AY / FA NA BLACK RHYNO WAZIONA TUZO ZA CHANNEL O

July 16, 2009
AY

katika wale waliotajwa kushindania tuzo za muziki za video za chanall o (chanall o video music awards)siku ya tarehe 14 ya mwezi huu kutoka tanzania tumebahatika kuwa na video ya AY NA FA NAONGEA NA WEWE kundi la BEST DUO OR GROUP, na video ya BLACK RHYNO inayoitwa BLACK CHATTA upande wa BEST HIPHOP VIDEO. Habari kwa mujibu wa Dee Jay Fatty mtembelee kwenye Kali na Mpya za Bongo ambapo utapata habari kadha wa kadha juu ya wasanii wa Bongo. Je wajua kuwa Ray C na Lord Eyes uhusiano umekufa? Gonga hapa usome zaidi.


Werason bado amlilia Bibiciya Mfwengi

July 16, 2009

Inasemekana kuwa mwanamuziki Werason bado analalamika na kukerwa mno na kitendo cha Koffi Olomide kumchukua mcheza shoo wake tegemezi Bibiciya Mfwengi. Habari za burudani zinasema kuwa Bibiciya ambaye awali alikuwa kwa Koffi kabla ya kwenda kwa Werason na kurudi kwa Koffi tena mwaka huu zoezi ambalo lilifanikishwa na mashabiki wakereketwa wa Koffi ambao wanataka kuiona bendi hiyo inawika na kung’ara jukwaani kama zamani.

Akiongea na muandishi Guy guy Mpeye hivi karibuni Werason alisema kwamba katika pigo analolikubali kwa mwaka huu basi ni kuondokewa na mcheza shoo huyo kipenzi cha mashabiki na anayejua kulitawala jukwaa. Bibiciya ndiye alikuwa mcheza shoo wa mwaka kwa mwaka jana.

Pata kionjo cha Bibiciya kwa sasa akiwa na Koffi


Mwingine Wenge BCBG atoka kivyake!!

July 16, 2009

image

Kwa wapenzi wa Wenge Musica na JB Mpiana huyu bwana si mgeni ni mcharaza gitaa anayekwenda kwa jina la Accompagnero Alba ambaye kwa miaka mingi amekuwa na wakongwe Wenge Musica BCBG lakini ameamua kutoka kivyake na albamu hii yenye takribani nyimbo nane. Kama ilivyo kwa wanamuziki wengine kutoka na Solo si kazi ndogo hayo ni maneno ambayo hata Mwanamuziki Muumini aliwahi kusema. Alba kwenye CD hii kwa kweli naweza sema kachemsha kwa mtazamo wangu hakuna wimbo ambao unaweza kumfanya mtu akairudia CD kusikiliza naweza sema kati ya wanamuziki ambao waliamua kutoka kivyao kwenye BCBG huyu kachemka sana kuanzia Alain Makaba, Mwamba Ficare, Werason, Dominguez, Blaise Bulla na wengineo. sina mengi ila itafute hii Albamu na we utupe mchango wako.


Anitha na Zecomedy

July 16, 2009

Jamaa wananiachaga hoi sana hawa hebu na we cheka ki spoti kidogo!!


Video ya Natamani kuwa Malaika ya Jay Dee iko jikoni

July 16, 2009

Wimbo wa Natamani Kuwa Malaika wakwake LAdy Jay Dee unatamba na Video yake ndio iko mbioni inapikwa sasa na kikosi cha Ogopa Dee Jays toka kwa Baba Moi, kazi ya shooting ya Video hiyo ilifanyika hivi majuzi na inatazamiwa kukamilika na kuanza kuonekana mwishoni mwa mwezi huu wa July au mwanzoni mwa mwezi ujao. Vazi la Jay Dee limebuniwa na Ali Remtullah

Jay Dee akiwa na baadhi ya watoto kwenye shooting ya wimbo huo pale Gymkhana Club

 

Marcell na Lucas wa Ogopa Dee Jays kwenye moja ya location Kwa habari na Picha zaidi mtembelee Binti Machozi kwenye Blog yake.