Mambo yameiva kwa wakazi wa Kigamboni, hii ni sehemu ya majengo ya utakao kuwa mji mpya wa Kigamboni kwa mujibu wa Mtandao wa Wizara husika.
Eneo hili litahusu maeneo ya makazi yasasa ambayo yanakaliwa na watu. Kwa mujibu wa Tangazo la Serikali la Mwaka 2008 wakazi wa kata zipatazo tano watafidiwa kuhamishwa kupisha mradi huu.
Eneo litakalo chukuliwa ni la Kigamboni likichukua zaidi ya kata tano ambazo ni Kigamboni, Vijibweni, Somangila, Mji Mwema na Kibada. Eneo hili lina wakazi wapatao 82,808 ambao watafidiwa kulingana na sheria na taratibu zilizowekwa.
Mradi huu ukikamilika mwaka 2030 utakuwa ni mji wa kipekee si tu kwa Tanzania bali kwa Afrika pia.

















Tungekuwa makini hili si la kuwezekana mwaka 2030 bali lilitakiwa liwe limewezekana miaka 30 iliyopita.Kwa maana hiyo hii ni ndoto nzuri ya mchana.Tukiamka tutakutana na ukweli.Uzuri wetu tu mabingwa wa kuunda miradi ya makaratasi kama vile mpira wa chandimu tuliocheza utotoni.Ili kuwa na eneo la namna hiyo,tunahitaji umeme,maji,barabara,ufuataji wa sheria na bila kusahau uongozi bora unaozingatia maslahi ya kizazi kilichopo,kijacho na kitakachokuja.Sasa piga picha,ni nani wa kusimamia mradi kama huo?Tuendelee kuota….wenzetu sasa wanatuita maprofesa mipango.
Mradi huu ni mzuri tatizo kubwa mradi umefuata watu badala ya watu kufuata mradi kama ilivyo kwa vituo vya jeshi. kama nia ni njema kwanini mradi usiombe eneo lisilo na makazi ya watu then watu wafuate huduma zitakazotolewa na mradi. Huo ndio ubunifu sio kuhamisha watu hizo pesa za kuhamisha zitumike kutukopesha matrekta. kilimo kwanza oyeeeeeeeeeee.
safiiiiiiiiiii sana, ombi langu kwa serikali wananch wa k/mboni wapewe malipo mazuri. hivi najiuliza kutaingilika baada ya ujenzi kukamilika? he he wadau hebu nisaidieni juu ya hili. naamini wataishi wazungu pamoja na watu wenye hali ya juu saana
NATAKA KUISHI KWENYE MJI HUU.
Kiukweli hii ni zaidi ya ndoto ya mchana hasa tukiangalia aina ya viongozi tulionao nchini kwetu. Mungu ibariki Afrika Mungu ibariki Tanzania!!!!!!
chamsingi selekali inatakiwa iache unyonyaji iwalipe hakizao staiki wananchi wakigamboni naiwapatie viwanja sio nyumba za frat ambazo mwananchi hata mchicha huwezi panda wakati kiwanja chako kina kisima sehem ya kuchezea watoto.