze kwa kirefu, maana hata timu za mikoani pia zinanitaka,” alisema Kaseja.

Alipobanwa zaidi ikiwemo kutajiwa namba ya gari iliyomchukua pamoja na muda alionekana na viongozi wa Yanga pamoja na mahali alipowekwa kwa sasa alijibu: “Naomba tuyaache.”

Makamuzi ya Ali Kiba Milton

Mwanamuziki kutoka Bongo Ali Kiba ameendelea kufanya makamuzi ya nguvu ndani ya tour lake nchini Uingereza na kudatisha karibu kila mji anaotia maguu.,Pichani ni show yake ya kukata na shoka iliyofanyika Milton Keynes.Kwa wadau wa Reading kaeni Mkao wa kula kwa Show bab’kubwa kutoka kwa Ali Kiba Tarehe 14 june 2008 ndani ya The FACE nite Club.Kazi Kwenu..
Kwa picha zaidi tembelea Haki Ngowi

Tanzania Vipaji vingi basi tuu

Rafiki yangu Hans Von Dykie ameniletea hii kutoka Ifakara ananiambia hawa jamaa huwa wanaburudisha baada ya kazi zao za Shamba wanajiita Big Tone Band hapa wanaimba kuwaelimisha vijana kuhusu gonjwa la Ukimwi. Hans Von Dykie ni mmoja wa wasamaria waliokwenda huko kwa ajili ya shughuli za kujitolea hasa kwa mradi wa Malaria na Ukimwi.

Wamkumbuka huyu?

Anaitwa Khamisa, alikuwa ndiye Miss Temeke 1998, kwa sasa yuko nchini Marekani alikojikita na kuendeleza maisha huko.

Njaa kipimo cha Akili

Kuna msemo unasema “Njaa Kipimo cha Akili”, Kama una njaa akili hufanya kazi mara dufu kufikiria ni jinsi gani utajitahivi kupata mkate wa kila siku, katika kutafakari mkate huo ndio hapo unapata Negative na Positeve ideas kwani hapo ndipo mawazo ya Ujambazi, U Richmonduli, na vipaji hujitokeza, Ninachotaka kumaanisha ni kuwa kuna njia nyingi za kujitafutia riziki moja wapo ikiwa huyu bwana akitoa burudani kupitia sanaa yake na hapo hapo kujipatia riziki yake.

Cape Verde yaisononesha Taifa Stars

Cape Verde 1-0 TanzaniaTaifa Stars ya Tanzania
Mechi ya pili ya Kundi 1 baina ya Cape Verde na Tanzania iliisha kwa kuwanyong’onyesha vijana wa nyumbani Taifa Stars katika mchuano mkali kuwania nafasi ya kufuzu katika kombe la dunia 2010.Mchezaji aliyeingia katika kipindi cha pili wa cape verde Babanco aliifungia timu yake mnamo dakika 73 na kuiwezesha Cape verde kunyakua pointi 3 zote.Taifa Stars sasa wanakabiliana na kazi kubwa mbele hasa baada ya kutoka sare ya nunge kwa nunge nyumbani na Mauritius wiki iliopita.Mechi yao ya tatu watamenyana na mabingwa mara nne wa kombe la bara Africa Cameroon nyumbani hapo June 14.

Pepe aipeperusha Portugal

Portugal 2-0 Turkey


Pepe na Cristiano wakishangilia baada ya goli la kwanza

Portugal wako kifua mbele katika Kundi A baada ya kuicharaza Turkey 2-0 kupitia mlinzi pepe na mshambulizi mdogo Raul Meireles.Portugal walicheza mechi ya kufana sana wakisaidiwa na mchezaji bora duniani mtarajiwa Cristiano Ronaldo.wangeongeza bao la tatu ambapo mchezaji matata Ronaldo kutoa kombora kali na kugonga chuma na kubanduka nje.Turkey vilevile walijikakamua na kukosa nafasi kadha wa kadha kupitia mchezaji Tuncay Sanli na hata kunyimwa penalti wanavyodai.Portugal sasa wanaongoza Kundi A juu ya Czech kwa sababu ya magoli mengi lakini pointi sawa.Mechi yao ya Pili ni dhidi ya wapinzani wao Czech.

Switzerland yashangazwa nyumbani na Czech.

Switzerland 0-1 Czech


Switzerland ilipigwa na mshangao baada ya kushindwa mbele ya mashabik wao mjini Basle Switzerland katika mechi ya kwanza la kombe la Bara Ulaya Euro 2008.Mchezaji Vaclav Sverkos’ aliengia katika kipindi cha pili na kuifungia Czech.Switzerland walicheza mechi nzuri na kuhatarisha lango la Czech lakini hatimaye kushindwa,timu hiyo inaongozwa na Senderos wa Arsenal,mchezaji mrefu kwa wote duniani Jan Koller wa Borussia Dortmund na wengineo ilhali Czech inaongozwa na Petr Cech wa Chelsea,Rosicky wa Arsenal vilevile wakiwemo wengine.

Saturday, June 7, 2008

Kenya yaiburuza Guinea 2-0.

Mshambulizi mkenya Mc Donald Mariga wa Parma FC Serie A Italy.


Kenya iliicharaza Guinea 2-0 hapo jana katika mechi ya kukata na shoka katika mashindano ya kufuzu kwa kombe la dunia na bara Africa.Mshambulizi matata anayoichezea Auxerre FC ya Ligi kuu ya ufaransa Denis Oliech aliiongoza Harambee stars ya kenya na kuitingisha nyavu mara mbili baada ya dakika tatu tu ya kipindi cha kwanza na ya pili baada ya dakika tano ya kipindi cha pili.Harambee stars ya kenya ilijipatia ari kubwa baada ya kushindwa mechi ya kwanza 2-1 na Namibia mjini Windhoek Namibia wiki iliopita.Guinea vilevile walishindwa kunyakua pointi tatu didhi ya Zimbabwe baada ya kutoka sare ya 0-0 nyumbani Conakry.Kufikia sasa kenya yaongoza kundi B baada ya Namibia,Guinea kisha Zimbabwe.Guinea walileta kikosi yote iliocheza kombe la Bara Africa mwaka huu ikiongozwa na mshambulizi na nahodha matata Pascal Feindouno wa Ufaransa St Etienne na beki hatari wa Celtic Bobo Balde na wengine walipigwa na butwaa na kubaki na kibarua kigumu ya kushinda mechi zilizobaki ilikujikomboa.

Mbwembwe za Mashabiki mitaani

Kijibwa kikiwa kimevalishwa jezi mitaani

Shabiki wa Croatia akiwa ameweka Tatoo ya bendera ya timu yake
Shabiki wa Germany

Mrithi wa Richa Adhia Dar Indian Ocean keshapatina

Mshindi wa Taji la Miss Dar Indian Ocean Joan Fast (katikati) akionesha tabasamu mara baada ya kutwaa Taji hilo katika ukumbi wa Cine Club Mikocheni Jijini Dar es Salaam usiku wa kuamkia leo.Kushoto kwake ni mshindi wa pili wa Taji hilo Grace na kulia ni mshindi watatu Groly. Picha na Global Publishers

Chris Tucker adata na Maajabu

Mwigizaji maarufu na mcheza sinema kutoka Marekani,Chris Tucker akiwaimbia wimbo wa mwanamuziki Michael Jackson,Wamasai aliowakuta katika Hifadhi ya Ngorongoro juzi.

——–
MCHEKESHAJI maarufu wa Marekani Chris Tucker amesema kuwa atakuwa “balozi wa hisani” wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro ili kuitangaza hifadhi hiyo duniani .Amesema kuwa baada ya kuvutiwa na maisha mseto kati ya wanyama na binadamu katika hifadhi hiyo.
Tucker ambaye alikuwa mjini Arusha kuhudhuria mkutano wa nane wa taasisi ya Leon Sullivan akizungumza na waandishi wa habari baada ya kutembelea kreta ya Ngorongoro na kujionea vivutio mbalimbali vya utalii vilivyoko ndani yake. Ifate kwa undani zaidi kwa Haki Ngowi

Logo, Wallpaper, Ring Tones na Video Ipod za EURO 08

Je unapenda Logo, Wallpaper, Ring Tones na Video Ipod za Euro 2008?
Basi Gonga hapa ujinafasi

Tutashinda bila Viera: Makelele

Mchezaji wa timu ya Taifa tya Ufaransa Claude Makelele amesema Ufaransa inawezakushinda bila Kepteni wao Patrick Vieira ambaye ataukosa mpambano wa ufunguzi kutokana na maumivu ya kwenye mguu sehemu ya paja.

‘Pat ni mchezaji muhimu lakini tunaweza kuishi bila yeye kwenye timu kama tunataka, Makelele aliwaambia waandishi wa Habari juzi walipotaka kujua anasemaje kuhusu kutokucheza kwa Pat.

Viera ambaye aliumia mazoezini wiki iliyopita hatocheza kwenye mechi ya ufunguzi wa Group C dhidi ya Romania hapo Jumatatu mchezo utakaochezwa Zurich. “Tunategemea Viera atakuwa fit kwa ajili ya mechi zilizobaki kwani tunamuhitaji kwenye timu yetu, na nadhani Mungu atabariki apone haraka”, alimalizia Makelele.

Nionavyo mimi

Maximo apewe Muda zaidi
Zimebaki siku chache kabla mkataba wa kocha Mbrazili Marcio Maximo (pichani) umalizike, Mengi yamesemwa kuhusu kocha huyu mgeni ambaye jukumu lake ilikuwa ni kutupeleka CAN, tunaiangalia leo Stars kwa macho mawili , Tujaribu kujiuliza je dhumuni lilifikiwa na tuangalie tulikotoka na tulipo sasa na nini kifanyike.
Kimsingi ni kweli Maximo ameinua kiwango cha Timu yetu ya Taifa kwa kiwango chake. Najaribu kuiangalia Taifa Stars ya wakati huo chini ya Kocha wazalendo na ndani ya ukwasi mkubwa wa pesa ambapo wachezaji walikuwaa hawana hata vifaa vya mazoezi, ni mara ngapi tulisikia wasamaria wema tu kama Mohammed Enterprises akijitolea viloba vya nafaka na carton za maji kwa Timu yetu?.

Ninachoona mimi ni kuwa tofauti pekee ambayo timu yetu ya Taifa inayo ni support. Kwa sasa angalao timu ina support licha tu ya serikali bali pia toka kwa makampuni makubwa kama Serengeti Breweries na NMB na mengineyo. Huu ni wakati mzuri kwa Timu yetu kufanya vizuri kama tuna Kocha Mzuri na support ipo ya kutosha kwa nini tusishinde basi?

Fikiria jinsi watu walivyohamasika kwa timu yao ya Taifa kipindi tunagombea kucheza CAN Ghana!! Nafikiri kwa kiasi kikubwa tumeona mabadiliko ingawa ni kweli mabadiliko hayawezi kuja mara moja. kwa mfumo wetu wa Soka wa kukusanya wachezaji dakika za mwisho hatuwezi kuona mabadiliko kwa muda mfupi kamwe. Ni lazima tuwe na Program ya muda mrefu na muda mfupi, muda mrefu ni kwa Serikali kuimarisha michezo kuanzia ngazi ya shule za msingi, na kuimarisha mashindano kama ya Taifa Cup.

Tujaribu kuangalia mechi za kirafiki za kimataifa, Taifa Stars imecheza michezo tisa ya kimataifa ya kirafiki chini ya Kocha Mkuu Mbrazili Marcio Maximo tangu aanze kibarua hicho karibu miezi 19 iliyopita.

Katika michezo hiyo Taifa Stars imeshinda mitatu dhidi ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, Uganda na Zambia na kutoka sare mara nne dhidi ya Kenya, Angola, Zambia, Uganda na juzi sare ya Malawi ya 1-1. na kufungwa na Yemen. Tukiangalia na tulikotoka haya tunayaita mafanikio.

Kimsingi ninachotaka kusema ni kuwa Kwangu mimi Maximo akipewa muda anaweza kuleta mabadiliko kwani ni mapema mno ikumbukwe kuwa anachokifanya Maximo ni kukutanishwa na wachezaji wanaotoka kwenye Vilabu vyao na kazi yake ni kuwafanya hawa wacheze kama Timu, sio kumfundisha mtu jinsi ya kutoa pasi hiy anafundishwa kwenye club yake huko. Ni lazima Club ziwe na mbinu mpya za ufundishaji, huko ndio soka linapoanzia. kwani vilabu ndio vinalisha Timu ya Taifa wachezaji, Pia kurudishwa kwa michezo ya Taifa Cup itakuwa Chachu ya mabadiliko kisoko kwani huko ndiko vipaji vinaanzia.

Friday, June 6, 2008

Salamu Toka kwa Kaka Chibiriti Italy

Habari yako Mkuu,

Nimekuwa nikifuatilia sana blog yako, kwakweli ni nzuri sana kwa sisi wapenda michezo, hasa soka mimi umenifikisha penyewe kabisa. Kila siku nilikuwa nikifikiri kukushukuru kwa kazi nzuri unayo ifanya ila mda ulikua ni mdogo, leo nimepata huu mda ninasema asante sana kwa habari zako, safi sana.

Ninakutakia kazi njema na mafanikio mema kila siku.

Ni mimi Baraka Franco Chibiriti

kutoka hapa Cesena-Italy.

Bila Hiyana nami nazipokea, nashukuru Kaka, Tuko Pamoja.

Pius

Collie Budz Show Ndani Ya Cine Club! Katika Picha

Picha na dar411 kupitia Sheria Mavazi Blog

Je wajua?

Wakati Mtanange ukikaribia kuanza si vibaya ukajikumbusha historia za timu husika.
Gonga Kwenye Timu Husika upate Data kuanzia Mechi za Kwanza za Matanange huu mpaka Hapo ilipo.

GROUP A
TURKEY TURKEY
CZECH REP CZECH REP.
PORTUGAL PORTUGAL
SWITZERLAND SWITZERLAND
GROUP B
AUSTRIA AUSTRIA
POLAND POLAND
GERMANY GERMANY
CROATIA CROATIA
GROUP C
FRANCE FRANCE
HOLLAND HOLLAND
ITALY ITALY
ROMANIA ROMANIA
GROUP D
SWEDEN SWEDEN
GREECE GREECE
SPAIN SPAIN
RUSSIA RUSSIA

Kila La heri

Dj Bonny Luv wa Mawingu Studio

Historia ya disco nchini Tanzania haiwezi kukamilika bila kumtaja DJ Bonny Luv (pichani). Ukifanya hivyo,wanaoielewa historia, ladha na utamu wa disco, enzi hizo lilipokuwa disco haswa, watakuona una lako jambo. Soma zaidi; http://bongocelebrity.com

Sebene la Werrason Usipime!!

Big Producer Maghambo, Mukubwa Mwemtsi, Collins na Fikiri wazee wa USA, Boss Chizenga na wapenzi wote wa Werrason inawahusu hii. Weekend njema

Simba yaipiga bao Yanga

Henry Joseph asajili Simba.

Uongozi wa Klabu ya Yanga umeanza kuchanganyikiwa baada ya wapinzani wao Simba juzi kufanya kufuru ya usajili kwa kuwasajili nyota wake wote waliokuwa wakitakiwa na timu hiyo.

Kuhaha huko kwa Yanga kumekuja baada ya Simba kuwasajili Musa Hassan Mgosi, Henry Joseph na Kelvin Yondani ambao wote walikuwa wakitupiwa macho na klabu hiyo kwa ajili ya kuimarisha kikosi chao kitakachoshiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa wa Afrika.

Baada ya Simba kufanya hivyo na jana kutangazwa kuwa wanawania kumsajili mchezaji wao Mrisho Ngasa kufuatia baba yake mzazi kuamuru mwanae aichezee Simba, viongozi wa klabu hiyo wamekuwa wakikutana mara kwa mara kujadiliana juu ya suala la usajili.

Habari za kuaminika kutoka ndani ya uongozi wa klabu hiyo zimeeleza kuwa imekuwa ni suala la kawaida kwa viongozi wa Yanga kukutana zaidi ya mara sita kwa siku.
IPP Media

Miss Tanga hiyoooo Kupekecha na Akudo mpaka Lyamba!!

Kati yao mmoja atamnrithi Victoria MArtin Kesho
Miss Tanga ndio hiyo si ya kukosa kama kawaida Akudo Sound watatumbuiza na Kijana toka Jumba la Vipaji – THT Andrew G pia atafanya mambo, ni Kupekechapekecha tuu.

Miss Tanga2007, Miss Tanzania Kanda ya Kaskazini, Redds fashion Ambassador Victoria MartinAmbaye amepata mikataba na kampuni za Modelling za South Afika. Hivi karibuni alikwenda South Afica kuangalia soko la uanamitindo na tayari kampuni mbili zimevutiwa naye na kumpa mapendekezo yao. Kampuni hizo ni O Model na EXTRA. Soma hapa zaidi

Simba yawatema Athuman Machupa, Joseph Kaniki na Yahya Akilimali.

KLABU ya Simba ya Dar es Salaam imewatema wachezaji saba waliochezea timu hiyo msimu uliopita akiwemo chipukizi Julius Mrope aliyesajiliwa mwaka jana akitokea Moro United.

Habari za uhakika kutoka ndani ya uongozi wa klabu hiyo, ziliwataja wachezaji wengine walioachwa katika kikosi hicho kuwa ni Athuman Machupa, Joseph Kaniki na Yahya Akilimali.

Chanzo hicho kiliwataja wachezaji wengine kuwa ni Said Sued, Soud Abdallah na Moses Odhiambo, ambaye amehamika APR ya Rwanda.

Hata hivyo chanzo hicho kilidai kuwa Machupa, Kaniki na Sued wameomba kuachwa kutokana na kutaka kwenda kucheza mpira wa kulipwa nchi za nje.

Kutokana na hatua hiyo ya kuacha wachezaji hao, chanzo chetu kilieleza kuwa hivi sasa Kamati ya Usajili ya Simba inahaha kukamilisha usajili kwa wachezaji 10 wapya kwa ajili ya msimu ujao.

“Simba imepanga kusajili wachezaji kumi wapya, kwa kuwa ilikuwa na jumla ya wachezaji 28 waliosajiliwa msimu uliopita, hivyo Kamati ya Usajili imepewa jukumu la kuhakikisha inasajili wachezaji imara,” kilieleza chanzo.

Tayari kamati hiyo imeshaanza kazi hiyo kwa kuwarudisha kundini wachezaji Henry Joseph na Kelvin Yondan ambao walikuwa wananyemelewa na Yanga, huku ikiwasajili chipukizi, Juma Jabu na Jabir Aziz.

Miss Dar City Centre atatoka hapa

Warembo wa Katikati ya jiji hawa hapa!

Vimwana wanaowania taji la Miss Dar City Centre 2008 wakiwa katika pozi la picha ya pamoja jana katika ukimbi wa Cine Club jijini Dar es Salaam ambako Juni 14 mwaka huu watachuana vikali kuwania taji hilo. Kampuni ya TSN kupitia magazeti yake ya HabariLeo/Daily News ni miongoni mwa wadhamini wa shindano hili.

Mitindo House na Kimasomaso

MAMBO YA TANZANIA MITINDO HOUSE AMBAYO INAKUJA NA FASHION SHOW AMBAYO WATAONYESHA NGUO ZA MAHARUSIIII KATIKA MATUKIO TOFAUTI IKIWEMO KITCHEN PARTY, SEND OFF, AQDI NA RECEPTION
HAYA KAZI ZENU WADAU POSTER CHINI HAPO INAJIELEZA!!!

Taifa Stars yaenda Cape Verde

TIMU ya taifa ya soka, Taifa Stars inaondoka leo alfajiri bila ya mchezaji wake nyota, Mrisho Ngassa na kiungo Abdi Kassim, huku kocha, Marcio Maximo akiahidi kwenda Cape Verde kupambana, na Naibu Waziri wa Habari, Michezo na Utamaduni, Joel Bendera akigeuka mbogo kwa wachezaji.

Stars, iliyopoteza pointi mbili katika mechi yake ya kwanza ya michuano ya awali ya Kombe la Dunia ilipolazimishwa kwenda sare ya bao 1-1 na Mauritius nyumbani, itavaana na Cape Verde Jumamosi.

Maximo alisema Ngassa bado hajapona vizuri na kwamba Abdi Kassim bado anahitaji muda zaidi wa kujiweka ‘fiti’ kabla ya kurudi uwanjani kikamilifu baada ya kutatizwa na nyama za misuli.

“Wataendelea na mazoezi hapa hapa kujiandaa kwa mechi ya Cameroon,” alisema Maximo.

Hata hivyo, kocha huyo Mbrazili alionekana kuwaamini wachezaji wengine waliosalia, aliposema kuwa wanaenda Cape Verde kupambana.

“Tulicheza na Mauritius, watu wakatupa nafasi kubwa ya kushinda lakini matokeo yakawa sare. Hii ndio itakavyotokea kwa Cape Verde. Watu wanasema Cape Verde ina timu nzuri, lakini na sisi tunakwenda kuwashangaza kama tulivyoshangazwa,” alisema Maximo.

Mziki wa EURO 2008

Sanamu kubwa zilizotengenezwa kwa sura na maumbo ya wachezaji kutoka Timu za Nchi tofauti duniani zanazoshiriki Kombe la EURO 2008 wakiwa ni pamoja na Michael Ballack na Philipp Lahm toka Germany, Karim Benzema na Patrick Vieira toka France, Angelos Charisteas toka Greece, Petr Cech wa the Czech Republic, Cristain Chivu wa Romania, David Villa toka Spain, Tanquillo Barnetta toka Switzerland, Andreas Ivanschitz wa Austria and Robin van Persie wa Netherlands.

U-Modo una karaha zake

Kusimama, Kutembea na hata Kuongea mbele za watu ni kazi kubwa inayohitaji ujasiri, fikiria uko mahala halafu watu zaidi ya 100 wote wanakuangalia wewe halafu ghafla kinatokea cha kutokea.
Ili uwe “Modo” inabidi uwe na vigezo fulani kama Figure, Urefu, na kikubwa kulitawala jukwaa ikiwa ni pamoja na mwendo, Angalia jinsi “Modo” huyu alipopata aibu ya mwaka jukwaani na kuwaacha hoi mpaka watangazaji wakifa kwa kicheko.
Bonyeza Player

Thursday, June 5, 2008

Ronaldo aweka wazi, Siku zake zahesabika Manchester

LONDON, Uingereza
HATIMAYE kiungo nyota na machachari wa klabu ya Manchester United, Christiano Ronaldo amesema ataihama klabu hiyo mwakani.

Kauli ya nyota huyo huenda ikatonesha donda la Kocha Mkuu wa United, Sir Alex Ferguson ambaye amekuwa hapati usingizi baada ya fununu kuvuja kuwa Ronaldo alikuwa na mpango wa kujiunga Real Madrid ya Hispania msimu ujao kabla ya kuvunja jaribio hilo.

Mwanzo mwa wiki hii, Ronaldo alimhakikishia Fergie atabaki Old Trafford kutokana na mafanikio aliyopata chini yake tngu alipojiunga na klabu hiyo mwaka 2003 akitokea Sporting Lisbon.

Kiungo huyo wa pembeni aliyeongoza kwa ufungaji mabao msimu huu katika Ligi Kuu England akipachika wavuni mabao 30 na 11 ya kimataifa, alisema kama ameshindwa kuhama msimu ujao basi itakuwa mwakani.

Ronaldo na wakala wake, Jorge Mendes wamefikia muafaka wa kuangalia ofa za klabu nyingine kutoka nje ya England. Real Madrid, Barcelona, AC Milan na Inter Milan zinammezea mate nyota huyo.

Ronaldo aliweka bayana kuwa kutwaa ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Ulaya na Kombe la Ligi Kuu England ni mafanikio makubwa na sasa wakati umefika wa kuondoka kwenda Real Madrid.

TEARS OF A CLOWN

Cristiano Ronaldo wa Ureno akipozwa baada ya kulia sana wakati wa mchezo wa Fainali ya EURO 2004 kati ya Ureno na Ugiriki (Portugal na Greece), Baada ya Ureno kupoteza mchezo huo kwa goli 1-0. hii ilikuwa Euro 2004, Je mwaka huu atalia au atacheka?

Kujifungua kwa Angeline Julie bado ni siri kubwa

NEW YORK – “Entertainment Tonight” walitangaza jana habari za kujifungua mcheza Sinema maaruf Angelina Julie ila kila wakati walikuwa wakisisitiza kuwa habari hizi ni kwa mujibu wa chanzo chao. Hata Shirika kubwa la habari la Associated Press katika taarifa yake limesema kuwa wao walipokea e-mail iliyotoka kwa mtu aliyejitambulisha kama mtu wa karibu na mcheza Sinema huyo. Kumekuwa usiri mkubwa kuhusu kujifungua kwa Angelina Julie tangu ijumaa ya wiki iliyopita, habari hizo zinasema mwanadada huyo amejifungua Mapacha.

Brazil yajipigia “debe” Olympic 2016

Tambara kuuubwa likipitishwa kwenye jukwaa la mashabiki katika Kupigia debe jiji la Rio De Janeiro kuwa muandaaji wa michezo ya Olympic 2016, Hii ilikuwa ni kwenye mchezo wa Mzunguko wa pili wa mchezo wa nusu fainali ya kombe la Libertadores Cup kati ya Fluminense ya Brazil na Boca Junior ya Argentina, Mchezo ulichezwa Rio de Janeiro, June 4, 2008. Fluminense alishinda 3-1

Amanda

Miss universe tz 2008 Amanda katika Pose, Mdau wangu Jimmy Mlay anasema wanakuwaga wapi hawa mbona mitaani hatuwaoni?
Picha na Issa Michuzi – Criss Tucker

Safari ya Ndoa ya Salma Msangi

Salma Msangi
Salma Msangi

Bi Khadija Kopa

Salma Msangi mtangazaji mahiri wa vipindi vya burudani Channel Ten hivi karibuni alifanyiwa sherehe ya Kitchen Party (sijui kiswahili chake tusaidiane) katika maandalizi ya awali ya Kufunga ndoa, Serehe hii ilifanyika katika ukumbi wa Water Front na ilinogeshwa na Malkia wa Mipasho Khadija Kopa na “Pembe” ilikuwa Live. Vazi lake limebuniwa na Asia Idarusi, Safari ya kuolewa inaanza na Kitchen Party, Send Off, Ndoa na baadaye Harus i duh!! si mchezo, Kila la heri dadaa, Kwa picha zaidi za sherehe hii na mengineyo Muone Mamaa Zeze hapa

Wednesday, June 4, 2008

Ali Kiba ndani ya Milton

INFINITY ENT’ ALONGSIDE BONGO FAMILY UK PRESENTS……SPRING BREAK TOUR ’08FEATURING ALI KIBAPERFORMING HIS HIT SINGLE CINDERELLA, NAKSHI NAKSHI MREMBO AND MANY MOREMILTON KEYNES ON SATURDAY 07TH JUNE@ SILK ROAD REST (MAHARAJA) 151 GRAFTON GATEMORE INFO
WWW.BONGOUK.COM

Cannavaro kuikosa UEFA – EURO 2008

Nahodha wa Italy Fabio Cannavaro akiwa ameshikilia Kombe la Dunia wakati timu yake iliponyakua kombe hilo mwaka 2006. Nahodha huyo na mchezaji wa timu ya Real Madrid hatokuwemo kwenye kikosi cha Italy cha sasa kitakachoshiriki mtanange wa kombe la UEFA – EURO 2008 baada ya kuumia mguu wakati wa mazoezi na daktari wake kuthibitisha kuwa hatoweza kucheza michuano hiyo.

Msiba wa Mama Mere Malou na Zadio Kongolo

Titina ambaye ambaye alimuwakilisha Koffi na Quartier Latin na Mpiga Gitaa la Rhythm wa Wenge BCBG Alba ambaye alimuwakilisha JB Mpiana na Wenge BCBG wakiwasili msibani.

Papa Wemba (wa pili) akiongoza waombolezaji kubeba jeneza la mama Mere Malou, Inasemwa kuwa Marehemu Mere Malou alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na Mzee Papa Wemba.

Fallu Ipupa Di Cap akiwa na Producer maarufu Manuru vaka kwenye msiba wa Mere Malou. Fally alitoa rambi rambi ya Euro € 1,500 kwenye msiba huo.

Kuna Post inayosema Zadio Kongolo shabiki namba mojawa Wenge BCBG,

Kwenye maoniya post hiyo Kuna mdau analalamika kuwa huyu bwana si maarufu kama tunavyomkuza na kusema hakwenda Bruxelles kwa ajili ya Onyesho la BCBG, ila alikwenda kwa ajili ya msiba wa Mama Mere Malou “madame ya poto“, ukweli ni kwamba kuna tofauti kubwa tangu mama Mere Malou afariki alizikwa siku ya Jumamosi tarehe 29 ya Mwezi March kwenye Makaburi ya jumping Jack na Onyesho la JB Mpiana lilikuwa tarehe 3 May 2008 huko huko Bruxelles. Si nia ya safu hii kubishana bali ni katika hali ya kuwekana sawa. Kwa faida ya wasomaji wangu, Mama Mere Malou alikuwa Mkongo anayeishi Paris Ufaransa, alishiriki kwa kiasi kikubwa kuukuza na kuutangaza muziki wa Kongo bara Ulaya, alikuwa ndio mdhamini na mpokezi wa wanamuziki wa Kongo kila wakifanya ziara Ufaransa.
Hii ndio “starehe” ya burudani, Big Producer Maghambo umesomeka.

Nastaafu 2010: Fergie

Kocha wa timu ya Manchester United Mkongwe Sir Alex Ferguson amesema kuwa atastaafu kazi ya ukocha rasmi akifikisha miaka 70, kwa sasa umri wa Ferguson ni miaka 66 hivyo basi ni wa “misimu” mitatu toka sasa.

Feruson aliweka wazi uamuzi wake huo jana alipokuwa akihojiwa kwenye mahojiano na Sir David Frost. Ferguson ataondoka huku akiwa na mafanikio makubwa na timu yake hiyo ya Manchester United kwa kipindi cha zaidi ya miongo miwili alichokaa na timu hiyo.
Aliongelea mambo mengi ikiwa ni pamoja na urafiki wake na Tony Blair na Gordon Brown pia aliongelea umuhimu kwa makocha na wachezaji kuwa na aliyoiita”njaa” ya ushindi.
“mchezaji mwenye kujituma ambaye timu ikishindwa anaumia huyo ndio napenda zaidi, pia nampenda mchezaji mwenye njaa ya magoli, njaa ya ushindi, hapo atafanya kila linalowezekana kimchezo timu ishinde, ndio kitu nawaambia kila siku wachezaji wangu. Hii ni changamoto kwa uongozi wa timu ya Manchester kwani ni kibarua kingine kutafuta mtu mwenye uwezo sawa na Ferguson.

UEFA – EURO 2008 Maandalizi ya timu moto!

Mchezaji wa timu ya Taifa ya Ufaransa Thierry Henry (R), akielekeza jambo kwa Mwanamuziki maarufu wa Ufaransa Grand Corps Malade, wakati wa kipindi cha mazoezi kwa klabu hiyo June 4 mwaka huu, kwenye kambi ya timu hiyo Clairefontaine, kusini Magharibi mwa Paris, mwanamuziki huyo aliitembelea timu hiyo kuipa moyo kwani Ufaransa wanacheza na Romania June 9, 2008 kwenye mechi yao ya kwanza ya mashindano ya UEFA – EURO 2008.

Tuesday, June 3, 2008

WANAITWA ‘ASHIERS’

HUYO WA KATI NI MADAM RITA AKIWA NA WASICHANA WAREMBO KWENYE MOJA YA EVENT HAO WASICHANA KITAALUM NAAMBIWA WANAITWA ‘ASHIERS’ SINA UHAKIKA NA SPELLING WAJUZI WATATUJUZA…ANAKUWA WANAWAPOKEA WAGENI N.K NAONA NI KAMRADI BONGO SIKU HIZI KWA WADADA HUSUSAN WENYE SHEPU ZA KIMISS,
Kwa Habari za Nyumbani za Burudani na mitindo tembelea 8020 Yuko Juu!!

Bingwa wa “Atalaku” kusakwa, Wadhamini ni Afrika Bambataa

Kuta kuwa na mpambanao wa marapa wa muziki wa dance Tanzania kutoka bendi mbali mbali ingawa hii haita husisha bendi bali mtu mmoja mmoja

Zawadi kubwa kutolewa waandaaji wakiwa ni kipindi cha African Bambataa ya clouds fm radio ya watu.

Mpaka sasa tayari marapa wamesha jaza fomu na kuanza kujitapa katika kipindi hiki kila mmoja akijiona yeye ni bora kuliko mwezie lakini ukweli utajulikana tu nani atatwaa taji la ufamle wa kurap katika muziki wa dance hapa nchini.

Akithibitisha hilo malkia wa bambataa ambae pia ni brand manager wa Nite X-Press amesema kuwa maandalizi yanaenda vyema na kuwa tayari baadi ya marapa wamesha jaza fomu za kukubali kushiriki katika kinyanganyiro hicho.

Mashindanpo haya yanataraji kuwa ya awamu 3 ambapo awamu ya kwanza ni ya utambulisho , awamu ya pili itakuwa ni ya kupiga live na mashabiki ndio watakao kuwa majaji na hatimae fainali.

Hii ni changamoto kwa vijana ambao tunasema ni kizazi kipya cha dance hapa Tanzania nia na lengo letu ni kuhakikisha marapa na wao kama sehemu ya ladha na burudani wanatambulika wanaheshimika na kudhaminiwa popote pale kwakuwa bila wao pia muziki unakuwa hauja kamilika. alisema Bi Sofia Kessy mmoja wa Waandaaji wa mpambano huo.
Na tutajitahidi kardi ya uwezo wetu kuhakikisha kuwa wanakubalika kudhaminiwa na kuheshimika pia kujulikana kote nchini.

Zadio Kongolo Shabiki nambari wani wa JB Mpiana na Wenge BCBG

Anaitwa Zadio Kongolo ukipenda muite ZK wengine humuita Sir Joe Kongolo, ni mfanyabiashara wa Kongo anayeishi Uingereza, Huyu ni mpenzi mkubwa wa JB Mpiana na Wenge BCBG kwa ujumla, ni maarufu kwa kutunza pesa, kwenye onyesho moja la JB alimtunza mwanzo hadi mwisho wa nyimbo (kwa nini asiimbwe!!!) kwenye kila onyesho la JB Mpiana Ulaya humkosi huyu bwana, kama anavyoonekana pichani alisafiri kwenda Belgium hii ilikuwa kwenye onyesho la JB Mpiana mwezi uliopita tarehe 3 May Bruxelles. JB Mpiana humuimba karibia katika kila wimbo lazima atamtaja ni kama vile unavyosikia PDG Ndama, Abdul Tall Omary Tall, Andrew Traders wanavyotajwa kwenye nyimbo za nyumbani, lakini Zadio amekwenda mbali zaidi kwani kwenye Albamu ya JB Mpiana ambayo inatamba sasa ya “Quel est ton probleme” akimaanisha Nini Tatizo lako?. Jb amemtungia wimbo kabisa Zadio unaoitwa Zadio Kongolo – ZK. Angalia na usikilize hapo chini, pia wimbo huu uwaburudishe wadau wangu PDG Mukubwa Ling’ande, Big Producer Magambo, Papaa Masabo, Mukulu Biloko Zadio wa Darisalama, Papaa Kasapila, Mukubwa Shabani, Ally Tandika – Tajiri mtoto, Batty William Mwafrica na wengine wengi, Mna nini bwanaaa. Pata burudani.
Leo Jioni JB Mpiana atahojiwa LIVE katika kipindi cha Afrika Bambataa, Clouds FM na Sophia Kessy tega sikio

Baba Januari akicheza Sebene la T Respect

Katibu Mkuu wa CCM, Yusuf Makamba (Babake Januari) akisakata sebene la T- Respect akiwa na Mbunge wa Kuteuliwa Mh. Al-Shymaa Kwegyir, kwenye ukumbi wa Travertine Magomeni Jumamosi.
Picha/GP

Ronaldo awatunisha vifua matajiri

Rais wa Real Madrid Ramon Calderon jana amesisitiza kuwa Timyake inayopesa ya kutosha kumnunua mchezaji machachari wa Manchester United Christian Ronaldo (pichani).
Katika taarifa ya hivi karibuni akinukuliwa na vyombo vya habari Kocha wa Man Sir Alex Furguson alisema mmiliki wa Manchester “the Glazer family” hawako tayari kumuuza Ronaldo kwa gharama yeyote ile na hawako tayari kumuona Ronaldo akiondoka Man kwa vyovyote, Kama ni kumnunua Ronaldo gharama itakuwa zaidi ya Pound Milioni 40 ambazo Real MAdrid alimnunua Mchezaji Zinedine Zidane miaka 6 iliyopita. Presidaa Calderon amesema “hakuna bei kubwa kwa mchezaji ambaye anachukuliwa kama ni the best duniani, kiwango chake ni cha juu hilo halina ubishi, bado nia yetu ipo pale pale kumsajili na nitafurahi kumuona Real Madrid msimu ujao” alisema kwa majigambo.
Kwa habari za sasa za uhamisho kujua nani kaenda wapi Kong’oli hapa.

Wengi wazimia baada ya uwanja “kufurika” watu Liberia

Wafanyakazi wa huduma ya kwanza wakimbeba mmoja wa mashabiki walipoteza fahamu kwa kukosa hewa kutokana na mrundikano wa mashabiki kwenye mchezo wa kuwania tiketi ya kombe la Dunia kati ya Liberia na Gambia, uliochezwa kwenye uwanja wa Samuel K. Doe . Uwanja huo wenye uwezo wa kuchukua watu 33,000 ulijaa kupita uwezo wake kwani inakisiwa zaidi ya watu 40,000 waliingia kuona mchezo huo uliochezwa jumapili ya juzi.

Ukisema chanini, wenzio wanasema watakipataje

Jose Mourinho (pichani) jana alilamba dume baada ya kuapishwa rasmi kuwa kocha wa timu ya Inter Milan, ambayo imemfukuza kocha wake Roberto Mancini.

Mourinho, aliondolewa kuifunza Chelsea September mwaka jana, amesaini mkataba wa miaka mitatu na klabu ya Inter Millan, ambao walighadhabishwa na matokeo ya timu yao kwenye michuano ya Champions ligi iliyomalizika hivi karibuni..

Mourinho aliiwezesha timu ya Porto kushinda kombe la Champions Ligi mwaka 2004 na akaiwezesha Chelsea kuchukua ubingwa wa England kwa mwana 2005 na 2006. Kila la heri kaka.

Mbwembe za Euro’08

Gari likipita mbele ya bango kuuuubwa likiwa na mchezaji mpira likiwakaribisha wageni kwa ajili ya Michuano ya Euro inayotarajiwa kuanza hivi karibuni. Bango hili limewekwa Airport Schwechat, kilomita 25 mashariki mwa jiji la Vienna, Mamia kwa maelfu ya wageni wanamiminika kwa ajili ya ichuano hii inayotarajia kuanza wiki ijayo.

Monday, June 2, 2008

Hasheem ndani ya Sullivan

supa staa hasheem thabeet na wadau wa boston pia wapo a-taun kwa ajili ya sullivan
Picha na Michuzi

Miaka 90 ya Mandela kwa Mbwembwe

Rais wa zamani wa Afrika ya Kusini, Mzee Nelson Mandela akiwa ameshikilia Kombe la Dunia, Afrika Kusini ndio waandazi wa Mtanange ujao wa Kombe la Dunia. Mandela atasherehekea miaka 90 ya kuzaliwa kwake mnamo tarehe 27 Mwezi huu katika Concert iliyoandaliwa Hyde Park mjini London ikiwa ni kuchangisha fedha kwa ajili ya Charity.
Miongoni mwa wanaotarajiwa kutumbuiza tamasha hilo ni pamoja na Amy Winehouse, Lady Jay Dee, Queen, Simple Minds, Leona Lewis na kikundi cha kwaya cha Soweto. Pia watu maarufu wamealikwa akiwemo Rais wa zamani wa Marekani Bill Clinton na Oprah Winfrey .

England yainyuka Trinidad and Tobago 3-0

Mchezaji wa England Dean Ashton (L) na Jerman Defoe wakipongezana baada ya timu ya kupata goli la pili dhidi ya Trinidad and Tobago wakati wa mechi yao ya kirafiki huko Hasley Crawford stadium nchini Spain. England alishinda 3-0.

D-Day Jumatano

Mchezaji wa Manchester United na Portugal Christiano Ronaldo akiwapungia mashabiki wakati wa mazoezi ya timu yake ya Taifa inayojiandaa kwa michezo ya EURO 2008, Ronaldo anatazamiwa kuwa na mkutana na waandishi wa habari siku ya jumatano kuzungumzia hatma yake kisoka ikiwa ni pamoja na tetesi za uhamisho wake kwenda Real Madrid.

Santos mabingwa wa Mexico

Wachezaji wa timu ya Santos wakiwa wameshikilia Kombe la Ubingwa Juu mwisho mwa mchezo wa fainali wa Ligi ya Mexico dhidi ya Cruz Azul Torreon, Mexico, Sunday, June 1, 2008. Santos walishinda kwa agregate ya 3-2.

Kutoka wazo hadi kitu kinachoonekana

Kufanya shooting ya Video za wanamuziki ni kazi ambayo inahitaji vipaji mchanganyiko kuanzia, mwanamuziki, Mpiga Picha, Muongoza Picha na mtu wa editing wote wawe wanazungumza lugha moja, wakati mwingine inagharimu sana kuzalisha wazo na kufanya “Imagination to became reality”. kutoka wazo mpaka kitu kinachoonekana na mi na wewe tukakubali ni kizuri patamu hapo!!. Naongelea kutoa wazo kichwani mwako na kumfanya mtu aelewe unataka nini. Angalia Jose Chameleon na Video yake ya Kipepeo wakati akijiandaa kuishoot na ilipomalizika, Huu nidio ulimwengu wa sanaa.

Na hii ndio baada ya Shooting

Naike Binti mtanzania mwenye ndoto kubwa

Binti wa kitanzania mwenye ndoto ya kuwa super model, bado yuko gado na anaonekana kufanya vizuri ndani mji wa Knoxville, Tennessee hapa Marekani. Kwa habari na picha zaidi mtembelee Teddy Kalonga kwenye Total Knock Out

Teddy Kalonga awashauri waandaaji wa maonyesho ughaibuni

Hii ni kwa wadau wote waishio pande hizi za dunia, USA, UK, Canada, na sehemu zote ughaibuni.

Nikiwa kama mtangazaji mzoefu, ambaye nilipokuwa kazini bongo niliipenda na kuifanya kazi yangu vyema, EATV(channel 5).

Wadau, najua kumekuwa na kawaida ya kualika wasaniii kuja nje na kufanya show. Lakini tatizo siku zote ni wasanii wale wale hivyo basi kupelekea baadhi ya wadau waishio nje kutowafahamu wasanii wengine wa bongo flava ambao nao wanasifa ya kuwapa washabiki wao burudani nzuri kabisa( bila maringo). Gonga hapa uisome zaidi

Mbunifu Yves Saint Laurent afariki dunia

Yves Saint Laurent (pichani), mmoja kati ya magwiji wa mitindo katika ufaransa kwa miaka 50 sasa amefariki dunia jana jioni huko PAris Ufaransa akiwa na umri wa miaka 71.

Habari zinasema kwamba Designer huyo alianza kuumwa tangu wiki iliyopita ambapo alilazwa hospitalini Paris, habari zinazidi kupasha kwamba hali ya Laurent ilizidi kuwa mbaya kuanzia jumatano ambapo alipoteza fahamu kabisa mpaka mauti yalipomkuta jana jioni.

Laurent alikuwa na mlolongo wa bidhaa za fasheni chini ya lebo yake (pichani) kuanzia viatu, nguo, manukato, mikoba ya akina baba na akina mama, kwa ujumla amejijenga kwa ulimwengu wa fasheni, Mwenyezi Mungu Amrehemu.
kwa habari zadi gonga hapa

Kanda Bongoman (KBM) awasha moto Dublin

Kijana wa Atalaku wa KBM akighani huku KBM akionyesha mambo na vijana


Hivi karibuni mwanamuzikii wa Congo Kanda Bongo Man alifanya onyesho huko Dublin Ireland ndani ya ukumbi wa Ambassador, onyesho ambalo lilivuta sio tuu wa Congoman bali waafrica wengi wanaoishi huko na viunga vya jirani, waliohudhuria onyesho hilo wanasema lilikuwa la aina yake kuanzia mangilio, sounding, ukumbi na hata Bongoman mwenyewe alianza kwa muda na kumaliza kwa muda ulitakiwa, alianza kwa kibao chake laini cha Yesu Kristu na kumaliza na kibao matata cha Inde Monii.
Wapenzi wa Muziki najua wanamkumbuka Kanda Bongoman, kwani ni kati ya wanamuziki wa kwanza kwanza kutoka Zaire wakati huo (Congo) kufanya shoo Tanzania, Shoo ya Kanda Bongo Man kwa East Africa ilikuwa ya kufa mtu kwani ilibidi atolewe mkuku na Mzee Moi kwa watani wetu wa jadi baada ya kuambiwa kwenye maofisi nusu ya wafanyakazi kama sio robo tatu hawapo wamekwenda kumuona Kanda Bongoman. Huyo ndiye KAnda Bongoman baada ya hapo walianza kumiminika wanamuziki toka Congo kwa shoo kadhaa jijini Dar Es Salaam na wenginewalilowea (usifanye mchezo na Dar Bwana) Muulize Mayaula Mayoni hahahaha alifikia hoteli ya laki na nusu kwa siku akaja ishia guest ya 5000 kwa siku, hii ndio Bongo yenye kisima cha burudani.

Mmoja wa wacheza shoo wa KBM akiwajibika

KBM na wacheza shoo wake

Wapenzi wakipata Burudani ndani ya ukumbi wa Ambassador

Sunday, June 1, 2008

Miss Chang’ombe ndio huyooooo!!

Mshindi wa taji la Miss Chang’ombe 2008 Angela Deo Lubala (katikati) mshindi wa pili Lilian Shayo (kulia) na mshindi watatu Shadia Ally (kushoto) katika picha ya pamoja mara baada ya kutangazwa washindi kwenye shindano hilo lililofanyika usiku wa kuamkia leo katika Ukumbi wa TCC Club Chang’ombe Temeke Jijini Dar es Salaam likishirikisha vimwana 10.
Waliokuwa washiriki wa shindano la Bongo Star Search (BSS) 2008, Maangaza Nyange (kushoto) na Rogers Lucas wakikonga nyoyo za mashabiki wakati wa fainali za kumsaka mrembo wa kitongoji cha Chang’ombe usiku wa kuamkia leo.
Picha/Habari na Global Publishers

Kitine na Majuto Jr

Jaji wa shindano la Bongo Star Search (BSS) John Kitine shoto akiwa na mpiga gita la Bass Majuto Jr wa Bendi ya Kalunde inayoongozwa na Deo Mwanambilimbi, Majuto ni mtoto wa muigizaji na mchekeshaji maarufu wa kwenye TV Majuto. Kalunde Band kila ijumaa na Jumamosi wanapiga Giraffe Ocean View Hotel

Brasil yainyuka Canada 3-2

SEATTLE – MAY 31: Robinho #11 wa Brazil akimrukia Diego #10 baada ya Diego kufunga goli katika kipindi cha kwanza cha mechi ya kimataifa ya kirafiki dhidi ya Canada jana may 31 kwenye uwanja wa Qwest huko Seattle, Washington. Brazil walishinda Canada 3-2.

Brasili utawataka kwa kushangilia, Samba uwanjani mpaka kieleweke. Hii ilikuwa jana kwenye mchezo dhidi ya CANADA ilibidi wacanada wenyewe kuwakodolea macho hawa jamaa.

Gianluca Zambrotta atua AC Milan

Fullback muitaliano Gianluca Zambrotta (pichani), aliyeichezea Barcelona kwa takribani misimu miwili amejiunga na klabu ya AC Milan, imesema taarifa ya klabu hiyo bila kueleza habari za undani wa pesa za uhamisho. Kabla ya hapo timu ya Manchester ilionyesha kumtaka na walikuwa wanangoja kumalizika kwa michuano ya EURO mipango ikamilishwe.

Bekham kuongoza England leo

Kwa mara ya kwanza tangu fainali za kombe la dunia 2006 mchezaji David Bekham amepewa jukumu la kuiongoza timu yake leo watakapo kuwa wakipambana na Trinidad and Tobago.

Responsible FatherSean “P. Diddy” Combs akiwa na watoto wake pacha D’Lila Star na Jessie James kwenye bustani ya michezo huko Beverly Hills, California.

Wakati wa Shida na Twanga Pepeta

Pata Burudani toka kwa Twanga Pepeta
video

Albam mpya ya mwanamuziki Koffi Olomide inatarajiwa kuzinduliwa June 6 huko Paris Ufaransa, Uzinduzi huo utatanguliwa na Utambulisho rasmi kwa wanahabari utakao fanyika June 5 World Press Presentation katika mgahawa wa Posh Fouquet’s restaurant, Paris. Kama kawaida Spoti na Starehe tutaleta habari na picha za uzinduzi huo.
Wakati huo huo mwanamuziki mwingine Werason Ngiama anatarajia kuzindua Albamu yake tarehe kama hiyo huko Beuxells Ubelgiji.

JB mpiana aendeleza mashambulizi Rotterdam

JB Mpiana na kundi zima la Wenge BCBG wikiend hii liliendelea na ziara yao ya Ulaya na usiku huu walipiga Rotterdam katika Concert iliyofana lakini kutonogeshwa na baadhi ya vijambo.

Ukiachilia mbali ufinyu wa stage ambao JB Mpiana aliulalamikia sana pia “hujma” na “fitna” ya kukatiwa umeme ilipunguza utamu wa onyesho hilo. Lakini wapenzi wa muziki waliofika mapema walifurahishwa na jinsi Mpangilio mzima wa onyesho ulivyokuwa kwani JB na kundi lake walipiga Non Stop nyimbo zaidi ya kumi na mbili jambo lililonogesha na kuwachengua zaidi mashabiki waliohudhuria onyesho hilo. Ukilinganisha na onyesho la Sweden au Bruxells kwa idadi ya mashabiki onyesha la jana halikuwa na mashabiki wengi ki viiile!! kwani palikuwepo na hati hati ya kutofanyika na wengi walisafiri kumuona JB Sweden na Bruxells kabla. Mdau Twaha Makau na kati ya IFM nafikiri tuko pamoja.
Papa Cherry JB Mpiana Sultan Bin adam akiwajibika jukwaani jana.

Baadhi ya wanamuziki wa Wenge BCBG wakishambulia Jukwaa ipasavyo
Mmoja wa wakongwe wa BCBG Chai Ngenge.

Mashabiki wakijinafasi

JB Mpiana Papa Cherry akimtambulisha mmoja wa mashabiki mpiga solo wa zamani wa bendi ya Chock Stars SOS Matondo.

Wapenzi wa muziki wakiwa karibu kabisa na Stage ili kuweza kuwaona Wenge BCBG

Taifa Stars yatoka Saew na Mauritius

Ilikuwa patashika Uwanja wa Taifa jana jioni lakini mashambulizi yetu yote hayakuzaa matunda. Tumepata nafasi zaidi ya 15 na kona kama 26 lakini tumetoka patupu!
Pamoja ana udhanmini wa nguvu lakini bado Stars haijakaa sawa, mpira ulikuwa bomba lakini magoli haba.
Mchezaji wa Taifa Stars Danny Mruanda akishangilia mara baada ya kupachika bao la kusawazisha,
(Picha na Mpoki Bukuku)

PAMOJA na kupata nafasi nyingi za kufunga, Stars jana ilijikuta ikishindwa kuzitumia nafasi hizo na kuambulia sare ya bao 1-1 dhidi ya Mauritius katika kampeni zake za kwanza za kuwania kufuzu kucheza fainali za Kombe la Dunia na Mataifa ya Afrika mwaka 2010.

Mauritius ndio ilianza kuziona nyavu za Stars dakika ya 39 ya mchezo kupitia mchezaji wake Wesley Marguette kutokana na uzembe wa Salum Sued, huku kipa Ivo Mapunda akiwa nje ya goli.

Stars ilisawazisha bao hilo dakika ya 64 kupitia kwa Danny Mrwanda akiwa amepokea pasi kutoka kwa Sued.

Mchezo huo uliochezwa kwenye Uwanja Mkuu wa Taifa, Stars ilianza kwa kasi mchezo huo huku ikishambulia lango la Mauritus lakini ubutu wa safu ya umaliziaji ndio uliyoingusha Tanzania.

Kwa hesabu za haraka haraka Stars imepoteza kona zaidi ya 18 na penati moja kutokana na umaliziaji butu.

Sekunde ya 10 Stars ilipeleka shambuzi kali langoni mwa Mauritus, lakini ilijikuta ikipata kikwazo kutokana na ngome imara ya wapinzani hao.

Dakika moja Mrwanda alishindwa kutumia vema pasi ya Ulimboka Mwakingwe na kujikuta akikosa bao, dakika ya nne Henry Joseph alipeleka mashambulizi hayakuzaa matunda na kuambulia kona butu, huku Emmanuel Gabriel akipoteza mipira mingi ya wazi dakika ya nne alipata nafasi lakini alipaisha mpira juu.

Stars itajutia nafasi ilizopata hasa kipindi cha kwanza dakika ya 16 Henry Joseph aliachia shuti kali mita 20 lakini kipa wa Mauritius, Francois Ammomoothoo alipangua, na dakika ya 30 alikosa bao la wazi.

Dakika ya 35 mwamuzi Marange Kenias kutoka Zimbabwe alitoa penati kwa Stars baada ya Henry Joseph kufanyiwa madhambi eneo la hatari, lakini Emanuel Gabriel alikosa penati hiyo baada ya kipa wa Mauritus kuiona.

Awali Gabriel alipata penati hiyo lakini mwamuzi Kenias aliikataa na kuamuru ipingwe upya baada ya wachezaji wa Stars kuingia ndani ya penalti kabla ya filimbi kupulizwa.

Akizungumza mara baada ya mchezo huo kocha wa Taifa Stars, Marcio Maximo alisema “Kiwango kilichoonyeshwa na wachezaji wangu ni kizuri lakini hatujashinda, wametengeneza nafasi nyingi nzuri lakini mpira si hesabu, Mauritius nawapongeza kwa jinsi walivyofanya kazi nzuri ya kuzuia inagawa tumeonyesha kiwango kizuri na mashindanio ndio yaanaza sasa,”alisema Maximo.


Kumbukumbu mwezi May

July 14, 2008

Taarabu yazidi kuchengua

Usiku wa kuamkia leo kundi la Jahazi Modern Taarabu kama kawaida yake lilipagawisha ile kinona na vibao vyake mbalimbali kikiwemo kile cha Msumali katika Ukumbi wa Mango Garden jijini Dar es Salaam na kufanya Mademu na Mabrazaneni waliofika kuwasarandia mademu hao kushindwa kukaa vitini mpaka majogoo.

VINARA AWARDS 2008: COPY YAIBUKA KIDEDEA, YANYAKUA JUMLA YA TUZO SABA!

Filamu ya COPY, usiku wa kuamkia leo katika ukumbi wa diamond jubilee jijini dar, imeibuka kidedea ya kuwa filamu bora ya mwaka na kuwa ndiyo filamu iliyonyakua tuzo nyingi kuliko filamu nyingine. Copy, ambayo imetengezwa kwa kutumia utaalamu wa kumfanya mtu mmoja kuwa na uhusika wa watu wawili tofauti kwa wakati mmoja, imeshinda kwenye vitengo vya filamu bora ya mwaka, mpiga picha bora, muigizaji bora wa kike na wa kiume, muongozaji bora, mhariri bora na mtunzi bora. Pichani, Naibu waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, Joel Bendera, akimkabidhi Ahmed Halfan ‘kelvin’ tuzo ya Filamu Bora ya Mwaka ambaye pia ndiye muongozaji na muigizaji msaidizi wa filamu hiyo. Mkewe pia, Elizabeth, ndiye aliyeibuka mwigizaji Bora wa kike 2007 kutokana na filamu hiyo hiyo ya Copy!!!
Hassan Bumbuli kutoka upande wa majaji, akimkabidhi tuzo ya adui bora kwenye filamu, Sebastian Mwanangulo ‘seba'(kulia) kutokana na filamu ya Misukosuko 2.

Rashid Mrutu (kulia) akipokea moja kati ya tuzo mbili alizojinyakulia usiku wa kuamkia leo pale diamond jubilee baada ya filamu yake ya COPY kumpatia tuzo ya mpiga picha bora na mhariri bora wa filamu.

Imani Kajula, kutoka NMB, akimkabidhi Elizabeth Chijumba (kulia) tuzo ya mwigizaji bora wa kike wa mwaka 2007. Filamu iliyompatia tuzo hiyo ni COPY.
Steve Kanumba (kulia) akipokea tuzo yake ya Heshima kutokana na mchango wake mkubwa wa kuitangaza nchi za nje tasnia ya filamu tanzania.
Washindi wa tuzo za heshima Thea na Kanumba wakiwa na nyuso za furaha mara baada ya kukabidhiwa tuzo zao usiku wa kuamkia leo pale diamond jubilee hall.

PICHA ZOTE: CHRISTOPHER LISA/RICHARD BUKOS/GPL)

Nyumba ya 50 Cent yaungua MOTO!!

Jumba la kifahari la mwanamuziki 50 Cents limeungua moto jana ijumaa majira ya saa saa kumi na moja alfajiri, Watu wote sita waliokuwemo ndani ya nyumba hiyo walikimbizwa hospitali na kupatiwa matibabu na bado walikuwa chini ya uangalizi wa madaktari lakini hali zao zinasemwa kuendelea vizuri. Rafiki wa kike wa zamani wa mwanamuziki huyo alikuwepo pamoja na Marquise mtoto wa kiume wa 50 Cent mwenye miaka 10.

Nyumba hiyo yenye vyumba sita vya kulala, mabafu matano, pamoja na vikorombwezo kadha wa kadha imejengwa kwenye eneo lenye ukubwa wa hekari moja, imeungua na kuteketea kabisa.

Habari zinasema moto huo wanahisi unahusiana na njama fulani lakini Mwanamuziki huyo bado hajasema kama anamhisi mtu yeyoye.

Gonga hapa kwa picha zaidi

Timu 40 za Africa zashuka dimbani leo, Taifa Stars yaikaribisha Mauritius

Wachezaji wa Timu ya Taifa ya Mauritius wakiwasili kwenye uwanja wa Taifa wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere tayari kwa mechi dhidi ya Timu ya Taifa Taifa Stars.

TIMU ya soka ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars‘ leo inatarajia kushuka dimbani kuvaana na Mauritius katika mchezo kuwania tiketi ya kufuzu kucheza fainali za Kombe la Dunia 2010 unaotarajia kufanyika Uwanja Mkuu wa Taifa, Dar es Salaam.

Mchezo wa leo ni kwanza kwa timu hizo zilizopo Kundi la Kwanza pamoja na timu za Visiwa vya Cape Verde na Kameruni.

Taifa Stars itashuka dimbani ikiwa kamili kuikabili timu hiyo, ikiwa ni wiki moja baada ya kucheza mchezo wa kirafiki wa kimataifa na Malawi na kufungana bao 1-1.

Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Mbrazili Marcio Maximo amesema timu yake ipo vizuri na ana imani watashinda leo na kujiweka vizuri katika msimamo kwa ajili ya kufuzu fainali hizo zitakazofanyika nchini Afrika Kusini.

Kwa wikiend hii tu zaidi ya timu za soka 40 toka Africa zinashuka dimbani kwa ajili ya kuwania kucheza nafasi ya fainali ya Kombe la Dunia na Kombe la Mataifa ya Africa.

………………………………………………………………………………

Misri Vs Congo DRC
Pharaohs ya Misri
(pichani juu) itawakaribiosha Simba wa Kongo, Jamhuri ya Kidemokrasia ya watu wa Kongo ,Kocha wa Kongo Mbelgiji Patrice Neveu amewaita wachezaji muhimu wa kikosi chake kama Shabani Nonda na Tresor Lualua kujiunga pamoja kwa ajili ya ichuano hii. Mchezaji wa Misri na mfungaji bora wa Kombe la Mataifa ya Africa mwaka jana Mohamed Abu Traika atakosa mchezo huo wa ufunguzi kwa kuwa ni majeruhi.

………………………………………………………………………………


Cameroon Vs Cape Verde
Timu ya Taifa ya Cameroon Indomitable Lions itawakaribisha Cape Verde, kikosi cha Cameroon kinaundwa na wachezaji chipukizi ambapo wameongeza vijana sita watakao ongozwa na kijana mwenzao Samuel Eto’o, Rigobert Song na Geremi Njitap.

…………………………………………………………………………….
Ivory Coast Vs Msumbiji

Ivory Coast wakiwa ndio kwanza wamerejea toka Japan walipokwenda kucheza Kirin Cup wakiwa ni wawakilishi wa Africa kwenye michuano hiyo watakutana na Msumbiji. Mkongwe Didier Drogba anakazi kubwa ya kukiongoza kikosi hicho ambapo mchezo huu ndio mtihani mwingine kwa kocha mpya Vahid Halilhodzic wa Bosnia.

………………………………………………………………………………

Nigeria Vs Bafana Bafana
Nayo Nigeria Super Eagles ambao wameonyesha kutojali tena makocha wageni baada ya kocha Mjerumani Berti Vogts wa Germany kushindwa kuwaridhisha wapenzi wa soka kwa michuano iliyopita ya Ghana. Kwa sasa timu hiyo inafundishwa na makocha wazalendo Shaibu Amodu na mkongwe Daniel Amokachi, watakuwa na kibarua kigumu kukabiliana na waandaaji wa fainali hizo kwa mwaka 2010 timu ya Bafana bafana ya Africa Kusini.

…………………………………………………………………..

Morocco Vs Ethiopia
Baada ya mafanikio mabovu Atlas Lions ya Morocco itawakaribisha Ethiopia kwa kile ambacho kocha wao anasema ni mchezo wa kuanza kurudisha heshima ya Morocco kwa mchezo wa soka kimataifa.
……………………………………………………………………..

Senegal Vs Algeria
Simba wa Teranga wa Senegal nao walimtosa kocha wao wa kigenibaada ya kutofanya vizuri Ghana kocha mpya Lamine Ndiaye ana kibarua kwa kukutana na timu ya Algeria.

………………………………………………………………………………

Ghana Vs Libya
Ghana wanakutana na Libya huko Kumasi Ghana. nao pia ni mtihani hasa baada ya kuaachana na kocha wao Claude Leroy.

………………………………………………………………………………

Togo Vs Zambia
Timu ya taifa ya Togo inakutana na Zambia katika tukio ambalo si la kawaida kwani watachezea Ghana katika jiji la Accra. Hii ni baada ya FIFA kuwafungia Togo kwa kufanya fujo kwa timu ya Malian.

Kolabo ya Celeo Scam na Fally Ipupa Dicap

Celeo Scam alikuwa kijana wa Werason lakini akaamua kutoka kivyake na kwa sasa yuko Juu kioma, Celeo pamoja na Fally wanaitwa Kizazi cha Tano cha Muziki wa Congo. (Kizazi cha nne ni akina JB, werason nk). Katika Albamu mpya ya Celeo Nzoto na Nzoto 10+, kuna wimbo ambao ni kolabo ya Celeo Scam na Fally Ipupa, Single hii ni moto wa kuotea mbali. Prodyuza Maghambo upooo?

BCBG Ndani ya Rotterdam

Mdau akiwa amepozi na Genta, mmoja wa wanamuziki wa kundi la Wenge BCBG, Picha hii imepigwa na Ronald mnazi hasa wa Wenge. Kundi la Wenge BGBG waliwasili Rotterdam majuzi kwa ajili ya onyesho lao ambalo limefanyika usiku wa kuamkia leo. hapa ni kwenye duka maarufu la Muziki wa Kiafrika la Tshobo shop linalomilikiwa na “Mjasiriamali” Papaa Danny Kulia.
Mwanamuziki Tshai Ngenge akiwa mitaani Rotterdam

Nono Fuji, Ni mmoja wa vifaa vya JB Mpiana, kijana hatari huyu, Picha na habari za shoo hii zaja.

Kablba ya onyesho la jana BCBG waliwasha moto Sweden usiku wa tarehe 24 May 2008, pata kipande cha shoo ya Sweden hapo chini.

MISS UNIVERSE TZ 2008 NI AMANDA

Mrembo Amanda Sululu(pichani) jana aliibuka mshindi katika kinyang’anyiro cha kumtafuta Miss Universe Tanzania 2008. Shindano hilo lilifanyikia jana usiku katika ukumbi wa Hoteli ya Movenpick jijini Dar-es-salaam.Kwa maana hiyo Amanda ndiye anarithi taji kutoka kwa Flaviana Matata mrembo ambaye mwaka jana alifanikiwa kuiletea sifa Tanzania baada ya kufanikiwa kuwemo katika tano bora ya mashindano hayo katika ngazi ya dunia yaliyofanyikia nchini Mexico.

Tatu bora-Katikati ni Amanda Sululu,kushoto ni Jamila Nyanga(mshindi wa pili) na kulia ni Eva Babuely(mshindi wa tatu)

Mashindano ya Miss Universe mwaka huu yanatarajiwa kufanyika tarehe 14 Julai katika ukumbi uitwao Crown Convention Center(Diamond Bay Resort) mjini Nha Trang nchini Vietnam.Zaidi ya washiriki 80 kutoka nchi mbalimbali wanatarajiwa kushiriki.

Habari na picha Bongo Celebrity

Ze Comedy waibukia TBC1

KUNDI la vichekesho la Ze Comedy jana lilitangaza kuingia mkataba wa mwaka mmoja na kituo cha televisheni la TBC 1.

Akizungumza kwa niaba ya kundi hilo, msanii Emanuel Mgaya ‘ Masanja’, alisema vituo vingi vya televisheni nchini waliomba kufanya nao kazi, lakini wao wamejali kituo kilichotoa mkataba mnono.
Alisema kwa sasa wameamua kuweka wazi mkataba huo, ili wapenzi wao wajue kuwa kundi lipo na sasa linaanza kazi rasmi kituo hicho walichokitangaza.
Pia alisema kundi hilo limepata mlezi mpya ambaye ni Yusuph Manji, hivyo wanaamini watafanya kazi vizuri.
Wasanii wanaounda kundi hilo ni Emanuel Mgaya ‘Masanja’, Vengu Shamba, Lucas Mhuvile ‘Joti’, Alex Chalamila ‘Mark Leagan’, Issaya Mwakilasa ‘Wakuvwanga’, Mjuni Sylvery ‘Mpoki’ na Sekion David.

Friday, May 30, 2008

Wazee wa Masauti kupamba Miss Tanga

Washiriki wa Miss Tanga mwaka jana, kabla ya mashindano, mwaka huu mashindano hayo yanafanyika uwanja wa Mkwakwani na yatasindikizwa na Wanapekechapekecha Akudo Impact wazee wa Masauti.

BENDI ya Muziki wa Dansi ya Akudo Impact ya Jijini Dar es Salaam, inatarajia kutumbuiza katika mashindano ya Urembo ya Miss Tanga yanayotarajia kufanyika Juni 7 mwaka huu Mkoani humo.

Akizungumza na Mwananchi Mkurugenzi wa Kampuni ya Five Brothers Intertainment Nassor Makau alisema kuwa shindano hilo litafanyika katika Uwanja wa Mkwakwani.

Akizungumzia mashindano hayo Makau aliwataja warembo watakaoshiriki kinyang’anyiro hicho kuwa ni Doris Steven, Judith Assey, Mariam Mhando, Amina Sadick, Halima Khalfani, Aisha Abdalah, Nuru Salim na Beatrice Lwimba.

Aliwataja wengine kuwa ni Oliver Mango Mwajuma Msangi, Agnes Mwakipesile, Hadija Ramadhani, Hawa Njama, Mariamu Hajibu, Marie Frederick, Mwanamina Bausi, Silvia Urio, Samia Mohamed, Shamim Said, na Evelyine Thomas.

Makau alisema kuwa warembo hao wamepatikana kutokana katika vitongoji vya Miss Usagara, Miss Korogwe, Miss Vyuo na Miss Lushoto.

Warembo watatui watakaopatikana katika shindano ya Miss Tanga, watapata tiketi ya kushiriki Miss Tanzania mwaka huu. Mrembo anayeshikilia taji hilo ni Victoria Martin ambaye alifanya vyema katika mashindano ya Taifa mwaka jana na kuingia tano Bora.

Blanchard Deplaizir anataka “Kolabo” na Alikiba

Msanii DePlaizer ameweka wazi kuhusiana na hisia zake za kutaka kufaya kazi na wanamuziki wa barani afrika ikiwa ni moja katika malengo yake katika kuunyanyua muziki wa kifrika duniani.

Kijana huyo mwenye umri wa miaka 29 anayeendeleza makamuzi huko nchini Uingereza katika jiji la Manchester ameweka wazi sana kuwa anavutiwa saaaaaana na msanii Alikiba na yuko mbioni kuangalia uwezekano wa kurekodi nae wimbo wa pamoja “nadhani nitafurahi sana iwapo nitapata nafasi ya kupiga nae mkono” alisema msanii huyo alipokuwa akifanya mahojiano na Bongo5.

Alitaja sababu zilizopelekea yeye kuvutiwa na msanii Alikiba, ni wimbo wake wa ‘cinderela’ kuanzia sauti na melody hata mpangili wa Beat vinamfanya jamaa azidi kupagawa na msanii huyu.
Wimbo wa Cinderela inasemekana uko juu sana nchini Uingereza kuliko ngoma kibao za watanzania ambazo husikika.

Msanii Alikiba ambaye yupo nchini Uingereza kwa sasa, kwa ziara maalum ya kimuziki ambapo ameshafanya maonesho kadhaa na hivi karibuni anatarajia kurejea nchini.

De Plaizir nusra achanganyikiwe baada ya kusikia msanii Alikiba amekuja nchini Uingereza kwa ajili ya maoenesho “nilipata taarifa ya ujio wa Alikiba Uk kutoka kwa meneja wangu wa Tanzania Sophia Kessy ambaye alikutana na Alikiba kabla ya kuja huku na kumtaka akutane na mimi na kupanga lolote kuhusiana na kazi za kisanii na yeye hakuwa na pingamizi, sasa nachokifanya nadhani nitahakikisha namtafuta kabla hajaondoka”

Unaweza kuona ni jinsi gani msanii De Plaizir anavyoweza kujitanga za pande hizi za bongo na afrika kwa ujumla, jitihada za kumtafuta alikiba bado zinaendelea na akipitakana tutasikia nae upande wake una lipi kuhusiana na show yake na kolabo yake na mtu mzima De Plaizir.

Bongo5

Thursday, May 29, 2008

Ali Kiba ndani ya Club Afrique – London

CLUB AFRIQUE LONDONPROUDLY PRESENTSALI KIBA
TANZANIA’S CHART BURSTING ARTISTEWHEN : FRIDAY 30TH MAY 2008WHERE:CLUB AFRIQUECANNING TOWN, LONDON


FEE: £10ALL EAST AFRICANS ARE WELCOME

Mtanange wa Taifa Stars na Mauritius

Mwenyekiti wa baraza la michezo nchini (BMT )Idd Kipingu,katikati,akifafanua jambo kwa wachezaji wa Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars),wakati wa Uzinduzi wa Kampeni ya kuhamasisha watanzania kwenda kuishangilia timu hiyo kwenye pambano la kimataifa na Mauritius litakalofanyika jumamosi wiki hii kwenye uwanja mpya wa taifa jijini Dar es Salaam, hafla hiyo ilifanyika kwenye ofisi za shirikisho la soka Tanzania (TFF) jana,kushoto ni Afisa habari wa Kampuni ya Serengeti Bia(SBL) Tedy Mapunda na kocha mkuu wa Stars Macio maximo.
Na Haki Ngowi

WENGE BCBG yawakati huo

Enzi hizo bado wakiitwa Wenge BCBG wakiwa wamekamili JB Mpiana, Werason Makanda, Adolph Dominguez, Engineer Blaise Bulla, Allain Makaba, Alan Mpella na Roberto Wunda Ikokota Machine, Typewriter,Honet F15 vyovyote utakavyomuita, Big Prodyusa Magambo upoo? Bonyeza hapa upate Sebene.

CHELSEA yatenga Paund M80 kwa ajili ya usajili

Didier Drogba akiwa na kombe la FA pamoja na tajiri Roman Abramovich, Abramovinch anatarajia kocha ajaye wa Chelsea atarudisha hadhi ya Chelsea kwa kurudisha Vikombe vya ushindi.

Kocha mpya wa Chelsea atapokelewa na kitita cha Paund milioni 80 kwa ajili ya kununua wachezaji wakuongeza nguvu kwenye timu hiyo. Hayo yalisemwa na mmiliki wa timu hiyo Bilionea Roman Abramovich alipokuwa akiongelea juu ya mstakabali ya kocha wa klabu hiyo alipokuwa anahojiwa na Television ya Chelsea.
“Kocha mpya lazima aelewe tunataka nini, pesa imetengwa kwa ajili ya usjili, tutasajili kutokana na mapendekezo ake pia, ila mwisho wa siku ni vikombe ndio tunataka” alisema Abramovinch
Chelsea imewataja Straika wa Valencia David Villa, Mchezaji kijana wa Barcelona Giovan Dos Santos pia wamemtaja mpachika mabao wa Inter Millan Zlatan Ibrahimovic

Celtel imejitosa kudhamini Gofu

KAMPUNI ya simu za mkononi ya Celtel imejitosa kudhamini kwa miaka mitatu mashindano ya kimataifa ya gofu yanayotarajia kuanza Dar es Salaam kesho kwa sh.milioni 120.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Meneja Uhusiano wa kampuni hiyo Beatrice Singano, alisema Celtel inaona fahari kudhamini mashindano hayo kwa vile ni mwendelezo wa sera yake ya kuboresha maisha.

Alisema Celtel ilisaini mkataba huo na klabu ya gofu ya Lugalo ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Februari mwaka huu, ambapo jana Celtel ilikabidhi sh. milioni 7 ikiwa ni sehemu ya mkataba huo, ambao ni sh.milioni 40 kwa mwaka.

Naye nahodha wa klabu ya gofu ya Lugalo, Brigrdia Jenerali, Julius Mbilinyi, aliishukuru Celtel kwa kuokoa mashindano hayo na kuyapa nguvu ya uhakika wa kufanyika kwa miaka mitatu mfululizo.

Alisema mashindano hayo ya siku tatu yatakayokuwa wazi kwa washiriki wa ndani na nje ya nchi yanatarajiwa kuanza kesho na yanatambuliwa na Shirikisho la Gofu Tanzania (TGU) na yanatarajia kushirikisha wachezaji 150 kutoka nchi mbalimbali duniani.

Alisema kwa udhamini huo wa Celtel, klabu hiyo ya Lugalo imeweza kumwagilia maji kwenye uwanja utakaotumika na kuupa hadhi ya kimataifa na kutoa zawadi bora kwa washindi, ambazo zitahusisha vikombe na fedha taslimu na pia kuboresha miundombinu mingine uwanjani hapo.

Serikali ya China yasimamisha burudani kwa siku 3 kuomboleza

Yao Ming

AFP/Shanghai
Television nchini China zilisimamisha kwa muda kutangaza aina yeyote ya michezo na burudani kwa siku tatu mfululizo ikiwa ni ishara ya kuomboleza walikufa kwa tetemeko ambalo limegharimu maisha ya maelfu ya watu nchini humu siku za karibuni.

Tangazo la serikali lilisambazwa kwenye vituo vyote vya Redio na Televisheni nchini humo, China imekuwa na idadi kubwa ya waangalia hasa mchezo wa ligi ya mpira wa kikapu ya NBA baada ya Mchezaji mwenye asili ya Uchina Yao Ming anayechezea timu ya Houston Rockets kujiunga na ligi hiyo. Ming kwa sasa ndio mchezaji mrefu kuliko wote kwenye ligi ya NBA akiwa na urefu wa 7 feet 6 inches (2.29 m). Katika mchezo wake wa kwanza kwenye ligi hiyo inakisiwa wachina wapatao milioni 200 duniani waliuangalia mchezo huo kati ya Houston Rockets and Milwaukee.
Pamoja na machungu ya kupotelewa na ndugu jamaa na marafiki bado wachina walilalamika kwa idara husika na kuomba walao mechi za NBA pekee ziruhusiwe. Kwa kuonyesha mchezo huu ni maarufu kwa sasa NBA wamefungua ofisi China ambayo pamoja na mambo mengine inaratibu shughuli zote za kibiashara ikiwa ni mauzo ya Jezi, usimamizi wa Matangazo ya biashara na mikataba kwani kwa sasa kampuni za huko zinatangaza zaidi kwenye ligi hiyo.

Wimbo wa Taifa

Kelly Rowland toka kundi la Destiny’s Child akiimba wimbo wa taifa wa USA kabla ya kuanza kwa mechi ya mpira wa miguu kati ya USA na England iliyofanyika Wembley Stadium hapo jana, England ilishinda kwa magoli 2-0.

BASATA wachimba mkwara kuzifungia FM Academia, TOT Respect na Akudo Impact

Mmoja wa wanenguaji wa Akudo Impact akipekecha jukwaani, Uvaaji kama huu ndio uliopigiwa mkwara na Baraza la Sanaa la Taifa.
Na Majira
BARAZA la Sanaa la Taifa (BASATA) limetishia kuzifungia bendi za FM Academia, TOT Respect na Akudo Impact kwa maelezo kuwa wanenguaji wake kuvaa vichupi wawapo jukwaani.
Kwa mujibu wa barua iliyoandikwa na BASATA kwenda kwa Wakurugenzi wa bendi hizo yenye tarehe ya juzi na kusainiwa na F.Magoti kwa niaba ya Kaimu Katibu Mtendaji wa BASATA, ilieleza kuwa katika siku za karibuni bendi hizo zimekuwa zikifanya maonesho ya muziki yanayoambatana na wanenguaji wa kike waliovaa ‘vichupi’.
Barua hiyo ilieleza kuwa kitendo hichoo ni ukiukwaji wa maadili ya Watanzania na ni kuwdhalilisha wanenguaji na watazamaji wanaohudhuria maonesho ya bendi hizo.
“Kwa barua hii Baraza la Sanaa la Taifa linawapa onyo kali kuacha kabisa vitendo hivyo na kuhakikisha kuwa wanenguaji wenu wanavaa nguo za heshima zisizoonesha kwa namna yeyote ‘vichupi’ hadharani.

” Baraza halitasita kuchukua hatua ikiwemo ya kufungia bendi zenu, ikithibitika kuwa mnaendelea na ukiukwaji huo,” ilisema sehemu ya barua hiyo.
Alizitaka bendi hizo kukumbuka kuwa maonesho yao hayaishii katika kumbi za burudani pekee, bali yamekuwa yakiharibu kwa kuwaonesha watoto wadogo kupitia vyombo vya habari kama vile magazeti na televisheni.
“Tukiamini kuwa lengo letu ni kuonesha umahiri na ustadi wa muziki wa bendi zetu, basi suala la kuonesha ‘vichupi’ halitajitokeza katika bendi zenu, “ilisema barua hiyo.

Nakala ya barua hiyo imepelekwa kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo, Mkurugenzi wa Maendeleo ya Utamaduni na Maofisa Utamaduni wa Wilaya za Temeke, Kinondoni na Ilala.

Bekham na kofia ya dhahabu

Mchezaji wa England David Beckham akiwa na Kofia yake ya Dhahabu aliyopewa na Mkongwe Boby Charlton, ikiwa ni kuthamini mchango wake wa 100 kwa timu ya Taifa ya England kabla ya kuanza kwa mchezo wa jana dhidi ya USA.

ENGLAND yaichapa USA 2-0

Mchezaji wa England John Terry (R) akishangilia goli lake dhidi ya USA wakati wa mechi baina ya England na USA wembley jana.

Wachezajiwa England David Bekham (l) John Terry namba 6 mgongoni wakishangilia baada ya kuwabwaga USA kwa goli 2-0 kwenye mchezo wa kirafiki jana.

Mchezaji Stephen Gerald akishangilia baada ya kupachika bao la pili dhidi ya timu ya USA kwenye mchezo wa kirafiki uliochezwa Wembley Stadium jana.

Wafungaji wa magoli ya England ya jana John Terry na Stephen Gerald wakipongezana.

LONDON (AFP) –
John Terry aliweka pembeni machungu ya Champions League na kuisaidia timu yake ya taifa ya England kushinda dhidi ya timu ya taifa ya USA katika mchezo wa kirafiki uliochezwa jana.

Krosi ya David Bekham ndio iliyozaa goli la Terry mwishonbi mwa kipindi cha kwanza ambapo England hawakuonyesha machchari ki viiile.

Gareth Barry Stephen aliingizwa na kocha Cappelo ili kuongeza nguvu na kusaidiana na Steven Gerrard aliyepachika bao la pili.

Nafasi pekee ambayo USA waliipata ya wazi ni pale Eddie Johnson mpira wake ulipogonga besela kwani walikuwa na wakati mgumu wakishambuliwa sana hasa kipindi cha pili.

Mechi ya jana ilikuwa muhimu kwa Terry kupachika bao kwanza kama Kepteni kwa wakati mwingine chini ya kocha Capello na pili ni kufuta machungu ya kukosa penati siku saba zilizopita kwenye mechi ya Champions Ligi dhidi ya Manchester United.

Kocha Fabio Capello alisema ni “nafasi pekee ya kumsaidia kisaikolojia vinginevyo angeona hatuna imani naye, penati ni 50 kwa 50, lakini tabia ya waingereza hawaoni ni kwa nini ukose penati, kipa anasamehewa kwa kufungwa penati lakini sio mpigaji” alisema Capello.

Kwangu mimi kama kocha naelewa ni nusu nusu lakini wapenzi wa huku hata kwa maoni yao hawaoni ni kwa nini ukose penati aliongeza Capello huku akicheka.

Hapakuwa na idadi kubw ya watu kama ilivyotarajiwa kwani baadhi ya viti vilikuwa wazi hasa upande mwekundu kwa kile kilichooelezwa ni “Low profile match” na mashabiki.

Wednesday, May 28, 2008

John Terry kuongoza kikosi cha England dhidi ya USA

Kocha wa timu ya England Fabio Capello amemtaja John Terry (pichani) kuwa ndiye captain katika mchezo wa kirafiki dhidi ya USA utakao fanyika leo.

Terry amepewa heshma hiyo ikiwa ni utaratibu wa sasa wa kubadilishana kabla ya kuteuliwa mchezaji mmoja kuongoza hilo jahazi kwa kipindi chote.

Capello amesema kuwa anatumai kumpa Terry ukepten ni kuonyesha imani yake kwake na kumfanya aone kuwa bado tunaimani naye hasa baada ya kukosa penalti dhidi ya manchester jambo ambalo Terry linamuuma sana na hataki kamwe kukumbushwa hilo, “nafikiri ataichukulia ile kama changamoto aweze kuonyesha umma kuwa kosa ni kurudia kosa” alisema Capello. Mchezo wa leo n wa kirafiki baina ya England na USA lakini kila mtu katika mataifa hayo mawili amekuwa akiuzungumzia.

Barcelona yamchukua Gerald Pique wa Manchester

Timu ya soka ya Barcelona imemsajili mchezaji wa Manchester United Gerard Pique katika mkataba wa miaka minne kwa gharama ya paund milion 5.

Mchezaji huyo mwenye miaka 21 alijiunga na klabu ya Manchester mwaka 2004 lakini alikuwwa hapangwei mara kwa mara kwenye kikosi cha kwanza cha Manchester kwani tangu aingie amecheza mechi 23 tuu na kufunga magoli mawili pekee dhidi ya Dynamo Kiev na Roma. Kocha wa Barcelona amesema anamjua Pique na combination ya mpira anayocheza ndio maana hakuweza kupata mafanikio Manchester na kusema ana hakika atafanya vizuri kwa combination aliyonayo Barcelona.

ESPN May 2008.

Liverpool yaichimbia mkwara Chelsea kuhusu Torres

Timu ya mpira ya Liverpool imechimba mkwara kwa klabu ya Chelsea na kuwaambia mchezaji wao mwenye uraia wa Spain Fernando Torres hauzwi hata kwa gharama yeyote!.

Chelsea inasemekana kuweka nguvu nyingi sana katika kumuwania kumchukua Torres hasa baada ya mchezaji huyo kumaliza msimu huu kwa mafanikio makubwa.

Chelsea walikuwa wameahidi kutoa kitika cha paund milioni 50 kwa klabu ya Liverpool kwa ajili ya kumuchukua nyota huyo wa zamani wa Atletico Madrid lakini Liverpool imekataa ofa hiyo kwa kusema kuwa bado wanamuhitaji ila kama Chelsea wana mchezaji mwenye kiwango cha Toress wao Liverpool wangemtaka pia.alisema Rafa Benitez.

Ufaransa mbabe kwa Ecuado

Mchezaji wa timu ya taifa ya Ufaransa Bafetimbi Gomis akishangilia mara baada ya kupachika kimiani goli la pili kwenye mechi ya kirafiki kati ya Ufaransa na Ecuado.

Mchezaji wa Ufaransa Hatem Ben Arfa, shoto, akisakata goma kumtoka mchezaji wa Ecuado Isaac Mina, wakati wa mchezo wa kirafiki wa kujipima nguvu dhidi ya timu hizo mchezo uliofanyika huko Alps stadium, Grenoble Ufaransa, jana jumanne, May 27, 2008. Ufaransa ilishinda 2 – 0. Ufaransa ilitumia mechi hii ya mwisho ya majaribio ili kuchagua kikosi chake cha watu 23 kwa ajili ya michuano ya EURO 2008, kwa sasa kikosi kina wachezaji 30.

Austria 1-1 na Nigeria mechi ya kirafiki

Mchezaji wa Austria Emanuel Pogatetz (L) akiwania mpira na Ikechukwo Uche wa Nigeria wakati wa mchezo wa kirafiki wa soka huko Graz, Austria wanajiandaa na mtanange wa kombe la EURO, mechi hii ilimalizika droo ya 1-1.

Tuesday, May 27, 2008

Fally kuwasha moto Ufaransa

Kila mtu na nyota yake, Tiketi za kumuona mwanamuziki toka Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo FALLY IPUPA “DICAP LA MERVEILLE” zimekwisha na zilikuwa zinauzwa Euro 100 kila moja, Waandaaji wa onyesho hilo wametenga kuuza Tiketi 200 tuu na hakutakuwa na tiketi ambayo itauzwa mlangini siku ya onyesho, ilisema taarifa hiyo toka kwa Yemima Ipupanaise. Onyesho hili litafanyika june 6. katika ukumbi wa Claude Makelele’s posh club, Paris.

Ferre Gora atimuliwa ulaya kwa kudanganya VISA!

Mwanamuziki wa Congo Ferre Gola (pichani) hivi karibuni alipata dhahma baada ya kitiwa nguvuni yeye pamoja na wanamuziki wa bendi yaki akiwa kwenye mpaka wa Belgium kuingia Ufaransa, akielekea kwenye shoo yake ambayo ilipangwa kufanyika Strasbourg ,inadaiwa kuwa Ferre alipata dhahma hiyo baada ya kutumia pasi za kusafiria ambazo zilikuwa zimekwisha muda wake, Akiongea nami mdau Mumuu Chizange alisema Kabla ya dhahma hiyo Ferre alifanya onyesho Belgium, onyesho ambalo linadaiwa kuwa na wahudhuriaji wachache sana hata baada ya kiingilio kushushwa toka Euro 30 hadi 10 bado hakupata watu, akizungumzia dhahma hiyo promota wa mwanamuziki huyo Lumba Bawu ambaye alikuwa akiratibu safari ya ke amesema kuwa kitendo alichofanya Ferre si cha kiungwana kwani alithubutu hata kudanganya pale alipoulizwa kuhusu Visa za Ufaransa akasema kuwa anazo ziko Valid hadi mwezi July, naye producer Fridolin Bokomo ambaye alikuwa akiratibu ziara ya mwanamuziki huyo Holland alisema kuwa Ferre amewatia hasara kwa ajili ya maandalizi ya maonyesho yake, Ina wezekana Ferre akapata adhabu kali kutokana na kitendo hicho kwani mwanamuziki Papa Wemba aliwahi kupata matatizo kama hayo pia.

Pichani ni baadhi ya matangazo ya maonyesho ya Ferre

Pichani ni baadhi ya matangazo ya maonyesho ya Ferre

Nani kumrith Grant Chelsea?

BAADA ya aliyekuwa Mocha Mkuu wa timu ya Chelsea Avram Grant (pichani) kufungashiwa virago mwishoni mwa wiki, tetesi zimeanza kusambaa juu ya makocha ambao watarithi mikoba yake.

Grant alitimuliwa Jumamosi baada ya Chelsea kufungwa na Manchester katika mechi ya fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya iliyofanyika Jumatano iliyopita na baada ya timu hiyo kumaliza Ligi Kuu ya England ikishika nafasi ya pili, hali ambayo imeacha milango wazi kwa kocha atakayechukua mikoba hiyo.

Kutokana na hali hiyo magezeti ya Uingereza tangu Jumapili yalikuwa yamejaa tetesi mbalimbali juu ya atakayekabidhiwa funguo na mmiliki wa timu hiyo Roman Abramovich kitendawili ambacho bado kinasumbua vichwa mashabiki wa Ligi Kuu hadi utakapokuwa umefikiwa uamuzi.

Kocha anayepewa nafasi kubwa kuchukua mikoba hiyo ni Frank Rijkaard, ambaye naye alifungashiwa vilago na timu ya Barcelona mara tu baada ya Grant kutimuliwa.

Rijkaard alitimuliwa katika nafasi yake baada ya klabu hiyo ya Catalan kukosa ubingwa msimu huu ikiwa ni mara ya pili mfululizo, lakini hata hivyo kocha huyo bado anaaminika ndiye kocha bora katika klabu kubwa duniani, hali ambayo inamfanya apewe nafasi kubwa kuinoa Chelsea.

Kocha mwingine ambaye ametajwa na vyombo vya habari vya Uingereza ni Guus Hiddink, ambaye anapewa nafasi hiyo kutokana na kuonesha ni kocha mzuri kufuatia mafanikio aliyoyaonesha katika kazi yake ya sasa ya kuinoa timu ya taifa ya Urusi, ambayo mshahara wake analipwa na mmiliki wa Chelsea, Abramovich.

Mbali na hayo pia kocha huyo ni rafiki wa karibu wa Abramovich na hivi sasa Hiddink tayari amekubali kwa masharti kuinoa timu ya taifa ya Urusi.

Makocha wengine ambao wanapewa nafasi hiyo ni Roberto Mancini, ingawa kocha huyo anapewa nafasi kama Rijkaard na Hiddink wataikataa nafasi hiyo wao wenyewe.

Pia kyumo Sven-Goran Eriksson ambaye kwa kipindi kirefu amekuwa akimvutia Abramovich na mara mbili kocha huyo amewahi kukutaa kuifundisha Chelsea .

Kocha huyo aliwahi kunaswa na kamera akifanya mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu wa Chelsea, Peter Kenyon wakati alipokuwa bado Kocha Mkuu wa timu ya taifa ya England na hivi sasa anakaribia kuwa huru baada ya mmiliki wa Manchester City, Thaksin Shinawatra kumtema.

Mark Hughes naye pia ni miongoni mwa kundi hilo, ambapo Hughes anapewa nafasi hiyo, baada ya kuifanya Blackburn Rovers kuwa moja ya timu ngumu msimu huu, hali iliyoifanya kumaliza msimu huu ikiwa nyuma ya timu nne za mwanzo.

Hughes vilevile ana uzoefu na timu za taifa baada ya kuiongoza Wales kutinga katika michuano ya fainali za mataifa ya Ulaya mwaka 2004 na pia amewahi kuichezea Chelsea hadi alipotundika daruga.

Mwingine ni aliyekuwa kocha wa timu hiyo Jose Mourinho, ambaye alikuwa kipenzi cha mashabiki wa timu hiyo ya Stamford Bridge na baada ya kuondoka mwezi Septemba mwaka jana uhusiano na Abramovich unaonekana kuwa mzuri.

Uhusiano huo ulidhihirika baada ya Mrusi huyo kumnunulia Mourinho gari aina ya Ferrari yenye thamani ya dola milioni 4 mwaka huu kama zawadi.
Na Majira

Picha zaidi za shoo ya BCBG

Mdau wa BCBG Twaha Makau pamoja na wadau wengine wameomba kuona picha zaidi za Papa Cherry na kundi zima la BCBG walipokuwa Bruxells Belgium hivi karibuni nami sina hiana ipo stock ya kutosha tuu hata kutumiwa watumiwa.

Anaitwa Virginie, Kifaa hiki kinasemekana kuwindwa sana na hasimu mkuu wa JB Werason na Koffi, angalia live za JB uone mambo yake.
Papa Cherry

Zadio Congolo akimtunza JB Mpiana, Jamaa huyu ni mpenzi mkubwa wa JB Mpiana husafiri kila mara JB anapokuwa na Onyesho nchi yeyote ya Ulaya.
Elodie Lipassa

[image]
Genta

[image]
Rio

[image]
JDL


Jules Kibens

Genta – Kibens – Chai Ngenge – Rio

Watu wakitawanyika hasubuhi saa moja kasoro baada ya shoo kuisha
Wadau wakitawanyika majira ya saa moja asubuhi baada ya shoo ya usiku kucha.

Monday, May 26, 2008

Marina Bay: Mahali pa maraha Singapore

Pamoja na njia mbali mbali za kufika Marina Bay ukitumia njia ya Boat maalum unapata mandhali nzuri zaidi na picha mwanana kama hii.
Uwanja wa Mpira ambao umo kwenye sehemu ya Bahari ambao uko mbioni kukamilika sehemu chache za nje ila uwanja waweza kutumika, picha hii niliipiga nikiwa ndani ya Singapore Flyer (picha ya chini).
Singapore Flyer ina urefu wa mita 165, ndio flyer kubwa zaidi duniani na ya kwanza kwa Asia imejengwa kwenye muinuko katika eneo maarufu la Marina Bay, Ndani ya hii flyer unaweza kuona mandhari ya mji mzima wa Singapore na nchi jirani kama Malaysia na Indonesia. ilizinduliwa tarehe 15 April na tiketi kwa ajili ya uzinduzi zilikwisha kwa siku tatu mfululizo zikiwa zinauzwa USD 8000, Booking ya Flyer inabidi ifanywe mapema kwani huwa imejaa kwa miezi miwili hadi mitatu kabla ila nafasi maalumu huwekwa kwa ajili ya wageni (watalii). soma hapa zaidi

Reuters – Pictures of the Year 2007

Kalbfleisch (anayechungulia) akijiandaa kumkabili mshindani wake katika michezo ya wazi ya Sumo huko Los Angeles, April 7, 2007. REUTERS/Lucy Nicholson.
Wakati huo akiichezea timu yake ya Arsenal, Thierry Henry akionyesha kuumiliki mpira kwa style ya aina yake huku David Bentley wa Blackburn Rovers akimuangalia wakati wa mchezo baina yao uliofanyika uwanja wa Emirates London February 17, 2007. Picha na Eddie Keogh.
Mchezaji wa Manchester United Nani (aliyeruka juu) akishangilia baada ya kufunga goli dhidi ya timu ya Tottenham Hotspur huko Manchester, Kaskazini mwa England, August 26, 2007. REUTERS/Phil Noble, Picha hizi ni baadhi ya picha zilizomo kwenye mkusanyiko wa Picha bora za mwaka jana za shirika la habari la REUTERS, kwa picha zaidi za Mwaka 2007 bofya hapa

Miss Tanzania Europe 2008

The mission of the Miss Tanzania Europe Pageant is to promote Tanzania and its people in the rest of the World: Tourism, culture, the beauty of this East African Nation.
We aim to further raise awareness on issues pertinent to Tanzania and most of all empower the Tanzania Queen to educate and enlighten communities as a goodwill ambassador for Tanzania.
The winner of Miss Tanzania Europe 2008,chosen on June 28th in Essen, Germany,and first runner up will represent Tanzania Europe*at the Miss Tanzania pageant to be held in Dar es Salaam in August 2008.
If you want to apply,
please go on the Application-
Page If you wish to apply for running in the Miss Tanzania Europe Pageant,you must be at least 18 years of age,of Tanzanian origin and residing in any State of the European Union which is a Member of the so called
“Schengen-Agreement”.
Na Haki Ngowi

Taifa Stars yatoka Sare ya 1-1 na Malawi

Jioni hii Taifa Stars ya Tanzania ilikuwa ikipimana ubavu na timu kutoka Malawi, The Flames, ambapo timu zilitoka sare ya bao moja kwa moja. Pichani ni mchezaji wa Taifa Stars Mrisho Ngasa(kulia) akijaribu kumtoka beki wa Malawi, Wisdom Ndlovu.

TIMU ya soka ya Taifa ‘Taifa Stars’ na ile ya Malawi jana zilifungana bao 1-1 katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa uliofanyika Uwanja Mkuu mpya wa Taifa, Dar es Salaam.

Maelfu ya mashabiki wa Taifa Stars iliwabidi wasubiri hadi dakika ya 79 kushangilia bao la kusawazisha lililofungwa na Salum Sued baada ya kutokea kizaazaa katika lango la Wamalawi.

Kabla ya bao hilo Stars ilifanya mashambulizi mengi langoni kwa Malawi, lakini umaliziaji haukuwa mzuri, huku washambuliaji Mrisho Ngassa, Danny Mrwanda, Emmanuel Gabriel kwa nyakati tofauti wakikosa nafasi nyingi za ushindi.

Iliwachukua dakika tano Stars tangu kuanza mchezo kwa kubisha hodi langoni mwa Malawi, baada ya Gabriel kukosa bao akiwa amebaki na kipa wa Malawi, kabla mpira haujaokolewa.

Stars ilizidisha mashambulizi, ambapo dakika ya 14 Mrisho Ngassa kidogo afunge, wakati shuti lake lilipookolewa na kipa Valence Kamzere.

Malawi nayo ilijipanga na kufanya mashambulizi ya kushtukiza, lakini nayo pia umaliziaji ulikuwa dhaifu, huku ngome ya Stars ikiondoa baadhi ya hatari.

Bao la Malawi lilifungwa dakika 54 na Essau Kanyenda aliyeunganisha vyema mpira kutoka wingi ya kushoto, huku mabeki wa Stars wakiwa wamezubaa.

Nafasi ambayo Stars itaijutia zaidi ni ile ya dakika ya 86 wakati shuti la Nadir Haroub ‘Cannavaro’ lilipogonga mwamba na mpira kurudi uwanjani, lakini mchezaji huyo alipigwa na butwaa huku akinyoosha mikono kushangilia, akijua tayari mpira ulitinga wavuni.

Wachezaji Nizar Khalfan na Godfry Bonny nao kwa nyakati tofauti walipiga mashuti langoni kwa Malawi na kutia matumaini.
Habari na Majira, picha na Global Publishers

Sunday, May 25, 2008

Photo Baraza na utani kwa picha.
Aaaah!! Bwana wee, kila mmoja ana jicho lake anavyouangalia mpira huo huo tulio uangalia mimi na wewe, tembelea Photo Baraza uone hizi na nyinginezo!!

Bwana wee, furaha haina mwisho atii


Bwana wee furaha haina mwisho mtu waweza sherehekea hata mwaka mzima Rukhsa!!!!

BOB Wine-From Zero to Hero

Bob Wine akiongea na mdau kwenye mahojiano maalum ambayo utayapata ndani ya jarida la Eastafrica Uk
Mhh wapo wengi waliwabeza wanamuziki wa kizazi kipya si Tanzania tuu hata Mwanamuziki kutoka Uganda Bob Wine hakutarajia kufika na kufanikiwa kama alivyosasa, pichani ni “mjengo” wa mwanamuziki huyo. Kwa mahojiano kamoli tembelea gazeti tando la Miss East Africa.

Mr & Miss East Africa, ha ha haa Habari ndiyo hiyooo!

Mashindano ya Mr & Miss East Africa Uk yanatazamiwa kufanyika tarehe 26 July 2008 na kushirikisha walimwende na vijana watanashati toka pembe hiyo ya Africa. Mshindi wa mashindano haya pamoja na mambo mengine husaidia kwenye shughuli za kujitolea kwa ajili ya watoto waliona shida huko nyumbani Africa ya Mashariki kwa ujumla. Kwa mwaka huu pamoja na burudani kadha wa kadha zilizoandaliwa usiku huo utapambwa na Mwanamuziki Ali Kiba
Kwa mengi zaidi Bofya hapa. Pia waweza tembelea gazeti lao linalopatikana online, pichani chini ni moja ya picha zilizomo kwenye Issue Mpya ya Gazeti hilo

Beauty in the Jungle
washiriki wakiwa kwenye pozi katikati ya Jungle
Blanchard De Plaizir Nyota mpya katika Muziki wa Congo

Wimbo huu umeandikwwa na Muimbaji kijana anayekuja kwa kasi kwenye fani ya Muziki wa Congo kwa jina ni Blanchard de Plaizir, Homme Plus inaongelea hadithi ya mdada mmoja mdogo mrembo ambaye aliangukia kwenye penzi la kijana mtanashati na maarufu ambaye binafsi alimuona kwenye Tv na magazeti ya watu maarudu (celebrity magazines) na kuamini kuwa hatoweza kukutana na kijana huyu kamwe katika maisha yake ya kawaida mdada analalamika na kuona kuwa dunia haimtendei haki katika ulimwengu wa mapenzi, kijana anajitahidi na muziki wake ni mzuri kwa kweli.
Cover ya CD ya Deplaizir

Blanchard anaishi Manchester Uingereza, alizaliwa Congo lakini alihamia Uingereza akiwa na umri mdogo ila anasema nia yake ni kuuendelez utamaduni wake hata kama yuko nje ya nchi yake. Katika albamu yake hii Blanchard amemshirikisha aliyekuwa mpiga Gitaa mahiri wa BCBG Burkina Faso Mboka lia. (utamsikia vizuri kwenye Albamu ya Pentagone)


Kwa sasa shughuli za kimuziki za Blanchard kwa East Africa zinaratibiwa na Meneja wake Mtanzania akiwa ni mtangazaji wa Radio ya Clouds FM Sophia Kessy ndiye anayeratibu shughuli za Blanchard na kwa sasa anamuandalia safari ya kuitambulisha Albamu yake ya kwanza nchini Tanzania.

Vichapo vya Man U vyaotesha nyasi “chibarua” cha Grant Chelsea.

Pamoja na kumaliza wakiwa nafasi ya pili kwa mashindano yote mawili la ligi na na la UEFA, bado sio kigezo kwa uongozi wa klabu ya Chelsea kumpa mkataba kocha Avram Grant.

Hayo yalitanabaishwa katika waraka uliotolewa na Klabu hiyo kwa media na kwenye mtandao wa Chelsea http://www.chelseafc.com.

“Chelsea inathibitisha kwamba mkataba wa kocha Avram Grant umevunjwa rasmi toka leo, hii inafuatia majadiliano ya siku mbili ndani ya klabu. Kila mmoja katika klabu ya Chelsea FC anampongeza na kumshukuru Grant kwa kuwa Manager wa timu hii tangu mwezi Septermber mwaka jana.”
Kwa sasa tunaegemeza nguvu zetu katika kusaka kocha mpya, hakuna lolote litasemwa mpaka uamuzi ufanyike,

Grant aliichukua timu hiyo toka kwa Jose Mourinho mwezi September mwaka jana, Grant hakuwahi kuiongoza timu yeyote katika Uingereza alitakiwa kuchukua mikoba na baadaye angepewa mkataba wa miaka minne kama timu ingefanya vizuri.

Hebu fikiria kama wamefika Fainali na mambo ndio hayo, je sie tunatolewa hatua za awali wa kwetu si ndio wasingekaa kabisa!!!.

Lyon mabingwa wa Ufaransa

Kepteni wa timu ya soka ya Lyon’s , Antonio Ribeiro Reis, shoto, Gregory Coupet, kati, na Sidney Govou wakiwa wameshikilia Kombea na kushangilia baada ya timu yao kuwachapa Paris Saint Germain 1-0 katika mtanange wa fainali ya soka Kombe la Ufaransa. Mchezo huu ulifanyija jana tarehe 24 May katika uwanja wa Stade de France stadium nje ya jiji la Paris.

Stars, Malawi leo, Mtihani mwingine kwa Maximo

TIMU ya soka ya Taifa ‘Taifa Stars’ leo inashuka Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuumana na Malawi katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa.

Taifa Stars ambayo Jumamosi wiki iliyopita ilifungana bao 1-1 na Uganda ‘The Cranes’ na kusonga mbele katika michuano ya Afrika inayohusisha wachezaji wanaocheza ligi za ndani itatumia mchezo wa leo kujianda na mchezo wake dhidi ya Mauritius wiki ijayo kuwania kufuzu fainali za Kombe la Dunia 2010.

Ni wazi kuwa yeyote atakayepangwa kati ya wachezaji hawa Fredy Mbuna, Shadrack Nsajigwa, Amir Maftah, Stephano Mwasika, Juma Jabu, Salum Swed, Nadir Haroub na Kelvin Yondani atakuwa na uwezo mkubwa wa kuimarisha safu ya ulinzi ya timu hiyo.

Pia katika safu ya kiugo yeyote kati ya hawa watawaunganisha vyema wenzao, ambao ni Geofrey Bonny, Athuman Iddy, Adam Kingwande, Kigi Makassy, Shaaban Nditi na Nizar Khalfan.

Tumaini la ushambuliaji litakuwa kwa Ulimboka Mwakingwe, Jerson Tegete, Uhuru Seleman, Mrisho Ngasa na Emmnauel Gabriel.

Hadi sasa Taifa Stars imecheza michezo nane ya kimataifa ya kirafiki chini ya Marcio Maximo tangu aanze kibarua hicho karibu miezi 19 iliyopita.

Katika michezo hiyo Taifa Stars imeshinda mitatu dhidi ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, Uganda na Zambia na kutoka sare mara nne dhidi ya Kenya, Angola, Zambia na Uganda na kufungwa na Yemen.
Source: Majira

Ilala bingwa Taifa Cup

TIMU ya Mkoa wa Ilala jana ilitwaa ubingwa wa michuano ya Kombe la Taifa 2008 baada ya kuifunga Kinondoni mabao 5-0 katika mchezo wa fainali uliopooza kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Kwa ushindi huo Ilala licha ya kutwaa kombe pia ilizawadiwa sh. milioni 30 na medali kwa wachezaji wote, wakati Kinondoni ilizawadiwa medali na sh.milioni 15.

Dalili kwamba Ilala ingetwaa ubingwa zilianza kujionesha dakika ya 8 mfungaji akiwa Mussa Hassan ‘Mgosi’ akiunganisha mpira wa adhabu uliopigwa na Matangalu Anthony.

Bao la pili lilifungwa dakika ya 43 na Mohammed Kijuso akitumia vyema pasi ya Athumani Machupa aliyeingia badala ya Mgosi aliyeumia.

Kijuso alifunga bao la tatu dakika ya 50 akiunganisha krosi ya Mohammed Banka na kuongeza la nne dakika dakika kumi baadaye kwa pasi ya Salum Kanoni, kabla ya Ramadhani Chombo kufunga bao la tano dakika ya 85.

Kinondoni iliyoingia fainali kwa kuitoa Mbeya kwa mabao 2-0 katika nusu fainali, haikuonesha cheche zozote kiasi cha muda mwingi mpira kuchezwa langoni mwao na hivyo kumpa nafasi kipa Juma Kaseja kupumzika.

Katika michuano hiyo iliyoshirikisha mikoa 23 ya kimpira, Juma Kaseja alitangazwa kipa bora, wakati kocha bora ni Madaraka Bendera wa Arusha na timu yenye nidhamu pia ikiwa Arusha, huku Mussa Mgosi akiibuka mfungaji bora baada ya kupachika mabao 8 wavuni. Wote walizawadiwa sh. milioni 2 kila mmoja.

Katika mchezo wa mapema jana, timu ya Mbeya iliifunga Arusha mabao 4-3 katika mchezo wa kuwania nafasi ya tatu, hivyo Mbeya kuikwaa nafasi hiyo na kuzawadiwa sh. milioni 7.5 kutoka kwa wadhamini wa mashindano hayo Kampuni ya Bia Tanzania (TBL).
Source:Majira

Tyson anakuja “Bongo”

BINGWA wa zamani wa ndondi katika uzito wa juu duniani, Iron Mike Tyson, anatarajiwa kutua nchini Septemba mwaka huu akiambatana na bondia Laila Ali, ambaye ni binti wa nguli wa masumbwi duniani, Muhammed Ali.

Wakati Tyson akiwa amestaafu ndondi, Laila ni miongoni mwa mabondia mahiri wa kike wanaotamba kwa sasa duniani.

Akizungumza katika Ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO), jijini Dar es Salaam jana, mratibu wa ujio huo, Zuwena Kibene, alisema mabondia hao wanakuja kwa mwaliko rasmi wa kutoa semina kwa mabondia wa Tanzania.

Alisema, kutokana na ujio huo, anatarajia kuanza ziara ya kuzunguka nchi nzima ili kuhamasisha mabondia kufika katika mikoa ya jirani ambako wageni hao wataifikia.

Kibene aliitaja mikoa ambayo mabondia hao wataifikia, ni Dar es Salaam, Arusha na Mwanza, hivyo amewataka mabondia wa jirani na mikoa hiyo, kufika katika mikoa hiyo kwa gharama zao.

Alisema, mabondia watakaokuwa wakitoka nje ya mikoa hiyo, watajigharamia usafiri, huku yeye (Kibena), akigharamia malazi, chakula na nauli za kurejea makwao.

bondia Laila Ali

Alipoulizwa kama mabondia hao watacheza pambano lolote, alisema hawatacheza pambano lolote kwani hakuna anayeweza kupambana nao.

Alisema, kitakachofanyika ni mabondia hao kutoa mafunzo kabla ya kushuhudia mapambano ya mabondia mbalimbali wa hapa nchini.

Tyson, mbabe aliyetamba vilivyo katika ulimwengu wa masumbwi duniani, ni miongoni mwa mabondia walio na mashabiki wengi kutokana na umahiri na vituko vyake.

Miongoni mwa kituko kinachokumbukwa, ni pale alipomng’ata sikio bondia mwenzake, Evander Hollyfield katika kuwania ubingwa wa dunia.

Source: Tanzania Daima

Saturday, May 24, 2008

Miss Tabata

Miss Tabata 2008 Anet John akiwa katika picha na mshindi wa pili Christin Sigala (kushoto) na Christine John baada ya kutangazwa washindi katika shindano la Miss Tabata lililofanyika kwenye Ukumbi wa Dar West Park jijini Dar es Salaam.
soma zaidi kwa Haki

Lionel Messi

Lionel Messi alizaliwa 24 June 1987 huko Rosario – Argentina. kwa sasa anachezea timu ya FC Barcelona. alionyesha uwezo mkubwa akiwa na umri mdogo sana na medi zilimpachika kuw ndiye “Diego Maradona Mpya”. Messi alikaraishwa sana na timu yake kutochukua Kombe lolote kwa mwaka wa pili mfululizo na alitajwa kuwaniwa na vilabu vya Uingereza lakini timu yake ya Barcelona inasema itafanya kila linalowezekana kuendelea kuwa naye Messi. na huyu ndiye mchezaji wetu wa wiki hii na hii chini ni moja ya Video zake.

Sweta la 50 Cent lilipoleta kizaazaa.

Ni kawaida kwa wanamuziki au wanamichezo kuvua mavazi yao na kuwazawadia watazamaji, hivi karibuni mwanamuziki 50 Cent alitua Bongo baada ya kupokelewa uwanja wa ndege wa Dar akiwa njiani aliwarushia mamia ya mashabiki wake Fulana yake, Kimbembe kilichotokea hapo si cha kitoto ilibidi askari wa usalam kuingilia ili kuamua mashabiki hao waliotaka kutoana macho.
Kwa video zaidi za Msanii huyo ndani ya bongo Bongo5.com hapa

England Vs USA, Mtihani mwingine kwa Capello

Baada ya kukosa fainali za michuano ya Euro 2008, timu ya soka ya England kwa sasa inajiandaa na mechi za kirafiki ikiwa imeegemeza nguvu kwenye michuano ya kombe la Dunia mwaka 2010. Tarehe 28 mwezi huu England wanawakaribisha USA katika mechi ya kirafiki ambayo itafanyika katika uwanja wa Wembley.

Kocha mpya Fabio Capello (pichani) anakibarua kigumu kuwahakikishia na kuwarudishia waingereza matumaini na timu yao hassa baada ya kuchapwa kwenye mchezo wao wa kirafiki na Ufaransa jambo ambalo lilileta kelele toka kwa mashabiki wa soka wa Uingereza na kuamsha hisia kuwa wachezaji wa kigeni wanachangia kuharibu soka la Uingereza kwa timu zinakuwa zinawategemea wao zaidi kuliko kukuza vijana kwa ajili ya Taifa lao. Hii ni nafasi nzuri kwa Capello kama watashinda itampa milege na kumjengea heshima kwa waingereza ambao wanaona timu yao ikifanya vibaya mfululizo. Mara ya mwisho mwaka 1994 walipokutana England waliichapa USA mabao 2-0 yaliyofungwa na Alan Shearer.

Pool hadi Mlimba!

Mchezo wa Pool umekuwa maarufu sana Tanzania kila kona si jambo la ajabu kukuta meza na watu wamerundikana, Hii ilikuwa Mlimba Ifakara Morogo nilikuwa na kijana wangu Robert Mwafrica akaomba game moja duh dogo alimtoa nishai katika michezo minne alishinda mmoja tuu, Batty ndiye mwalimu wangu wa Pool na vijana wake wengi kwa sasa wanatisha. Ama kweli jogoo wa mjini hawiki shamba pia.

Laiti kamaaa……!


Hebu pata picha ndio Tanzania ingefanikiwa kufika Fainali tuu za Ghana ingekuwaje, Pichani ni watanzania wakiongozwa na Rais Kikwete (picha katikati) kipindi tunajongea kwenye mashindano ya Kombe la Mataifa ya Africa. Watanzania wanapenda sana Mpira basi tuu.

Serikali/TFF yaunda Kamati kusimamia Uwanja wa Taifa

Serikali kwa kushirikiana na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), imeunda kamati itakayosimamia Uwanja mkuu wa Taifa na timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’.

Kamati hiyo itafanya kazi kwa kusimamia uwanja huo pamoja na timu kwa michezo mitatu itakayofanyika nchini ukiwa kati ya Stars na Malawi unaotarajia kufanyika kesho pamoja na michezo kati ya Mauritius na Kameruni.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa TFF, Fredrick Mwakalebela, alisema kamati hiyo itaongozwa na Mwenyekiti wake Kijazi Mtengwa ambaye ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari Utamaduni na Michezo, chini ya Katibu Mkuu wake Lawrance Mkwaji ambaye ni Kaimu Mkurugenzi wa wizara hiyo.

Mwakalebela alisema kamati hiyo pia itakuwa na wajumbe ambao watakuwa wenyeviti katika kamati ndogo ndogo zitakazosimamia shughuli hiyo.

Aliwataja kuwa ni Tido Mhando (Habari, itifaki na uelimishaji), Leodger Tenga (Ufundi na matumizi ya uwanja), Aloyce Mushi (mtaalamu wa uwanja), Alfred Tibaigana (Ulinzi na usalama) na Laison Mwanjisi (fedha).
Na Majira

Tibaigana achimba mkwara Polisi kuingiza “Dezo” Taifa mechi za Stars

JESHI la Polisi limesema limeimarisha ulinzi na kuwataka askari wa majeshi yote nchini kuingia uwanjani kwa kulipa kiingilio katika mechi mbili za kimataifa kati ya timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) dhidi ya Malawi na ile ya Maritius zitakazochezwa Uwanja mpya wa Dar es Salaam.

Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Alfred Tibaigana alisema jana kuwa askari walioteuliwa kulinda usalama katika mechi ya kesho kati ya Taifa Stars na Malawi watakuwa na beji maalum zitakazowatofautisha na askari wengine wanaovaa sare za jeshi kwa lengo la kuingia mpirani bure.

Tibaigana ambaye ni Mjumbe wa Kamati ya Taifa ya kusimamia uwanja wa Taifa na Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama, alisema wanajeshi si masikini wa kutaka kila mara kuingia mpirani dezo, hivyo amewataka kuchangia timu yao ya Taifa kwa kulipa kiingilio.

Alisema mechi ya pili ambayo Stars itacheza na Maritius, Jumamosi ijayo pia kutakuwa na ulinzi wa kutosha na kuagiza kuwa magari yatakaoruhusiwa kuingia ni yale yaliyokatiwa tiketi za kuingia uwanjani.
Na Majira

Friday, May 23, 2008

Kung Fu Panda, Filamu ya Vikatuni iliyoshirikisha Magwiji wa Filamu

Kung Fu Panda ni picha ya Vikatuni inayomhusu mnyama Panda ambaye aliamua kujifunza Sanaa ya Kung Fu na baadaye kutumia ujuzi huu kupigana na kujihami na maadui zake. ni Filamu ya vichekesho sana na inafurahia sana. Picha hii imeongozwa na John Stevenson na Mark Osborne na producer ni Melissa Cobb. Wazo la picha hii lilibuniwa na Michael Lachance, Boss wa kampuni ya DreamWorks Animation . Filamu hii itakuwa sokoni June na itaonyeshwa rasmi June 6, 2008. na kusambazwa na Paramount Pictures.

Katika picha hii sauti za vinara wa Sinema zimetumika kama Jack Black, Seth Rogen, David Cross, Jackie Chan, Dustin Hoffman, Angelina Jolie na Lucy Liu. kama wanavyoonekana hapo chini. kwa habari zaidi Bofya hapa.

Angelina Jolie voices Master Tigress in DreamWorks Animation’s Kung Fu Panda – 2008
David Cross voices Master Crane in DreamWorks Animation’s Kung Fu Panda – 2008
Dustin Hoffman voices Shifu in DreamWorks Animation’s Kung Fu Panda – 2008


Jackie Chan voices Master Monkey in DreamWorks Animation’s Kung Fu Panda – 2008


Lucy Liu voices Master Viper in DreamWorks Animation’s Kung Fu Panda – 2008

Wakutanapo Celebrities wa Sinema

Angelina Jolie & Brad Pitt
Aishwarya Rai Kulia toka Bollywood
Jean-Claude Van Damme
Madonna
Star Jones

Marcio Maximo!

Marcio Maximo, Kocha mwenye uraia wa Brazili, aliteuliwa na serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kama kocha mkuu wa Taifa Stars .

Kuchaguliwa kwake kumefuatia ahadi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Jakaya Kikwete kuhakikisha anaboresha sekta ya michezo kwa kuanzia na mpira wa miguu.

Amewahi kuifundindisha Livingston Football Club huko Scotland mwaka 2003/2004. Pia ni mwanachama wa Chama cha makocha cha Brazil’s .

Kwa mujibu wa wikipedia.

Yanga kuwakosa Chuji, Cannavaro

Hivi karibuni Chuji aliweka wazi kwamba hategemei kuwepo ndani ya kikosi cha Yanga msimu ujao kutokana na kuitwa na mjomba wake nchini Hispania kwa lengo la kutafutiwa timu ya kufanya majaribio na baadaye kucheza soka huko.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi mwishoni mwa juma lililopita jijini Dar es Salaam, Cannavaro (pichani jezi kijani) alisema kuna mtu ambaye anashughulikia mipango yake ya kwenda kufanya majaribio nchini humo na kama mambo yatakamilika ataondoka hivi karibuni.

Alisema amefikia hatua hiyo kutokana na kuliangalia zaidi soka la kulipwa baada ya kwenda mara ya kwanza na Timu ya Taifa ya Zanzibar na kufanya majaribio na baadhi ya timu lakini kipindi hicho hakubahatika kupata soko kwa sababu hakuwa katika kiwango cha juu kama ilivyo sasa.

“Nategemea kwenda tena Ujerumani kufanya majaribio na nikifanikiwa nitacheza huko, kuna mtu anasimamia kila kitu na amefikia hatua nzuri kwa sasa, awali nilifanya lakini sikufikia kiwango kilichokuwa kinahitajika,” alisema Cannavaro.

Mlinzi huyo wa kati aliyeitumikia Yanga kwa misimu miwili sasa, amesema ana uhakika mkubwa wa kupata timu nchini Ujerumani kwani kiwango chake kimeimarika kuliko ilivyokuwa awali.

Aidha Cannavaro aliweka bayana kuwa, kwa sasa hana mkataba na Yanga baada ya ule wa awali kumalizika pindi Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara ilipofikia ukingoni mwezi uliopita.

“Kama Yanga wakinihitaji kwa msimu ujao, nitasaini kuichezea, lakini mambo yangu yatakapokamilika muda wowote nitaondoka kwenda kusaka maisha mapya nchini Ujerumani,” alisema mlinzi huyo.

Hata hivyo, kwa mujibu wa chanzo chetu kilichopo ndani ya uongozi wa Yanga, kilitueleza kwamba, piga ua lazima beki wa Simba Kelvin Yondan arithi mikoba ya Cannavaro endapo ataondoka.

“Ni kweli kuna uwezekano wa kumkosa Cannavaro endapo mipango yake itakamilika mapema, lakini hilo hatuna wasiwasi nalo kwani Yondan anatua Yanga kwa milioni 18, kwa ajili ya kuziba pengo hilo.

“Hata kama Cannavaro hataondoka, lazima tumnase Yondan ili aweze kusaidiana naye, kwani huyo ndiye chaguo la kwanza la kocha, kwa sasa mipango inaendelea vizuri,” kilieleza chanzo chetu huku kikitahadharisha kutotajwa jina gazetini.

Kiliongeza kuwa, uwezekano wa kumnasa kiungo ambaye ametupiwa virago na Timu yake ya Al Tadhamon ya Kuwait, Nizar Khalfan bado ni tata kutokana na mchezaji huyo kudai dau kubwa ambalo ni milioni 20 huku Meshack Abel anayeichezea Mujis ya Oman akitaka milioni 12.

Kadhalika Yanga imedaiwa pia kuwa mbioni kumnasa mlinzi machachari wa pembeni wa Klabu ya Tanzania Prisons ya Mbeya, Stephano Mwasika ambaye kwa sasa anakichezea kikosi cha Taifa Stars.

“Ukweli ni kwamba Klabu ya Yanga imenipa ofa ya nyumba pamoja na milioni kadhaa endapo nitakubali kuichezea msimu ujao, sitaweza kuikataa ofa hiyo,” Mwasika aliliambia Championi jana.

Wakati huo huo, Kondic anatarajia kurudi nchini kesho sambamba na wachezaji wawili kutoka Afrika Kusini alikoenda mapema wiki hii kufanya mazungumzo nao.

Kondic alimwambia mwandishi wetu kabla ya kuondoka kuelekea Afrika Kusini kuwa, tangu kumalizika kwa ziara yao alikuwa na mawasiliano ya karibu na wachezaji hao ambao walicheza mchezo wa kirafriki na Yanga ilipokuwa imeweka kambi nchini humo.

Alisema wachezaji hao ambao walikuwa wasumbufu katika mchezo wao wa majaribio nchini humo wanatokea katika Klabu ya Might Blues na kwamba wote ni washambuliaji.

“Wachezaji ambao naenda kukutana nao ni wazuri na kikubwa ambacho walinivutia ni kasi yao wawapo katika eneo la hatari, naamini wanaweza kuisaidia Yanga ambayo inakabiliwa na michuano migumu ya kitaifa na kimataifa,” alisema Kondic.
Habari na Global Publishers, Picha na BBC

Wanja la Liverpool likikamilika


Wanja la Liverpool likikamilika, Katika picha hizo zilizotolewa na The Daily Mail zinaonyesha jinsi wanja likikamilika litavyokuwa, Wanja hili litakuwa na uwezo wa kuchukua watazamaji 60,000 wakiwa wamekaa “Konfotabo” na uwezo wa kuegesha magari mengi kwa wakati mmoja, utakamilika mwaka 2010. Gharama yake inakadiriwa kufikia Paund Milioni 300.
Soma habari za uhamisho wa Klabu hii hapa chini:-

Liverpool

Liverpool
Latest News:

Udinese left-back Andrea Dossena is said to be close to a £9 million deal to join Liverpool, although Tottenham and Juventus have reportedly entered the fray. Liverpool are close to sealing a £9 million deal for Udinese left-back Andrea Dossena. Liverpool appear to be in pole position for the 26-year old after opening negotiations recently with Udinese sporting director Pietro Leonardi.

Rafa Benitez is lining up former France ‘keeper, and current Bordeaux number one Ulrich Rame to deputy for Pepe Reina. 20-year-old Napoli midfielder Marek Hamsik and Espanyol’s £6m-rated winger Albert Riera are other names being linked with the club. Riera could be a likely option as he has informed his club that he would like to leave this summer.

Liverpool have reportedly turned down a £25 million bid from Inter Milan for Steven Gerrard. The Italian giants want to make the 27-year-old their main signing as they begin their centenary celebrations.

Xabi Alonso is being linked with a £12 million move to Juventus.

Peter Crouch is up for sale and though a £15 million price tag has been hung around the striker’s neck there is still plenty of interest. Martin O’Neill and Roy Keane would be interested in buying Crouch and have the funds to pay the asking fee, as do Villareal, who, unlike Aston Villa and Sunderland, would be able to offer him Champions League football next season. At the same time the club have checked on Barcelona’s French left-back Frank Abidal, and are allegedly considering an £8 million offer.

Liverpool are preparing alternatives in case their bid to sign Gareth Barry falls through. Stewart Downingis one option that is currently being considered at Anfield, with Rafael Benitez ready to pay £12 million for the Middlesbrough winger.

Kwa habari zaidi za uhamisho wa klabs mbali mbali Gonga The Daily Mail Hapa

Miss Tanzania EU 08

Nyote mnakaribishwa

Ali Kiba kuanza makamuzi leo UK

Pichani Alikiba akiwasili UK
Ali Kiba akiwa na Wadau ndani ya Uk tayari kuanza makamuzi Leo

Kwa mara nyingine tena mwanamuziki wa Bongo Flava, Ali Kiba yuko ziarani UK kwa Mualiko wa Bongo Family UK, Ali Kiba anaye tamba na nyimbo zake kam Cinderela, Nakshi Nakshi, yuko kwenye Tour iliyopewa jina la “SPRING BREAK TOUR ’08 (A BIG BANK HOLIDAY WEEKEND)”


Ratiba za Ziara hiyo iko kama ifuatavyo


Ijumaa ya leo 23rd May atakuwa :
SCOTLAND 23RD @ TIGER TIGER CLUB, GLASGOWJumamosi 24th May:

MANCHESTER @ AQUA BAR


Jumapili 25th May:

BIRMINGHAMNa Onyesho la mwisho ni Ijumaa 30th May:


IN LONDON @ CLUB AFRIQUEKwa habari zaidi watembelee
http://www.bongouk.com

Thursday, May 22, 2008

David Cook ndiye American Idol Mpya!!

David Cook – American Idol Mpya!!

David Cook alisherehekea jana usiku baada ya kuibuka mshindi wa American Idol 2008 kwa kumshinda mpinzani wake David Archuleta , David mwenye miaka 25-alimshinda David (17) kwa kura Milioni 12 zaidi.

Na katika jambo la kushangaza jaji Simon Cowell aliomba msamaha kwa Cook kwa kile alichosema kumkosoa wakati akiimba wimbo wake wa mwisho.

Cowell alisema kuwa, maoni aliyotoa kwa Cook usiku mmoja kabla ya fainali hiyo hayakuwa ya busara na hayakumstahili David.

Alisema, nilipokwenda nyumbani na kuiangalia tena nilijiona nimemkosea kwa maoni ambayo niliyatoa. Hatimaye Cowell aliwapongeza wote wawili kwa ushujaa waliounyosha mpaka kufikia fainali hiyo, “kwa mara ya kwanza tangu nianze sitojali nani atashinda, kwangu wote mko sawa”

Kinyume na matarajio ya wengi ambao kwa kiasi kikubwa walimpa nafasi Archuleta ya ushindi wa mashindano haya, David Cook na David Archuleta kwa kiasi kikubwa waliwagawa mashabiki kiasi wasijue nani wa kumchagua kwani kila mmoja alikuwa na hisia na mvuto wa kipekee.

Rafiki yangu Tanzania Dream naona una kila sababu ya kufurahi.

Pamoja na kupata mkataba wa kurekodi na promotion ya Albam na pesa Taslimu mshindi wa kwanza na wa pili wa American Idol wameibuka na gari hii aina ya Ford Escape Hybrid SUV.

RONALDO MFUNGAJI BORA UEFA CHAMPS LIGI

Christian Ronaldo (pichani) ndiye mfungaji bora wa mashindano yaliyoisha jana ya UEFA Champions Ligi kwa kupachika jumla ua magoli 8.
Msimamo wa wafungaji na timu zao ni kama ifuatavyo:-
2007/08 UEFA Champions League top scorers
Player Club Goals
Cristiano Ronaldo Manchester United FC 8
Lionel Messi FC Barcelona 6
Didier Drogba Chelsea FC 6
Steven Gerrard Liverpool FC 6
Fernando Torres Liverpool FC 6
Ryan Babel Liverpool FC 5
Dirk Kuyt Liverpool FC 5
Raúl González Real Madrid CF 5

Ni Manchester Kombe la UEFA Champions Ligi!

Wachezaji wa Man U (juu na chini) wakishangilia mara baada ya kukabidhiwa kombe

Cristiano Ronaldo akiwa na Kombe la Ubingwa

Mchezaji wa Chelsea Didie Drogba akisononeka mara baada ya timu yake kutolewa kwa penalti

Kocha wa Chelsea akimfariji kijana wake, Tunaomba radhi kwa kutokuwa hewani tangu jana kwa sababu za kiufundi hasa kwa siku na mechi kali kama ya jana.
Ila pata yaliyojiri hasa kipindi cha Penalti kwa kubofya hapa.

video

Wednesday, May 21, 2008

Serge Mavili aka Celeo Scram kijana wa Wera anayekuja juu kwa kasi

Celeo kwenye Cover ya CD/DVD yake

Pichani Celeo kulia akiwasili kwenye msiba wa Madilu na kwa mbaali anaonekana Boss wake wa Zamani Werason akiwa na Miwani Nyeusi.

Kwa wale wapenzi wa Wenge Musica Maison Merre Watakuwa wana Mjua “Serge Mavili aka Celeo Scram” ni mmoja wa wanzilishi wa Maison Merre alikuwa anasaidiana na Bill Clinton kwenye Atalaku (kughani), Walipoondoka akina Bill yeye alibaki, kwa sasa hivi naye ametoka kwenye Maison Merre, kama ujuavyo wanamuziki Kitendo chake cha kuondoka hakikumfurahisha bosi wake Werason, na tangu hapo Celeo amekuwa anajizolea umaarufu na sifa kila uchao, maana alikutana na Bosi wake wa zamani kwenye Msiba wa Madilu,ameshindwa hata Kumuangalia usoni, Seleo ametoa Album inaitwa ” Nzoto na Nzoto”,inatamba sana kwa sasa na hata kwenye Soko la Ulaya, Seleo na shabiki mkubwa wa “Shabani Nonda” kwenye kila nyimbo lazima amtaje “Shabani Nonda”,Shabani Nonda aliwahi kumnunulia Celeo gari lenye thamani ya Usd 20,000. Wapenzi wa mpira Shaban Nonda aliwahi kuichezea timu ya soka ya Yanga kabla ya kwenda kucheza mpira wa kulipwa nje, Celeo anaishi Ufaransa ameoa mwanamke wa kizungu na ana watoto wawili wa kiume.


Tuesday, May 20, 2008

Rooney amkandia Drogba

MSHAMBULIAJI wa Manchester United Wayne Rooney amemwambiamshambuliaji wa Chelsea, Didier Drogba kwamba hana lolote.

Nyota huyo wa Manchester United amempiga madongo mfungaji wa Blues muda mfupi kabla ya kufanyika kwa pambano la fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya litalozikutanisha timu zao.

Mchezaji huyo wa timu ya taifa ya England alisema: ” Wakati (Drogba) yuko katika kiwango cha juu, ni mchezaji asiyeaminika. ni mkubwa, imara, anafunga magoli kwa mguu wa kushoto, mguu wa kulia, kichwa na wakati wote si wa kumchezea,” alisema.

Hii si mara ya kwanza kwa Drogba kushutumiwa katika mashindano haya ambayo yanakutanisha timu za Uingereza tupu.

Kocha wa Liverpool, Rafa Benitez aliponda mchezaji huyo kutoka Kodivaa kwamba amekuwa akijiangusha kabla ya mechi ya pili ya nusu fainali mwezi uliopita.

Rooney na mchezaji mwenzie Nemanja Vidic pia wamemshutumu kuwa amekuwa akidanganya.

Rooney alisema kuwa alijisikia uchungu kuona Liverpool ikitwaa ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Ulaya miaka mitatu iliyopita itamfanya yeye kujiamini zaidi mjini Moscow.

Alisema: Ni vigumu kuona mmoja wa wapinzani wako anafanikiwa vitu. Wakati Liverpool ilipotwaa ubingwa, ilitia uchungu sana. Ilitufanya sisi tutake kutwaa na hata zaidi,” alisema.

Mdau akiwa “Vakesheni”

Mdau wangu Abuu “Mr Bean” wakongwe wa Mjini akiwa mbele ya Twin Tower ndani ya Kuala Lumpur Malaysia. Kazi na dawa.

Ni David Archulete ama David Cook American Idol

Kindumbwendumbwe cha mashindano ya American Idol ndio kinafikia ukingoni wiki hii huku mashabiki wakishuhudia mpambano mkali kati ya wawili hao pichani David Archulete (shoto) na David Cook ambao kwa kiasi kikubwa wamewagawa mashabiki hasa baada ya kutoka msichana pekee Syesha wiki iliyopita. Kila mmoja anapewa nafasi ya kushinda na kila mmoja ana mashabiki wake, wakati wa mwanzo wa mpambano wawili hawa walikuwa wakishabikiwa na watu wote lakini imefika mahala ni lazima kuchagua mmoja hilo ni jukumu gumu sana hata siwezi kusema nani ni zaidi ya mwingine, binafsi nawaona wote wana vipaji, kwangu huu ni mtihani kila mmoja na mvuto wa kipekee na wote wana kipaji alisema Simon, Jaji maarufu wa shindano hilo alipokuwa akiongea na Television ya FOX.

Bekham awatakia ushindi Manchester.

Fainali zilizopita Bekham aliisaidia Manchester kuchukua Kombe.

“Nimevunja ratiba yangu yote kwa ajili ya mechi ya jumatano” ndivyo alivyoaanza Bekham akiongea na Yahoo Sports, sitabahatika kwenda lakini nitaangaliazia nyumbani mechi pamoja na familia yangu na marafiki zangu, ni tukio kubwa, linanikumbusha enzi za maisha yangu ya mpira Manchester” alisema Bekham.
Manchester wanakutana na Chelsea kwenye fainali ya Mtanange wa Kombe la UEFA hapo kesho.
Mapenzi ya Bekham kwa Manchester yalianza tangu akiwa mdogo alipokuwa na miaka 12 na baba yake Ted alikuwa akimchukua umbali wa Maili 400 hadi Old Trafford kwenda kuwaona Manchester bila kukosa mechi zote muhimu, hapo ndipo Bekham alipoanza kuipenda timu hiii na kutimiza ndoto ya kuichezea.
“Nitaangali mpambano huu kwa na wasiwasi mkubwa, tuna mapumziko ya mazoezi kwenye klabu yetu, najua ni mpambano mkali maana timu zote zinajuana na zina wachezaji wazuri, ila nina imani kubwa na Manchester kushinda ila wasiidharau Chelsea ni wazuri”

Monday, May 19, 2008

Bono amshawishi Bekham kupanda Mlima Kilimanjaro

Katika kampeni ya kuchangisha fedha kwa ajili ya kusaidia kampeni za Unicef, Mwanamuziki wa kundi la Muziki la U2 na muanzilishi wa The ONE Campaign and (PRODUCT) RED, Bono ameamua kumshawishi na kumshirikisha Bekham (Pichani-si halisi) katika mpango huo kwa kupanda Mlima Kilimanjaro. Bado tarehe rasmi haijajulikana lakini itakuwa ni nafasi nzuri kwa Bodi yetu ya utalii na wadau wa Utaliii kwa ujumla kutumia nafasi hii kuutangaza utalii wetu na nchi yetu kwa ujumla.

Katika mashindano ya Kombe la Dunia Korea/Japan chumba alicholala nyotan huyo hadi leo bado kinauzwa aghali mnoo na muda sasa umepita. Tanzania tunaweza kuitumia nafasi hii kutangaza package za utalii na kupata watalii wengi zaidi kwani wapo wengi ambao wangependa kupanda Mlima Kilimanjaro na nyota huyu.
Bono akiwa na Mama Eusebia nchini Tanzania

ziara hiyo inaweza kumjumuisha pia golikipa wa West Ham Robert Green.
Bono amekuwa mstari wa mbele na kwa kipindi amekuwa nchini Tanzania kishiriki kwenye shughuli mbali mbali akisaidiana na Kampuni ya FOX/American Idol na Spoti na Starehe tuliwahi kumtoa habari zake bofya hapa humu.
Kujua zaidi ya Bekham angalia gazeti la The Sun hapa.

Portmouth alipochukua Ubingwa wa Kikombe cha FA

Goli moja lililofungwa na Kanu lilifanya timu ya Portmouth kunyakua ubingwa wa Kikombe cha FA. Kulikuwa na kila sababu kwa klabu ya Portmouth kusherehekea ubingwa huu baada ya kuichapa Cardiff kwa goli moja bola (1-0) katika mchezo wa Fainali wa kombe la FA uliochezwa hivi karibuni. kwani Portmouth wameshinda kikombe hicho baada ya miaka 69 kwani mara ya mwisho ilikuwa mwaka 1939 walipowachapa Wolves. baada ya hapo wamekuwa wakijitahidi bila mafanikio, Hata hivo Portmouth walikuwa na nafasi nzuri ya kushinda kwa magoli zaidi mchezo wa jana, baada washambuliajia wake akiwembo Kanu kukosa magoli ya wazi tangu dakika za awali za mchezo.

Mashabiki wa Portmount na Cardiff wakiingia uwanja wa Wembley kushuduhia mpambano kati ya Portmouth na Cardiff

Kanu akishangilia na mwenzie kwa Style ya chamukwale baada ya kuwatandika Cardiff bao 1-0.
Jikumbushe yaliyojiri hapa.

Ujasiriamali wa Kitamaduni

Ukipita mitaa ya Kuala Lumpur-Malaysia muda wa Usiku Eneo la Burkit Bintang utakutana na hawa jamaa ni wajasiriamali huwa wanajaza watu kwa aina ya Ngoma wanayopiga hizo ala zinatoa mlio mzuri na wamerekodi kwenye CD na hutumia nafasi hiyo kuuza CD zao ambazo hununuliwa kama njugu na bei yao ni 12 Ringit (3500) kwa kila CD.

Emillian na Irene
Napenda kuchukua nafasi hii kuwapongeza Bwana na Bi Emillian Samwel Kiwehle baada ya kufunga ndoa katika kanisa la Mtakatifu Joseph na baadaye kwenye Sherehe ya Harusi iliyofanyika katika Hoteli ya Giraffe Ocean View Hotel hivi karibuni. “…My Loving Shem Irene (Irene Maugo) all the best katika maisha yako mapya, Inshallah Mungu atawabariki na kuwaongoza”.

Ziara ya BCBG Ulaya


Pichani ni Papa Chery akilishambulia jukwaa katika onyesho la kwanza Bruxells Belgium
Mwanamuziki JB Mpiana na kundi zima la Wenge Muzika BCBG bado wanaendelea kukonga nyoyo za mashabiki na wapenzi wa Muziki wa lingala katika ziara ambayo inampitisha nchi za mbali mbali za Ulaya, katika onyesho lililofanyika wiki mbili zilizopita inasemekana palitokea fujo ambazo ziliwazidi nguvu walinzi, katika siku za karibuni kumekuwa na hati hati ya onyesho ambalo limepangwa kufanyika nchini Uingereza kutokana na masuala ya kiusalama kutokana na mashabiki kusababisha fujo kwenye onyesho la mwisho la mwanamuziki Koffi Olomide.
Ratiba ya kundi hilo iko kama ifuatavyo:-

 • 24 May – Stockholm
 • 30 May – Rotterdam
 • 31 May – Paris
 • 06 June – Lyon
 • 07 June – Switzerland
 • 13 June – Dublin
 • 14 June – Liège — farewell concert Belgium
 • 20 June – Portugal
 • 21 June – Bruxelles — Onyesho limefutwa mpaka itakapotangazwa vinginevyo
 • BCBG watarejea Kinshasa tarehe 26 June.

  Jikumbushe live hii ya Zenith (Audio Studio Version)

  JB Mpiana :: 14 June 08 :: Liège Belgium

  Kaunazi kwa mbaaaaaali!!

  sio “Unazi” ila sometimes ukikutana na kajibango ka namna hii na we unakaupenzi si mbaya kuchukua kumbukumbu atii. hii ni ndani ya Twin Tower KLCC-Kuala Lumpur Malaysia

  MIRIAM CHEMMOSS: muigizaji,mwimbaji,mtunzi wa nyimbo na pia mwanamitindo (model)

  Endapo kuchanganya utaifa,damu na tamaduni mbalimbali ni mojawapo ya chachu za mafanikio fulani hapa duniani, basi ushahidi wa dhana hiyo unaweza kuupata kwa kuangalia maisha ya mrembo Miriam Chemmoss(pichani).

  Miriam ni muigizaji,mwimbaji,mtunzi wa nyimbo na pia mwanamitindo (model) ambaye mpaka hivi leo ana haki ya kusimama na kujivunia rekodi yake katika ulimwengu changamani wa sanaa na maonyesho.Mwenyewe anasema safari yake ndio kwanza inaanza kwani bado ana ndoto na malengo chungu mbovu ya kutimiza.Hivi leo kazi zake nyingi anazifanyia kutokea jijini New York nchini Marekani anapoishi.

  Bofya hapa upate mahojiano kamili na Bongo Celebrity

  Inter Milan wachukua Ubingwa tena!!!

  MILAN, May 18 (Reuters) – Zlatan Ibrahimovic akiwa ameifungia timu yake mabao mawili na kuihakikishia ushindi na kuchukua kikombe tena, katika mchezo uliochezwa leo dhidi ya Palma na kushinda magoli 2-0 na kuwafanya kuchukua kombe kwa miaka mitatu mfululizo.

  Mechi ya leo ilikuwa ngumu na kila timu ilikuwa inataka ushindi, mashabiki waliipania na wachezaji walipania, jambo lililofanya mashabiki kadhaa kuumia vibaya ikiwa ni pamoja na polisi mmoja kwenye fujo zilizotokea nje ya uwanja mara baada ya mpira kumalizika.

  Mc wa Uzinduzi wa Akudo wamuona atiii?

  Maimatha Jesse, mtangazaji wa Channel 5 ndiye alikuwa MC katika uzinduzi wa Akudo Impact Diamond Jubilee.

  Uzinduzi wa Akudo wawachengua mashabiki

  Sehemu ya kundi la Akudo Impact likishambulia jukwaa wakati wakitambulisha nyimbo za albamu yao mpya ya Impact, katika ukumbi wa Diamond Jubilee usiku wa kuamkia jana katika onesho ambalo lilisindikizwa na Jahazi Modern Taarab na Bozi Boziana kutoka DRC. Mtindo wa Pekechapekecha uliacha mashabiki wakipagawa!

  Wazee wa masauti wakikabidhiwa ‘mikoba’ na Bozi Boziana wakati wa uzinduzi wa albamu yao alfajiri ya jana Diamond Jubilee.

  Mwanamuziki kutoka DRC, Bozi Boziana, ‘Benz’ akiwa katika jukwaa la Akudo Impact alfajiri ya jana wakati akiwasindiza ‘wazee wa masuati’ katika uzinduzi wao. Bozi alikonga nyoyo za mashabiki wa vibao vyake vya zamani ambavyo wabongo wanavikumbuka.
  Huyu ni miongoni mwa safu ya wanenguaji machachari wa Akudo Impact akipagawisha mashabiki katika uzinduzi wa albamu yao uliofanyika jana pale Diamond Jubilee na kuacha gumzo jijini Dar.

  Picha zote na habari na Global Publishers

  Defao na Wazee wa Mujini!

  Mwanamuziki kutoka Kongo Jenerali Defao akionyesha umahiri wake wa kunengua katika onyesho la sherehe za kutimiza miaka kumi ya bendi ya FM Academia zilizofanyika usiku wa kuamkia jana katika ukumbi wa Msasani Club.

  Mc wa onyesho la bendi ya FM Academia kutimiza miaka kumi Beni Kinyaia akimtambulisha mwanamuziki kutoka Kongo Jenerali Defao mara baada ya kupanda jukwaani usiku wa kuamkia jana.
  Habari na picha na Global Publishers

  Mbwembwe za wanasoka!!

  Mchezaji wa Sevilla Dragutinovic akishangilia baada ya timu yake ya Sevilla kushinda 4-1 dhidi ya Athletic wakati wa mchezo wa ligi ya Spain taree 18 May 2008.

  Furaha ya ushindi!!

  MADRID, SPAIN – MAY 18: Marcelo (kati) wa Real Madrid akiwa amelishikilia kombe la ubingwa wa Ligi ya La Loga akiwa na wenzake Sergio Ramos (L) na Ruud van Nistelrooy (R) mara baada ya kumalizika kwa mchezo wao na Levante huko Santiago uwanja wa Bernabeu.

  Raha ya Ubingwa Real Madrid

  Wachezaji wa Real Madrid wakiwa wamelishikilia kombe lao la Ubingwa baada ya kushinda ligi ys Spain kwa msimu huu huko Santiago kwenye uwanja wa Bernabeu, Madrid mnamo May 18,2008

  Saturday, May 17, 2008

  Ronaldo: “Napenda kucheza La Liga Spain”

  Cristiano Ronaldo amedokeza kuwa ataifikiri zaidi klabu yake ya Manchester United zaidi mara baada ya Fainali ya dhidi ya Chelse ingawa anashawishika na ligi ya Spain La Liga kupitia klabu ya Real Madrid.

  Ronaldo (23) amekuwa gumzo katika soko la wachezaji soka ulimwenguni kwa sasa hasa baada ya kuifungia timu yake jumla ya magoli 41 msimu huu,

  Madrid wameonyesha nia ya kumtaka Ronaldo na kwa siku za karibuni harakati zinasemekana zimepamba moto na wamesema wako tayari kutoa kitita cha Pound £100million. Sijaamua lolote kwa sasa najisikia raha kucheza hapa, mawazo yapo kwenye mchezo na Chelsea kwa sasa ngoja tuangalie baada ya mchezo huo, alisema Ronaldo akihojiwa na Spanish TV network Antena 3.

  ‘Najua Real Madrid wanavutiwa na uchezaji wangu, najua pia kuna Timu Spain zinavutiwa na mimi pia, ni vizuri kujua kuwa kuna timu zinavutiwa na wewe, nimesema mara milioni kuwa ninapenda sana kucheza Spain, alimalizia Ronaldo.

  Viera: Arsenal watampoteza Gallas wasipokuwa makini

  Kapteni wa zamani wa timu ya Arsenal Patrick Vieira anasema anahofia matokea kama kocha Arsene Wenger ataamua “kumvua” nafasi ya kepten mchezaji William Gallas.

  Uongozi wa Gallas’s umeleta kelele sana kwa siku za karibuni kutokana na timu yake ya Arsenal kutofanya vizuri na hata kutochukua kikombe kwa mara nyingine tena, matokeo ambayo inasemekana yatamfanya Wenger kubadili na kumtoa Gallas kama Kepten wa timu hiyo.
  “Arsenal wanahitaji ubembeleza wachezaji wao, kwa mujibu wa malipo ya Arsenal kwa sasa ni rahisi kwa mchezaji kuondoka, tayari wamepata pigo kwa kuondokewa na Flamini aliyekwenda AC Milan alisema Viera, ni lazima watoe mikataba minono ili kuwafanya wachezaji wazuri wakae, vinginevyo timu haitakuwa wachezaji”.

  Bayern Bango kuuuuuuubwa!!

  Mafundi wakimalizia kuweka bango kubwa likiwa na wachezaji wa timu ya Bayern Munich katika eneola “Alte Boerse” (Soko la zamani la Hisa) katikati ya jiji la Munich. Bango hilo lina ujumbe usemao “Sisi ni FC Bayern ! Tuna rekodi ya ubingwa!, Tunarekodi ya Vikombe vya ushindi!, Tuna rekodi ya bango kubwa!, Twashukuru wapenzi wetu!, Bango hilo lina ukubwa wa Mita za mraba 180.

  Oliver Kahn Kucheza mechi yake ya mwisho leo

  Golikipa wa Bayern Munich Oliver Kahn, Jumamosi ya leo anacheza mechi yake ya mwisho kabla ya kustaafu mchezo wa soka rasmi baada ya kutumikia mchezo huo kwa miaka 21, Mchezo wa leo ni mgumu kwani timu inayocheza na Bayern ni nzuri pia na Oliver Kahn atataka kustaafu vizuri kwa ushindi kwa timu yake na bila yeye kufungwa, Bayern Munich wanawakaribisha Hertha Berlin leo kwenye ligi ya Bundesliga.

  Miss Chang’ombe Mazoezini

  Pilika pilika za kumsaka Miss Tanzania zimeanza hivo pichani baadhi ya wanyange wanaowania Taji la Miss Chang’ombe 2008 wakijifua katika Ukumbi wa Sigara (TTC), Chang’ombe Jijini Dar es Salaam.

  Na Global Publishers

  Philipp kuichezea Bayan Munich mpaka 2012.

  Beki wa Ujerumani Philipp Lahm, ameamua kuongeza mkataba na timu yake ya Bayan Munich baada ya kuwa na maongezi na kocha wake Jugen Klinsmann, katika mkataba mpya Philipp atakaa na timu hiyo mpaka mwaka 2012.

  Thursday, May 15, 2008

  Ngoma Inogile American Idol

  Wanafainali wa shindano la American Idol David Cook na David Archuleta, hii ni baada ya Syesha Mercado mwanadada pekee aliyekuwa amebakia “kupata kura chache” katika onyesho la jana.

  Syesha Mercado, Kura hazikutosha na hivyo kupigiwa kura ya kutoka na kubaki kindumwendumbwe kwa vijana wawili.
  Majaji wa American Idol toka shoto Randy Jackson, Paula Abdul na Simon Cowell
  Mshiriki wa American Idol David Archuleta pamoja na mama yake, Lupe Archuleta, shoto, wakiwapungia mashabiki kwenye shule anayosoma May 9, 2008, huko Murray, Utah. Mashabiki wanampa David nafasi kubwa ya kushinda.
  David Cook akiimba wimbo wa ‘Take Me Out to the Ball Game’ kwenye mchezo wa ligi ya Baseball kati ya Baltimore Orioles na the Kansas City Royals uliofanyika Kansas City, Mo.

  Video na Mchezaji wa Wiki: Didier Drogba

  Tarehe ya kuzaliwa 11-Mar-1978

  Mahali alipozaliwa Abidjan, Ivory Coast
  Urefu 6’2
  Uzito 13st 3lbs
  Club Chelsea
  Nafasi Forward

  Didier Drogba
  Kwa mujibu wa gazete la Sports Gazzette la Italy, Dgrogba ni mmoja wa washambuliaji hatari sana katika bara la ulaya, linizungumzia sifa binafsi za Drogba gazeti hilo lilisema, “Drogba haogopi, ana mbio, ana nguvu na uwezo wa kumiliki mpira, misuli yake imeshika vyema, ni aina ya washambuliaji ambao mabeki wengi wanawaogopa”.

  Akiongea na Televishen ya Chelsea kuhusu kucheza kwake mpira Uingereza Drogba alisema anafurahia sana kwani ligi ya uingereza inakutanisha wachezaji toka nchi mbali mbali duniani wenye vipaji lakini kitu pekee anacholalamikia ni ubaguzi, Drogba aliongelea hili alipoongea na Televisheni ya CFI (Chanal Franc Internationa) wakati wa kombe la mataifa ya Africa juu ya kitendo chake cha kumshika korodani mchezaji mwenziwe Van Bommel’s wakati timu yake alipocheza na Netherlands, Drogba alisema

  “natamani ningekuwa na tape recorder ili niweze kuyarudia maneno ambayo wanasemaga hawa watu yenye ubaguzi, huwezi kuvumilia, wakati mwingine huoni adhabu anayofaa kupewa hivyo unaamua lolote lililoko kichwani kwa muda huo.

  Bozi Boziana ndani ya Africa Bambataa

  Toka kushoto mfanyakazi wa Clouds Fm Nasoro, Mwanamuziki wa Bozi, Prodyuza wa Africa Bambataa Joyce Kiria, Dj Too Short, Bozi Boziana, Malkia Sofia Kessy na Agape Msumari wakipiga picha ya pamoja baada ya mahojiano ya moja kwa moja na Bozi Boziana kwenye kipindi cha Africa Bambataa jana jioni.
  Muzee Bozi Boziana akiwa na muimbaji wake walipokuwa Live kwenye kipindi cha African Bambataa Jana jioni.
  Mtangazaji wa Clouds FM African Bambataa Malkia Sofia Kessy akirusha kipindi cha mahojiano na Bozi Boziana Jana. Sofia leo anasherehekea siku yake ya kuzaliwa, Happy Birthday Dadaa.

  Toka kushoto Muimbaji wa Bozi, Prodyuza wa Africa Bambataa joyce kiria , Agape Msumari na Bozi Boziana.
  Muimbaji wa Bozi Boziana, Prodyuza Joyce Kiria, Malkia Sofia Kessy, Bozi Boziana na Baunsa wa Akudo jana kwenye studio za Clouds Fm.

  Akiongea kwenye kipindi hicho jana, pamoja na mambo mengine yahusuyo muziki Bozi aliongelea mabadiliko ya muziki kama haya walioyafanya akudo impact kuufanya muziki wa dance kuwa tofauti na wazamani yani kuuweka katika sura ya kizazi kipya cha muziki wa dance. Bozi alisema “Ni vizuri nakubali na nafurahia sana kuona mabadiliko na ndio maana leo nipo hapa Tanzania kuwarithisha mikoba yangu vijana wa masauti kwakuwa na mimi ni baba wa masauti Pia Bozi alizungumzia suala la kijitoa kwa wanamuziki na kuanzisha bendi zao wenyewe au wanakuwa Solo na kusema “Unajua watu wamekuwa na mitazamo tofauti tofauti tofauti wakidhani kuwa akiondoka katika bendi fulai ndio kupata mafanikio lakini sivyo na wakati mwingine ndivyo so sikatai kuhama kwao ila wajiangalie kabla ya kufanya maamuzi maana unaweza kutoka ukafanikiwa na unaweza ukatoka na usifanikiwe pia, lakini mara nyingi nyota ya mtu hung’aa akiwa na bendi husika na unaweza usifanye vizuri, kwani katika muziki watu hutegemeana pia.
  Mwanamuziki Bozi Boziana atawasindikiza Akudo sound kwenye uzinduzi wa albamu yao kesho.

  Jikumbushe na wimbo huu wa Bozi Boziana

  Wednesday, May 14, 2008

  Bozi ndani ya Zizou Fashion  Mwanamuziki Bozi Boziana akifanya shopping kwenye dula la Zizzou Fashion Sinza leo asubuhi, akiwa ameongozana na stage shoo wake, pichani Bozi Boziana akichagua kiatu kutokea huku mnenguaji wake Blaisesse Ayembe akimsistiza kutokiacha kibuti hicho ambacho mabrazameni wamekipa jina la Ngwasuma.
  Na Global Publishers

  Uzinduzi wa Akudo Bozi atua Dar

  Baadhi ya warembo waliojitokeza kumlaki Muzee Benzi, aliyeipa mgongo camera na kaptula ya khaki ni Aunt Lulu aliyekuwa Bingwa wa shindano la Kimwana Manywele wa Twanga Pepeta mwaka juzi.

  Mkongwe wa DRC – Congo Bozi Boziana (kushoto) akisalimina na King Kikii na Kassim Mapili (katikati) alipowasili jana jijini Dar es Salaam.


  Mwanamuziki mkongwe kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Mbezu Bokili maarufu kama Bozi Boziana akizungumza na waandishi wa Habari baada ya kuwasili nchini jana katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwal Nyerere Dar es Salaam. Atasindikiza uzinduzi wa albam ya Akudo.
  Leo Bozi Boziana atakuwa na mahojiano na Kipindi cha Africa Bambataa kinachorushwa na Clouds Fm. Clouds ni mmoja wa wadhamini wa uzinduzi wa wanapekechapekecha Akudo Impact.
  HAbari na picha na Father Kidevu

  Concert ya JB Mpiana Rotterdam

  Kagera Yapeta kombe la TAIFA

  TIMU ya soka ya Mkoa wa Kagera ‘Lweru Eagles’ jana ilitinga robo fainali ya michuano ya Kombe la Taifa baada ya kuifunga Ruvuma kwa penalti 4-2.
  Hatua hiyo ya kupigiana matuta ilikuja baada ya timu hizo kufungana mabao 2-2 katika dakika 90 za mchezo huo. Katika utaratibu huo Kagera ilipata penalti 4, huku Ruvuma ikipoteza penalti 2 na hivyo Kagera kutinga hatua hiyo, ambapo sasa itacheza na Arusha.
  Penalti za Kagera zilikwamishwa kimiani na David Charles, Martin Muganyizi, Juma Seif na Yahya Khan, wakati za Ruvuma n Ramadhani Kudunda na Paston Chawinga, huku Idd Ajira na Abdallah Ausi wakipoteza. Katika dakika 90 za mchezo huo, Kagera ilikuwa ya kwanza kupata bao lililofungwa dakika ya pili na Mussa Ngunda akiunganisha krosi ya Shamte Ally Ruvuma ilisawazisha bao hilo dakika ya 31 mfungaji akiwa Abdallah Ausi aliyetumia vyema makosa ya kipa Odo Nombo wa Kagera aliyetoka langoni. Kagera ilipachika bao la pili dakika ya 45 mfungaji akiwa Paul Ngwai kwa shuti lililomshinda kipa Faraja Luanda, ambapo Ruvuma ilisawazisha dakika ya 69 mfungaji akiwa Omari Kapilima.Paul Kabange wa Kagera alioneshwa kadi nyekundu na mwamuzi kwa mchezo mbaya.

  Scolari: Nategemea Ronaldo kuwa kwenye kiwango hichohicho

  Ronaldo ameifungia klabu yake ya Manchester magoli 41 kwa msimu huu.
  kocha wa Timu ya Taifa ya Ureno (Portugal) Luiz Felipe Scolari amemtaka Ronaldo kuonyesha umahiri wake kama anapokuwa na kikosi chake atakapojiunga na timu ya Taifa mara baada ya Mechi yao n Chelsea tarehe 22 mwezi huu kwenye kinyang’anyiro cha Euro 2008.
  Ronaldo na Nani wote wakiichezea Manchester United wametajwa kuwemo kwenye kikosi cha wachezaji 23 cha timu ya taifa ya Ureno kwa ajili ya michezo hiyo inayotazamiwa kuanza tarehe 7 June.
  “Hakuna wasiwasi Ronaldo yuko fit na kwenye kiwango, ila siwezi kuahidi kuwa atacheza kwa kiwango mnachomuona nacho leo hii akiwa na klabu yake ya Manchester, alisema Scolari.
  difenda wa Chelsea Ricardo Carvalho na Paulo Ferreira ni miongoni mwa wachezaji waliomo kwenye kikosi cha Scolari.
  Hivi majuzi Chelsea wametangaza kumnyakuwa mchezaji mweingine machachari toka Urno mzaliwa wa Kongo Jose Bosingwa kwa kitita cha £16.2milioni.

  Drogba, Terry kucheza na Man U.

  Boss wa Chelsea Avram Grant anategemea wachezaji wake John Terry (shoto) na Didier Drogba (kulia) wanatarajia kupona na kuwemo kwenye kikosi cha Chelsea kitakachocheza kwenye fainali Moscow.
  Terry na Drogba wote kwa pamoja waliumia wakati wa mchezo na Bolton jumapili iliyopita.

  akiongea kuhusu wachezaji hao Grant alisema: “Tunahitaji kusubiri mazoezi ili siku ya Jumatano ili tuone hali zao, lakini Terry nafikiri atakuwa ok mpaka siku ya Mechi, Drogba alipata maumivu makali kwenye kisigino ila daktari anasema ataweza kucheza, nafikiri atafanya linalowezekana tuwe naye uwanjani tunamhitaji”.
  Drogba aliliambia gazeti la Ufaransa L’Equipe kuwa kuumia kwake si saaaana na aliongeza kuwa hakuna anayetaka kuikosa hii mechi, nitakuwepo.”
  Drogba alisema kuwa mguu alioumia ni ule ule alioumia na kufanyiwa upasuaji mdogo mwezi December mwaka jana, ila si kitu nitakuwepo mazoezini wiki hii.
  Chelsea wanatarajiwa kukutana na Manchester United kwenye Kinyang’anyiro cha Fainali za Kombe la UEFA kitakachofanyika Moscow Urusi tarehe 22 May 2008.

  Thiery Hanry ndani ya Champion for Africa.

  ‘Kanoute’s friends’ team player Thierry Henry (R) shakes hands with International Team’s goalkeeper Casillas before thier friendly football match “Champions for Africa” at the Sanchez Pizjuan stadium in Sevilla, southern Spain, on May 13, 2008.

  Champions for Africa

  Kanoute’s friends team and International Team players are pictured before their friendly football match “Champions for Africa” at the Sanchez Pizjuan stadium in Sevilla, southern Spain, on May 13, 2008

  Atlas na Boca leo

  Kocha wa timu ya Atlas ya Mexico Miguel Brindisi, wa tatu toka kulia, akiongea na wachezaji wake wakati wa mazoezi kwenye uwanja wa Amalfitani Stadium huko Buenos Aires, jana, Timu hii itacheza na Boca Junior ya Argentina leo tarehe 14, katika mtanange wa kinyang’anyiro cha Copa Libertadores.

  Mashabiki wa Bekham

  Mashabiki waliofika kwenye uwanja wa Commonwealth Stadium, Edmonton huko Alberta kuangalia mpambano wa soka wa kirafiki kati ya Los Angeles Galaxy na Vancouver Whitecaps, jana May 13, 2008.Timu ya Los Angels Galaxy ndiyo timu anayochezea David Bekham kwa sasa.

  Tuesday, May 13, 2008

  Mwana wa Rais Bush, Jenna Bush Afunga ndoa.

  Rais Bush akila Pose la Picha muda mfupi kabla ya kufungwa ndoa kati ya Mwanaye Jenna na Henry Hager Jumamosi tarehe 10 May, 2008

  Familia ya Rais Bush toka shoto Barbara ambaye ni pacha mwenzie Jenna, Laura na George
  siku ya harusi ya Jenna.

  Jenna na Henry wakishikana mikono mbele ya Kiongozi wa Kanisa wakati wakifungishwa ndoa Jumamosi ya tarehe 10 May, 2007.

  Rais Bush alitumia mwezi mzima kwa maandalizi ya harusi ya kipenzi binti yake Jenna. hatimaye Jumamosi yakatimia katika harusi iliyofanyika katika Ranchi ya Rais huyo.

  “Mwanetu kipenzi Jenna amefunga ndoa na kijana mzuri kwa kweli, ni rafiki yake wa siku nyingi Henry Hagga, alisema Bush akiwa sambamba na na mkewe Laura wakati wakipanda ndege kurejea Ikulu kwa shughuli za ujenzi wa Taifa.

  Ndoa hiyo ilifungwa huku kukiwa na ilinzi mkali eneo lote ikiwa ni tangu siku kadhaa kabla ya harusi eneo hilo lilikuwa kwenye ulinzi mkali, ndugu jamaa na marafiki wa familia zote mbili walijumuika kula na kunywa.

  Tukio hili la kifamilia halikuonyeshwa moja kwa moja na Televisheni za Marekani kwani familia ya Bush haikupenda hilo.

  Na southernledger.com

  Mkongwe Suge Knight alambwa kichapo

  Mkongwe Suge Knight alilambwa kichapo katika ugomvi ambao ulihusisha kundi la watu wakiwa Club.

  Kwa habari na picha zaidi mtembelee Haki Ngowi

  Kapt. Komba Awakoromea Misambano,Hegga


  Mkurugenzi wa T-RESPECT (T.O.T), Kapteni John Komba (pichani) ,mwishoni mwa wiki iliyopita aligeuka mbogo na kutaka kuwalamba vibao wanamuziki wake,Rogart Hegga na Abdul Missambano ambao walishindwa kusimamia vizuri mazoezi ya bendi yao, yaliyokuwa yakifanyika ndani ya Ukumbi wa Dar West Park, Tabata, Dar es Salaam.
  “Nononooo, hebu njoooni hapa, bado sijaridhika na safu ya unenguaji, kuna sehemu wanakosea, nataka warudie kucheza na makosa kama hayo nisiyaone tena,” alisikika akifoka Kapteni Komba.Pamoja na makosa hayo madogo madogo, bendi hiyo kwa sasa inakuja juu katika sanaa ya dansi na tayari imeshaonesha kuwakuna mashabiki kibao wanajitokeza mazoezini.Habari hii kwa hisani kubwa ya Haki Ngowi

  Bekham aitwa Kikosi cha Uingereza

  NYOTA wa zamani wa Manchester United, David Beckham ametajwa katika kikosi cha England kitakachocheza mechi za kirafiki na Marekani, Trinidad na Tobago. Kocha Mkuu wa England, Fabio Capello amemtaja kiungo huyo ambaye hivi sasa anakipiga katika klabu ya Los Angeles Galaxy kuwa ni miongoni mwa wachezaji 3, ambao wataivaa Marekani kwenye Uwanja wa Wembley Mei 28 na katika mechi nyingine dhidi ya Trinidad itakayofanyika Juni mosi.
  Terry aliyepata majeraha wakati wa mechi ambayo Chelsea ilitoka sare ya bao 1-1 na Bolton anatarajiwa atakuwa amepona na ni miongoni mwa wachezaji watano kutoka kikosi chaBlues. Mbali na wachezaji hao, pia kocha Capello ameita wachezaji wanne kutoka timu ya Manchester United, ambayo juzi ilitwaa ubingwa wa Ligi Kuu kwa mara ya 10 katika kipindi cha miaka 16 na mara ya pili mfululizo baada ya kuichapa Wigan mabao 2-0 katika mechi ya mwisho ya ligi hiyo. Katika kikosi hicho Capello amewaita mabeki watatu wapya akiwemo wa Everton, Phil Jagielka wa Middlesbrough, David Wheater na wa Blackburn, Stephen Warnock na pia amemuingiza mshambuliaji wa West Ham, Dean Ashton ambaye alitajwa katika kikosi ambacho kiiikabili Ugiriki mwaka 2006, lakini akakabiliwa na matatizo ya enka akiwa mazoezini.
  Kiungo wa Tottenham, Tom Huddlestone mshambuliaji wa Aston Villa, Gabriel Agbonlahor na mlinda mlango wa Manchester City, Joe Hart pia kwa mara kwanza wataonekana kwenye kikosi hicho. Kikosi kamili kilichotajwa na kocha huyo ni walinda mlango, David James (Portsmouth), Joe Hart (Manchester City) na Chris Kirkland anayedakia Wigan.
  Mabeki ni Wayne Bridge (Chelsea), Wes Brown (Manchester United), Ashley Cole (Chelsea), Rio Ferdinand (Manchester United), Phil Jagielka (Everton), Glen Johnson (Portsmouth), John Terry (Chelsea), Stephen Warnock (Blackburn), David Wheater (Middlesbrough) na Jonathan Woodgate (Middlesbrough). Viungo ni Gareth Barry (Aston Villa), David Beckham (Los Angeles Galaxy), David Bentley (Blackburn), Joe Cole (Chelsea), Stewart Downing (Middlesbrough), Owen Hargreaves (Manchester United), Tom Huddlestone (Tottenham), Steven Gerrard (Liverpool), Jermaine Jenas (Tottenham), Frank Lampard (Chelsea), Theo Walcott (Arsenal) na Ashley Young (Aston Villa). Washambuliaji ni Gabriel Agbonlahor (Aston Villa), Dean Ashton (West Ham), Peter Crouch (Liverpool), Jermain Defoe (Portsmouth), Michael Owen (Newcastle) na Wayne Rooney (Manchester United).

  Maradona uwanjani tena


  Mchezaji wa Argentinean Mkongwe Diego Armando Maradona akionyesha mbwembwe katika mchezo wa Hisani jana.

  Maradona na Zico

  Wakongwe wa soka Diego Armando Maradona, kushoto, na Mchezaji wa zamani wa Brazili ace Zico wakati wa mchezo wa Maalum wa hisani wa Soka kwenye uwanja wa Rome Olympic stadium, jana jumatatu May 12, 2008.

  Bekham wa makeke…

  Mchezaji wa Los Angeles Galaxy’s David Beckham akipita kwenye uwanja wa ndege wa Edmonton International Airport akiwa na timu yake Jumatatu May 12, 2008 huko Edmonton, Alberta. The Galaxy wako Edmonton kucheza na timu ya Vancouver Whitecaps leo jumanne, May 13. Tangu mchezaji huyo ahamie Ligi ya Amerika kumekuwa na ongezeko kubwa la wapenzi wa mchezo huo ikilinganishwa na awali na amekuwa kivutio kila anapopita.

  Ferguson ahaidiwa Mshiko kuimarisha Kikosi

  Mkurugenzi Mtendaji wa Manchester David Gill

  Mkurugenzi mtendaji wa Manchester United David Gill amemuahidi Sir Alex Ferguson kitika kwa ajili ya kuimarisha kikosi chake cha ushindi kwa msimu ujao.
  Gill alisema: “Tuko kwenye nafasi ambayo tunahitaji kuiimarisha ili tuweze kubaki juu”.
  “Mi ligi bora katika dunia, kama tunahitaji kuwa bora zaidi ni lazima kuangalia katika kikosi chetu, tuanzie hapa tulipo kuhakikisha kila udhaifu unafanyiwa kazi”
  Mkurugenzi huyio aliyasema hayo katika shamrashamra za kusherehekea ubingwa wa timu yake iliyoupata jumapili hii.

  Tunafurahia kuwa pamoja na Owen Hargreaves, Anderson, Carlos Tevez pamoja na Nani ambao kwa pamoja waliongezwa kwenye kikosi na matunda tunayaona.

  CHELSEA yamnyakuwa Mcongo toka Porto

  Timu ya soka ya Chelsea imekamilisha kutia saini mkataba na mchezaji wa Porto Jose Bosingwa mkataba wa miaka mitatu kwa thamani ya Pound £16.2milioni.
  Mchezaji huyo mwenye miaka 25 raia wa Ureno na mzaliwa wa Congo ataungana na timu yake mpya ya Chelesea mara baada ya michezo ya Euro 2008.
  Bosingwa, ambaye pia alikuwa akiwaniwa na Manchester United, alizaliwa katika Jamhuri ya watu wa Kongo lakini alihamia Ureno akiwa bado mdogo.
  Ndoto zangu ni kucheza timu kubwa, nilikuwa nachezea timu kubwa lakini kwa sasa nakwenda wenye timu kubwa zaidi, nina marafiki kule Chelsea, nia na ndoto yangu ni kuona tunabeba Kombe, na natumai tutafanikiwa nikiwemo pia. alisema Bosigwa alipokuwa akiongea na Chelsea Televisheni.

  FM V/s Akudo Ngoma inogile

  Vita ya Akudo ya Akudo na FM inaendelea na FM kusisitiza uwepo wa onyesho lao, likiwa na kila kitu kimeshabihiana na maandalizi ya Uzinduzi wa Akudo “wazee wa masauti”, Katika Onyesho la FM ambalo linatazamamiwa kuwa katika ukumbi wao wa nyumbani wa Msasani Fm wapepanga kumleta General Def Defao akiwa na Montana ambaye alijitoa kipindi fulani na kuwa na Koffi pia wameweka kikundi cha Taarabu cha zanzibara star ambapo katika uzinduzi wa Akudo wao wanamleta Nguli Bozi Boziana na watasindikizwa na Mzee Yusuph na Jahazi Morden Taarab.
  Pamoja na wadhamini wengine Akudo wanadhaminiwa na mabingwa wa Burudani Redio ya watu Clouds FM kupitia kipindi chao cha Africa Bambataa.
  Wakiongea baadhi ya wapenzi wa burudani wametoa maoni yao wengi wakikilaumu kitendo cha FM kwa kusema kuwa FM wangewaachia Akudo wamalize Uzinduzi wao, “sio kweli kila mmoja ana wapenzi wake” alisema mmoja wa wadau hao. Ukienda FM mashabiki ndio hao hao unaowkuta kwenye shoo za Akudo, sikiliza hata ma PDG wanaoimbwa ni wale wale tuu, hiii inaonyesha kuwa wanategemea kwa upande wa wapenzi”.
  Binafsi nafikiri FM wanatumia nafasi ya kuwa kwenye soko siku nyingi na ni kweli FM wana waenzi wakudumu ambao pia huenda kwa Akudo, lakini wao kwa vile wako kwenye game siku nyingi wangewaacha Akudo wamalize tu haiwapunguzii chochote, alisema shabiki mwingine ambaye ni maarufu kwa bendi zote mbili.

  Monday, May 12, 2008

  Yaliyojiri Viwanjani Jana

  Baada ya miezi tisa ya Mchakamchaka wa Mtanange wa Premier League hatimaye Manchester wanatawazwa mabingwa kwa kushinda pointi mbili zaidi ya Chelsea ambao waligawana point na Bolton katika michezo yote ilochezwa jana.


  Ferguson akifurahia ushindi wake wa 10 tangu ashike usukani na timu hiyo ya Old Trafford, Manchester wanakibarua kingine wanapokutana na Chelsea kwenye mtanange wa fainali za Champions League.

  Chelsea wakishangilia goli lao katika uwanja wao wa nyumbani, hata hivyo Bolton walikaza na kumalizika 1-1.

  Birmingham 4-1 Blackburn: Mcameron Jerome akishangilia baada ya kupachika bao katika mchezo wa Birmingham na Blackburn ulikwisha kwa mabao 4-1.

  Derby 0-4 Reading: Reading walipata goli la kwanza dakika ya 15 ya mchezo kwa shuti maridhawa lililoacha mlinda mlango wa Derby akigaagaa asijue la kufanya.

  Everton 3-1 Newcastle: Yakubu aliumalizia vizuri mpira wa adhabu uliopigwa Manuel Fernandes na kuwapa goli la kuongoza mnamo dakika ya 28 ya mchezo, mpaka mwisho Everton 3-1Newcastle.

  Middlesbrough 8-1 Man City: Ilikuwa ni karamu ya Magoli, Stewart Downing ndiye aliyefungua karamu hii kwa kupachika bao kwa mkwaju wa Penati baada ya Richard Dunnes kumchezea madhambi Tuncay ndani ya Boksi.

  Sven-Goran Eriksson akiangalia timu yake ikikabiliwa na mtihani mgumu jana, hii itakuwa mechi yake ya mwisho kama Meneja wa Klabu kwani kichapo cha magoli 8-1 kimepigilia msumari wa mwisho kwenye jeneza la Bosi huyo.

  Portsmouth 0-1 Fulham: Danny Murphy ndiye aliyekuwa shujaa wa mchezo baada ya kuwasaidia Fulham wasishuke daraja baada ya kupachika bao mwanana dakika ya 76 ya mchezo wao na Portmouth uliochezwa Fratton Park.

  Sunderland 0-1 Arsenal: Theo Walcott alisukuma mpira kiulaini na kumuacha golikipa wa Sunderland Marton Fulop asiwe na la kufanya na kuipa Arsenal ushindi wa 1-0.

  West Ham 2-2 Aston Villa: Mpira wa adhabu uliopigwa na Nobby Solano dakika ya 8 ya mchezo, uliwapa wagonga nyundo “The Hummers” bao la kuongoza lakini mpaka mwisho wa mchezo mabao yalikuwa 2-2.

  Ashley Young alipachika bao la kusawazisha kwa Villa kabla ya Gareth Barry hajafunga na kufanya Villa waongoze mechi hiyo ilofanyika Upton Park.

  Baada ya Filimbi ya mwisho kupulizwa, wachezaji na mashabiki wa Manchester walilipuka kwa furaha na kuanza kushangilia ushindi wao wa 10 chini ya Bosi Alex Furguson, Man U walikuwa na kila sababu ya kushangilia kwani Vinara wenzao Chelsea walikuw wamewakalia kooni na wao kutoka droo ya 1-1 dhidi ya Bolton.

  Sunday, May 11, 2008

  Ni Manchester United

  Cristiano akipiga penati kufunga goli la kwanza

  Giggs Chini akipongezwa baada ya kupachika bao la pili.

  Timu ya Manchester United imefanikiwa kuchukua kombe la Ubingwa wa Premier League kwa pointi mbili zaidi ya Chelsea ambao walikuwa kwenye kinyang’anyiro kwa kuwa na pointi sawa mchezo ulikuwa mkali kwa upande wa Manchester na Wigan huku Wigan wakionyesha kuwabana na kutowapa nafasi Manchester kipindi cha kwanza ingawa kulikuwa na kosa kosa nyingi kwa kila upande, mpaka mapumziko matokeo yalikuwa 1-o Manchester wakiongoza kwa bao moja lililofungwa na Cristian Ronaldo kwa njia ya Penati baada ya Rooney kuchezewa madhambi ndani ya boksi. Kipindi cha pili kilianza kwa kasi huku Manchester wakilishambulia lango la Wigan na Wigan kurudisha mashambulizi ingawa hayakuwatisha sana ManU kwani baada ya kubadilishwa Scholles na kuingia Gigs alileta changamoto kwa upande wa Manchester na alifanyikiwa kupachika bao la pili baada ya kupewa pasi akiwa karibu kabisa na kipa na ku press mpira ule na kuandika bao la pili, hadi mwisho ManU 2-0 Wigan.
  Matokeo ya michezo ya leo yalikuwa kama ifuatavyo.


  Mabingwa ni :
  Manchester United
  Klabu zitakazo cheza Champions League ni:
  Manchester United, Chelsea, Arsenal, Liverpool
  Uefa Cup ni: Everton
  Intertoto Cup ni: Aston Villa
  Walioshuka ni: Reading, Birmingham, Derby
  PREMIER LEAGUE
  FT Birmingham 4-1 Blackburn
  FT Chelsea 1-1 Bolton
  FT Derby 0-4 Reading
  FT Everton 3-1 Newcastle
  FT Middlesbrough 8-1 Man City
  FT Portsmouth 0-1 Fulham
  FT Sunderland 0-1 Arsenal
  FT Tottenham 0-2 Liverpool
  FT West Ham 2-2 Aston Villa
  FT Wigan 0-2 Man Utd

  Mashabiki matumbo moto

  Huku zikiwa yakiwa yamebaki masaa kadhaa kabla ya mitanange ya fainali mechi za mwisho kuamua mshindi, mashabiki wako roho juu kila mmoja akijaribu kutetea upande wake kuwa utashinda kikombe hicho. Hakuna mechi inayotabirika leo kwani kwa droo yeyote Man anabeba “chikombe” kwani Man U wanatofauti kubwa ya magoli, kwa Upande wa Chelsea wanatarajiwa kubebwa na mashabiki 62,000 walioshakata tiketi kwa ajili ya kuuona mtanange huu, ambapo inakadiriwa 90% ni mashabiki wa Chelsea, kwani Chelsea wanacheza nyumbani leo na Man U wanacheza ugenini.

  Mechi za leo ni kama ifuatavyo:-

  15:00 Birmingham C. ? – ? Blackburn R.
  15:00 Chelsea ? – ? Bolton W.
  15:00 Derby County ? – ? Reading
  15:00 Everton ? – ? Newcastle U.
  15:00 Middlesbrough ? – ? Manchester C.
  15:00 Portsmouth ? – ? Fulham
  15:00 Sunderland ? – ? Arsenal
  15:00 Tottenham H. ? – ? Liverpool
  15:00 West Ham U. ? – ? Aston Villa
  15:00 Wigan Athletic ? – ? Manchester U.

  Saturday, May 10, 2008

  Mchizi wangu Remix

  Wimbo wa wasanii Nako 2 Nako ‘We ndo mchizi wangu’ hivi karibuni umerudiwa na kufanyiwa remix ambayo imewakutanisha wasanii kibao na wakali akiwemo, Jay Moe, Fid Q, Mansu-Li, Geez Mabovu, Dr K wa Mapacha, Adili Chapakazi, Chidi Benz, Mwanafalsafah, Mheshimiwa Temba, Babuu wa King’oko na wenye ngoma yao ambao ni Nako 2 Nako Souldierz. Bofya hapa ukausikilize

  Taboo Fatoo Top Model

  Mwanamuziki Faustin Ipupa Nsimba aka Fally Ipupa Di Caprio, Album yake ya “Droit Chemin” ndiyo Album bora ya Mwaka 2007/2008, kwa sasa Albamu hiyo ndio inauza na kufanya vizuri kwenye soko, katika Album hiyo kuna wimbo unaitwa “Liputa” kwenye huo wimbo amededicate kwa Taboo Fatou ” Mama na Compressor”(pichani), huyu ni Mfanyabiashara Mrembo anaishi Belgium, ana miliki maduka kadhaa ya Nguo huko Paris(France) na Beligium,na inasemekana zile Pamba zote za Fally, Taboo Fatou ndiyo anamvalisha, kwa wale wapenzi wa JB Mpiana watumbuka katika Album yake ya Kwanza(Solo) Feux D’Lamour,kuna wimbo unaitwa “Top Model” utampata humo Tabu Fatou.

  Gonga hapo umsikie Jb Mpiana na Taboo Fatoo Top Modele”.

  Ze Comedy wajitoa East Africa TV

  KUNDI maarufu la sanaa za maigizo The Comedy (pichani) limemaliza mkataba wake na kituo cha televisheni cha East Afrika (EATV) kinachorushwa kila siku ya Alhamis.

  Kutokana na kumalizika mkataba huo kipindi hicho maarufu hakitarushwa kuanzia Alhamis ijayo. Kundi hilo liliingia mkataba wa mwaka mmoja na miezi nane kufanya kazi na EATV uliofikia ukingoni juzi.

  Ukiondoa Ze Comedy, naye Mratibu wa kundi hilo Sekioni David amesitisha mkataba na kituo hicho na sasa anaelekeza nguvu zake ndani ya kundi hilo.
  “Baada ya kuufahamisha uongozi nia yetu, nilipatwa na mtihani mgumu sana, maana niliambiwa nichague kuendelea kutangaza au kupumzika na Ze Comedy. Nimechagua kupumzika na kundi hili na sitajutia uamuzi huu hakika, mimi ni msanii msanii wa siku nyingi na nina uzoefu wa muda mrefu. Kama nilivyoweza mwazo kuiinua Ze Comedy, ndivyo nitakavyoweza kuiendeleza zaidi,’’ alisema Seki.

  Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Mkurugenzi Mtendaji wa Kundi hilo, Isaya Mwakilasa (Wakuvanga) alisema wameamua uamuzi huo ili kupata mapumziko kwa muda kabla ya kuendelea na sanaa hiyo.

  Mwakilasa alisema wanasikitika kumaliza mkataba na EATV na hivyo wameamua kurudi nyumbani kujipanga upya lakini pia wanaweza kuingia mkataba mpya endapo watakubaliana.

  “Mkataba wetu na EATV umeisha nasi tumeamua kurudi nyumbani kupumzika kwa nia njema, hasa kwa maslahi ya wengi zaidi na tulikuwa tukifanya kazi nao vizuri na huu si mwisho wetu,” alisema Mwakilasa.

  Mwakilasa alikanusha taarifa kuwa Ze Comedy lina mpango wa kuingia mkataba mpya na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC 1) na kuongeza kuwa sanaa ni ajira yao hivyo kama watahitajika hawasita kuingia mkataba na kituo hicho.

  Kamali ya Mpira yawanufaisha mashabiki

  Kilomita 50 toka mji wa Kuala Lumpur Malaysia, Genting (pichani) ni maarufu kwa starehe za aina zote kuna kasino kubwa ambayo hukutanisha mataikun wa kila sehemu ikiwa ni pamoja na Singapore, Malaysia, Thailand na hata Indonesia, ukifika usiku ni milio ya Helcopter kila mmoja akiingia na kutoka kwenye jumba la Casino la sehemu hii changamfu.

  Kuanzia wiki iliyopita mahoteli yamejaa kwa ajili ya weekend hii ambapo wacheza kamali wanamiminika kwa ajili ya kubashiri ushindi wa mchezo wa Mwisho unaowajumuisha Manchester na Chelsea kila mmoja akiwa na kibarua chake.

  Asia mpira ni biashara, toka kuuza jezi, sticker hadi matokeo kwani kunawaopoteza nyumba, magari na pesa taslimu kila siku, imekuwa ni sehemu ya utamaduni na ndio maana hizi timu kubwa haziishi kuja alisema Raj, Tax driver anayefanya shughuli zake Genting.

  Kuna wanaotegemea mechi hizi kula na kulisha familia, nimekuwa nikicheza kamali ya mpira kwa mika nenda rudi, ni rahisi kupoteza na kupata pia kwani kwa mechi ndogo dau ni dogo kwa mechi kubwa ambayo matokeo hayatabiriki hapo ndio wengi hucheza na wengi hupoteza alisema Raj.

  Binafsi nimenunua ticket za Ringit 800 (dola 250) nategemea ikishinda napata mara mara nne ya hapo, nasali Man washinde, siku ya Chelsea na Man nilipata Ringit 5000 (sawa na dola 1600). Nilifurahi mke wangu alikuwa na wasiwasi lakini Inshallah tukapata.

  Ronaldo na Drogba, nani ataibeba timu yake?

  Ni wazi kuwa mtanange huu wa kesho unawategeme hawa watu wawili kufanya maajabu, thamani ya magoli kwa ushindi wowote utaibeba timu husika, na nani atabaki na Kombe muamuzi ni dakika 90, kwani Machester anacheza ugenini na Chelsea anacheza nyumbani, Chelsea ana historia nzuri ya kuutumia uwanja wa Nyumbani lakini pia Manchester bado ana rekodi ya kushinda mechi nyingi hata za ugenini, hii inawapa matumbo joto mashabiki kwani kuna uwezekano mkubwa mtanange huu ukaamuliwa kwa idadi ya magoli ambayo mpaka sasa Man wako mbele kwa tofauti ya magoli 17.

  Swali langu bado lipo pale pale kombe litawekwa wapi kusubiria mwenyewe apewe kwani timu zote zinacheza kwenye viwana tofauti na kipigo cha timu moja ni furaha ya ushindo kwa mwingine iwe atatoka sare au atashinda kwa idadi yeyote ya magoli.

  Porto wapigwa faini kwa tuhuma za kupanga matokeo

  Raisi wa FC Porto Jorge Nuno Pinto da Costa, katikati na maofisa wa klabu hiyo Adelino Caldeira, right, naFernando Gomes wakiinuka kumaliza mkutano na waandishi wa habari uliofanyika kwenye uwanja wa Dragao Porto, Portugal, ijumaa May 9, 2008. Kamati ya nidhamu ya chama cha mpira wa miguu nchini humo kimewanyang’anya point Porto na Uniao Leiria kwa madai ya kupanga matokeo katika kashfa kubwa ya mchezo wa soka ambayo haijawahi kutokea. Kamati hiyo iliamua kwamba Porto walimhonga Refarii kwenye mechi mbili katika msimu wa 2003-04 na kuamua kuwanyang’anya pointi 6 na kuwapiga faini ya Euro150,000 (US$230,000) na kumzuia Mwenyekiti Jorge Pinto da Costa kwenye kuonekana kwenye benchi la akiba kwa miaka miwili.

  Figo ana imani na Pep Guardiola

  Midfielder wa Inter Milan Luis Figo, ambaye amechezea klabu ya Barcelona kwa misimu mitano mfululizo amesema, Kocha mpya wa klabu hiyo ambaye alikuwa Kepteni ya timu hiyo zamani Pep Guardiola anauwezo mkubwa na anaweza kuleta matumaini mapya kwenye klabu hiyo. Barcelona ambayo haijafanya vizuri kwenye ligi ya na hasa mechi zake za kribuni pia imeongeza nguvu kwa kumpa timu mchezaji huyu wa zamani nafasi ya kuifunza timu hiyo.
  Na BBC sports

  Wenger asema Adebayo na Hleb bado ni wa kwao

  Mchezaji mahiri wa klabu ya Arsenal Emmanuel Adebayor amekanusha uvumi kuwa anataka kuondoka klabu yake ya Arsenal na kukimbilia Italy.

  “Nina furaha na amani sana kwenye klabu yangu ya Arsenal,” alisema mshambuliaji Adebayor. “habari zinazosema nataka kuondoka ni uzushi mtupu.”

  Hleb ana husishwa na kutaka kujiunga na klabu ya Inter Milan na agent wake amekuwa akiliongelea suala hilo la mchezaji huyo mwenye miaka 27 kuwa anataka kutoka Arsenal.

  LAkini akiongea na BBC Radio 5 Live: Wenger alisema “bado hatujawa na maongezi na klabu yeyote juu ya Adebayo wala Alexander Hleb.” Hivyo mpaka sasa hawa bado ni wachezaji wetu.
  Habari za kuondoka wachezaji hawa ziliwatia matumbo joto mashabiki wa Arsenal hasa baada ya kuondoka mchezaji Flamini.
  Na BBC Sports

  Jose Mara: Akudo waache maneno tufanye kazi.

  Pichani ni Baadhi ya wanamuziki wa FM wakimpongeza Jose Mara siku ya harusi yake, Nyoshi, Pablo masai, Patchou mwamba, roger muzungu,King blaise na kushoto kabisa ni Collins (mzee wa USA), mshabiki wa FM

  Mwanamuziki Jose Mara amemsihi mwenzake Christian Bella wa Akudo Impact kuacha maneno maneno na kufanya kazi, “mashabiki hawataki maneno, mashabiki wanataka kufurahishwa” alisema Jose Mara.

  “Nilisikitishwa na kitendo cha Bella kuongea na vyombo vya habari na kusema hawezi kufananishwa na mimi, kuwa eti mi ni mchafu mchafu, na bado mtoto kisanaa ya Muziki, Bella hapaswi kusema maneno hayo, alisisitiza Jose.
  Hii yote ilitokana na suhindanishwaji wa wanamuziki hawa wawili kwenye kipindi cha kinachorushwa kwenye TV cha (Nyumbani ni Nyumbani) cha C2C na (Afro Beat) cha East Africa TV, Huwa wanashindanisha wanamuziki wawili au vikundi vinavyofanana, Kumetokea kushindanishwa zaidi ya mara mbili kati ya mwanamuziki Jose na Bella, na Jose amekuwa akishinda.

  Inasemekana hili lilimuuma sana Bella, na alipoongea na gazeti moja akasema mimi nashang’aa kushindanishwa na Jose, Kwanza Jose si wa rank yangu,Kwanza Mchafu Mchafu, yeye yupo sawa na kila Fally, Jose anasema yeye awezi kumjibu sababu majibu anayo yeye Bella, wakati wanatoka Congo, Jose alimlea Bella kwa kila kitu kula hadi Mavazi ni kama mdogo wake, anasikitishwa na kauli za Bella.

  Ushindani wa bendi hizi umekuwa kwa kasi na hasa habari za hivi karibuni ambapo Akudo wanazindua albam yao na kumleta Mzee Bozi Boziana na FM wameandaa shoo usiku huo huo wa tarehe 16 ambapo walikuwa kwenye mipango ya kumleta Bozi Boziana, jambo linalotafsiriwa kuwa wanataka kuvuruga uzinduzi wa Akudo.

  Friday, May 9, 2008

  Ronaldo aomba msamaha.

  SAO PAULO, Brazil – Kufuatia kesi ya kugombana na “mashoga” siku kadhaa zilizopita, Mchezaji nyota MBrazilia Ronaldo ameomba msamaha na jamii imusamee kwa kilichotokea kwani anajua amewakasirisha baadhi ya watu, haikuwa nia yake ila ni mapungufu ya kibinadamu. Ronaldo ameita hiyop ni aibu kubwa ya mwaka na ni kosa ambalo atajutia maisha yake yote. Huku akitoa sauti ya huruma na kuonyesha majuto Ronaldo aliiambia Televisheni maarufu ya Brasil Globo TV kuwa anajuta kwa kilichotokea, “Kwa kipindi kifupi nimeshtukia nimepungua kilo kwani hii kitu inanitesa, kama binadamu wa kawaida inauma, najuta, natamani ningeweza kurudisha wakati nyuma ili kufuta yaliyotokea, tatizo ni kuwa kumbukumbu zinahifadhika na kudumu milele, Najua kumbukumbu yangu ya mpira itadumu milele nilijivunia hilo, ila sasa nikifikiria hili nalo litadumu naombea hata niitoe vichwani mwa watu, alisema Ronaldo kwa sauti ya huruma.
  Ronaldo alituhumiwa kuchukua wanawake watatu ili akafanye nao mapenzi katika chumba chake cha hoteli lakini baada ya kufika aligundua kuw wale walikuwa si wanawake bali ni mashoga na kuwataka waondoke lakini wao walitaka mchezaji huyo awalipe jambo ambalo lilianzisha ugomvi mpaka polisi kuitwa.

  Kesi ya R. Kelly yaanza kuunguruma

  Mwanamuziki R. Kelly, lakiwasili mahakamani ya Cook County Criminal Courthouse, Chicago leo hii (ijumaa) akiwa ameongozana na mlinzi wake katika siku ya kwanza ya kusikilizwa kesi inayomkabili, Mwanamuziki huyu anashtakiwa kwa kujihusisha na udhalilishaji watoto kijinsia kutokana na makanda wa Video ambao unadaiwa kuwa unaonyesha akifanya mapenzi na mtoto wa miaka 13.

  Video na Mchezaji wa Wiki: Samuel Etoo’

  Video yetu ya wiki hii tunammulikia mchezaji wa Barcelona, Raia wa Cameroun Samuel Etoo’, mpira una matamu na mchungu, hasa kadamnasi ikionyesha kukuamini na unapoangaliwa na watu wapatao 60,000 na wote wanategemea uwafurahishe na kuwatia machungu inaumiza sana, Etoo anasema katika vitu vinavyomnyima raha kuliko vyote ni hicho. Angalia Video hii ili ujue machungu na uwezo binafsi wa mchezaji huyu.

  Jina:
  Samuel Eto’o Fils
  Uraia: Cameroon
  Tarehe na Pakuzaliwa: March 10, 1981 Nkon, Cameroon
  Nafasi anayochezea: Mshambuliaji wa kati / winger
  Klabu anayochezea: FC Barcelona (Spanish La Liga)
  Historia ya Vilabu: 1997-1998 Leganes – Mechi 28, magoli 3

  1998-1999 Real Madrid – Mechi 3 , bila goli

  1999-2004 Real Mallorca – Mechi 133, magoli 54.

  2004-mpaka sasa FC Barcelona

  Uchezaji wa kulipwa: 1996-Mpaka sasa

  Samuel Eto’o anaheshimika kama mchezaji mwenye uwezo na mmoja wa washambuliaji bora duniani kwa sasa kutokana na uwezo wake mkubwa wa kuumiliki mpira na akili ya maamuzi ya haraka sana hasa awapo karibu na goli. Katika muda alocheza kilabu ya Real Mallorca Eto’o ndiye aliyekuwa mfungaji bora katika historia ya Klabu hiyo akimaliza na jumla ya magoli 54. uwezo huu ndio ulivutia vilabu vingi vya ulaya na kutaka kumsajili Mhcezaji huyu matata.

  Eto’o baadaye alihamia FC Barcelona 2004 kwa donge nono la ada ya uhamisho jumla ya Pound Milioni £24.
  2006 Eto’o alizawadiwa taji la “pichichi” (Mfungaji bora kwenye ligi ya La Liga) baada ya kuifungia Barcelona goli kwenye mechi ya mwisho ya msimu wa ligi dhidi ya Athletic de Bilbao.

  Etoo alipata maswahibu kwani aliumia mwaka 2006 na tangu hapo imekuwa ikimletea matatizo mara kwa mara na kumfanya kuwa nje ya dimba, ingawa timu yake haikufanya vizuri kwa msimu huu lakini bado kijana huyu amerudi kwa kasi kwenye uwezo wake wa kawaida, ingawa kuna tetesi kuwa anawaniwa na timu za Uingereza, iwe ni Spain au Uingereza bado nyota ya Etoo inaashiria kuendelea kuwaka kwa muongo mwingine kwani bado umri unamruhusu.

  Nani kuwa American Idol wa 7?

  Baada ya matokeo ya wiki hatimaye walibari watatu David Cook, David Archuleta & Syesha Mercado, mchuano bado ni mkali hasa katika ya David wawili ingawa Syesha anatoa upinzani kwa wa aina yake, ila mvuto wa akina David unamfanya awe kwenye wakati mgumu. Nani ataibuka mshindi? swali juu yako msomaji.

  Burudani ya Mpira na Muziki Giraffe Hotel

  Kwa wapenzi wa mpira, Giraffe Ocean View Hotel wanaonyesha mechi zote kwenye mandhari mwanana ya Makuti Bar ikitazama Bahari ya Hindi, Bila kusahau ijumaa ya Leo Deo Mwanambilimbi kama kawaida anatumbuiza na bendi yake ya Kalunde Band, hii ni kila ijumaa na Jumamosi, nyote mnakaribishwa.

  Allex Miller abwaga manyanga Liverpool

  Pihani ni Miller na Benitez enzi wakifanya kazi pamoja Liverpool

  Kocha namba moja wa LIVERPOOL Alex Miller amemwaga manyanga na kujiunga na timu ya JEF United Chiba ya Japan. Vyombo vya habari vya Japan vimeripoti kuwa timu hiyo ya JEF imemchukua Miller baada ya kumtimua kocha wao M-Croatian Josip Kuze wiki hii.

  Katika mkataba mpya na timu hiyo kocha Miller atalipwa mshahara wa £500,000.

  Miller, ambaye amekaa kwa kipindi cha takribani muongo mmoja Anfield, alikuja kuwa kocha wa kwanza wa Liverpool mwaka 2004 wakati Rafael Benitez alipochaguliwa Meneja.
  Ni habari njema kwa Alex, alisema Benitez jana, hii ni nafasi nzuri kwake kufanya kazi Japan, napenda kuchukua nafasi hii kumtakia mafanikio mema katika kibarua chake kipya, alimalizia Benitez.

  Kombe litakuwa wapi?

  Kwa kuwa timu zote mbili Manchester United na Chelsea wananafasi ya Kuchukua Kombe na wote wanacheza kwa siku moja, Je Kombe hili litaa wapi kwani hawa wanacheza kwa miji tofauti. Kwani inajulikana Kombe hukabidhiwa kwa Timu husika mara baada ya Mchezo kumalizika, Je kwa mpango huu Kombe litakaa mji gani?

  Manchester United: Tutajitahidi yasijirudie ya 1968

  Alex Stepney (Pichani) aliyekuwa golikipa wa Manchester United Mwaka 1968 anakumbuka sikuiku ya fainali huku wakipewa shinikizo na mashabiki kutokana na habari za mchezo uliokuwa unaendelea uwanja mwingine huku timu zote mbili zikigombea ushindi ili kuchukua kombe.

  ManU walikuwa na pointi 56 sawa na pointi 56 za mahasimu wao Manchester City, ManU walikuwa wakicheza dhidi ya Sunderland. Mashabiki walikuwa walikuwa akimpa Stepney maendeleo juu ya mchezo wa ManCity ambao kwa wakati huo huo walikuwa wakikipiga dhidi ya timu ya Newcastle. Mashabiki walikuwa wakiufatilia mchezo ule kwa njia ya redio na kutupa matokeo ili kutuhamasisha kwa ushindi, lakini mhhhh alisema Alex.

  Kiukweli sikupenda nilichokuwa nakisikia wakati ule kwani kiukweli mpaka mwisho wa mchezo tulifungwa 2-1, City wakashinda 4-3 na kuchukua ubingwa, upinzani ule haujajirudia tena mpaka sasa ndio tunaona kwenye mtanange wa jumapili hii.

  “Mashabiki walikuwa karibu kabisa na uwanja na walikuwa akipiga kelele kutwambia matokea ya City ambayo yalitutia tumbo joto na kutufanya kupanic na kushindwa mchezo ule” alisema Stepney, mwenye miaka 65 sasa.

  Mtanange wa Premier League ndio unafikia ukingoni wiki end hii huku tukishuhudia timu mbili zikikabana makoo kwa point sawa mpaka sasa Manchester United na Chelsea, wote wana point 84. ManU wanamagoli mengi zaidi ya Chelsea kwani mpaka sasa wana magili 17 zaidi ya Chelsea , kwa hivo basi matokeo ya sare yeyote kati ya timu hizo nne zitakazo cheza yanawafanya Man kuchukua ubingwa la hasha ni kuwa Chelsea ashinde na Man ashindwe, au Chelsea atoe droo na Man ashindwe, Safari ya Man U wigan na huku Chelsea ikicheza uwanja wa nyumbani inaweza kuwapa faida Chelsea kwani hizi timu ndogo zikiwa kwao huwa zinadinda sana kwa timu kubwa.

  Kimbembe hakitaishia hapo kwani kwa matokeo yeyote bado wawili hao wanakwenda kuumana tena kwenye mtanange wa fainali ya kufa mtu itakayofanyika Mei 21 jijini Moscow kwenye mtanange wa kwanza wa fainali kuzikutanisha timu zote toka Uingereza.

  O’Neill: Ofa ya Liverpool inamshusha thamani Barry

  Martin O’Neill amesisistiza kuwa kitendo cha Liverpool cha kusema kumtolea mchezaji wao Gereth Barry kiasi cha Pound 10milion ni kumshusha thamani.

  O’Neill na Barry watakauwa na maongezi katika kikao kitakachofanyika baada ya kumalizika kwa mchezo wa jumapili wa fainali ya Barclays Premier League dhidi ya West Ham kuhusu majaliwa ya baadaye ya mchezaji huyo ambaye Liverpool wanamtaka kwa nguvu zote.

  Ofa ya Liverpool ni kutoa mchezaji mmoja pamoja na donge hilo la Pound milioni 10 ambapo walitoa dau hilo hivi karibuni lakini O’Neill bado anaona kama dau ni dogo. Pia O’Neil alisema Liverpool hawajasema watatoa mchezaji gani kwani wanaweza wakakupatia mtu ambaye humuhitaji kwenye timu yako ndio maana tunakazia kwenye pesa zaidi au wangeweka wazi.

  Mazungumzo yetu si kwamba hatumtaki Barry, kwani dhamira yetu si kuuza wachezaji, dhamira yetu ni kuwa na kikosi imara na kizuri ili na sisi tufike hapo juu na ndio nafasi tunayoitaka, sasa kama mtu kampenda mchezaji wetu basi ajichinje mwenyewe, tutafanya kila linalowekana Barry abaki kwetu la haiwezekani basi tukipata dau nono litatuwezesha kutafuta mbadala wake alisema O’Neil.

  Marcio amfagilia Ivo Mapunda


  • Asema kwa Tanzania Hakuna kipa kama yeye.

  KOCHA Mkuu wa timu ya soka ya Taifa ‘Taifa Stars’, Marcio Maximo amesema atamtumia katika kikosi cha kwanza kwenye mchezo dhidi ya Mauritius kipa Ivo Mapunda (pichani) badala ya Farouk Ramadhani.

  Mapunda aliitwa katika kikosi hicho hivi karibuni ikiwa ni miezi sita tangu awe benchi kutokana na kufungiwa na klabu yake ya Yanga kwa madai ya utovu wa nidhamu.

  Kufungiwa kwa Mapunda aliyekuwa chaguo la kwanza la Maximo kulimfanya amuite kipa Farouk Ramadhani katika mchezo wa awali wa michuano mipya ya Afrika inayoshirikisha wachezaji wanaocheza ligi za nyumbani tu, ambapo katika mchezo wa kwanza Stars iliitoa Kenya ‘Harambee Stars’ kwa jumla ya mabao 2-1. Mchezo wa kwanza uliofanyika Kenya, Harambee ilishinda bao 1-0, lakini ziliporudiana Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam Taifa Stars ilishinda mabao 2-0, kipa akiwa Farouk.

  Pia katika mchezo wa kwanza hatua ya pili ya michuano hiyo dhidi ya Uganda ‘The Cranes’ uliofanyika Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza, Taifa Stars ilishinda mabao 2-0, kipa pia akiwa Farouk.

  Akizungumza Dar es Salaam jana, Maximo alisema analazimika kuanza kumtumia Mapunda kwa kuwa ni kipa mzuri zaidi ya Farouk na ana uwezo mkubwa kuliko kipa yeyote nchini, hivyo ana umuhimu kumtumia kwa mashindano makubwa.

  Alisema tofauti na Farouk, Mapunda amecheza michezo mingi ya kimataifa ana uwezo mkubwa kumudu mashindano yeyote makubwa na kwamba tangu kipa huyo arudi kwenye kikosi chakr amesharudi kwenye chati.

  Hata hivyo alisema katika mchezo wa marudiano dhidi ya Uganda wiki ijayo huenda akaanza Farouk, lakini mchezo wa kuwania kufuzu fainali za kombe la dunia 2010 dhidi ya Mauritius mwishoni mwa mwezi huu jijini Dar es Salaam atacheza Mapunda, ambapo Farouk atakuwa benchi.

  Kuhusiana na mchezo dhidi ya Uganda, Maximo alisema kikosi chake kipo katika hali nzuri isipokuwa kuna majeruhi wachache, ambao ni Uhuru na Abdi Kassim aliosema huenda wasiwepo katika mchezo huo wa marudiano kwani watakuwa nje kwa muda mrefu.

  Majeruhi wengine ni Ulimboka Mwakingwe na Henry Joseph, ambao hata hivyo watarejea uwanjani wakati wowote.

  Mheshimiwa Pinda kuupamba Uzinduzi wa Akudo

  WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda anatarajia kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa albamu ya bendi ya muziki wa dansi ya Akudo Impact utakaofanyika Mei 16, mwaka huu.

  Akizungumza Dar es Salaam jana Mratibu wa tamasha hilo, Bahati Singh alisema katika uzinduzi huo, bendi hiyo itasindikizwa na mwanamuziki kutoka Kongo, Bozi Boziana na Jahazi Morden Taarabu na utafanyika ukumbi wa Diamond Jubilee.

  Alisema Kamati ya Maandalizi ya uzinduzi huo imeahidi kutoa sh. milioni moja kwa ajili ya kusaidia kununua vitanda na magoro katika wodi ya wazazi ya hospitali ya mwananyamala.

  “Wanamuziki wametamba kutoa burudani ya kukata na shoka, ambapo wapenzi wataulizwa kama ni funika bovu au la, kama burudani haitakonga nyoyo za mashabiki, hiyo ndio itakuwa mwisho wa bendi ya Akudo,” alisema Singh.

  Singh alisema uzinduzi huo umedhaminiwa na Kampuni ya Bia Tanzania kupitia bia yake Ndovu, Vodacom, QSSP Group LTD, Clouds FM Dotnata Decoration, C2C televisheni na CM LTD.

  Tchasho Mbala

  Kwa wale wapenzi wa Muziki wa Kikongo watakuwa wanamjua au kumsikia Richard Tshasho Mbala aka Kashogi (Pichani na mkewe),ukisikiliza nyimbo nyingi za Congo utasikia jina hili, yeye ndiyo mdhamini mkuu wa Album ya Fall Ipupa (Droit chemin’) amemuoa Elvira Mujinga Mukuna,katika harusi ya kifahari ilifanyika huko Orléans (France), Inasemekana watu maarufu katika Congo na wanamuziki wakubwa wa Congo walialikwa ikiwa ni pamoja na wengine kupatiwa Ticket za Ndege kushuhudia harusi hiyo.
  Na Big Producer Maghambo

  Celtel Idols

  Hatimaye lile shindano la kumsaka kijana mwenye kipaji cha kuimba, maarufu kama Celtel Pop Idols limefanikiwa kuwapata wakali 24 (Top 24), Julius Kihampa anaanguka nayo.Washiriki hao ambao walichaguliwa na majaji Angela Angwenyi, TK Siyandi na Scar, walipatikana juzi kupitia mchujo mkali uliofanyika nchini Kenya ambapo kati yao 19 ni wasichana na wavulana 5.
  Waliotajwa kuingia Top 24 na nchi zao kwenye mabano ni pamoja na Adiona Maboreke (Zimbabwe), Alice Chinyimbe (Zambia),Alice Kalufyanya (Zambia),Ammara Brown (Zimbabwe), Chibwe Chapenuka (Zambia),Christine Apondiadda (Kenya),Cynthia Kuto (Kenya),Deborah Chansa (Zambia),Doris Onyango (Kenya),Eric Moyo(Zimbabwe),Faycal Birikunzira(Uganda) na Irenne Njunguna (Kenya).Habari hii na Abdallah Mrisho.
  Na Haki Ngowi

  Thursday, May 8, 2008

  Real Madrid walipomuua Barca 4-1

  Real Madrid wamesherehekea ubingwa wa Ligi ya Spain kwa kuwachapa watani wao Barcelona mabao 4-1 kwenye kinyang’anyiro cha El Clasico derby.
  Bonyeza Player upate uhondo

  KIJIWE MAARIFA

  Karibuni kwa mara nyingine tena, husika na WAPI …tukio la kila mwezi. Kama kawaida”WAPI” inaendelea. safari hii tunajumuika na watu wa mataifa mbali mbali kwenye mada yetu BILA KUJALI TOFAUTI… kwenye KIJIWE MAARIFA tutakuwa na Kemi KALIKAWE, FATMA AMOUR WANAMITINDO/WABUNIFU mahiri. WASAMBAZIE huu waraka watu wengine kwenye orodha yako ya anuani


  Yawaletea

  Mboli -MC mahiri chipukizi, Rage- mwakilishi wa MC Afrika TZ, Enika

  Mitindo na Kemi Kalikawe, Fatma Amour.

  Wasanii wa sauti ya handaki(undeground), Katika harakati.

  Madijei, ma emsii, machata, mabreka ,michoro mbali mbali, ushairi,ngoma, maigizo na usanifu mitindo.

  Mahali: British Council, Dar Es Salaam
  (maelekezo: Samora na Ohio, mkabala na Steers kati kati ya jiji)


  Mbali na kukutwa na Kichwa cha binadamu Rama ni msanii pia…

  Mchoro huu (Uliopigwa picha na Global Publishers) unaweza kutoa majibu ya akili ya mtoto Rama na fikra zake, Rama ni mtoto ambaye alitawala vichwa vya habari vya magazeti siku za karibuni kuhusu kukutwa na kichwa cha Mtoto Salome na kukinyonya damu mbele ya kadamnasi.

  Sanaa ya uchoraji huwa inamuwezesha Mchoraji kutoa kilichomo mawazoni mwake na kukiweka katika muonekano, mara nyingi unaweza kuona picha tuu lakini akatokea mtu na kuitolea maana na maelezo lukuki picha hiyo hiyo moja, ama kuweza kutafsiriwa na watu tofauti pia.

  Sijui huyu mtoto alikuwa akiwaza nini alipochora picha hii, lakini nafikiri wataalamu wa Saikolojia (Noel Kilonzo) wanaweza kuoanisha picha hii na tabia ya mtoto husika. Je wewe unafikiria nini?

  FM wadaiwa kupanga kuvuruga uzinduzi wa AKUDO

  Kundi la Muziki la FM Academia linatarajia kumleta mwanamuziki General Defao kuja kutumbuiza nao siku ya May 16 katika onyesho lililoitwa “Uchwara” ambalo dhamira yake ni kuvuruga uzinduzi wa Akudo Wazee wa Masauti, ambapo siku hiyo pia watakuwa na Uzinduzi wa Albamu yao mpya, Ikumbukwe pia Akudo walishatangaza kumleta Mwananamuziki Bozi Boziana ili kuwasindikiza kwenye uzinduzi huo ambao unasemekana kuwa wa aina yake. Lakini habari zinasema endapo Defao akitia timu hapa Tanzania, huenda akalakiwa na pingu kutokana na tuhuma mbalimbali zinazomkabili.
  Defao anatarajia kuja nchini hivi karibuni kwa mwaliko wa bendi ya FM Academia ambapo inadaiwa atatumbuiza na bendi hiyo katika onesho ‘uchwara’ linalodaiwa kuandaliwa mahususi kwa ajili ya kuvuruga uzinduzi wa bendi ya Akudo Impact ‘Vijana wa Masauti’ Mei 16 mwaka huu.

  Madai ya Defao kutiwa mbaroni yamekuja kutokana na kile kinachodaiwa kuwa alipofanya ziara ya mwisho hapa nchini alitoroka akiwa anadaiwa mamilioni ya hela za pango katika Hotel ya Sea Cliff pamoja na fedha ya matibabu katika Hospitali ya TMJ.
  Kumekuwa na mashindano kati ya Bendi hizi nchini siku za karibuni na kwa sasa ushindani unatarajia kuwa mkubwa kwani ujio wa TOT Respect utanogesha burudani ukizingatia bado kuna Twanga Original na Twanga Chipolopolo, Patamu hapo mwanangu.

  Source: Global Publishers

  Taifa Stars wapongezwa

  Kampuni ya Bia ya Serengeti Breweries iliandaa chakula cha jioni katika kuwapongeza wachezaji na makocha wa Timu yetu ya Taifa Stars, hii inasaidia kuwatia moyo na morali wachezaji na kuona kuwa watu wanatambua mchango wao. Mgeni Rasmi alikuwa waziri wa Habari na Michezo Mh. George Mkuchika.
  Pia inanikumbusha jinsi watanzania walipojitoa wakati timu yetu ikishiriki hatua za awali za kombe la Africa, natuma Taifa Stars itawapa raha watanzania na kuleta kombe nyumbani, inshallah kila kiti chawezekana.

  Pichani Kocha wa Taifa Stars na msaidizi wake akikokokotwa na watoto wa kikundi cha sanaa ya Ngoma na Sarakasi kwenda kucheza Sindimba.

  Golikipa wa Taifa Stars, Ivo Mapunda akitoa mkono baada ya kukamata kilicho chake
  Deo Mwanambilimbi pia alikuwapo kutoa Burudani na Bendi yake ya Kalunde.
  (picha zote na Sir Michuzi.)

  Wednesday, May 7, 2008

  Mbwembwe za Wanamuziki mazishi ya Madilu System

  Wazaire wanaongoza kwa mbwembwe iwe kwenye shughuli yeyote hata msiba!! ilibidi Polisi na wanajeshi kuingilia kati kutuliza umati hasa walipokuwa wakiwasili wanamuziki wakubwa wenye uhasimu kwenye msiba wa Nguli wa Muziki wa Kilingala Madilu System. angalia video hii jinsi JB Mpiana na Werason walipoweza kushikana mikono na mbwembwe zao hata mazikoni.

  Wenger asikitishwa kuondoka Flamini

  Kocha Arsene Wenger ameonyesha kusikitishwa kwake na mpango wa mchezaji wake Mathieu Flamini ambaye anaondoka kwenda AC Milan msimu ujao.

  Mfaransa huyo mwenye miaka 24 amekamilisha uhamisho wake wa kwenye kucheza ligi ya Seria A na klabu yake mpya ya AC Milan. Arsenal walijitahidi kwa hali na mali kuendelea kwa na mchezaji huyu ambaye kwa kiasi kikubwa alikuwa anaelewa sana kiuchezaji na Cesc Fabregas kwa uhai wa timu na aina yao ya uchezaji. Pamoja na ahadi ya donge nono kwenye mkataba mpya ambapo waliahidi kumpatia kitita cha Pound £55,000 kwa wiki lakini mchezaji huyo hakubadili nia.

  Kwa sababu alikuwa ni mchezaji huru tayari basi Flamini alionelea kuwa anaweza kupata “Handsome Package” mahala pengine zaidi ya hiyo. na habari ambazo hazijathibitishwa zinasema Inter Milan wamepania kumchukua mchezaji mwingine Alexander Hleb au hata Fabregas kabisa bado haijajulikana kama atakuwa bado kwa washika bunduki hao kwa msimu ujao ama la!!.

  “I Am Because We Are” Makala ya Filamu ya Madona juu ya umasikini

  BLANTYRE, Malawi – Ni umbali wa maili 100 toka mji mkuu wa Malawi, ndipo kilipo kijiji cha Lipunga, huko hakuna huko hakuna TV wala jumba la sinema kwani hakuna hata umeme,, lakini mwanakijiji Yohane Banda (Mzazi wa mtoto David Band) amesikia kuwa Makala ya Filamu mpya ya sasa ambayo mwanamuziki Madonna inakusudia kuamsha uelewa wa jamii kuhusu suala la umasikini mkubwa unaolikabili eneo hili lililopo kusini mwa jangwa la sahara.

  Pichani Yohana Banda Mzazi wa David Banda akiwa nyumbani kwake

  “I Am Because We Are,” ndio jina la makal ya filamu hiyo ambayo Madona ameitengeneza. Nia ni kuamsha uelewa wa watu kuhusu umasikini wa sehemu ya pili ya dunia, hatufanyi hivi kubeza, la hasha nia yetu ni kuwaonyesha watu kujua maisha halisi ya jamii nyingine na taabu wanazo pata ili kuamsha hari ya kujitolea kusaidia, alisema Madona.

  Kati ya watu waliohudhuria uzinduzi huo walitaka kujua uguu uliopo katika kuchukua mtoto nchini malawi,

  Madona alisema, “si kazi ndogo, inabidi ujitolee, inataka muda kwani ni suala geni kwenye utamaduni wao, halipo ama halijazoeleka”.

  Filamu hii inaonyesha umasikini na maradhi yanavyochangia kugharimu maisha ya watu wa eneo husika. Madona ametaka watu kujitolea kusaidia, yeye alikutana na Banda alipokuwa katika harakati zake za kutoa misaada nchini Malawi.

  Siku JB walipokutana na Koffi kwenye harusi ya Titina Alcapone.

  Ni muda umepita tangu hii itokee lakini Je unamkumbuka Titina Alcapone? huyu aliwahi kuwagombanisha wanamuziki magwiji JB Mpiana wa Wenge BCBG na Koffi Olomide kwa kile Jb alicholalamikiwa Koffi kumchukulia wanamuziki wake akiwamo huyu Titina, kwa kipindi hicho Titina alipokuwa anaoa alimfanya Koffi kuwa Best Man wake lakini alimualika JB Mpiana pia. Kwa sasa Titina anasema ameamua kufanya muziki kivyake zaidi.
  Koffi Olomide akisalimiana na Wageni wengine waalikwa
  Mwanamuziki kiongozi wa Wenge Musica BCBG JB Mpiana akiserebuka na Bi harusi Nene, mke wa Titina Alcapone siku ya harusi yao.
  Meza ya wageni waalikwa anaonekana JB Mpiana, Alain Mpela (aliyevaa kiarabu), Dadé Mpoko, Papito Mbala, Thitsho Lembe
  JB Mpiana na tajiri mtoto PDG Patrick Bolognia, aliyesimama nyuma yao suti nyeusi ni Titina Alcapone. Majina haya wengi wa wapenzi wa Lingala watakuwa wamezoea kuyasikia kwenye kila wimbo na leo kubahatika kuwaona katika picha hizi.

  Lugha kuwabana wahamiaji ila si wachezaji waliopo.

  Mchezaji wa Manchester United mwenye uraia wa Argentina Carlos Tevez akishangilia ushindi baada ya kuwachapa Barcelona katika mechi ya kombe la UEFA Champions League mzunguko wa pili, April 2008. Idara ya uhamiaji ya Uingereza imesema hakuna raia mchezaji ambaye si raia wa European ambaye hawezi kuzungumza “kidhungu” atafukuzwa chini ya sheria mpya ngumu za uhamiaji ambazo zitaanza kutumika mwaka huu ambapo lugha ni suala muhimu.

  Chelsea wamuwania Sergio Ramos

  Mchezaji wa Real Madrid Sergio Ramos akishangilia ushindi baada ya kushinda mechi ya fainali ya ligi ya Spain dhidi ya Osasuna katika uwanja wa Reyno de Navarra stadium, Pamplona, tarehe 4 May. Imesemekana kwamba Chelsea wametoa ofa ya dau nono kwa Real Madrid jumla ya 70 million euros (108 million dollars) kwa ajili ya mchezaji huyu na kama mambo yakienda kama ilivyopangwa basi atahamia kucheza ligi ya UK, kwani Real Madrid wameonyesha kuridhia ofa hiyo. imeripotiwa na gazeti la michezo la El Mundo.

  Tottenham wamtaka Etoo

  Mchezaji machachari wa Barcelona’s Samuel Eto akishangilia wakati wa mchezo wa ligi wao ya Spanish dhidi ya Valencia huko Camp Nou stadium Barcelona, May 4.
  Inasemekana kuwa klabu ya Premier League ya Tottenham iko kwenye maongezi na klabu ya Barcelona kuhusu mchezaji huyu Mcamerun Samuel Etom limeripoti gazeti la michezo la Spain la sports daily Marca. Habari hazijafafanua kwambu ni wapi wamefikia kwenye maongezi hayo ila wanasema maongezi yanakwenda vizuri.

  Schorali kumrith Ericson Manchester City?

  Timu ya Manchester City wamefanya uamuzi wao na kuamua kumpendekeza Luiz Felipe Scolari kuwa kocha wao ajaye.

  Kwa sasa mkataba unafanyiwa kazi kati ya Manchester City na Mwakilishi wa Kocha huyo Mreno Scolari ili aweze kuja Eastlands, Imefahamika kuwa Manchester City watavunja mkataba na kocha wa sasa Sven-Goran Eriksson baada ya msimu huu.

  Thaksin kwa sasa anangojea jibu tu toka kwa Scolari, kama mkataba huo utakwenda kama ilivyopangwa basi kocha huyo ataondoka na donge nono la Paundi £3.2milioni kwa mwaka na mkataba unangoja jibu la mwisho ili upigwe muhuri. kwani kwa sasa kocha huyo yuko busy na kazi ya kuinoa timu Portugal kwa ajili ya Euro 2008.

  Suala la kuondoshwa Ericson lilikuwa gumzo na hata katika mechi ya Manchester City na Chelsea majuzi mashabiki walionyesha kumuunga mkono kocha Ericson lakini ni suala la mmiliki na uongozi.

  Mashabiki wameonyesha kukerwa sana na uamuzi wa klabu yao lakini uongozi umechukua jukumu la kumtangaza Scholari haraka ili kupunguza ghadhabu za mashabiki wao.

  Kombe la Taifa na mfufuko wa soka letu

  Michuano ya Kombe la Taifa imeanza kwa kasi na msisimko wa ajabu huku mikoa yote 23 ikishiriki kwenye kinyang’anyiro hicho, pichani Wachezaji wa Timu ya Manyara kushoto Zawadiel Stephen na Marwa Gabriel wakiwania mpira mshambuliaji wa timu ya Iringa Bunda Oden. Iringa ilishinda 4-1 katika mashindano ya Taifa Cup yanayodhaminia na Safari Lager.

  Kwa kiasi kikubwa watanzania ni watu wanaopenda michezo sana hasa mchezo wa kandanda, itakumbukwa jinsi watanzania walivyojitolea kwa uzalendo mkubwa wakati Timu yetu ya Taifa ilipokuwa ikishiriki katika michuano ya Awali ya African Cup of Nations, kila mtu alionyesha uzalendo na watu wote walikuwa ama wanapeperusha bendeka iwe kwenye magari binafsi, daladala, Teksi, hata magari ya Serikali au ya Umma, iwe vibanda vya Chipsi au mabanda ya Mitumba, watu walinunua Jezi za timu ya Taifa lakini kama kamaida bahati haikiwa yetu.

  Wengi walisema soka letu lingefanya vizuri kama michuano mbali mbali ingefufuliwa mbayo inachangia kupata wachezaji chipukizi kuchangia katika timu kubwa na Timu ya Taifa pia ili kuondoa utegemezi wa wachezaji wengi toka klabu kubwa za Simba na Yanga. Wengi wa wachezaji chipukizi jicho la TFF haliwafikii huko waliko, lakini kwa mpango kama huu wa Kombe la Taifa (TAIFA CUP) ni rahisi kuwaona wachezaji wenye moyo na chama cha makocha wakishirikiana na timu ya Ufundi ya TFF na Kocha mkuu pamoja na Msaidizi wanaweza kupata vijana wazuri kwa ajili ya timu yetu ya Taifa. Hongera Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) na makampuni mengine pamoja na wadau bila kuwaacha TFF kwa kufanikisha hili.

  Tunaimani kuwa kama michuano hiyo ikitumiwa vizuli inaweza kulisha timu kongwe na kuwa chachu ya kupata wachezaji wa Timu ya Taifa.

  Tuesday, May 6, 2008

  JB Mpiana: Tatizo lilo wapi?

  Wapenzi wa muziki wa Kizaire haya tena Video ya JB mpiana iko sokoni, ile video ya albam mpya ya Quel Est Ton Probleme?” Tatizo ni nini au shida iko wapi? na mtindo mpya wa uchezaji unaojulikana kwa jina la Kizubanata.
  Bonyeza Playa upate vitu:-

  Msimamo wa Ligi Primier mpaka sasa.

  Msimamo wa Ligi ni kama ifuatavyo:-

  2007/2008 English Premiership

  Kwa Ujumla
  Nyumbani Ugenini

  GP W D L GS GA W D L GS GA W D L GS GA GD P
  1 Man Utd 37 26 6 5 78 22 17 1 1 47 7 9 5 4 31 15 56 84
  2 Chelsea 37 25 9 3 64 25 12 6 0 35 12 13 3 3 29 13 39 84
  3 Arsenal 37 23 11 3 73 31 14 5 0 37 11 9 6 3 36 20 42 80
  4 Liverpool 37 20 13 4 65 28 12 6 1 43 13 8 7 3 22 15 37 73
  5 Everton 37 18 8 11 52 32 10 4 4 31 16 8 4 7 21 16 20 62
  6 Aston Villa 37 16 11 10 69 49 10 3 6 34 22 6 8 4 35 27 20 59
  7 Blackburn 37 15 13 9 49 44 8 7 4 26 19 7 6 5 23 25 5 58
  8 Portsmouth 37 16 9 12 48 39 7 8 3 24 13 9 1 9 24 26 9 57
  9 Man City 37 15 10 12 44 45 11 4 4 28 20 4 6 8 16 25 -1 55
  10 West Ham 37 13 9 15 40 48 7 6 5 22 22 6 3 10 18 26 -8 48
  11 Tottenham 37 11 13 13 66 59 8 5 5 46 32 3 8 8 20 27 7 46
  12 Newcastle 37 11 10 16 44 62 8 5 6 25 26 3 5 10 19 36 -18 43
  13 Wigan 37 10 10 17 34 49 8 5 5 21 15 2 5 12 13 34 -15 40
  14 Middlesbrough 37 9 12 16 35 52 6 5 7 19 22 3 7 9 16 30 -17 39
  15 Sunderland 37 11 6 20 36 58 9 3 6 23 20 2 3 14 13 38 -22 39
  16 Bolton 37 9 9 19 35 53 7 5 7 23 18 2 4 12 12 35 -18 36
  17 Fulham 37 7 12 18 37 60 5 5 9 22 31 2 7 9 15 29 -23 33
  18 Reading 37 9 6 22 37 66 8 2 9 19 25 1 4 13 18 41 -29 33
  19 Birmingham 37 7 11 19 42 61 5 8 5 26 22 2 3 14 16 39 -19 32
  20 Derby 37 1 8 28 20 85 1 5 12 12 39 0 3 16 8 46 -65 11

  Msimamo wa wafungaji hadi tarehe 5May na idadi ya magoli yao kwa ligi ya FA Primier

  Rank Mchezaji Timu Idadi ya magoli
  1 Cristiano Ronaldo Man Utd 30
  2 Emmanuel Adebayor Arsenal 24
  3 Fernando Torres Liverpool 23
  4 Roque Santa Cruz Blackb