Man na Orlando Pirates uwanjani leo Durban Afrika ya Kusini

July 22, 2008
Man U

Man U

Captain Rio Ferdinand wa Manchester United , wa tatu toka shoto, akiwaongoza wenzake kwenye mazoezi katika uwanja wa ABSA Stadium huko Durban, South Africa, jana jioni, July 21, 2008, Timu ya Manchester United leo inacheza na Orlando Pirates ya Afrika ya kusini kwenye mechi Vodacom Challenge.


Brazil yamtema Robinho kikosi cha Olympic

July 22, 2008
Robinho

Robinho

Mchezaji wa Timu ya Taifa ya Brasil na Real Madrid ya Hispania Robinho jana ametemwa kwenye kikosi cha timu ya Taifa kitakachokwenda kwenye ngija ngija za kuwania medali ya dhahabuu kwenye michezo ya Olympic huko China imefahamika leo.

Sababu za kumtema Robinho zimesemwa kuwa ni kutokana na machezaji huyo kuwa majeruhi kwa mujibu wa daktari wa timu ya Real Madrid.

Hata hivyo Shirikisho la soka la nchini Brazili limelaani uamuzi wa Real Madrid na kuuita wa dharau kwa nchi yao na wabrazili kwa ujumla kwa kusema hizi ni njama za kutaka kumtumia mchezaji huyo. akizungumzia sakata hilo, daktari wa timu ya Brazili Luiz Alberto Rosan alisema kuwa alijua kuwa Robinho ni majeruhi lakini bado alikuwa na nafasi ya kupona kwani aliumia kidogo sio vya kumfanya ashindwe kucheza kwa muda mrefu. Aidha akiongea juu ya sakata hilo Robinho mwenye miaka 24 anayecheza nafasi ya forward alisema kuwa amesikitishwa na kuikosa nafasi ya kuichezea timu yake kwenye mashindano muhimu ya Olympic huko Beijing.

Akizungumzia suala hili agent wa Robinho Wagner Ribeiro alisema sijawahi kumuona Robinho aliwa na huzuni kiasi a hiki, mara ya mwisho ni kipindi mama yake mzazi alipotekwa nyara na maharamia mwaka 2004. ingawa baadaye aliachiwa bila kudhuriwa.


10 Kuunda timu ya Taifa ya Pool

July 22, 2008
Mtanange wa Ubingwa wa Pool ukiendelea, Picha na Michuzi

Mtanange wa Ubingwa wa Pool ukiendelea, Picha na Michuzi

Kikosi cha wachezaji 10 watakaounda kikosi cha awali cha Timu ya Taifa ya Mchezo wa Pool ya Tanzania kilitarajia kuingia kambini jijini Dar es Salaam jana kwa ajili ya kujiandaa na michuano ya dunia. Michuano hiyo ya dunia imepangwa kuanza Agosti 16 hadi 23 Ezulwini, Swaziland

Mwenyekiti wa Kamati ya Mchezo wa Pool Taifa, Isaac Togocho alitangaza majina ya wachezaji hao baada ya kukamilika michuano ya Taifa katika Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam juzi. Togocho alisema wachezaji hao 10 wanaounda Kikosi hicho cha awali cha Taifa baadaye watapunguzwa hadi kufikia watano ambao wataiwakilisha Tanzania Swaziland.

Aliwataja wachezaji hao kuwa ni Francis Christopher ‘Dogo’, Iddi Abbas na Robert Mgassa kutoka klabu ya mchezo huo ya Shoko ambayo katika fainali za juzi ilitwaa ubingwa wa taifa na kuzawadiwa kitita cha Sh milioni 2.5. Wengine ni Omary Obiara, Rajabu Matumla, Ismail Jumanne (Topland), Rahim Kajuna (Bashnet), Omary Akida (Twiga) Mohamed Jumanne (Royal Mwanza) na Cornel Michael kutoka klabu ya Central Market ya Arusha. (Habari hizi kwa mujibu wa Habari Leo la Leo)


Insha

July 22, 2008
Sadr Iraq

Sadr Iraq

Picha hii iliyopigwa na Hadi Mizban wa AP huko Sadr Iraq mwaka jana, ikimuonyesha mtoto wa Iraq akiwa na toy yake ya RPG (Rocket-Propelled Grenade launcher) akicheza mitaani. Picha hii ndiyo imetumika kwenye shindano la Insha la Wanafunzi wa Sekondary kwa mwaka huu. Wanatakiwa kuandika Insha yenye maneno elfu tatu kwa kuangalia tuu picha hii, Shindano hilo ambalo limeandaliwa na shirika lisilo la kiserikali linalojishughulisha na haki za watoto wa Kiislamu-Malaysia, na kudhaminiwa na Kampuni ya mafuta ya Petronass ambapo mshiriki hutakiwa kufanya presentation mbele ya majaji na kuulizwa maswali hii ni katika kuhakikisha alichoandika je anakijua? aidha mshindi atapata Scholarship ya kusomeshwa Chuo kikuu. Nambie wewe ungeandika nini hapa?


Kuelekea Olympic

July 22, 2008
Kichaka cha madish

Kichaka cha madish

Kuelekea michezo ya Olympic wananchi wengi wa Asia wamekuwa wakinunua Dish kwa ajili ya kuona michezo hiyo Live kwenye Luninga zao, Pichani ni Dish za Astro (DSTV ya huku) kama nilivyopiga hii ni jirani na nyumba ninayokaa ambapo kwa sasa kuna punguzo hakuna gharama ya kuweka/Kununua ila yapasa ulipe miezi mitatu ambapo ni Ringit 72 kwa mwezi sawa na Tsh. 23,000 hii ni package ambayo inakuwezesha kuona Channel 42 zikiwezo zote za michezo, Za wanyama, Habari, za watoto na Cinema, Mwee DSTV wahurumieni wa nyumbani jamani