Nionavyo mimi: Akina TID wako wengi
July 25, 2008
Habari za kuwekwa ndani kwa mwanamuziki Khalid Mohammed AKA TID wiki hii zimewastua wengi hasa wapenzi wa muziki nchini na nje ya nchi kwa ujumla. Hii inatokana na comments ambazo zimekuwa zikiwekwa kwenye blog mbalimbali zilizoweka habari za mwanamuziki huyu. Ikumbukwe TID alihukumiwa kwenda Jela baada ya kumuumiza kijana mwenzie wakiwa katika ulevi wa pombe.
Sio kama natetea au nataka kulaumu maamuzi ya chombo cha dola au wale wanaomuhurumia la hasha, lakini ninachotaka kusema huu ndio utaratibu wa kawaida na hukumu za kawaida za kimahakama kwa maisha ya watanzania walio wengi. Kuna watu ambao kwa kiasi kikubwa wamelaumu kitendo cha hakimu cha kumhukumu TID kutumikia mwaka mmoja jela kwa kosa la kumuumiza mtu, kosa ambalo kimsingi wangeweza kulimaliza nje ya mahakama au kama ni hukumu wengi walitegemea kuwa angelipishwa fine, kwa vile kosa hili huchukuliwa kiwepesi hata watu wengi hawakujua kama TID ana kesi ila walistukia wakisoma vichwa vya habari TID aswekwa rumande, au TID atupwa Segerea na vingine vinavofanana na hivyo, Wapo walioko ndani na ni hukumu hata ya miaka miwili au mitatu kwa kosa la kuiba kuku, haya yote tunayasoma kwenye magazeti ya jioni (Dar Leo na Alasili) ambayo ni maarufu kwa kuandika kesi kama hizi. Kwa vile hawa hatuwafahamu huwa tunasoma kama story na kupita na kwa kuwa huyu tunamjua basi imemstua kila mmoja wetu. Ninachotaka kusema ni kesi nyingi za watu kama hawa wanatumikia vifungo na wengine kufia jela au kutoka na magonjwa ya kuuambukizwa kwa sababu ya makosa kama haya ya akina TID au tuseme makosa ya wizi wa Kuku.
Utaratibu wa kuitumikia jamii
Mwaka 2006 mwanzoni Nikiwa mwanafunzi huku Singapore nilivunja sheria ya barabarani na kugeuza gari kwenye traffic lights (Uturn) kosa lile lilirekodiwa kwenye video ya polisi jioni kurudi nyumbani nilikuta karatasi ya fine (huku wanaita Denda) ikinitaka kuripoti kwenye kitengo cha Polisi Jamii ( Singapore Westland Police Station) nilipofika nilionyeshwa kosa langu na kusomewa shtaka papo hapo, kisha nilitakiwa kuchagua adhabu ya kwanza ikiwa ni kuendesha gari la kumwagilia maua kwa wiki 3, Pili kufanya usafi Hospitali ya serkali (Singapore University Hospital), tatu Kufanya kazi za kujitolea kwenye kituo cha watoto yatima, hizi zote ni kwa wiki tatu na unatakiwa kufanya masaa 12 kwa wiki, hivyo utapanga mwenyewe utafanya masaa mangapi kwa siku. Hii inafanya wewe kwa vile umekosa unaitumikia jamii na utakuwa huru nyumbani kwako. na kama utakaidi hili basi kifuatacho ni jela na kazi ngumu.
Hapa tunajifunza nini? Kimsingi kwa kosa la TID na wengine wenye makosa kama yake kwa kuwaweka jela ni kumaliza hela ya serikali bure kwani atahitajika kulishwa na hii ni nguvu kazi ambayo unaiweka ndani kwa mwaka mzima. Inasemwa hakuamini aliposomewa shtaka kwani alitarajia atasomewa hukumu kwa kutakiwa kulipa fine au kwenda jela au vyote viwili, hii inatoa mwanya kutunisha mfuko wa serikali kwa fine zinazokusanywa. Kwa nini tusitatumie hawa watu kufanya shughuli za kijamii kutokana na kipaji au ujuzi ulionao, nadhani hili lingemanya mtu ajifunze zaidi kwani kwa kumuona TID akifagia Muhimbili kungefanya wengine waogope makosa madogo madogo na kujifunza zaidi.
Binafsi napinga kuwapeleka jela watu wenye makosa kama ya TID. Ni kutumia pesa ya Kuwepo kwa kitengo cha polishi shirikishi au polisi jamii kunaifanya vyombo vya dola kufanya kazi karibu zaidi na jamii na kuifanya jamii kuona ni sehemu ya majukumu yao. Hii inasaidia kupunguza makosa madogo madogo katika jamii pia. Leo tunasoma kwenye gazeti moja la kila wiki kuwa wababe wa gereza walifurahia kumpokea TID gerezani wakiahidi kumfanyia kitu mbaya akiwa huko ili akitoka akahadithie, Je unafikiri kama atafanyiwa kitu mbaya huyu mtu akitoka utakuwa umemsadia au ndio umemharibu kabisa? itamfanya mtu kuwa na visasi zaidi au na roho mbaya zaidi na kufikiria ni jinsi gani na yeye atamlipizia aliyesababisha haya yote. Kwa njia moja au nyingine yapasa tuwe na njia mbadala kwa makosa akama haya. Ni mtazamo tu wadau.
Nakuacha na kibao nilikataa cha Top Band TID akimshirikisha Mr Blue na Q Chilla.
Salamu zangu kwako Mjomba
July 25, 2008
Irene Sanga(kushoto) akiwa jukwaani na Elidadi Msangi. (Picha na Bob Sankofa)
Blog ya Bongo Celebrity kama kawaida ijumaa hukupatia wimbo mmoja kwa ajili ya kukupoza na mchakamchaka wa wiki nzima, weekend hii wamekuja na kibao Salamu Zangu tokakwake Irene Sanga akimshirikisha Mrisho mpoto na Elidadi Msangi ikiwa ni ombi langu rasmi, Bofya hapa ukakisikilize kibao hiki mwanana chenye mahadhi ya mashairi ya kimapokezo.
Aidha mashairi ya wimbo huo kama ulivyoandikwa na Irene Sanga ni haya hapa:-
Kiitikio
Taifa liwapo na huzuni lazima wote tufunge mikanda kiunoni ili matanga yaishe upesi, majanga yanapozidi kimo mioyo ya wanadamu huota kutu hizo ni salam zangu…
Pepo hazina sifa ila pawapo Jehanamu, uzuri ni kipimo cha ubaya, kwani kiumbe chenye uhai na mauti huongozwa na tamaa salam zangu kwako eeehh! Bonyeza hapa kusoma zaidi Read the rest of this entry »
Shaggy kutumbuiza Nane Nane Leaders
July 25, 2008
Shaggy akikamua
MWANAMUZIKI wa miondoko ya Ragga kutoka nchini Marekani, Shaggy atawasili nchini Agosti 7 kwa ajili ya kutumbuza katika siku kuu ya Wakulima, maarufu kama Nane Nane, kwenye viwanja vya Leaders jijini Dar es salaam.
Shaggy, ambaye jina lake halisi ni Orville Richard Burrell na ambaye kwa sasa anatamba na vibao cha ”Bonafide Girl”, ”Sexy Lady” pamoja na ”Why Me”, atakuwa akifanya ziara ya pili nchini baada ya kuja mwaka 2006 kuja na kukonga nyoyo za mashabiki.
Mkurugenzi wa Prime Time Promotions, Godfrey Kusaga alisema mwanamuziki huyo ataongozana na wasanii mbalimbali maarufu kama Fabian Smith,Robert Livingstone, Maro Gordon na wengine wengi.
”Shaggy ataambatana na wasanii na wanamuziki 15 na watatumbuiza ‘laivu’ ili wasanii wa hapa nyumbani waweze kujifunza mambo mbalimbali kutoka kwake,” alisema.
Kiingilio katika onyesho hilo kitakuwa ni Sh 7000 na Kusaga alisema wameweka kiwango cha chini ili kila shabiki aweze kushuhudia onyesho hilo la mwanamuziki anayetamba duniani.
Alisema wanatarajia kuwa onyesho hilo litafungua sura mpya katika utamaduni wa matamasha nchini.

Posted by piusmickys
Posted by piusmickys 
Posted by piusmickys 









