Diabate azidi kukonga nyoyo za mashabiki

July 19, 2008
Picha mwanana ilopigwa na Mpiga picha maarufu Michuzi, ikimuonyesha Diabeta wakati wa Tamasha la Ziff mapema wiki hii.

Picha mwanana ilopigwa na Mpiga picha maarufu Issa Michuzi, ikimuonyesha Diabate wakati wa Tamasha la Ziff mapema wiki hii.

Baada ya kujifua kwa siku tatu na Watanzania waishio Bara, Kundi la Wazee Sugu, mcharaza gita maarufu wa Guinea Sekou Bembeya Diabate aliwaliza wapenzi wa muziki wakati alipotumbuiza kwa mara nyingine katika ukumbi wa Mambo Club.

‘Mchawi’ huyo wa gitaa ambaye alitumbuiza siku ya kwanza ya tamasha la ZIFF akiwa peke yake na kuwafanya watu wachanganyikiwe kwa furaha kutokana na nyuzi zilivyokuwa zikikamatwa kiustadi, juzi aliwafanya wapenzi wa muziki wa dansi kutambua kwamba lugha si tatizo, tatizo ni muziki.

Akiwa na kundi zima la King Kiki (wazee sugu), Diabate ambaye ni gumzo katika anga za muziki wa kimataifa, aliwaonyesha wapenzi wa muziki nchini Tanzania kuwa wanaweza kwenda pamoja naye katika burudani.

Akiwa anacharaza kwa mfumo wa Mande na jazi, Diabate ambaye anajulikama kama mtu mwenye vidole vya kito cha almasi, aliwadhihirishia Watanzania kwamba anapoitwa yeye kama kisasili cha gita la Afrika Magharibi, si kumkweza.( Habari hii ni kwa mujibu wa Beda Msimbe, Zanzibar, Habari Leo) Pata Kionjo toka kwa Diabate akiwa na bendi yake ya Bembea Jazz, Hii ilikuwa katika Tamasha la African Festa 2008, huko Yokohama Japan mwaka huu.


Serikali kuwasomesha mashujaa wa Brazil

July 19, 2008

Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda akijadili jambo na Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo Mh. George Mkuchikaijamsikia tena, katika hafla aliyoawaandalia vijana wa Under 17 kuwapongeza.

Waziri Mkuu Mizengo Pinda amesema serikali itasaidia kuwasomesha wachezaji wa timu ya soka ya vijana chini ya miaka 17, iliyotwaa ubingwa wa Kombe la Copa Coca-Cola nchini Brazil wiki iliyopita. Read the rest of this entry »


Enyimba yalowa kwa Al Hilal 3-2

July 19, 2008

Goli la dakika za mwisho la toka kwa Ifeanyi Onigbo liliipa Al Hilal ya Sudan ushindi dhidi ya Enyimba ya Nigeria kwenye mchezo wa fungua dimba kwenye makundi kwa ajili ya michezo ya Kombe la mabingwa 2008.

Enyimba ndio walioanza kuliona lango la wapinzani wao kupitia kwa Cletus Itodo mnamo dakika ya 35 ya mchezo kipindi cha kwanza. lakini goli hilo halikudumu sana kwani Al Hilal walisawazisha dakika tano baadaye kwa mkwaju wa Penatiuliopigwa na captain Haitham Mustafa na kufanya mabao kuwa 1-1.

Yousuf Mohamed alipachika goli kwa upande wa Al Hilal dakika moja kabla ya mapumziko kufanya Alhilal kuongoza kwa 2-1.

Stephen Worgu wa Enyimba alisawazisha na kufanya 2-2 dakika ya 86, kabla ya mchezaji wa Al hilal anayetoka Nigeria Onigbo, kufunga bao la ushindi kwa timu yake.

Leo jumamosi Coton Sport ya Cameroon inawakaribisha  TP Mazembe toka DR Congo kwenye mechi za kundi B.