July 16, 2008
Starehe Mita 1800 juu ya usawa wa Bahari
Sehemu ya Genting kama inavyoonekana jioni, taa zinazoonekana kwa mbali ni mji wa Kuala Lumpur unavyoonekana toka Milima ya Genting.
Panaitwa Genting Highland, Ni umbali wa Kilomita 50 toka Kuala Lumpur mjini kuelekea Genting Highland, sehemu ya milima nchini Malaysia, kwa kawaida Malaysia ni nchi ya joto kama ilivyo Dar Es Salaam lakini tofauti ni kuwa joto la malaysia ni 30c to 36c na Fukuto ila kuna mvua mwaka mzima, wastani wa mvua kunyesha ni kila baada ya siku 2 hadi tatu. Hii hufanya mji huu kuwa wa kijani mwaka mzima lakini huwezi amini kuna sehemu ya Malaysia jotoridi lake ni 12c to 20c na wakati wa baridi hasa kunadondoka barafu, Huku ndio kunaitwa Gentini umbali wa Mita 1800 toka usawa wa bahari.
Huku hasa ni mji wa mapumziko, naita mji kwani panajitosheleza kwa kila kitu kuanzia mahoteli hadi Hospitali ambapo watu hupendelea kwenda kupumzika na kupata starehe mbali mbali kama Cable Car ambazo zina urefu wa Kilomita tatu na nusu, na inapita katikati ya misitu minene ya Tropiki na ubaridi mwanana pia utaona ndege na wanyama kama nyani wakiruka kwenye miti huku ukipita kwenye kijikombe kilichobebwa na mkanda (cable) ambacho kina tembea mwendo wa wastani wa kilomita 10 kwa saa, ni burudani tosha ambayo inahitaji ujasiri kwani kama hujazoea utatamani kushuka.


Safari ndio imeanza ndani ya “Cable Car”
Ndani ya Cable Car kule kwenye ukungu ndio tunakoelekea na ndio raha zote zilipo, kuzifikia sasa kasheshe.
wadau washafika kwenye safari ya mashaka hehehe
Siku yapili “vakesheni” inaendelea
Baadaye unafika Theme Park huku kuna michezo zaidi ya 60 ya kila aina ikiwa ni pamoja na Roller Coaster yenye urefu wa Kilometa moja, Train, Speed Car, Speed Boat, Mashua, Michezo ya Jukwaani, Maonyesho ya Wanyama mbali mbali, Muziki, Vyakula vya kila aina, utamaduni, Bustani ya Ndege, Bustani ya Mamba, Bustani ya Nyoka, kwa ujumla panakufanya ujione uko mahali tofauti.
Live Performances usiku ni sehemu ya starehe za Genting
Pia kuna ukumbi wa Concert mkubwa ambao una uwezo wa kuchukua watu zaidi ya 10,000 na ukumbi huu ni full kipupwe, ambapo wanamuziki maarufu wakija pia hutumbuiza huko.Usiku kuna burudani za aina mbali mbali ikianziwa na sarakasi toka kwa akina dada ambao nadhani hawana mifupa, ije ngoma na utamaduni wa Wamalay (kama taarab) hadi Vikundi vya Kizazi kipya na nyimbo za kimagharibi pia, Kwa ujumla ni raha yaani mpaka unaona unapewa zaidi kuliko gharama halisi.
Mambo ya mwambao hata huku yapo atii
Pia kuna uwanja wa Golf kwa wenye mchezo wao, ambao wengi ni wageni mahoteli zaidi ya 30 yaliyopo kwenye kijiji hiki cha maraha. Mbali na hiyo kuna Casino kubwa, hii ndio Licensed Casino kwa Malaysia na inakusanya wacheza kamali toka Singapore, Malaysia, Indonesia na Brunei ambao wote hufika kucheza kamali hapa.
Leave a Comment » |
Burudani | Tagged: Genting |
Permalink
Posted by piusmickys
July 16, 2008

Jalada la juu la jarida la New Yorker
Kikaragosi kilichotumika kwenye jalada la jarida la New Yorker, kimewakasirisha sio tu Obama na Mkewe bali pia jumuiya za kidini nchini humo. Katika kikaragosi hicho ambacho kinaonekana hapo juu amechorwa Obama katika nguo za kiasili zenye maudhui ya kidini zaidi na mkewe akiwa amevaa bunduki mgongoni huku picha ya Osama Bin Laden ikiwa imetundikwa ukutani na kwa mbali inaonekana bendera ya Marekani ikiwa kwenye tanuri la kuotea moto ikiteketea, Picha hii imetafsiriwa kwa aina mbali mbali na wadau wa habari huku wengi wakisema imedhalilisha dini moja na wengine wakilaumu kitendo cha jarida hilo kumhusisha Obama na ughaidi.
Wakitolea maelezo kuhusu kikaragosi hicho Mhariri wa Jarida la New Yorker alisema nia yao wao ilikuwa ni kusafisha Mind za watu juu ya Uislamu na ughaidi, Je imekaa njema hii?
1 Comment |
Burudani | Tagged: Katuni, Obama |
Permalink
Posted by piusmickys