Blanchard Deplaizir kurekodi na Jay Dee, Ali Kiba pamoja na Akudo

July 23, 2008
Blanchard De Plaizir katika pozi

Blanchard De Plaizir katika pozi

Mwanamuziki anayekuja kwa kasi toka Jamhuri ya Congo Blanchard Deplaizir amesema kuwa yuko katika maandalizi ya kwenda Dar Es Salaam kwa ajili ya kurekodi nyimbo tatu ambazo amesema atafanya kolabo na wanamuziki wa Kitanzania. Blanchard ambaye anapiga muziki wenye mahadhi ya Rhunba, na hata Rap pia maskani yake yako jijini London baada ya kuhamia huko yapata miaka 20 iliyopita na shughuli zake za kimuziki anaziendeleza huko.

De Plaizir akiwa na kikosi chake mbele ya mashabiki lukuki nakati ya Londone.

De Plaizir akiwa na kikosi chake mbele ya mashabiki lukuki nakati ya Londone.

Akiwa Tanzania Blanchard atafanya kolabo na Ali Kiba, Lady Jay Dee na Akudo ili kuweka vionjo vya muziki wa Africa Mashariki hasa Tanzania ambao anasema kwa kiasi kikubwa anauhusudu sana.

Akiongea na Spoti na Starehe jioni hii Blanchard alisema, “nimeongea na Meneja wa Lady Jay Dee Gadna Gee Habash, kimsingi wamekubaliana na terms na nia yangu nafikiri safariitakuwa mwezi wa nane au hadi wa tisa”

“Nimesikia nyimbo za Akudo nimewapenda sana wanaimba vizuri nafikiri safari yangu itakuwa na mafanikio huko” aliongeza Deplaizir.

Aidha kwa sasa Blanchard anasema anafanya kazi na Bongo Dj, timu ya madj watanzania walioko nchini Uingereza ambao ni mabingwa wa matamasha kwa wanamuziki toka Afrika hasa Tanzania, katika mwezi ujao Blanchard atafanya maonyesho mawili yaliyoandaliwa na Bongo Family/DJ tarehe 22 atakuwa reading na tarehe 23 watafanya Milton Keynes, hii yote ni live band akishirikiana na akina dada mastage shoo wake.

Katika Albamu yake ya sasa Blanchard alishirikisha watu mbalimbali akiwemo Titina Alcapone ambaye alipata kuwa mwanamziki wa Wenge BCBG kwa muda mrefu kabla ya kwenda kwa Koffi Olomide na kisha kutoka kivyake.


TID aswekwa Segerea!

July 23, 2008
TID

TID

MSANII maarufu wa muziki wa kizazi kipya (Bongofleva), Khalid Mohamed maarufu kama T.I.D jana amehukumiwa kutumikia kifungo cha mwaka mmoja jela kufuatia kupatikana na hatia ya kushambulia na kujeruhi.
T.I.D mwenye umri wa miaka 26 alisomewa adhabu yake hiyo na Hakimu Hamisa Kalombola wa Mahakama ya wilaya ya Kinondoni baada ya Hakimu huyo kuridhika na ushahidi ulitolewa na mashahidi wanne walioletwa mahakamani na upande wa mashtaka.
katika utetezi wake TID aliiomba mahakama imhurumie kwani alitenda kosa hilo sababu ya ulevi na kuwa familia yake inamtegemea hasa mama yake.
Hata hivyo Hakimu Kalombola alitoa hukumu hiyo kwa kumwambia mshtakiwa “kwa vile huwezi kujimudu ukilewa na huwezi kujizuia kunywa na kuhukumu uende jela mwaka mmoja ujifunze ili usiwe unakunywa hizo pombe” Read the rest of this entry »


Asha Baraka aja kivingine

July 23, 2008

Mkurugenzi wa Kampuni ya African Stars Entertainment Tanzania (ASET) Asha Baraka (kulia) Akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo juu ya kuanzishwa kwa bendi yake mpya itakayofahamika kama Vibration Sound.Kushoto kwake ni Eriston Angai (kiongozi wa bendi hiyo) na anayefuatia ni mwimbaji wa bendi hiyo Dispatch. PICHA NA GPL


Kaijage unawaona wanabadilishana jezi hawa!!!?

July 23, 2008
South Africa Jana

South Africa Jana

Mchezaji wa Manchester United Wayne Rooney (L) akibadilishana Jezi na mchezaji wa Orlando Pirates ya Afrika ya Kusini and Fraizer Campbell (R) mara baada ya mechi yao huko Durban jana July 22, 2008. Manchester United walishinda kwa goli 1-0. Tukio hili linanikumbusha tukio la hivi karibuni ambapo mchezaji wa timu ya Taifa ya Tanzania alidaiwa kulipa jezi na uongozi wa TFF kwa kubadilishana na Samuel E’too kwenye mchezo wao na Cameroon, lakini baadaye Kiongozi mkuu wa TFF Leodgar Tenga alitoa ufafanuzi na kumaliza sitashiriki ya msuguano huo (AFP PHOT).


Simba yaipiga STOP APR! Mtihani mgumu kwa watani zao Yanga leo

July 23, 2008

Na Sophia Ashery wa Majira

Wachezaji wa Simba ya Dar es Salaam wakishangilia baada ya kuifunga 2-0 timu ya APR ya Rwanda katika michuano ya Kombe la Kagame, jijini Dar es Salaam Jumanne

Wachezaji wa Simba ya Dar es Salaam wakishangilia baada ya kuifunga 2-0 timu ya APR ya Rwanda katika michuano ya Kombe la Kagame, jijini Dar es Salaam Jumanne

“BADO Yanga..bado Yanga,” hivyo ndivyo walivyokuwa wakiimba baadhi ya mashabiki wa timu ya Simba ya Dar es Salaam, baada ya timu yao kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya APR ya Rwanda.

Yanga ambao ni watani wa jadi wa Simba wanajitupa kwenye uwanjani leo kuikabili Vital’O ya Burundi katika mchezo mwingine wa robo fainali ya michuano hiyo utakaofanyika uwanja huo huo wa Taifa, Dar es Salaam.

Ushindi huo wa Simba umeiwezesha kutinga nusu fainali ya michuano hiyo, lakini pia umeifanya iivue ubingwa APR moja ya timu zilizokuwa zikiogopwa katika mashindano ya mwaka huu na iliyokuwa ikipewa nafasi kubwa ya ubingwa. Read the rest of this entry »


Rogert Hega naye alalamikia Kili Music Award

July 23, 2008
Rogert Hega Katapila

Rogert Hega Katapila

Mwanamuziki mahiri wa bendi ya TOT Respect Rogert Hegga “Katapila” ameibuka na kuungana na wadau wengine wa muziki kuziponda tuzo za kili Music Award kwa kuwataka wandaaji kuwa Makini wakati mwengine wakiandaa ili kupata washindi wa kweli.

Akiongea na Dar411 mapema jijini Rogert alisema inaelekewa waandaji wa tuzo hizo hawana uzoefu na mambo ya muziki kwa jinsi wanavyoyaendesha mashindano hayo hii inatia mashaka kuamini ujuzi wao katika fani hiyo.

“Mimi nimeshangazwa na kitendo cha waandaji kuweka wasanii katika orodha bila ya wao kujuwa kwa mfano T.I.D aliwekwa katika orodha bila ya yeye kujuwa na mbaya zaidi wakamnyima ushindi” alisema Katapila

Alizidi kuongeza kwa kusema kuwa ingekuwa ni jambo la busara kwa waandishi hao kuwashirikisha wananchi katika kuandaa tuzo hizo ili uwazi uwepo katika kuchagua washindi.

Aidha alisema kama waandaji hawatabadilika na kuzingatia vitu muhimu na vya msingi basi kazi hiyo itakuwa imewashinda na hakuna kamwe atakaiweza zaidi ya marehemu Dandu mwanzilishi mwenyewe.

Kwa kutoa malalamiko yake hayo Dandu atakuwa amejiunga na wadau wengi wa muziki ambao kwa siku za hivi karibuni wamekuwa wakitoa lawama kutokana na tuzo hizo

Tuzo za Kili Music zilianzishwa mwaka 2000 na Marehemu James Dandu zikijulikana kwa jina lake ila zilibadilishwa na mpaka leo hii sababu ya kubadili jina haijulikani.