Simba Chaliii!!

July 24, 2008
Yachapwa na URA ya Uganda kwenye Nusu fainali
Kimoja tu hoii

Kimoja tu hoii

Simba ya Tanzania leo imeshindwa kufanya kile walichotazamiwa kukifanya baada ya kuchapwa na URA ya Uganda 1-0 katika mchezo wa kwanza wa Nusu Fainali wa kombe la Kagame, Pamoja na Simba kupata penati dakika za mwishoni penati ambayo mchezaji wa Simba Mnigeria Emeeh Izechukwu  alipiga fyongo na kipa wa URA kuicheza jambo lililofanya mashabiki kuloa ukimya, Hii inawapa watani wao cha kusema kwani nao leo katika uwanja huo mpya wanakutana na Tusker ya Kenya, Yanga ambao jana walikuwa wakishangilia kwa kuimba Aki na Ukwa… aki na ukwa.. ikiwa ni kejeli kwa watani wao wa jadi ambao wamesajili wachezaji wawili toka Nigeria. Simba watakutana na timu itakayopoteza mchezo wa leo. URA, washindi wa kwanza wa kundi la Morogoro ambao walianza kwa kuichakaza Rayon Sports ya Rwanda kwa mabao 4-1 na kuonyesha safu kali ya ushambuliaji. habari ndiyo hiyoo.


Mwali kamuona mwali…

July 24, 2008
Warembo wa Miss Tanzania, Picha na Father Kidevu

Warembo wa Miss Tanzania, Picha na Father Kidevu

baadhi ya warembo wanao wania taji la Vodacom Miss Tanzania 2008 wakiwa katika picha ya pamoja katika gari ambalo mshindi wa kwanza atazawadiwa. gari hilo Suzuki Grand Vitara linathamani ya sh milioni 42.


Brazili wako Singapore

July 24, 2008
Brazil

Brazil

Nyota wa Brazili Ronaldinho akiwasili kwenye hotel huko Singapore tayari kwa chakula cha mchana leo hii  July 24, 2008. Timu ya Taifa ya Brazil iko Singapore kwa ajili ya matayarisho ya michezo ya Olympic itakayoanza baadaye mwezi ujao huko Beijing China. (AFP PHOTO)


Yanga yatinga Robo Fainali

July 24, 2008

Yaitwanga Vital’O ya Burundi 2-0

Kikosi cha Timu ya Yanga ambacho kiliitoa Kamasi Vital'O ya Burundi, Picha na Mrocky Mrocky

Kikosi cha Timu ya Yanga ambacho kiliitoa Kamasi Vital'O ya Burundi, Picha na Mrocky Mrocky

YANGA imewapa raha Watanzania baada ya kuiadhibu Vital’O ya Burundi kwa mabao 2-0 na kufuzu kuingia nusu fainali ya Kombe la Kagame ambako sasa itakutana na Tusker ya Kenya, kesho.

Tusker, ilifuzu kwa mbinde katika mchezo wa awali ilifuzu kwa hatua hiyo baada ya kuilaza kwa penalti 7-6 Rayon Sports ya Rwanda. Read the rest of this entry »