Timu za watanzania zenye maskani yake jiji la Helsinki na Tampere Ufini zimefanikiwa kuanza vema kampeni zao za kutangaza taifa la Tanzania kwenye medani ya soka kwa kutoa vipigo kwa wapinzani wao.
Timu ya Tampere Africans Sports(TAS) yenye makazi yake kwenye jiji la Tampere,chini ya kocha wake George Matovu (mtv) waliibuka washindi kwa goli 4-1 kwenye mechi ya kirafiki dhidi ya timu ya Wakongomani iliyochezwa mwisho mwa juma.
Wakati huo huo ndugu zao wa Bongo Fc wenye makazi yao jijini Helsinki walifanikiwa pia kuwabamiza bila huruma timu ya wacameroon kwa mabao 3-1.Helsinki ambayo inanolewa na mdau mkubwa wa Soka Ezza.
Helsinki inajiandaa kwa mtanange wa kukata na mundu wa kirafiki dhidi ya timu ya watanzania kutoka sweden Kilimanjaro Club utaofanyika June 27,jijini Helsinki.
Kocha wabongo FC amewahakikishia mashabiki wa timu ya Bongo FC ushindi mnene siku ya jumamosi kutokana na maandalizi mazuri waliyonayo.
Mdau ufini







