Hepi besdei tu mi…

July 28, 2008
Happy Birthday Daddy

Happy Birthday Daddy


The Ngoma Africa Band kupelekana mchaka mchaka na mashabiki Frankfurt

July 28, 2008
Ngoma Africa aka The Golden Voice of East Africa!

Ngoma Africa aka The Golden Voice of East Africa!

Habari na Msema Kweli
Bendi ya Mziki wa dansi The Ngoma Africa band aka The Golden Voice of East Africa!
Inatarajiwa kupanda jukwaani 9-08-2008 katika maonyesho makubwa ya African and Caribbean Cultural Festival yatakayo fanyika katika mji wa mapesa ya euro!, Frankfurt City,kwenye viwanja vya Robesotck Park,nchini Ujerumani. Bendi hiyo mashuhuri kwa kuwapeleka puta na kuwadatisha akili maelfu ya washabiki
kwa mdundo wake ambao umetajawa kuwa ni “Extraordinary”bongo dansi kutoka Uswahilini Tanzania,imejikuta inafunika katika maonyesho makubwa kwa kuwatia kiwewe washabiki na mziki wao dansi wa bongo. Read the rest of this entry »

Michezo mingine bana…!!

July 28, 2008
Michezo mingine bwana..!

Michezo mingine bwana..!

Pichani ni moja ya wachezaji wa mchezo wa soka la kwenye tope unaitwa “Mudflat football”, Mchezo huu huuchezwa kwenye fukwe za bahari maji yakipwaa na kuacha sehemu ya tope, Hii ilikuwa huko Kaskazini mwa Ujerumani mji unaitwa Brunsbuettel (PHOTO ROLAND MAGUNIA)


Man U yailamba Portsmouth 2-1 – huko Nigeria

July 28, 2008
Mambo ya Mashabiki

Mambo ya Mashabiki

Mashabiki wa Manchester United na Portsmouth FC kila mmoja akitamba kivyake wakati wa mchezo wa kirafiki baina ya Manchester United na Portsmouth uliofanyika jana jumapili huko Abuja Nigeria, Manchester ilishinda 2-1.


Chelsea watua Malaysia kwa mchezo wa kirafiki

July 28, 2008
Deco

Deco

Mchezaji wa Chelsea Deco akiwasili kwenye Hotel waliofikia jijini Kuala Lumpur Jana tarehe 27 July 2008, Chelsea wamewasili Malaysia wakiwa na kikosi chao cha kwanza chote isipokua Drogba na kesho watacheza na timu ya Taifa ya Malaysia katika uwanja wa Shah Alam.