Koffi akiteta na “Jongwe”.

March 19, 2014

President Mugabe chats with Congolese musician Koffi Olomide after their arrival at Harare International Airport from DRC on Wednesday. The rhumba musician will perform at Bona’s wedding to Simba Chikore tomorrow. — (Picture By Presidential Photographer Joseph Nyadzayo

Mwanamuziki Koffi Olomide akiteta jambo na Mheshimiwa Robert Mugabe walipokuwa Harare International Airport tayari kwa harusi ya binti wa Mugabe Bona (24) ambaye ameolewa na kijana Pilot Simbarashe Chikore. Koffi alikuwa mburudishaji kwenye sherehe hiyo iliyofanyika hivi karibuni. Koffi alishutumiwa na mashabiki kwa kuwa hicho kilikuwa kipindi cha msiba wa nguli King Kester Emeneya shutuma ambazo alizijibu aliporejea DRC.


“Wasafi Classic” Show ya Jb Mpiana kama kawa

March 19, 2014

Tour Eiffel ya Wenge BCBG utunzi wake Titina Alcapolne

March 18, 2014

Nilipotea kidogo jamvini kutokana na majukumu ya kitaifa, mambo ni mengi lakini kuanzia wiki hii tutakuwa pamoja na mambo yataenda kama awali. Nilipokuwa Katavi nilikutana na mdau wangu mmoja nilifarijika sana alipojitambulisha na kuniambia kuwa nai mdau mkubwa sana wa Blog yetu na ni shabiki mkubwa wa JB Mpiana na anaipenda sana aliniomba niseme chochote kuhusu wimbo huu na Mpella.

Moja kati y wanamuziki wa Wenge ya JB Mpiana ambao waliondoka na bado nawalilia Allain Mpela, Huyu bwana alikuwa anauwezo mkubwa si tu wa kutunga bali alikuwa anakarabati Verse, yaani wimbo ukitungwa wakisikilizishana yeye huwa anazirekebisha na akirekebisha na kuzitengenezea mtiririko wa sauti hakuna anayepinga na moja ya albamu ambazo alishiriki kwa kiasi kikubwa kuiratibu ni hii ya Titanic (Titanike) ambayo waliitoa baada ya kuparaganyika na akina Werason na wao kuunda WMMM.

Japokuwa wimbo huuu ulitungwa na mpiga drums maarufu Titina Alcapone ukisikiliza beti ya Allain Mpella Afande utakubaliana na mimi kuwa alikuwa jembe, msikilize kuanzia 3:20 kisha unipe maoni yako.

Mwingine ambaye kwa sasa mepotezwa kabisa na hajawahi kuwika tangu atoke kundini ni Aimelia Lyase Doming’ong’o ambaye kwa kiasi kikubwa JB Mwenyewe ameweza kuziba pengo lake kwa kuimba sauti yake ingawa ya Aimelia ni kali na nyembamba zaidi lakini pengo lake haijaonekana sana.

Wimbo huu ni kwenu Jay Single Suvereigh Mukullu, Papaa Mabamba Maregesi pamoko sana mkuu (Full Mzaire), Papaa Julie We Ston Presidaa Bana Kongolee na Darisalama, Papaa Sultan ndani ya jiji la Dar, Engineer Mboneka Mwana BCBG, Juma Mukulu nakati ya Airport, Hadji Le BeeCeeBeeGeeque Nambari wani, Mapenzi Club tuko pamoja, Muzee ya Tunduma sina haja ya kukutaja, Papaa na kati ya Muscat unajijua, Wenge BCBG Arusha Club pamoja sana.


WERRASON, KOFFI OLOMIDE, JB MPIANA, ROGA ROGA, ALAIN MPELA na EVOLOKO Wakimuomboleza KESTER EMENEYA

March 18, 2014

King Kester Emeneya ni mmoja wa wanamuziki mwenye heshima zake huko Kongo na atakumbukwa daima kwa umahiri wa utunzi wake akiwa na nyimbo zaidi ya 1000 mpaka anafariki dunia, Sikia hapo wanamuziki  WERRASON, KOFFI OLOMIDE, JB MPIANA, ROGA ROGA ALAIN MPELA Afande na  EVOLOKO, Pia wamo Tshalla Muana, Blaise Bulla na wengineo wengi wakiwa studio kupika kibao rasmi kwa maombolezi.


BREAKING NEWS: King Kester Emeneya afariki dunia

February 13, 2014
Wimbo Zinzi wake King Kester Emeneya

Habari zilizotufikia punde zinasema kuwa mwanamuziki King Kester Emeneya amefariki dunia. Habari zilizopatikana kutoka kwenye chanzo cha habari zinasema kuwa Emeneya amefariki leo huko Ufaransa alipokuwa akiishi na familia yake bila kueleza kwa undani chanzoo cha kifo hicho.

 Jean Emeneya Mubiala Kwamambu alizaliwa November 23, 1956 huko Kikwit Bandundu, amefariki leo February 13 2014 huko Paris, Ufaransa.  

Emeneya alizaliwa huko Kikwit nchini Congo alikulia huko na alijiunga na bendi ya Viva la Musica mwaka 1977 akiwa mwanafunzi wa   political science katika chuo kikuu cha Lubumbashi. Katika miaka ya 80 mwanamuziki Emeneya alikuwa ni miongoni mwa wanamuziki maarufu wa Africa na mnamo December 24 1982 aliamua kuanzisha bendi yake ya Victoria Eleyson.

Emeneya Djo Kester alikuwa ni mbunifu na ni mwanamuziki wa kwanza toka Africa ya kati  (central African musician) kuchanganganya muziki wake na ala za ki electronic (synthesizers) katika albamu yake iliyotamba ya Nzinzi ambayo iliuza zaidi ya kopi Milioni moja. Baada ya mafanikio hayo Emeneya hakuishia hapo kwani mwaka 1993 alitoa albamu yake iliyoitwa kwa kiingereza “Every Body” ambayo ilisambazwa na kampuni maarufu ya Sonodisc, Albamu hii ilifanya vizuri sana ndani na nje ya nchi ya Congo DRC na mwaka 1997 baada ya kimya cha takribani miaka 7, King Kester aliamua kurejea Congo. Inakadiriwa watu karibu 80,000 walihudhuria onyesho lake la kwanza aliporejea DRC, rekodi ambayo haijavunjwa kulingana na media za Congo.

Ama kwa hakika  Emeneya ni mmoja ya wanamuziki nguli walio na mafanikio ambao Afrika kwa ujumla imewahi kuwa nao. Tangu mwaka 1991 marehemu Emeneya alikuwa akiishi Ufaransa na familia yake, mpaka kifo kinamkuta Emeneya alikuwa na nyimbo zaidi ya 1000 elfu moja na ameshatumbuiza kwenye maonyesho makubwa kwenye mabara yote matano.  Huyu ni mwanamuziki wa tatu CONGO inampoteza kwa mwaka jana na mwaka huu.

Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi.


HISTORIA YA MWANAMUZIKI FERRÉ GOLA. SEHEMU YA TATU

January 30, 2014

Baada ya kuangalia sehemu ya kwanza jinsi Ferre Gola alivyoingia Wenge Musica akiwa ni mwanamuziki wa mwisho kuwa recruited kabla ya bendi hiyo kuvunjika na pia sehemu ya pili kuangalia maisha yake ndani ya BCBG mpaka alipoamua kutoka kivyake na kuanzisha bendi yake…. Leo ni sehemu ya Tatu kama inavyoletwa kweu na msimulizi wako mahiri Lubonji wa Lubonji.

Mwanamuziki Ferre Gola akiteta jambo na mke wa mfanyabiashara maarufu Macheni hii ilikuwa alipokuja nchini kutoa burudani.

FERRE GOLA na Group Les Marquis de maison Mère, wakafaanikiwa kutoa Album yao MIRACLE, Utazikuta nyimbo Amour ya Intérêt na 100 kilos utunzi wa FERRE GOLA,
Ecole utunzi wa JUS D’ÉTÉ MULOPWE, TRAHISON wa BILL CLINTON KALONDJI.
ALBUM MIRACLE ilipokelewa vizuri sana, mashabiki, wapenzi wa muziki pia wajuzi wa maswala ya muziki wakawaweka kwenye nafasi ya kwanza kabisa kwa wanamuziki wa kizazi kipya huko CONGO (5th generation).
Ingawa mambo yao yawaendea vizuri kutokana na SHOO zao kujaa watu wengi, kushangiliwa kwa nguvu, na pia kupata mashabiki wengi, kadhalika Album yao kupokelewa vilivyo, Baadhi ya wandishi wa Habari wakasema:” VIJANA HAWA WANAVIPAJI VYA HALI YA JUU, WANAWEZA KUSONGA MBELE KABISA, ILA WANATATIZO MMOJA KUBWA SANA, NALO NIKUTOKUWA NA LEADER KATI YAO. NA NDILO LILILO WAPONZA.”

MGAWANYIKO WA GROUP LES MARQUIS DE MAISON MÈRE

Hali yakutoelewana ikazidi kukua,mikokotano huku na huku, kila Mmoja kajidai ndie yu LEADER, wengine wajidai ndio wakali kuzidi wengine ,mizozo ya hapa na pale ikazidi kujitokeza.
Hali hiyo ya Utata ikaleta chuki na dharau, ndipo mgawanyiko ukatokea.
FERRE GOLA na BILL CLINTON wakawa pande mmoja, huku JUS D’ÉTÉ MULOPWE na salio la Group pande zao.
FERRE GOLA na BILL CLINTON wakachukua uamuzi wa kurudi mjini KINSHASA kujifiriria na kupata ushauri ili wajiendeleze kimuziki, Kwa upande wake JUS D’ÉTÉ kaamua kubaki PARIS na kujichukulia kama kiongozi pekee wa Group LES MARQUIS DE MAISON MÈRE.

MJINI KINSHASA MAELEWANO KATI YA BILL CLINTON NA FERRE GOLA YAKATOWEKA.
Wa kwanza kuchukua ndege na kurudi KINSHASA alika BILL CLINTON, katua kwenye uwanja wa ndege wa NDJILI tarehe 15 February 2005, siku nne baadae yaani tarehe 19 February 2005 FERRE GOLA naye katua MJINI KINSHASA. Huku Mashabiki wakisubiria kuwaona pamoja kwenye Press conference, FERRE GOLA kapata tetesi ya kwamba BILL CLINTON hatokuja kushirikiana naye kwenye Press conference ,na tayari ameshakua na kundi lake na kalipa jina la ” LES MARQUIS SAMOURAÏS”. FERRE GOLA kwa upande wake, kalizimika kuunda kwa haraka kundi lake kalipa jina la “ MARQUIS DES BEAUX – GARÇONS “.

MKONGWE KOFFI OLOMIDE KAINGIA UWANJANI :
KOFFI OLOMIDE LE GRAND MOPAO kamtaka kwa hali na mali FERRE GOLA ili ajiunge na Group lake la QUARTIER LATIN. Kafanya juu chini kwa kuwarubuni ndugu wa karibu wa FERRE GOLA ili wamshawishi ajiunge naye,na hajafaanikiwa. Basi ikabidi amtafute Jamaa wa karibu sana na FERRE GOLA ambae FERRE GOLA hua kampa heshima zote, Jamaa anaishi barani Ulaya, Jina lake JÉRÔME MONTIGIA, huyu ndie kafaanikisha ujio au uhamisho wa FERRE GOLA kujiunga na Group QUARTIER LATIN ya MOPAO MOKONZI. Ndipo FERRE GOLA kafanyiwa mkataba maalum, na baadhi ya vipengele vya mkataba huo ni kwamba FERRE GOLA atapeya DOLA elfu 15000, na mkataba ni waku renew kila baada ya mwaka mmoja, kwa makubaliano ya pande zote mbili.

KOFFI AMKABIDHI FERRE 15,000 USD

Kitendo cha KOFFI OLOMIDE kumkabidhi FERRE GOLA kitita cha DOLA elfu 15000, kilileta gumzo kubwa hasa kwenye vyombo vya habari, kwa sababu ni jambo ambalo halijawahi kutokea. Ndipo walivyo weka kwenye vichwa vya habari (LE TRANSFERT LE PLUS CHER (THE MOST EXPENSIVE TRANSFER ).

WAPAMBE WA WERRASON WAJA JUU :
Kitendo alicho kifanya KOFFI OLOMIDE kumchukua FERRE GOLA,kiliwaudhi saana wapambe,wapenzi na watu wa karibu wa WERRASON. Kwa madai yao, wanasema ya kwamba, KOFFI OLOMIDE ndie aliye washawishi kina FERRE GOLA, BILL CLINTON, JUS D’ÉTÉ, SERGE MABIALA, JAPONAIS na kadhalika watoroke na waunde Group LES MARQUIS DE MAISON MÈRE. Nia yake halisi ni kumdhuru na kumuathiri WERRASON aumie na aanguke kimuziki, kwa hali hiyo hatokua na mpinzani.

MJINI PARIS, Waliandamana hadi kwenda kwenye nyumba ya KOFFI OLOMIDE huku wakitoa matusi makali dhidi yake. kwa bahati nzuri hapaja tokea madhara yeyote.
Kwa upande wake KOFFI OLOMIDE kajitetea kwa kusema hana jambo lolote na WERRASON ambae kamchukulia kama Ndugu, na wala hajamchukua FERRE GOLA kutoka kwa WERRASON bali kwenye Group LES MARQUIS DE MAISON MÈRE.

AJIRA YA FERRE GOLA KWA KOFFI OLOMIDE MOPAO MOKONZI
mwishoni mwa mwaka 2005, FERRE GOLA kajumuika na KOFFI OLOMIDE na kundi lake kwenye SHOO nyingi Mjini KINSHASA, ULAYA, na sehemu mbalimbali ulimwenguni. FERRE GOLA akiungana na Group QUARTIER LATIN, wakaingia STUDIO na kutoa SINGLE ” BOMA NGAI NA ELENGI ” (BONA NGA N’ELENGI). Uhondo na utamu utaupata utakapo sikiliza marudio ya wimbo “SISI SILIVI” usikilize hapo chini.
Baada ya hapo, FERRE GOLA katia kwenye ALBUM DANGER DE MORT wimbo wake maarufu INSECTICIDE.

 

MZOZO WAJITOKEZA KATI YA FERRE GOLA NA KOFFI OLOMIDE
Tukiwa tayari Mwaka 2006, maelewano kati ya FERRE GOLA na tajiri wake KOFFI OLOMIDE yakawa sio mazuri. FERRE GOLA akawa anagoma kufika mazoezini, hadi kufikia kutotokea kabisa kwenye SHOO zilizo fanywa kwenye ukumbi wa BATACLAN na ELYSÉE MONTMARTRE MJINI PARIS.
Kitendo hicho hakijamfurahisha KOFFI OLOMIDE, akawatuma wajumbe wamshauri kijana ili apate kujirekebesha na aendelee na muziki.
Tarehe 07 AUGUST 2006, KOFFI OLOMIDE na kundi lake walikua MJINI BRUSSELS (BRUXELLES) kwa ajili ya SHOO kwenye ukumbi wa MARIGNAN, huko pia FERRE GOLA hajaonekana huku akitoa sababu ya kwamba anaumwa. Sawa sababu inaeleweka, ila kwa mshangao Mkubwa kesho yake kaonekana kwenye sehemu maarufu MJINI BRUSSELS inayoitwa ATOMIUM akiimba kwenye KERMESSE iliyo andaliwa na wa KONGOMANI waishio hapo.

Subira za KOFFI OLOMIDE ziliisha, ndipo kamtafuta jamaa JÉRÔME MUTINGIA, alie faanikisha ujio wa FERRE GOLA QUARTIER LANTIN ili aingilie kati kwa kumshawishi FERRE GOLA atekeleze mkataba walio saini kati yao.
KWA NINI FERRE GOLA KASUSA KUFANYA MAZOEZI ? ITAENDELEA…

 


Koffi akanusha kumhujumu Mpiana onyesho la Zenith

January 28, 2014

Mwanamuziki Koffi Olomide ambaye kwa siku za karibuni urafiki wake na JB Mpiana uliwashangaza watu kadri ulivyokolea, amekanusha kuhusika na hujuma ya kufutwa kwa onyesho la JB Mpiana ambalo lilipangwa kufanyika Zenith mwaka jana.

Koffi aliyasema hayo alipozungumza na waandishi wa habari mara baada ya kusaini mkataba wa kufanya show mboli mjini Brazavile mwisho wa mwezi huu na mwanzoni mwa mwezi ujao. Koffi amesema anasikitishwa na habari zinazovumishwa kuwa ameshiriki katika kuwachochea “wanazi” wa JB wafanye fujo kupinga show hiyo isifanyike “Hizo ni habari za uvumi na zinafaa kupuuzwa na wapenzi wa muziki wetu, sina sababu ya kufanya hivyo kwa sababu sifaidiki na chochote kwani mimi nina mashabiki wangu na yeye ana wakwake” alisema Koffi akionyeshwa kukerwa na swali hilo. Koffi aliripotiwa na vyombo vya habari kuwa amekuwa na ukaribu na JB Mpiana siku za karibuni jambo ambalo liliwashangaza watu.

Koffi atafanya onyesho lakwanza la VIP January 31 katika ukumbi wa Olympic Palace huko Brazaville ya Congo na siku ya tarehe 1 Feb atafanya onyesho jingine la wazi akiwa na Honorable Cindy le Cœur na bendi nzima ya Quartier Latin International pia atamtambulisha muimbaji mpya ambaye ameshiriki pia kwenye albamu mpya ya kundi hilo ya 13 ème apôtre


Follow

Get every new post delivered to your Inbox.

Join 94 other followers

%d bloggers like this: