Yasemavyo magazeti michezoni jumapili hii.

July 20, 2008

Chelsea kumchukua Kaka kwa dau la kuvunja rekodi ya mwaka!

July 20, 2008
Kaka huenda akaenda Chelsea

Kaka huenda akaenda Chelsea

LONDON: Mchezaji wa AC Milan nyota Mbrazili Kaka anakaribia kutua kucheza English Premier League kwa klabu ya Chelsea kwa kile kinachosemwa rekodi ya dunia ya uhamisho ya Paund £80milioni (sawa na 100mil euros), alisema mshauri wa Kaka jana.

Kama kaka ataondoka itakuwa pigo kwa mshambuliaji Ronaldinho ambaye alisema amefurahi sana kucheza timu moja na Kaka na ni katika vito vilivyomfanya asisite kuhamia timu hiyo ni kuwepo kwa Kaka. na msemaji wa Kaka ambaye ni Meneja wake binafsi Diogo Kotscho aliongeza kuwa pande zote mbili ziko tayari kumaliza deal hiyo na kuifanikisha.

“Real Madrid walitaka kutoa euro 90milioni msimu uliopita kwa mchezaji Kaka lakini Milan hawakuwa tayari kumuachia kwa wakati huo, alisema” Kotscho akiongea na gazeti la The Guardian.

“Wakati huu ni tofauti na nafikiri huu ni muda muafaka wa kufanya hii deal, ni wakati pekee tunafikiri huu mpango twaweza ufanikisha na hii ni kwa sababu ya hali ya kifedha iliyopo klabuni hivyo ni muda muafaka kumalizana na jambo hili”.

Kama Kaka atakwenda Chelsea basi mashabiki wanaipa nafasi kubwa kwa kampeni yake ya kuchukua vikombe vyote viwili ambao ndio mission ya mmiliki wa klabu hiyo alipomkabidhi jahazi Philipe Scollari.

Wakati huo huo Chelsea imekataa mpango wa Real Madrid wa kubadilishana Samuel E’too na wao wamtoe Didie Drogba. HAbari kamili inakuja.


Maharamia ya Kinigeria yamuachia kakae Joseph Yobo

July 20, 2008
J.Nobo

J.Yobo

Maharamia waliokuwa wakimshikilia kaka wa mchezaji wa Everton na Nigeria defender Joseph Yobo baada ya wiki mbili na mashaka.

Norum Yobo alitekwa nyara na maharamia watatu waliokuwa na silaha tangu July 5 mwaka huu wakati Norum alipokuwa akitoka klabu kujivinjari na wenzie kwenye klabu ya usiku huko Port Harcourt, Rivers State, Nigeria.

Noram aliachiwa juzi tarehe 17 July baada ya siku takriban 12, kuachiwa kwa Norum kumethibitishwa na kumethibitishwa na John Ola Shittu ambaye ni meneja binafsi wa Joseph. hata hivyo Shitu aligoma kueleza endapo kuna pesa yeyote au makubaliano yaliyofikiwa mpaka kumuachoa Norum, Maharamia wa Nigeria ni kawaida yao kuwateka nyara ndugu vipenzi wa watu mashuhuri (Celebrities) au yeyote mwenye pesa na kuitisha kiasi kikubwa cha pesa kbla ya kumuachia.


LIVERPOOL yatoka droo na WISLA KRAKOW

July 20, 2008
.

.

Kocha mkuu wa Liverpool Rafael Benitez toka Spain, kulia akitoa maelekezo kwa mchezaji wake Emiliano Mascherano wakati wa mechi ya kirafiki kati ya Liverpool na Wisla Krakow toka Poland, ilofanyika Fribourg, Switzerland, jana jumamosi, July 19, 2008, Mchezo uliisha kwa droo ya 1-1 ambapo goli la Liverpool lilipatikana dakika ya sita ya mchezo kupitia kwa Andriy Voronin, goli la Liverpool halikudumu kwani dakika sita baadaye Wisla Krakow waliweza kusawazisha kupitia kwa Tomas Jirsak na kumuacha kipa Cavalieri asijue la kufanya, mpaka mwisho babao ni 1-1 (AP Photo).