Werasson: Niko tayari kupiga na JB Mpiana Tanzania

Pichani ni Rais wa Kongo RDC Joseph Kabila akiwa na timu ya Wanamuziki akiwemo Marehemu Madilu System alipokutana nao na kuwapatanisha baadhi yao akiwemo JB Mpiana na Werasson mwaka juzi.
MWANAMUZIKI hodari kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Ngiama Makanda ‘Werrason’ amewasili Dar es Salaam na kusema yupo tayari kupiga pamoja na Jean Bedel Mpiana ‘JB Mpiana’ endapo atapatikana promota wa kuwaleta Tanzania kwa ajili ya kutoa burudani kwa Watanzania.Msanii huyo aliwasili juzi jioni akitokea Jamhuri ya Kongo ambapo na kundi la wanamuziki 24, anatarajiwa kutoa burudani kesho kwenye Ukumbi wa Ubungo Plaza kabla ya kupiga Arusha Jumapili kwenye Hoteli ya Naura Springs.

Endapo ‘Werrason’ atapiga pamoja na ‘JB’ Mpiana itakuwa ni historia baada ya nyota hao kuingia katika mzozo mkubwa ulioibua vita kati yao.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Makanda alisema atafurahi kupiga pamoja na Mpiana ambaye inadaiwa ni wapinzani na chanzo cha kuvunjika kwa kundi maarufu la Wenge BCBG lililowahi kutamba Afrika.

“Sina matatizo na Mpiana ni rafiki yangu napenda siku moja nije naye hapa tufanye onesho la pamoja nipo tayari hata sasa cha msingi apatikane promota mwenye uwezo nitamwambia lakini naomba nipate uhakika kama mnatuhitaji kabla ya mwaka huu kumalizika,” alisema Makanda.

Makanda alisema anapenda kuona muziki wa Tanzania unapiga hatua kama ilivyo Jamhuri ya Kongo na kuongeza kuwa endapo atapata fursa ya kuzungumza nao atawashawishi watengeneze albamu ya pamoja.

Msanii huyo alisema alishindwa kutoa burudani mwaka jana kutokana na sababu zilizokuwa nje ya uwezo wake na alitumia nafasi hiyo kuwaomba radhi Watanzania kutokana na tukio hilo.

Alisema amejiandaa kuacha historia kwa kupiga nyimbo zake mfululizo ili kukata kiu ya mashabiki wa burudani ambao walikuwa na shauku kubwa ya kumuona nyota huyo akiwa jukwaani katika ardhi ya Tanzania.

Ziara ya mwanamuziki huyo imedhaminiwa na Kampuni ya Sigara Tanzania (TCC) kupitia chapa yake ya Embassy kwa kushirikiana na Club E.

Advertisements

2 Responses to Werasson: Niko tayari kupiga na JB Mpiana Tanzania

  1. Peter paa MUKULU says:

    ….wakuu mwenye update ya Bibliciya

  2. is good this work It my gracia your my friend byebye

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: