Mchezo kati ya timu ya Taifa Stars na Egypt umemalizika huko Cairo huku timu ya Taifa ikiwa imebugizwa mabao 5-1.
Mchezo huo ambao ulikuwa wa kusisimua umeshuhudia timu yetu ikiendeleza wimbi la kufungwa huku timu ikionyesha ukomavu wenye ukame wa magoli.
Ssiwezi kusema hasa tatizo la Taifa Stars ni nini ila kwa mujibu wa mchezo wa leo kwa upande wangu naona beki ilikuwa inakatika sana na washambuliaji kutokuwa na coordination ambayo inawafanya wacheze kama timu zaidi.
Mpaka mapumziko Taifa Stars ilikuwa imeshakunywa jumla ya mabao 4-1 huku Wamisri wakiwa wanalishambulia lango la Taifa Stars vilivyo na kuufanya mchezo kuwa wa upande mmoja zaidi.
Mpaka kipyenga cha mwisho, Egypt 5-1 Taifa Stars










