Kwa wapenzi wa wanyama tuu

July 21, 2008

Battle at kruger-Winner! YouTube’s Best Eyewitness Video 2007.

David “Buzz” Budzinski na Jason Schlosberg walipokuwa wakipiga video hii katika mbuga ya wanyama ya Kruger iliyopo Afrika ya Kusini, watalii hawa hawakutegemea kama siku moja itakuja kuwafanya wawe matajiri, Video hii yenye dakika 8 na sekunde 24 tu ndio imekuwa Video inayoangaliwa mara nyingi kwenye mtandao maarufu wa Youtube ikiwa imeangaliwa mara Milioni 35,307,170 mpaka ninapoandika habari hii ikiwa ni katika kipindi cha mwaka mmoja.

Video hii inahusu kundi la simba na kundi la nyati walivyofarakana na kwa wakati mwingine Mamba pia aliingilia, Video hii ilipigwa na David “Buzz” Budzinski na Jason Schlosberg walipokuwa kwenye matembezi yao ya utalii, na mara walipoiweka kwenye mtandao wa You tube ilipata umaarufu hadi kufikia kutajwa kwenye shindano la Youtube Video of the Year katika kundi la Eye Witness kwa mwaka jana na ikashinda kwa kura nyingi ambapo watazamaji ndio waliokuwa wakipiga kura online.

Baadaye September mwaka jana waandaaji wa kipindi maarufu cha National Geographic ambacho kunarushwa na DSTV, ASTRO na Stesheni nyingine kiliwapeleka David “Buzz” Budzinski na Jason Schlosberg huko Kruger National Park Afrika ya kusini ili kutengeneza Makala (Documentary) ya tukio hilo ambalo baadaye lilirushwa hewani kwenye Stesheni ya National Geographic Channel siku ya Mother’s Day, May 11, 2008, saa 9pm EST. Kipindi ambacho kinakadiriwa kilitazamwa na watu zaidi ya milioni 50 kwa siku hiyo ya kwanza.

Baada ya hapo ilibidi kampuni nyingine kununua leseni ya kuonyesha ama picha za mnato au za video kwa ajili ya kuonyesha tukio hili ambalo wengi wetu unaweza kuona ni la kawaida kabisa. Kwa habari zaidi waweza soma hapa

Bonyeza kitufe cha player upate kuiona video hii.


Chelsea kucheza na Guangzhou Pharmaceutical keshokutwa

July 21, 2008
Chelsea

Chelsea

GUANGZHOU, CHINA – JULY 21: Wachezaji wa Chelsea (L-R) Petr Cech, John Terry na Kocha Luiz Felipe Scolari wakiongea na waandishi wa habari jioni ya leo (ikumbukwe huku tuko masaa matano mbele ya masaa ya nyumbani Tanzania) kuhusu ziara yao ya nchi za Asia ambapo keshokutwa watacheza mechi Guangdong Olympic Stadium na klabu ya Guangzhou Pharmaceutical (Photo:MN Chan/Getty Images)

Scolari shoto na Lampard.

Scolari shoto na Lampard.

Pichani ni Phillipe Scolari akiwa na Lampard wakati wa mazoezi mepesi jioni hii huko Guangzou China, Kocha Scollari amewathibitishia washabiki kuwa Lampard amemuhakikishia kuwa hatoondoka Chelsea ana atamaliza msimu na ikiwezekana ataongeza mkataba. Natumai hizi ni habari njema kwa mpenzi mkubwa wa Chelsea Yassin Mkalimoto wa Mkurugenzi wa YAATE Investments Sinza madukani.


Chelsea yaja bila Drogba

July 21, 2008
Moja ya matangazo ya Chelsea nchini China ambapo inasema mashabiki toka miji tofauti watasafiri hadi jimbo la Guanzou kuweza kushuhudia timu hiyo. Ligi ya Uingereza inawapenzi wengi sana bara Asia

Moja ya matangazo ya Chelsea nchini China ambapo inasema mashabiki toka miji tofauti watasafiri hadi jimbo la Guanzou kuweza kushuhudia timu hiyo. Ligi ya Uingereza inawapenzi wengi sana bara Asia

Timu ya soka ya Chelsea inatuaa China jioni hii ikiwa na wachezaji wote mashuhuri isipokuwa Drogba.

Drogba ambaye ameumia mguu na yuko kwenye matibabu kwa sasa amekumbwa na lawama za kutaka kutoka kwenye klabu hiyo jambo ambalo mashabiki na viongozi hawalifurahii, hii inafuatia pia habari zilizosemwa kuwa Drogba hakufurahia kitendo cha klabu yake kukataa ofa ya Barcelona ya kubadilishana na E’too jambo ambalo yeye Drogba alikuwa yuko tayari.

Akiongea na waandishi wa habari kocha mgeni wa klabu ya Chelsea Phillipe Scollari alisema kuwa ataitumia ziara hii ya Asia ambayo itawapeleka China, Vietnam na Kuala Lumpur Malaysia kuijenga timu yake kuwa tayari kwa kindumbwe ndumbwe cha ligi kuanzia baadaye mwezi ujao.

Timu ya Chelsea itakuwa hapa Malaysia kwa mechi ambayo imepangwa kuwa katika uwanja wa Shah Alam tarehe 29 ambapo itacheza na timu ya taifa ya Malaysia katika mechi ya kirafiki, Tiketi kwa ajili ya mchezo huo sehemu mbali mbali zilikuwa zimemalizika na mashabiki wengi kulalamika kulanguliwa kwani Bei za awali ni Ringiti 30 kwa wanafunzi (sawa na Tsh. 10,000) na ya juu kabisa ni Ringit 103 (sawa na Tsh 33,000).


Maximo kuelekeza nguvu Kombe la Mataifa ya Afrika

July 21, 2008

KOCHA wa Taifa Stars, Marcio Maximo amesema hatawatumia wachezaji Danny Mrwanda na Erasto Nyoni kwenye mechi zilizobaki za kufuzu kucheza fainali za kombe la Dunia 2010.

Stars yenye pointi mbili kwenye kundi la kwanza linaloongozwa na Cameroon yenyev pointi 10, imesaliwa na mechi mbili dhidi ya Cape Verde na Mauritius na haina nafasi ya kusonga mbele.

Maximo alisema jijini Dar es Salaam juzi kwamba kwa hali ilivyo sasa atatumia michezo hiyo kwa ajili ya kuisuka zaidi timu yake kwa michezo miwili ya mwisho dhidi ya Sudan ya kufuzu fainali za kombe la Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani.

“Sitawatumia hao wachezaji wa nje ili kutoa nafasi kwa hawa wachezaji wa ndani ambao ndio wana kazi kubwa sasa kwenye mechi dhidi ya Sudan, nataka mpaka Novemba niwe na kikosi imara zaidi,”alisema Maximo ambaye alikuwa mapumziko Brazil.

“Nimewahi kuja ili niangalie haya mashindano ya Kagame yanayoendelea ninaamini timu zilizokuja ni ngumu na naweza kupata nafasi ya kuwaona zaidi wachezaji wa hizi klabu za Simba, Yanga na Miembeni,”alisisitiza Maximo ambaye klabu ya Yanga imepanga kumuuza kwa St.Georges ya Ethiopia kipa wake namba moja, Ivo Mapunda.

“Nataka kuangalia ni nani naweza kumuongeza kwa ajili ya kuisadia timu kwenye mechi zetu na Sudan Novemba, ndio kazi kubwa iliyobaki mbele yetu, pamoja tutafika,”alisema Maximo ambaye timu yake iliingia kwenye nafasi hiyo baada ya kuzitoa Uganda na Kenya.

Mrwanda anacheza kwenye klabu ya Al-tadhamon ya Kuwait huku Nyoni akiichezea Vital’o ya Burundi ambayo jana jioni ilikwaana na Simba kwenye michuano ya Kagame inayoendelea jijini Dar es Salaam.

Endapo Stars itaipata sare au kuifunga Sudan ugenini itakakoanzia na kushinda mchezo wa marudiano kwenye uwanja wa Taifa itafuzu kucheza fainali za michuano hiyo mipya, Januari mwaka nchini Ivory Coast.


Masikini Ronaldo

July 21, 2008
Masikini Ronaldo
Masikini Ronaldo

Timu ya Manchester United imemwambia mchezaji wake Cristiano Ronaldo kuwa hakutakuwa na mabadiliko yeyote yamshahara kutegemeana na deal ya kwenda Real Madrid kutofanikiwa, Real Madrid ambao walikuwa wameweka dau kubwa kwa Ronaldo ambaye aliwekewa ngumu na timu yake, wamesema kuwa walitaka kumsajili Ronaldo na walikuwa tayari kumpa mkataba mnono lakini kama imeshindikana basi ni heri akabaki huko.

Kwa kiasi fulani Manchester hawakupendelea kitendo cha Ronaldo kutoficha hisia zake kuhusu hamu yake ya kujiunga na Real Madrid na wao wameichukulia hii kama ilikuwa njama ya Ronaldo kuongezwa mshahara alisema Mkurugenzi Mkuu wa klabu hiyo David Gill.

Aidha Gill alisema kuwa Ronaldo atabakia kwenye mkataba wake wa awali wa dila 240,000 kwa wiki ambao bado una miaka minne kumalizika.


‘The Dark Knight’ yavunja rekodi ya $155.34M kwa weekend ya kwanza

July 21, 2008

Kwa wapenzi wa Cinema hapa tuko pamoja, Cinema ya The Dark Knight ambayo ndio ilitoka kwa weekend hii ilivunja rekodi kwenye majumba ya Cinema kwa kuingiza jumla ya dola $155.34 million katika weekend ya kwanza kwa siku ya jumamosi ukilinganisha na ile ya “Spider-Man 3″ ambayo ilitoka mwaka jana iliingiza $151.1 million.

Mapato haya yanatazamiwa kuongezeka na kufikia Dola $253 million kwa hizi siku tatu za weekend (Ijumaa, jumamosi na Jumapili) na kuvuka rekodi ya Spider Man 3 kwani ilipata $218.4 million.

Kwa huku Malaysia tiketi kwa ajili ya onyesho la Cinema hii zimeuzwa zote hadi weekend ijayo ndio zinaweza waweza kupata nafasi.

Hata hivyo mmoja wa waigizaji ambaye aliigiza kama Joker (mwenye kijamba koti pichani) hatoweza kuona mafanikio ya picha hii kwani alifariki baada ya kumaliza upigwaji wa picha hii na ikiwa studio inatengenezwa, Heath Ledger alifariki mapema mwaka huu kwa kile Polisi walichosema kuzidisha dose ya madawa ya Kulevya aliyokuwa akitumia. Bwana Heath Ledger ambaye wakani anafariki jina lake lilikuwa kwenye list ya watu walipendekezwa kwa ajili ya Academy Award.

Pata Trailer ya picha hii kwa kubofya hapa.


Makamuzi ya Ziff

July 21, 2008
Prof. Jay akifanya vitu vyake jukwaani katika tamasha la Ziff

Prof. Jay akifanya vitu vyake jukwaani katika tamasha la Ziff

Vijana wa THT wakifanya vitu vyao katika Tamasha la Ziff, ikumbukwe kuwa huku THT ndi hata Hafsa Khazinja alikotokea.

Vijana wa THT wakifanya vitu vyao katika Tamasha la Ziff, ikumbukwe kuwa huku THT ndi hata Hafsa Khazinja alikotokea.

Mwanamuziki Khamis Mwinyijuma au Mwana FA akiwa jukwaani katika tamasha la Ziff

Mwanamuziki Khamis Mwinyijuma au Mwana FA akiwa jukwaani katika tamasha la Ziff

Kadri siku zilivyokuwa zikienda ukingoni ndio Tamasha la Ziff lilizidi kunoga, Pichani wadau na nguli wa burudani wakifanya vitu vyao. (Picha kwa hisani ya Haki Ngowi/Peter Benedict)


Twatoka migodini…

July 21, 2008
Daimondo

Daimondo

Wanamuziki wa bendi ya dansi ya Diamond Musica wakiwa Uwanja wa Ndege wa zamani mara baada ya wanawasili jijini Dar es Salaam wakitokea katika mgodi wa wa dhahabu wa Tulawaka uliyoko Wilayani Kahama ambako walienda kufanya onyesho. (Picha na Issa Mnally wa GPL)