Tanzia

July 29, 2008
Marehemu Jackson Goa - Jack Bai

Marehemu Jackson Goa - Jack Bai

Familia ya Mikongoti wa Dar Es Salaam na Familia ya A.Goa wa Ifakara – Kilombero, Inasikitika kutangaza kifo cha ndugu yao Jackson Goa au Jack Bai kilichotokea leo katika hospitali ya buruhani. Mipango ya mazishi inafanya nyumbani kwa Kaka wa Marehemu Dar es Salaam. Habari ziwafikie ndugu jamaa na marafiki popote pale walipo.

E. Mikongoti – 0784 431154


Mamiss na mguso wa jamii…

July 29, 2008
Mamiss na mguso wa jamii

Mamiss na mguso wa jamii

Washiriki wa Miss Tanzania 2008 wakizungumza na mtoto aliyejitambulisha kwa jina moja la Josephine, aliyekuwa anatoka kuokota kuni katika vichaka vya Mjimwema Kigamboni Dar es Salaam juzi. Warembo hao walikuwa kwenye ufukwe wa South Beach katika maandalizi ya shindano lao linalotarajiwa kufanyika Agosti 2, mwaka huu. (Na na HabariLeo).


Yanga yapigwa Mvua ya Michuano mitatu nje!!

July 29, 2008

KLABU ya Yanga imefungiwa kushiriki michuano inayoandaliwa Shirikisho la vyama vya soka vya nchi za Afrika Mashariki na Kati (Cecafa) kwa miaka mitatu sambamba na kupigwa faini dola za Kimarekani 35,000 kutokana na kugomea mchezo wa kuwania nafasi ya mshindi wa tatu ya michuano ya kombe la Kagame. Read the rest of this entry »