kila siku kuna sauti mpya, wimbo mpya, mwanamuziki mpya, Hivi karibuni kundi la Rhumba la Muziki lilifanya rekodi ya albamu yake chini ya Kiongozi Pitshou Lumiere na mwanamuziki huyu anasemekana kutumia pesa nyimngi katika kutengeneza Video za Nyimbo za Albamu yake, kwa sasa Koffi Olomide anatajwa kuwa ndiye Mwanamuziki wa Zaire ambaye hutumia pesa nyingi katika kutengeneza Video za nyimbo zake ikiwa ni kuanzia Kampuni ya Utengenezaji, Mavazi na sehemu anazotengenezea Video hizo, lakini Video za Muziki za Pitshou zilipigwa kwa mbwembwe kama picha zinavyoonyesha.
Kava la juu la CD ya Bendi ya Rhumba la Muzika
Kiongozi Pitchou Lurmiere akiwa kwenye shooting ya wimbo wa Chez Ntemba 

Mbwembwe za Pitshou wakati wa shooting ya wimbo wa Moise Katumbi unaopatikana kwenye Albamu hiyo. 
Vimwana wakiwa wamekula pozi wakati wa shooting ya wimbo wa Chez Ntemba kwenye albamu ya kundi la Rhumba la Muzika.
Lumiere akiwa na Vimwana katika moja ya vibwagizo vya nyimbo zake.Wanamuziki wa Kongo katika suala la burudani ya muziki wa dansi wamepiga hatua, hivi karibuni mjadala wa kuhusu kitendo cha kundi la TOT Respect chini ya uongozi wa Kamarade Ali Choki kwenda Kongo kutafuta wanamuziki kwa ajili ya kuipa nguvu kikosi chake lilipigiwa kelele na wengi wakaonyesha kuwa ni kuua na kutothamini muziki wetu, lakini katika dunia ya leo ya utandawazi ambapo kimsingi hakuna mipaka kila mmoja anajaribu kuangalii kama si unafuu basi kiwango katika kukamilisha liziko la nafsi (satisfaction). Je ni kweli kuna haja ya kufanyiwa mabadiliko muziki wetu? Kwani tumeona jinsi bendi zilnazopiga muziki wetu kuchanganya na Rhumba ya Congo kama Twanga Pepeta zinavyofanikiwa.
Posted by piusmickys 









