
.
Start Time: Friday, July 18, 2008 at 9:00pm
End Time: Saturday, July 19, 2008 at 4:00am
Location: Klubi Tampere
Street: Tullikamarin aukio 2, Tampere
City/Town: Tampere, Finland
Phone: 358449571438
Email: www.festafrika.net

.
Start Time: Friday, July 18, 2008 at 9:00pm
End Time: Saturday, July 19, 2008 at 4:00am
Location: Klubi Tampere
Street: Tullikamarin aukio 2, Tampere
City/Town: Tampere, Finland
Phone: 358449571438
Email: www.festafrika.net

.
Mchezaji mpya wa Barcelona Alexander Hleb (L) akiwa na Rais wa Barcelona Joan Laporta wakiwa wameshikilia Picha ya kikaragos kinachomuonyesha Hleb na ngao mpya ya BArcelona hapo jana July 16, 2008, Nou Camp stadium huko Barcelona wakati Raisi huyo alimpomtambulisha mchezaji huyo kwa wanahabari na wapenzi wa Barca, Hleb amejiunga na mabingwa hawa wa Catalan timu ya Barcelona akitokea timu ya Arsenal ya Uingereza kwa kitita cha Euro 15million katika mkataba utakaodumu kwa miaka minne ambao utamkutanaisha na mkongwe mwenzie toka washika bunduki hao Thierry Henry. (AFP PHOTO)
TFF jana ilitangaza mapato ambayo yalipatikana kwenye ufunguzi wa michuano ya Tasker kati ya mechi za timu za Simba na Tusker ya Kenya na ile ya mahasimu wao Yanga na APR ya Rwanda.
Akitangaza mapato ya mechi ya ufunguzi, Dar es Salaam, jana ambayo ilizikutanisha Simba na Tusker ya Kenya, Katibu Mkuu wa TFF, Fredrick Mwakalebela, alisema zilipatikana sh. milioni 79.6, ambapo watu 18,420 walilipa kiingilio.
Alisema mechi kati ya Yanga na APR ya Rwanda iliyochezwa Jumapili katika uwanja huo zilipatikana sh. milioni 95 kutokana na watu 23, 719 kulipa viingilio, ambavyo vilikuwa sh. 25,000, sh.20,000, sh. 15,000, sh.10,000, sh.7,000, sh.5,000 na sh.3,000.
Wachunguzi wa mambo ya kispoti wanasema kuwa hii inaonyesha umaarufu wa timu ya Yanga umeongezeka kulinganisha na Simba, na huenda ikatokana na usajili wa Timu ya Yanga ambapo Kusajiliwa kwa kipa Juma Kaseja kumefanya mashabiki wa Mpira kutaka kumuona awapo uwanjani.
Katika mtanange huo wa Yanga na APR mashabiki walilipuka pale KAseja alipokuwa akiingia n wachezaji wenzie uwanjani na kuwa akishangiliwa kila awapo na mpira na mashabiki wa Simba walisikika wakimzomea na kumtupia maneno ya kejeli ingawa hayakufua dafu kutokana na mashabiki wa Yanga kuwa wengi na wenye nguvu zaidi.
Aidha Mwakalebela alisema kuwa kutokana na mwamko uliooneshwa na mashabiki wa mpira wa miguu, mechi za kukamilisha mzunguko wa kwanza ambazo zilipangwa kuchezwa katika Uwanja wa Taifa zamani sasa zitachezwa Uwanja Mkuu wa Taifa.
Fainali za mchezo wa Pool wa Safari Lager Pool zitafanyika jumapili wiki hii katika ukumbi wa Diamond Jubilee kwa kushirikisha Timu za mkoa wa Dar Es Salaam na timu nyingine za mikoa ya Tanzania Bara.
Timu hizo zimeshawasili jijini Dar Esalaam tayari kwa ajili ya michuano hiyo ambayo maandalizi yake yameshakamilika. Mgeni rasmi atakuwa Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Leonard Thadeo.
Akiongea na waandishi wa habari Meneja wa bia ya Safari kutoka Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) ambao ndiyo wadhamini wa michuano hiyo, Fimbo Batullah alizitaja timu zitakazoshiriki michuano hiyo kuwa ni Royal Pub A kutoka Mwanza, Central Maraket (Arusha ), Flamingo (Kilimanjaro), Deluxe (Dodoma), Africana (Mbeya), Member Of family (Tanga).
Na kwa mkoa wa Dar es Salaam wawakilishi ni Top Land Pool Club (Kinondoni), Twiga Pool Club (Ilala) na Bashnet Pool Club (Temeke), wakati wawakilishi wa mkoa wa Mwanza walitarajia kuingia jijini wakati wowote jana, michuano hiyo ambayo inafanyika kwa mara ya kwanza nchini, mbali ya kuwa sehemu ya kuendeleza mchezo huo pia itatumika kuchagua wachezaji watakaounda kikosi cha timu ya Taifa kitakachokwenda nchini Swaziland kushiriki michuano ya mchezo huu kwa Dunia itakayofanyika kuanzia Agosti 16 hadi 23 katika mjini wa Ezulwini.