Jumamosi Timu ya Taifa Tanzania, Taifa Stars, iliibugiza timu ya Taifa ya Sudan mabao 3-1 katika mchezo wa kufuzu kucheza fainali za mataifa huru ya Afrika kwa wachezaji wa ndani uliofanyika Uwanja mpya wa taifa jijini Dar, pichani mshambuliaji wa Taifa Stars Mrisho Ngassa akiwatoka mabeki wa timu hiyo na kupeleka dhahama golini kwao. Mogoli yote ya mchezo huo yalifungwa na wachezaji wa klabu ya Yanga.









December 4, 2008 at 8:58 am |
kaka Pius mimi ni mdau wa blog yako lakini kwa kweli hili uliloandika leo limeniskitisha sana haswa nikizingatia umetamka wewe. Wakati umefika sasa kwa Watanzania tuelimike na kuachana na kasumba za Uyanga na Usimba na kufikiria kama watanzania hatuwezi kusema ni Yanga iliifunga Sudan bali ni timu ya Taifa ya Tanzania ambapo ndani yake kuna wachezaji kutoka timu mbali mbali kama JKT Ruvu, Simba, Yanga, Mtibwa, Moro United na kadhalika bila ya ushirikiano wa hawa wote ushindi usingepatikana tafadhali naomba urekebishe kauli yako kwani sio sahihi badala ya kujenga tulenga kubomoa.
December 6, 2008 at 2:13 pm |
Mdau naheshimu mawazo yako lakini nilichoandika mimi kama alivyosema mchangiaji hapo ni mtazamo ni ukweli ambao haupingiki, sio wote wnaosoma ni wapenzi wa mpira wa miguu wa Simba na Yanga kiasi kujua nani ni wa wapi kuna watu wanapenda kujua habari za Taifa Stars kwa sababu ya Uzalendo tuu, hii ni kwa faida ya wale wasiojua mdau punguza hasira hehehehe.
Pius
December 5, 2008 at 6:45 am |
Mdau hapo juu,anachoongea Kaka Pius ni cha msingi,ni ukweli usiopingika kuwa mafanikio ya timu yetu ya mpira wa miguu ya Taifa kwa kipindi hiki yamekuwa yaking’arishwa na wachezaji wa Yanga,hii kila mfatiliaji wa masuala ya soka atakuambia ndiyo kwahiyo mimi sioni ubaya wowote kwa Mshikaji kuandika hivyo,hata kwenye blog yangu nilitoa habari inayoshabihiana na hiyo,inaweza isisemwe hadharani lkn ndo ukweli wenyewe sasa tutafanyeje?
Taifa Stars Oyeee!
December 7, 2008 at 12:41 am |
Pius umechemka ndugu yangu kubali
December 7, 2008 at 3:23 am |
Siwezi kusema nimechemka!! Tatizo hapa ni Uyanga na Usimba tuu habari hii ingeandikwa kuwa wachezaji wa Simba mtu huyu huyu angeisifia hehehehe usijali mkuu ukiichukulia ki binafsi utaona inapendelea hehehe.