Kama una maoni yeyote unaweza kuandika hapa na tutajitahidi kadri ya uwezo wetu kuyafanyia kazi.
Maoni yawe yakujenga na tutumie lugha ambayo haitomkwaza mwingine.
Pius – Mhariri
Kama una maoni yeyote unaweza kuandika hapa na tutajitahidi kadri ya uwezo wetu kuyafanyia kazi.
Maoni yawe yakujenga na tutumie lugha ambayo haitomkwaza mwingine.
Pius – Mhariri

piusmicky@yahoo.co.uk
Mob: +60176452510
Ken Damansara Condo
SS 2/72 - Darul Ehsan
47400 Selangor
Petalling Jaya
Kuala Lumpur - Malaysia






Theme Contempt by Vault9.
Blog at WordPress.com.
August 16, 2008 at 11:44 am |
kaka huwa unatuwambia tubonyeze prea.harafu hatuoni kitu vip. unatunyima huondo kaka.turetee prea kweri nihayo tu. mimi.mudy toka lstamburi.turuky
August 16, 2008 at 12:45 pm |
Pole sana mkuu lakini ina cheza kwa wengine kunweza kuwa ni sababu ya Vitu viwili.
1. Labda hauna Flash Player kwenye MAchine yako au unahitajika ku update.
2. Kama unatumia Kaspersky Anti virus basi huwa inakataa kuruhusu player ya Google au Youtube, cha kufanya ni kuiruhusi Google na Youtube au ku Pause au Stop ile Kasper kila ukitaka kucheza Google Movie au Youtube Movie.
August 19, 2008 at 3:22 pm |
kaka mimi nishabiki wko nanimpezi wa webu yako toka lreyazamani mpaka hii ya sasa hivi rakini kira hukireta prea sizipati mbona zingine nazipata kama za haki ngoi,bongo5,bongo serebret, lstiafrikayoutbe.nk.yako tu ndio lnakataa.hatapicha sikunzingine huweki tunaona maandishi tuu. turekebishie kaka prea zako. tuzipate. nimimi mdogo wako kutoka lstamburi turuky
August 28, 2008 at 11:48 am |
kaka video ya aminata hakuna wara prea zako sisi huku hatuzioni umeacha sehemu wazi tu. mbona prea zingine tunaziona kama vire ya bongoserebureti.hakingoi.bongo5.nk.yako tu.ndio lnamatatizo.au wewe unatumia prea gani?nimimi mdogowako pamoja na wadau wezangu kutoka lstamburi turkye
August 28, 2008 at 2:23 pm |
Kaka naomba u download hii flash player labda itasaidia
http://www.adobe.com/shockwave/download/download.cgi?P1_Prod_Version=ShockwaveFlash
Pius
September 1, 2008 at 4:24 am |
Mkuu ulianza kwa kutupa habari za BBA imekuwaje tena?
Tulikuwa tunapenda uchambuzi wako wengine hatupati wasaa wa kuona na kutembelea vyombo mbalimbali tunapenda kupata kila kitu kwa wakati mmoja hata weka mara 2 tu kwa wiki ili useme itakuwa lini na lini.
Ni hayo tuu vingenevyo kazi nzuri sana kuanzia muonekano hadi content.
Umekuja kwa kasi na umekubalika.
Ndise Mkanjala.
Indiana Polis
September 2, 2008 at 2:48 am |
Naungana na Ndise jamani tujulisheni basi walau mara mbili kwa wiki yatosha jamani au hata fanya kila ijumaa tuu una compile ya wiki nzima.
Sameer UAE
September 7, 2008 at 2:13 pm |
kaka bora uturudishe kwenye blog yetu ya zamani sasa hivi ndio imezidi hata picha hatuoni umeziweka eksi.kama prea.tunaona maadishi tu.yureyure mdau wako.wa lstamburi
September 10, 2008 at 7:06 am |
Kaka kuna msomaji alijaribu kukusahihisha kuhusu post ya “SERENA APOTEZA US OPEN”, Imekuwaje mbona ndo umeitoa kabisa….mkweli ni yeye au wewe na taarifa yako kuwa kapoteza US OPEN?
September 11, 2008 at 1:46 am |
Ndugu Colibry Salaam!
Nashukuru kwa kuniandikia na zaidi kwa kunitembelea,
Kimsingi nilipaswa kuomba msahama kwa Post ile kwani niliupdate Blog kupitia Simu yangu na matokeo yalikuwa sio ya mwisho, ilikuwa ni ile set ambayo Serena alipoteza.
Samahani mdau kwa kosa lile la kiufundi na wengine wote ambao walikwazwa na kosa lile.
September 17, 2008 at 10:07 am |
nahitaji kuchati na wewe personal kama hutojali
vipi uko tayari
September 17, 2008 at 10:45 am |
piusmicky@yahoo.co.uk au text me at +60176452510 haiko noma mkuu!
October 7, 2008 at 10:25 am |
kaka mbona utupi matokeo yaligi ya tz asa kwasisi tuliombali na nyumbani.pamoja na matukio asa yanga na simba.pamoja namsimamo wote waligi unavyo enda.nani anaongoza ligi.kwaniaba ya wa bongo tulio uturkey tuna omba kuwakilisha
November 27, 2008 at 1:01 pm |
kaka wewe huwa unatumia prea gani ebu tufahanishe ili tupate hizi video zako na sisi uliniambia nidarodi prea uliyı nitumia nimefanya hivyo kama ulivyo niambia lakini haichezi hata kidogo kwanza mimi hata prea sisioni tunaona patupu tu chini ndio tunaona mandishi tu kuwa boyeza hapo kusikiliza kwakifupi hatuoni kitu zidi ya wewe umecha nafasi tu nihayo tu 1UNATUMİA PREA GANİ?
December 17, 2008 at 5:24 pm |
nataka kukutumia picha za miss burundi lakini sioni email yako
December 18, 2008 at 10:42 am |
tuma kwa piusmicky@yahoo.co.uk
Nitashukuru sana
January 11, 2009 at 5:54 am |
Mdam naomba msaada kwenye tuta kidogo wa kunitangazia hii blog yangu ya michezo.
http://worldspoti.blogspot.com
Shukran
January 15, 2009 at 2:01 pm |
Aisee tuwasiliane niko hapa Japan , Nataka kuja huko Kutembea
Simu Yako Nilipoteza , tumia hiyo Mail Nitumie simu Yako
Sonda Shukran Robert
January 23, 2009 at 1:28 pm |
KAKA HII IPO SAWA KWELI?
TUNAPOKWENDA SIO KAMA KWELI HII NI KAQULI YA MH.PINDA
MDAU THESSALONIKI,UGIRIKI)
Kutoka mtandao wa gazeti la Mwananchi)
Date::1/23/2009
Pinda ataka jino kwa jino
Na Victor Kinambile, Tabora
KATIKA hali ya isiyo ya kawaida, Waziri Mkuu Mizengo Pinda jana aliwaambia wananchi kuwa wanaoua watu wenye ulemavu wa ngozi (albino) pamoja vikongwe ni hawana budi kuuawa kwa kuwa wakisubiri mahakama kuwahukumu, watakuwa wanakosea.
Waziri Pinda, ambaye ameanza ziara katika mikoa ya Kanda ya Ziwa yenye lengo la kuhamasisha vita dhidi ya mauaji ya vikongwe na albino, aliutaka Umoja wa Vijana wa CCM kuongoza vita hiyo, akisema lina jeshi zuri.
Mauaji ya albino yamekuwa ni tatizo kubwa nchini na hasa katika mikoa ya Kanda ya Ziwa.
Pamoja na serikali kutangaza hatua kadhaa za kupambana na wauaji hao, bado matukio ya kuuawa kwa watu hao wenye ulemavu wa ngozi yamekuwa yakiendelea kuripotiwa, lakini Waziri Pinda ameenda mbali zaidi katika kukabiliana na tatizo hilo alipotaka wauaji hao wauawe badala ya kufikishwa mbele ya vyombo vya sheria.
Kauli ya Pinda, ambayo inaweka maswali katika suala la utawala bora, imekuja wakati ambao wananchi wamekuwa wakijichukulia sheria mkononi na kuua vikongwe kutokana na imani za uchawi.
Akihutubia wakati wa kufungua mkutano wa 16 wa Shirikisho la Vyama vya Kuweka na Kukopa (SCCULT) kwenye ukumbi wa Chuo cha Utumishi Umma mkoani hapa, Waziri Pinda alisema iwapo wananchi wataendelea kuwahurumia wauaji hao ambao wanatafuta viungo vya albino wakitegemea mahakama itatenda haki huku nao wakiongeza kasi ya mauaji kwa Watanzania, watakuwa wanakosea.
Hivyo alisema kwamba kuanzia sasa mtu yeyote atakayemuona mtu amemkata shingo au mkono mweziwe basi naye auawe papo hapo hii itakuwa ndiyo dawa kwani vingozi wote tumechoka na mauji hayo.
“Mkimuona mtu akamkata mwingine shingo naye muueni kwani sasa viongozi wote tumechoka… no more, I can’t tolerate anymore (imetosha, siwezi kuvumilia tena),” alisema Pinda huku akiwaacha watu midomo wazi.
Aliviomba vyama vya siasa kushirikiana na wananchi kuhakikisha suala hili la mauji linakwisha kwani wauji “tunaishi nao na ni rahisi kulimaliza iwapo tutakuwa kitu kimoja katika kuondoa kashifa hii ambayo imekuwa mbaya kwa nchi yetu”.
Aliuagiza Umoja wa Vijana wa CCM kuhakikisha mauaji hayo yanatokomezwa kabisa, akisema kuwa ni jeshi zuri ambalo likiamua kutokomeza kabisa mauaji ya vikongwe na ndugu zetu maalbino inawezekana.
“Umoja wa vijana mna jeshi zuri ambalo naamini mkiamua mnaweza kutokomeza mauaji ya wazee wetu pmoja na ndugu zetu maalbno na kazi hiyo nawaagiza muanze leo msisubri auawe mwingine tena,” alisema waziri mkuu.
Baada ya kumalizika kwa mkutano huo, baadhi ya watu wanaoonekana kuwa ni wa “serikali” waliwafuata baadhi ya waandishi wa habari, akisihi suala hilo lisiripotiwe magazetini kwa madai kuwa kauli hiyo ya Waziri Pinda inaweza kusababisha matatizo.
Rais Jakaya Kikwete, ambaye pia amekuwa mstari wa mbele kupiga vita mauaji hayo, alitofautiana na Waziri Pinda katika moja ya hotuba zake aliposema kuwa adhabu ya kuua haitofautishi muuaji wa albino na muuaji mwingine na kwamba watakaopatikana na hatia ya kuua albino, atakabiliana na adhabu ya kifo kama ilivyo kwa muuaji mwingine.
Waziri Pinda alionekana kukerwa na mauaji ya albino wakati alipopata taarifa kwamba kuna mama mwingine aliuawa usiku wa kuamkia juzi.
“Nimeambiwa kuwa juzi wilayani Sengerema kuna mama mmoja ambaye ni mlemavu wa ngozi amekatwa mkono na wauaji wakaondoka na mkono huo na tayari mama huyo amekufa,” alisema Pinda na kusisitiza kushughulikia wauaji hao.
Akitoa takwimu za mauaji ya vikongwe na malbino alisema mwaka 2003 waliuwawa vikongwe 517, mwaka 2004 waliuawa vikongwe 444, mwaka 2005 (494), 2006 (vikongwe 386), mwaka 2007 (vikongwe 526) na albino sita na mwaka 2008 (vikongwe 526 na albino 28).
Alisema tayari mwaka huu wameuawa albino watatu hivyo kufanya albino na vikongwe waliouawa kufikia kuwa jumla 2,900.
Waziri mkuu ameanza ziara ya siku nne kutembelea mikoa ya Shinyanga, Tabora na Mwanza ili kuhamasisha wananchi watokomeze vitendo vya mauaji ya vikongwe na watu weye ulemavu wa ngozi.
Tuma maoni kwa Mhariri
January 27, 2009 at 6:28 pm |
kaka ulituweka shindano la kumtafuta mchezaji bola kiafrica natukapiga kura zetu vipi matokeo yake nan, kashinda au bado bbc hawajatoa matokeo naomba kuwakilisha
February 20, 2009 at 9:38 pm |
PAPA nimekutana na hii mtandao wa NIFAHAMISHE nngependa kuchangia na wadau……
jinsi nilivyokipokea kifo cha Jose Maina ‘Mbunge wa Mkuzi’
Marehemu Jose Maina, ‘Mbunge wa Mkuzi’ Friday, February 20, 2009 9:00 PM
‘Ghafla namsikia Maina akitupa mashairi yenye maneno mazito ‘Lakini kumbuka Ndugu Sama, using’ang’anie mtu asiyekupenda, iliyobaki, oa mwingine’Wakati Maina anaimba mashairi hayo, Moshi William anamchagiza kwa kumuita Jose Maina, Mbunge wa Mkuzi’
NI saa sita mchana niko ofisini mara simu yangu ya mkononi inaita na ninapoiangalia nakutana na jina la Hassan Moshi.
“Vipi baba” Hasani ananisalimia mara baada ya mimi kupokea simu.
“Salama sijui wewe” nami namjibu.
“Mimi Salama. Vipi umepata habari za Maina?” ananiuliza.
“Hapana, kwani vipi?” namjibu na kumuuliza.
“Maina amefariki leo asubuhi”.
“Amekufa?” namuuliza
“Ndiyo, amekufa ghafla kwenye daladala maeneo ya Temeke Mikoroshini wakati akiwa anaelekea studio. Leo tulikuwa tunakwenda kurekodi” alizungumza Hassan na kukata simu.
Wakati Maina anakutwa na umauti, wanamuziki wenzake walikuwa wanamsubiri studio ili akaingize sauti katika nyimbo mbili kati ya sita za albamu yao mpya.
Nyimbo hizo ni Kimya Kingi uliotungwa na Papa Upanga na Nyumba ya Urithi uliotungwa na mpiga rhythim wa bendi hiyo, Uluka Uvuruge. Nyimbo ambazo tayari zilisharekodiwa ni Mama Cossy uliotungwa na Maina, Suzana (Mabela), Kiapo (Hussein Jumbe) na Cheo ni Dhamana (Eddo Sanga)
Taarifa hiyo inanishtua na haraka haraka nawapasha habari wafanyakazi wenzangu, Mawazo Lusonzo, Jimmy Chika na Said Mmanga ambao pia ni wadau wakubwa wa muziki wa Kitanzania.
Wakati mjadala unaanza ofisini juu ya kifo cha Maina, mimi najikuta mawazo yangu yakihama pale ofisini na kuelekea moja kwa moja kwenye ukumbi wa Amana uliopo Ilala Dar es Salaam ambako bendi ya Msondo Ngoma iliutumia kama ukumbi wake wa nyumbani na kutumbuiza kila siku ya jumapili.
Kwa sasa bendi hiyo inautumia ukumbi wa Afri Centre uliopo maeneo ya Mchikichini, jijini Dar es Salaam.
Nakumbuka miaka mingi nyuma siku za jumapili, nikiwa nimekaa upande wa kushoto wa stejini ya ukumbi huo nikiwa na wadau mbalimbali wa muziki baadhi yao wakiwa wanahabari wenzangu ambao ni wakereketwa wa bendi ya Msondo Ngoma tangu ilipokuwa inamilikiwa na Jumuia ya Wafanyakazi nchini (JUWATA) na hata pale ilipoanza kumilikiwa na wanamuziki wenyewe.
Namuona Angetile Osiah, Masoud Masoud, Muhidin Issa Michuzi na mwanadada Suzy ambao wote ni wana habari, wapo pia makocha SyllerSaid Mzirai na Jamhuri Kihwelo kila mmoja wetu akiwa kama yuko dunia nyingine, kutokana na kunogewa na muziki mzito unaoporomoshwa na bendi hiyo kongwe.
Ghafla wote tunapagawa zaidi pale mpiga solo mahiri wa bendi hiyo, Abdu Ridhiwani Pangamawe, anaposhuka jukwaani na kuja kati kati yetu na kuanza kucharaza gita lake kwa umahiri wa hali ya juu, huku akituchezesha.
Macho yangu yanatoka pale tulipo, na kuangalia karibu na mlango wa kuingilia, pamoja na ukumbi kufurika, lakini namuona Boniface Wambura ambaye mara nyingi ulikuwa huhitaji kuhaha kumtafuta kutokana na urefu wake pamoja na tabia yake ya kupenda kusimama kipindi chote cha shoo. We angalia tu ukiona mtu mrefu kuliko wote ujue ni yeye.
Namuona Wambura akiwa mwenye tabasamu lenye kila aina ya furaha, huku macho yake akiwa ameyaelekeza jukwaani.
Haraka haraka nayarudisha macho yangu jukwaani, na naiona safu ya mbele ya uimbaji ya Msondo Ngoma, ikiwa imepambwa na mijibaba mitano iliyojaa vyema jukwaani. Namuona Othumani Momba, Suleimani Mbwembwe, Tx Moshi William, Joseph Maina na Muhidin Maalimu Gurumo.
Safu hiyo kwa pamoja, inalishambulia jukwaa vilivyo kwa sauti zao tamu na zilizopangiliwa vyema katika kila nyimbo wanayopiga, huku wakichagizwa vilivyo na wapiga ala, Said Mabela, Pangamawe, Zahoro Bangwe, na Uluka Uvuruge ‘Smart Boy’.
Ghafla namsikia Maina akitupa mashairi yenye maneno mazito “Lakini kumbuka Ndugu Sama, using’ang’anie mtu asiyekupenda, iliyobaki, oa mwingine”.
Wakati Maina anaimba mashairi hayo, Moshi William anamchagiza kwa kumuita “Jose Maina, Mbunge wa Mkuzi”.
Tx Moshi alikuwa anapenda kumtania Maina kwa kumuita Mbunge wa Mkuzi, akiwa na maana kuwa mwanamuziki huyo alikuwa anawawakilisha vyema wakazi wa Mkuzi Wilayani Korogwe mkoani Tanga katika medani ya muziki. Kwa hiyo alikuwa ni sawa na Mbunge wa Mkuzi kama kungewepo na bunge la wanamuziki.
Maneno hayo yanapopenya masikioni mwangu yananikumbusha uchungu mkubwa, kwani leo hii nayakumbuka, kwa kumbukumbu mbaya ya kupoteza moja kati ya nguzo mbili muhimu zilizobaki ndani ya safu ya uimbaji ndani ya Msondo.
Nguzo ya kwanza kung’oka ndani ya safu hiyo ambayo ilikuwa haina mpinzani kwa bendi za Kitanzania, alikuwa Suleiman Mbwembe na kufuatiwa na Othuman Momba na kisha Tx Moshi William, na sasa Maina.
Nadiriki kusema kuwa marehemu Maina ilikuwa nguzo muhimu katika safu ya waimbaji wa bendi ya Msondo Ngoma, kwani mbali ya kutegemewa zaidi katika uimbaji kwa sasa, lakini pia alikuwa anategemewa katika suala zima la upangaji wa muziki.
Ingawa sauti yake haisikiki katika baadhi ya nyimbo, lakini ukweli ni kwamba nyuma ya pazia, alishiriki vyema katika kila nyimbo na kila hatua ya maendeleo ya bendi hiyo.
Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi, Bwana ametwa jinalake libarikiwe Amin
Na kaimanzila, Nifahamishe Dar
March 17, 2009 at 10:19 pm |
SAMAHANI SANA KAKA PIUS NA POLE SANA KWA KAZI,MIMI NI MDAU MKUBWA SANA WA BLOG YAKO NA NAKUPAPONGEZI SANA KWA KAZI NZURI UNAYOIFANYA KWA KWELI TUNAINJOI SANA.SASA,MIMI NI MSHABIKI MKUBWA SANA WA NYIMBO ZA KICONGO HASA ZA ZAMANI KAMA WEWE VILE.SASA NILIKUWA NAOMBA UNISAIDIE KITU KIMOJA,KINA NYIMBO MOJA ILIIMBWA MUDA KIDOGO NA HUYU JAMAA ANAITWA KING KESTER EMENEYA,INAITWA “ZINZI”.KWA KWELI HII NYIMBO NAIPENDA SANA NA INANIKUMBUSHA MBALI SANA,SASA MIMI NILIKUWA NAOMBA UNISAIDIE KUTAFUTA TAFSIRI YA HUU WIMBO A;AFU UNIWEKEE KATIKA HII BLOG YETU YA JAMII KAKA TAFADHALI,WE IWEKE TU NITAISOMA KWANI NAPITIA SANA HII BLOK KILA WAKATI HAINA HAJA YA KUNITUMIA KWENYE MAIL KWANI NATAKA WATU WENGINE WAIFAIDI PIA.NAMAANISHA TAFSIRI YA MASHAIRI YA HII NYIMBO KWA KISWAHILI KWANI IMEIMBWA KIZAIRE,NAMI NAIPENDA BUT SIIELEWI NA NASIKIA INA TAFSIRI NZURI SANA.
NATEGEMEA USHIRIKIANO WAKO KAKA,NA MUNGU AIZDI KUKUBARIKI.
March 18, 2009 at 2:29 am |
Sawa mdau ngoja nifanye kazi ya kuitafuta kwenye Library yangu na nitaifanyia kazi.
Nashukuru kwa kuwa unasoma Blog yangu pia usisite kuniambia unapenda habari gani zaidi.
Pius
March 18, 2009 at 2:10 pm |
kaka masoud tunaomba historia za hao washiriki maana tumeisikia ya adluli na efransia tu, kipindi ni kizuri tulikuwa tunapenda kuangalia live tokea asubuhi lakini….
March 18, 2009 at 2:12 pm |
NASHUKURU SANA KAKA PIUS KWA KUJIBU,MAOMBI YANGU.NATEGEMEA KUTIMIZIWA HILO OMBI LANGU KAMA ULIVYONIAHIDI.
POLE SANA KWA USUMBUFU KAKA.
March 26, 2009 at 1:03 pm |
Kwanza pole sana kwa kazi kaka Pius
mimi ni mpenzi wa blog yako nakupongeza kwa kazi yako ya kuelimisha watu kwani uko juu zaidi kaza buti kakaangu usikate tamaa kwa kuwaelimisha watu
April 1, 2009 at 10:57 am |
hivi yule mrembo afransia mangii,yeye ndio hajapata kazi? msaidieni jamani, kama mlivyomsaidia huyo mganda putiri,nae msaidieni ajisikie faraja. hiyo maisha plus iwe kuibua vipaji na kuvisaidia vipaji hivyo.
April 1, 2009 at 11:07 am |
kaka pius, naomba kujua prea ni nini? nami nadhani nitaomba unisaidie kuwapelekea jamaa wako nje wananiomba miziki ya taarab
April 1, 2009 at 11:07 am |
kaka pius, naomba kujua prea ni nini? nami nadhani nitaomba unisaidie kuwapelekea jamaa wako nje wananiomba miziki ya taarab
April 3, 2009 at 1:31 pm |
VIP KIPINDI CHA MAISHA PLUS NI KIZURI ILA MBONA SIJA ONA ALBINO HATA MMOJA SI WATAONA KAMA WAMETENGWA NA WATANZANIA WENZAO? NINGE PENDA WAWEPO KWA KWELI
NIVIGEZO GANI MNAVYO TUMIA KUWATOA WASHIRIKI,NINGE PENDA PIA MTOE MAELEZO MAFUPI KUHUSU MAISHA PLUS KWANI WATU WENGINE HAWAJUI MAANA YAKE!!!!!!!
April 4, 2009 at 8:17 am |
kamusi Kindamba yazinduliwa Dar
Huwezi kuutamalaki utamaduni mahalia kama hujui lugha ya wenyeji. Pengine hili ndilo limemsukuma Agathon Kipandula kuandika kamusi hii ambayo ameizundua leo katika ukumbi wa hoteli moja ya Mery’s iliyopo mtaa wa Jamhuri Dar es salaam.mwenyewe anasema wazi kwamba yeye hafanyi kwa sababu ya fedha lakini kutunz aklugha ambayo inaonekana kutoweka, lugha za wenyewe. Pengine wengi tungeunga mkono kazi yake kwa kuangalia pia vitu vingine vya kuhifadhi kwa vizazi vijavyo.
kwa maneno yake mwenyewe Kipandula ambaye ni ofisa wa benki na mtaalamu wa masuala ya mifedhaameandika ili kusaidia watafiti wa ndani na nje ya nchi wanaofanya kazi katika Bonde la Mto Kilombero na Rufiji, mkoani Morogoro.
Amesema aliamua kutoa kamusi hiyo ikiwa ni mchango wake kwa jamii husika kwa vizazi vijavyo.
“Lengo kuu watoto wetu wajue lugha yao, kama unavyojua hivi sasa u-mjini unatusahaulisha lugha za asili, pamoja na kwamba tuna Kiswahili lakini ukweli unabaki kuwa tuna lugha zetu hivyo ni zawadi kwa jamii yangu,” alisema Ofisa huyo.
Kipandula alisema imemchukua miaka miwili kuandaa kitabu hicho cha kamusi kiitwacho ‘Chindamba, Kamusi ya Kindamba’ kutokana na kuhitaji muda mrefu wa maandalizi uliyomuwezesha kuitoa ikiwa na maneno 6,000 katika ukurasa 138.
Alisema kamusi hiyo ilimezingatia kutunza utamaduni kuliko biashara. kava yake inapendeza inaonyesha utamu wa maeneo ya malinyi, samaki.
April 8, 2009 at 1:12 pm |
NIAJE MASOUD NA KAKA BONDA?KIPINDI CHA MAISHA PLUS NI KIZURI NA KINAELIMISHA JAMII ILA HUYO MODESTA ANABOA KUPEWA UANGALIZI WA STORE ANAONA KAMA KAPATA MILIONI 10 HAFAI KUBAKI KIJIJINI,MLIPO NIFURAHISHA NIPALE CHAZ NA STIVU WALIPORUDI KAMBINI HONGERENI KWA HILO.
April 14, 2009 at 8:23 am |
Mimi nafurahia sana kipindi cha maishaplus mara zote nimekuwa mfuatiliaji na mpiga kura mzuri. Mpaka sasa hivi nampigia debe charles yuko juu, ila kazi mnayotuonyesha watanzania iko safi. Napenda tu kuwaomba hao watoto wanapoona kitu kama ile irizi wasiwe wepesi wa kusema ni ya nani kwani watajenga uhasama
April 16, 2009 at 11:46 am |
kipindi ni kizuri tena sana, nategemea mwakani kitakuwa kizuri zaidi mkiongeza ufanisi na ubunifu zaidi, ila kitu kimoja kilichoniuzi kupita kiasi ni huu uchawi ulionyeshwa na upendo na kundi lake tunajifunza nini watanzania kutoka kwake? kwanini amekitia dosari kubwa kipindi chako kaka Masound na Bonde? ila nampa bigup sana Abdul na mungu amsaidie awe mshindi wa Maisha plus
April 19, 2009 at 9:41 pm |
hi kaka kipanya na bonda,kazi mnayoifanya nzuri sn,nauliza inamana hao wengine hawtpata hata sent tano yakifuta jasho,pia nikipiga kura kwa charles mbona haziongezeki.
April 19, 2009 at 9:51 pm |
pia hivi hizi kura 2nazopiga zinahesabiwa pamoja na zile za sms ya mitandao mingine ya voda,tigo,zain?
April 24, 2009 at 12:04 pm |
Hongereni kwa ubunifu mzuri watanzania wenzangu.Je maoni tunayo toa kwa washiriki wa maisha plus, Huwa wanayasoma ili kujirekebisha walipokosea haswa Pendo na Wambea Wenzake?
July 24, 2009 at 5:14 pm |
Hello Maoni ya Maisha Plus huwa na Compile na yanakwenda kwa wenyewe huwa nampatia Masoud Kipanya kwani wao ndio waandaaji.
Asanye nashukuru kwa kunitembelea
May 1, 2009 at 6:41 am |
Kaka mambo vp!
Nimekuona kwenye blog yako unatisha kaka
kaka ebu niwekee haka ka blog kangu ukapigie promo japo kidogo ndo kibiashara chetu kingine na wewe unahusika kaka,na kama kuna marekebisho nikutumie user name na password urekebishe na uweke na wewe hayo magari yako unayoyauza huko,si unajua tena riziki ya mbwa iko miguuni mwake!!
http://www.showroomautoaccesories.blogspot.com
Regards,
Japh E.M
June 7, 2009 at 10:14 pm |
mjomba nimeomba tuwe tunawasilian na unasema nibonyeze pale nahapa lakini ni .0-00000000000000000000
July 24, 2009 at 5:10 pm |
dear friends,
i real like this as it may subjected as room of chatting,exchanging some idears like vijanaz,
Would like to let you know about our new propaerty which located at Ngorongoro, next to Gibsfarm, to the fireline of ngorongoro highland forest!
unfortunately this couldnt be a right place to announce! but still we can talks about other jobs, opportunities, etc.
i m a good in poems, english/swahili, writing a stories/movies and ………..
for any anybody interesting with the above…… please karibu.
find me to the website with Masai cover in a local marriege but ……………….. funy one!!!!
hope to get back soon… nakuja,,,,,, subiri
August 29, 2009 at 9:45 am |
Vipi mwandishi kama wewe,tena wa siku nyingi kidogo,lakini lugha bado inakupiga chenga.Utawezaje kuandika “hairisha”badala ya “ahirisha”rejea habari yako hapo juu,imuhusuyo yule dada mwandishi,aliehukumiwa kupigwa viboko.
Ni aibu kwa Mtanzania kutokujua vizuri Kiswahili.
Na ndio maana unaruhusu wachangiaji wengi tu,wanaandika utumbo,lafudhi mbovu lakini wewe unatoa upuuzi wao humu kwenye globu yako.Weka mkakati,lugha mbovu,hurushi ujumbe.
September 2, 2009 at 4:12 am |
Balozi Dola – Ndani ya video kali ya Youtube “Connect”
*WATCH IN HQ FULL SCREEN* New Video Comic directed by 3rdi featuring Regime Change (NYC/Haiti), Negus World Order (Haiti/France), Saba Saba (Uganda), Narcy (Iraq), Dola from (Tanzania)
September 6, 2009 at 1:35 pm |
As I would not be a slave, so I would not be a master. This expresses my idea of democracy. Whatever differs from this, to the extent of the difference, is no democracy.” Abraham Lincoln
Thereupon I concluded: As I would not be a dhimmi, so I would not be a Muslim.
September 7, 2009 at 10:55 am |
hongera sana ndg mhariri na safu nzima ya majira usikatishwe tamaa na maoni ya baadhi ya watu wasio wastaarabu ni haki yao kusema chochote binafsi nawafagilia kwa saaaaaaaaanaaaaaaaaaaaaaaa.from K.S.A
September 29, 2009 at 9:17 am |
Mdau, pole na majukumu….kuna tangazo hapo la biashara la Isamilo lakini lina makosa kidogo kwenye hiyo logo badala ya kuandika LODGE wameandika LODEGE au ni luganyingine mbadala ya lodge?
October 8, 2009 at 3:46 pm |
Kaka mbona contact info zako haziko wazi… tunashindwa kukutumia habari
October 9, 2009 at 1:21 am |
Samahani kaka email yangu ni piusmicky@yahoo.co.uk na nimeiweka hapo mbele, Nashukuru kwa ushauri.
October 13, 2009 at 8:26 pm |
Kaka heshima yako. Ninaomba uniangalie gari zuri Rav-4 milango iliyo nzuri kibei na kihali. majibu hapa hapa kaka. Asante sana.