Ze Comedy watinga Bungeni

July 15, 2008

Ze Comedy wakiwa katika moja ya maonyesho yao jijini.

Ze Comedy wakiwa katika moja ya maonyesho yao jijini.

Waigizaji wachekeshaji maarufu Ze Comedy jana walivamia ukumbi wa Bunge na kufanya kila mmbunge kutaka kuongea ama kupiga nao picha ya kumbukumbu.

Ilikuwa ni kipindi cha asubuhi cha Bunge kama kawaida Naibu Spika Mheshimiwa Anne Makinda alikuwa akisoma majina ya wageni waliokuwemo ukumbini humo kama ilivyoada na ndipo aliposhtuliwa kuwa miongoni mwa majina aliyosoma ni wanachama wa kikundi cha Ze Comedy na kushtuka na wabunge kulipuka kwa kicheko.

Kwa mujibu wa Naibu Spika kundi hili lilihudhuria kwa mualiko maalum wa wabunge wa majimbo ya mkoa wa Dar Es Salaam.

Nje ya Ukumbi wa Bunge baada ya kipindi cha Bunge cha Asubuhi wabunge na maofisa wengine wa Bunge waliungana kwa pamoja na wasanii hao kwa maongezi ya hapa na pale na kupata picha kadhaa za kumbukumbu, Akiongea na waandishi wa habari kiongozi wa kundi hilo Wakuvanga alisema wameamua kwenda Dodoma ili kujua ni jinsi gain Bunge linafanya Kazi zake.

Miongoni mwa waliokuwepo ni Masanja, Joti, Mpoki na Seki.

Hivi karibuni serikali kupitia Wizara ya habari ilitoa tamko la kuingilia mgogoro uliopo kati ya kikundi hicho na tajiri yao wa zamani EA Television na kuagiza asasi zinazohusika kukaa pamoja na kulitolea maamuzi suala hilo haraka inavyowezekana.
Akiongea bungeni Naibu waziri wa Habari Utamaduni na Michezo bwana Joel Bendera alisema suala hilo limekabidhiwa kwa Chama cha Haki Miliki (Cosota) na kuongeza kuwa mkataba kati ya Ze Comedy na EATV umekwisha na kundi hilo limeingia mkataba mpya na TBC1 lakini wameshindwa kuendelea kwa sababu ya SAGA hilo. Spoti Starehe inawatakia kila la heri.


Ally Remtullah kupamba usiku wa ZIFF Bwawani Hotel Ijumaa

July 15, 2008
Mwanamitindo Ally Remtullah

Mwanamitindo Ally Remtullah

Mwanamitindo anayekuja juu kwa Afrika Mashariki Ally Remtullah atafanya onyesho la Mavazi kwenye Gala Night Dinner siku ya ijumaa tarehe 18 July katika hoteli ya Bwawani.

Katika usiku huo wa kukumbukwa Ally Remtullah atawatumia vijana mamodel toka Zanzibar ikiwa ni jitihada za kukuza vipaji vya wanamitindo toka visiwani. Hii ni moja ya shamra shamra za International Film Festival mwaka huu. Maudhui ya ZIFF mwaka huu ni “Culture Crossroad” ikiwa ni kutaka kuonyesha muingiliano wa kitamaduni katika jamii na Remtullah atathibitisha hilo kwa mavazi ambayo yatakuwa na radha ya kitamaduni zaidi. (Picha na Michuzi)


SAMSUNG Yawaleta Chelsea MALAYSIA

July 15, 2008

Klabu ya soka ya Chelsea ya Uingereza inafanya ziara ya Asia ambapo tarehe 29 July watakuwa Uwanja maarufu wa Shah Alam kwenye mechi ya Kirafiki na timu ya Malaysia mchezo utakaochezwa saa 8.45pm kwa saa za Malaysia ambapo ni saa 3.45 pm kwa saa za Nyumani Tanzania. Tiketi katika mchezo huo zinauzwa kuanzia RM 33 sawa na (10,ooo Tsh) hadi RM 103 (sawa na 30,000 Tsh).

Gonga hapa kukata Tiketi yako


Miss Tanzania EU ajiengua Kinyang’anyiro cha Miss Tanzania

July 15, 2008

Miss Tanzania EU 2008 – LUCY MWIZA FUNDIKIRA amejitoa katika kinyang’anyiro cha Miss Tanzania kinachotarajia kutifua baadaye mwezi ujao jijini Dar Es Salaam.
Akizungumza na wanahabari Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya Lino Agency waandazi wa Miss Tanzania Uncle Hashim Lundenga amesema kuwa walipata taarifa toka kwa muaandaaji wa shindano hilo EU kuwa Miss Fundikira hatoshiriki kwenye kinyang’anyiro hicho bila kusema kiundani sababu hasa za kufikia maamuzi hayo.
Hata hivyo habari zinasema Miss Lucy ni mmoja wa mamiss wanne ambao hawatoshiriki kwenye kinyang’anyiro hicho.
Mrembo namba mbili Kinondoni, Joan Faith pia amejitoa katika shindano na nafasi yake imechukuliwa na Miss Temeke namba nne Lilian Shayo baada ya warembo namba nne na tano wa kanda hiyo kushindwa kufika katika kambi hiyo,” alisema Lundenga.


Prof Jay naye alalamikia Kili Award

July 15, 2008

Mkali wa miondoko ya muziki wa Bongofleva Mc Shupavu a.k.a Pro Jay akijimiminia kinywaji taraatiibu hivi karibuni ndani ya tuzo za Kill music awards huku akiwa amevalia kimasai.Pro Jay nae ameonekana kuzikandia tuzo hizo za 2007 kwa kudai kuwa maandalizi yake hayakuwa ya umakini wa kutosha,kwani aliyestahili kupewa tuzo hakupewa,asiyestaili ndiye aliyepewa tuzo,hali hiyo imekuwa ikiwavunja nguvu baadhi ya wadau na wasanii wenyewe.Kulalamika huko si kwa msanii huyo tu hata Bushoke pia amezilalamikia tuzo hizo kwa kuwa zilikosa umakini, kwani yeye alipewa tuzo ambayo haikuwa sahihii yeye kupewa,kutokana na uugwana alionao, Bushoke akaamaua kuirudisha tuzo hiyo kwa waandaji kwani tuzo hiyo ilipaswa kwenda kwa msanii wa kike nchini Kenya habari hii kwa msaada wa MichuziJr


Uraia wa Avram Grant almanusura ungeikatisha ziara ya Chelsea Malaysia

July 15, 2008

Kuondoka kwa kocha wa Chelsea Avram Grant na ujio wa Kocha mpya F. Scolari kumeokoa Ziara ya klabu ya Chelsea hapa Malaysia ambayo awali ilitishia kuifuta kutokana na Kocha huyo wa Zamani kutoruhusiwa kuingia Malaysia kwa sababu ya uraia wa Israel, Malaysia haina mahusiano yeyote ya kibalozi au kibiashara na Israel kwa vile Malaysia inatambua Taifa la Palestina ambalo ni mahasimu wakubwa wa Islael. Marufuku hiyo isingeishia kwa Kocha Grant pekee bali hata mchezaji Tal Ben Haim ambao kwa pamoja walihitaji kuomba vibali maalum ili kutembelea baadhi ya nchi za Kusini Mashariki mwa Asia. (Habari hii kwa Mujibu wa Aljazeera)


Amigolas ajitoa Twanga Pepeta

July 15, 2008
Mwanamuziki muanzilishi wa Bendi ya Twanga Pepeta Amigolas (Mwenye Miwani) ametangaza rasmi kujitoa katika bendi hiyo ya Twanga Pepeta. Akizungumza jana mwanamuziki huyo amesema kuwa ni wakati sasa kuangalia maisha yake na familia yake ya watoto watatu ambayo amesema inamtegemea.

Aidha Amigo ambaye amekuwa na bendi hiyo kwa muda wa miaka 13 amesema hana kinyongo wala matatizo na mwanamuziki wala Mmiliki wa bendi hiyo Asha Baraka na kuwa kuondoka ni hiari yake mwenyewe.
Pata kibao cha Aminata ambacho ni utunzi wake amigolas enzi hizo akiwa na akina Jesca Charles, Aly Choki, Banza Stone na wengineo.


Pekecha pekecha

July 15, 2008
Mnenguaji na muimbaji wa Bendi ya Akudo Impact Chai Jaba (kulia) akiserebuka sambamba na mashabiki wa bendi hiyo katika Bonanza lililofanyika New Msasani Beach Club Jijini Dar es Salaam, usiku wa kuamkia leo. (Picha na GPL)

Mnenguaji na muimbaji wa Bendi ya Akudo Impact Chai Jaba (kulia) akiserebuka sambamba na mashabiki wa bendi hiyo katika Bonanza lililofanyika New Msasani Beach Club Jijini Dar es Salaam, usiku wa kuamkia leo. (Picha na GPL)


FINAL CALL FOR ARTISTS 2009

July 15, 2008
 .

.

Final Call for Artists

The final deadline for receiving applications from artists interested in performing at the next Sauti za Busara is 31 August 2008.

The sixth edition of Sauti za Busara [Sounds of Wisdom] music festival takes place in Zanzibar during 12 – 17 February 2009.

The main aim of the Festival is to bring people together in celebration of the wealth and diversity of Swahili music. Every year the festival features more than forty groups, including thirty from East Africa and ten from other parts of Africa and beyond.

This year, the festival is especially keen to encourage more applications from Ethiopia and Horn of Africa, Southern Africa as well as more traditional music groups from East Africa.

Please note that without receiving your application and at least one recent recording, the festival selection committee will not be able to consider your participation when it meets at beginning of September 2008.

You can apply online in English, Kiswahili and French.

Assuming your group is selected and that it is possible to find sponsors for international flights, the festival will cover costs for local travel, accommodation and meals in Zanzibar, a modest performance fee – and a magical and unforgettable experience is guaranteed!

Yusuf Mahmoud, Festival Director


Kaijage unawaonaaaa??????

July 15, 2008
Wachezaji wakibadilishana jezi

Michael Ballack na Clarence Seedorf

Mchezaji wa Ujerumani Michael Ballack (L) na Clarence Seedorf Msuriname mwenye uraia wa Holland wakibadilishana  jezi baada ya mchezo wa hisani hapo majuzi tarehe 12 July, Mchezo huu ulishirikisha Nyota wa dunia katika kuchangia Taasisi ya  “Goal4Africa” ambayo inatoa misaada mbali mbali kwa nchi za Africa, mchezo uliochezwa huko Allianz Arena stadium, Jijini Munich, kusini mwa Germany, Picha hii inanikumbusha sakata la mchezaji wa Taifa Stars aliyedaiwa Jezi baada ya kubadilishana na mwenzie Samuel E”too baada ya mchezo kuisha, Ingawa Rais wa TFF alitoa ufafanuzi lakini kitendo hicho kililaaniwa vikali na wapenzi wa soka. (AFP PHOTO DDP/PHILIPP)


Ronaldinho: Bye bye Barcelona

July 15, 2008

Mchezaji wa Barcelona Ronaldinho akiingia kwenye gari yake mara baada ya kikao na viongozi wa Klabu yake ya Barcelona hapo jana 14 July, 2008, Rais wa klaby ya Barcelona Joan Laporta amesema wamepokea ofa ya Euro 32 million (sawa na Dola 51 million) toka klabu ya Manchester City kwa ajili ya kumuachia mchezaji huyu ambaye alipata kuwa mchezaji bora wa Dunia kwa miaka miwili said. AFP PHOTO / JOSEP LAGO (Photo credit should read JOSEP LAGO/AFP/Getty Images)


Michael Ballack aoa jana

July 15, 2008
Balack na Mkewe baada ya ndoa yao jana.

Balack na Mkewe baada ya ndoa yao jana.

Mwasoka wa Ujerumani na klabu ya Chelsea Michael Ballack, na mkewe Simone wakiwaaga ndugu, jamaa na marafiki baada ya kufunga Ndoa jana huko Kempfenhausen, kusini mwa Ujerumani, (AP Photo/Christof Stache).


‘Eto’o + Euro milioni 10 = Adebayor’

July 15, 2008
Emanuel Adebayor uwanjani

Emanuel Adebayor uwanjani

BARCELONA inajiandaa kutuma ofa ya kutaka kumchukua Emmanuel Adebayor wa Arsenal kwa kumbadilisha na mshambuliaji wake Samuel Eto’o na kutoa euro milioni 10, kwa mujibu wa gazeti la Sport.

Gazeti hilo la kila siku la Catalan linaamini kuwa ombi lake la kutaka kumchukua mshambuliaji huyo kutoka Emirates litapata nguvu wiki hii.

Eto’o thamani yake ni euro milioni 30, ina maana kuwa kwa kuongeza euro milioni 10 itakuwa imefikia dau linalotakiwa na Arsenal.

AC Milan ilikuwa ikimtaka mshmabuliaji huyo wa Arsenal, lakini imeonekana kusuasua baada ya timu yake kuonekana kushikilia dau la kuuzwa mchezaji huyo ni euro milioni 40.

Kocha Pep Guardiola wa Barcelona, amekuwa akitaka kumchukua mshambuliaji mwenye nguvu baada ya kutangaza kuwa Eto’o hayumo kwenye mipango yake na taarifa zinasema Adebayor ni kipaumbele cha kocha huyo.