
Michael Ballack na Clarence Seedorf
Mchezaji wa Ujerumani Michael Ballack (L) na Clarence Seedorf Msuriname mwenye uraia wa Holland wakibadilishana jezi baada ya mchezo wa hisani hapo majuzi tarehe 12 July, Mchezo huu ulishirikisha Nyota wa dunia katika kuchangia Taasisi ya “Goal4Africa” ambayo inatoa misaada mbali mbali kwa nchi za Africa, mchezo uliochezwa huko Allianz Arena stadium, Jijini Munich, kusini mwa Germany, Picha hii inanikumbusha sakata la mchezaji wa Taifa Stars aliyedaiwa Jezi baada ya kubadilishana na mwenzie Samuel E”too baada ya mchezo kuisha, Ingawa Rais wa TFF alitoa ufafanuzi lakini kitendo hicho kililaaniwa vikali na wapenzi wa soka. (AFP PHOTO DDP/PHILIPP)







