Kwa wale wapenzi wa Twanga Pepeta,watakuwa wanamkumbuka sana,alitamba sana kwenye album ya Mtu Pesa,hasa kwenye wimbo wa Mtu Pesa na Wakati wa Shida, Kipaji chake kilionekana na Banza Stone,alimchukua kwenye Bendi yake ya Bambino Sound,Baada ya Bambino kufa,wakaenda Twanga,ndiyo wakatoka na Album ya Mtu Pesa, Twanga walipata safari ya Ulaya,Walipo rudi yeye alibaki ulaya(alijipiga) sasa hivi yupo Beligique,yupo na Group inaitwa VIBRATION SHENGEN, ikiongozwa na BABY SHENGEN, wametoa album inaitwa PRESSION (Musukusuku), Huyo si mwingeni ni HUGUES MOYOBA (Papa na Gemina) au huku tulikuwa tunamwita Ige Moyaba, Katika album hiyo pia ameimba na Kiswahili,kila mtu na mtu wake,lazima amtaje Pitchuo Kongo na Fred Elima. Habari hii kwa ushirikiano mkubwa wa Big Producer Maghambo.
Hebu jikumbushe kibao cha Mtu pesa, Kwenye kibao hichi Ige Moyoba aliimba ubeti baadaya Jesca Charls, amevaa Tshirt Nyekundu na Kofi ya Pama, kisha Pata kibao cha Vibration Shengen.
Mchezaji wa Chelsea Frank Lampard (mbele) akikokota ngom akuelekea langoni mwa timu ya Chengdu ya China jioni ya leo 26th July 2008, Mchezo huu umemalizika kwa timu ya Chelsea kushinda bao 7-0, Timu ya Chelsea itacheza na Timu ya Taifa ya Malaysia siku ya Jumanne. Mchezo huu umemalizika dakika chache zilizopita.
Baada ya kimya kirefu toto la kihehe mahiri ktk miondoko ya muziki wa kizazi kipya Rehema Chalamila (Ray C) ameachia track mpya iitwayo ‘Nihurumie Wangu’.
Ray C anasema aliamua kukaa nje ya ‘gemu’ kwa muda akiwa anausoma muziki na soko linavyokwenda,huku akiwapa nafasi wasanii chipukizi kuonyesha uwezo wao. ”Sio siku zote unapenda kuonekana wewe tu, ni vizuri kupisha wengine kuonyesha uwezo wao,nimekuja tena upya ndani ya ‘gemu’ sasa ni moto mkubwa unawaka na hakuna kurudi nyuma tena,mambo ni mbele kwa mbele,”amesema Ray C.
Msanii huyo amesema ujio wake huo,ni moja ya maandalizi ya kuachia albamu yake mpya itakayotoka hivi karibuni ikiwa imesheheni nyimbo kibao zilizosimama sambamba na kkuwashirikisha wasanii maarufu wa ndani na nje ya nje ya Bongo.
Aidha, amesema amejifunza mengi kuhusu muziki, baada ya kufanikiwa kufanya maonyesho kadhaa nchi za Uingereza,Marekani,Sweden,na kuweza kumpa mwanga zaidi kimuziki.
Mwanamuziki nyota wa Tanzania, Judith Wambura ‘Lady Jaydee’ ameteuliwa kuwania tuzo ya Mwanamuziki Bora wa Afrika Mshariki katika Tuzo za Kora 2008. Kwa mujibu wa gazeti la New Vision la Uganda, Jaydee ni mwanamuziki pekee kutoka Tanzania kuchangulia kwenye kinyang’anyiro cha mwaka huu.
Jaydee ambaye anawania tuzo hiyo pamoja na Susan Kerunen, Klear Kut, Michael Ross na Blu3 kutoka Uganda na nyota wa Kenya, Nameless, Valerie Kimani na Wahu. Mwanamuziki huyo pekee wa bongo fleva kutoka Tanzania anawania kunyakua tuzo hiyo ambayo fainali zake zitafanyika Desemba 6, Tinapa, Nigeria.
Kwa mara ya kwanza msanii bora wa Afrika ataondoka na kitita cha dola za Marekani milioni moja kutoka First Bank of Nigeria. Tuzo za Muziki za Kora ni kubwa Afrika zinazojumuisha wakali kutoka nchi mbalimbali.
Jaydee ambaye amewahi kutwaa tuzo kadhaa za kitaifa na kimataifa aliwahi kuchaguliwa kuwania tuzo za Kora mwaka 2003 (Mwanamuziki wa kike anayechipukia Afrika) na mwaka 2005 (Mwanamuziki Bora wa Kike Afrika). Katika tuzo za mwaka jana Ambwene Yesaya ‘AY’ alikuwa ni msanii wa Tanzania aliyechaguliwa kuwania tuzo hizo. (Na Habari Leo)
Wiki hii nilibahatika kukuitana na Mchoraji vikatuni maarufu Bw. Nathan Mpangala, Ingawa alikwa na haraka lakini nilipata kumuuliza machache na kwa ufupi kuhusiana na dhaana nzima ya Katuni, Bwana Nathan ni Mchoraji wa magazeti mengi ikiwamo lililokufa la Sanifu, Majira na Dar Leo, Majira Jumapili na magazeti mengi ya udaku. Pia bwana Nathan ni mchoraji wa katuni ya Mtu kwao ambayo hurushwa mara baada ya taarifa ya habari ya ITV, Katuni kama Kijasti na Daladala live zilimpatia umaarufu kwa jinsi ya kufikisha ujumbe kwa njia ya vikaragosi. Mchoraji huyu pia ni bloga mwenzetu ingawa ndio kwanza yuko kwenye kipindi cha kuscan michoro yake ili aiweke hewani kwa sasa anapatikana http://nathankatuni.wordpress.com Read the rest of this entry »
After being sacked as Bolton Wanderers manager on Wednesday, Gary Megson has defended his record at the club despite the antipathy shown to him by Trotters supporters.
Tottenham striker Roman Pavlyuchenko may well have hastened his likely departure from White Hart Lane by accusing manager Harry Redknapp of "mocking" him.
ESPN Soccernet can reveal that Portsmouth plan to take out an injunction against the decision by HM Revenue and Customs (HMRC) to issue them with a winding-up order.
Liverpool defender Glen Johnson suffered a medial ligament injury to his right knee during Tuesday night's 1-0 victory at Aston Villa, but it has not yet been confirmed how long he will be out for.
Manchester City midfielder Stephen Ireland will be out of action for two weeks after a scan revealed he suffered a damaged hamstring in the 3-0 victory over Wolves.
Fulham manager Roy Hodgson has signed a new twelve month rolling-deal with the Cottagers. The former Inter Milan and Switzerland boss has been rewarded for guiding Fulham to seventh place in the Premier League last season - their highest top-flight finish - and for a strong start to the current campaign
Wigan Athletic have taken Sporting Lisbon's Serbia goalkeeper Vladimir Stojkovic on loan to provide cover until the end of the season, the Portuguese club have revealed on their official website.
Manchester United boss Sir Alex Ferguson has slammed England coach Fabio Capello and Inter Milan manager Jose Mourinho for claiming that the Old Trafford club are in decline. Ferguson was responding to comments made by Capello that United are no longer a "war machine".
Chelsea have announced that, as of the end of 2009, the club have cleared virtually all of their outstanding £340 million debt, and also revealed reduced losses for a fourth consecutive year.